Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 53,537
- 133,017
Acha uongo kijana unapata nini kudanganya umma?Kaka 1300 ni nyongeza kama bonas. Yanga wanamkata na gsm wanawapa zaidi ya 2b kwa mwaka mkataba ulisainiwa 2022 unaelekea mwisho. Simba kwenye huo mkataba ndio wanapata 3b bila bonas yoyote. Pole sana kwa kukosa taarifa kamili.
Yanga inajaza ukiona wamefungulia mbwa tiket zishauzwa tiyari mapato yameingia.
Hoja yako kuhusu Yanga kupata bilioni 2 kupitia mauzo ya jezi ni ya kupotosha na inadhihirisha kiwango cha juu cha miss information kuhusu klabu yako.
Taarifa rasmi kutoka kwenye mkutano mkuu wa mapato na matumizi ya Club yenu chanzo (Mwananchi) zinaonyesha wazi kuwa kwenye bajeti ya msimu wa 2021/2022, Yanga ilipanga kukusanya Tsh milioni 350 tu kupitia mauzo ya jezi na si bilioni 2 kama unavyodai kwa kujiamini bila rejea.
Ukweli wa Bajeti ya Yanga
Kwa mujibu wa bajeti iliyowasilishwa kwa wanachama kwenye mkutano mkuu:- Mapato ya jezi yalipangwa kuwa Tsh milioni 350
- Mapato ya udhamini: Tsh bilioni 4.9
- Ada za wanachama: Tsh bilioni 2.04
- Mapato ya mechi: Tsh milioni 565
- Mapato ya mitandao ya kijamii: Tsh milioni 960
Kwa hiyo, jezi zilichangia chini ya 5% ya bajeti nzima ya Tsh bilioni 7.9. Hii inaonyesha kuwa mauzo ya jezi si chanzo kikuu cha mapato kwa Yanga, na hakijawahi kufikia kiwango cha bilioni 2 hata kwa makadirio ya juu.
2021/2022 ndio mwaka ambao kwenye industry ya Club kits ni Simba ndio ili break record kwa kuingia mkataba mnono na kampuni ya Vunjabei ambao kwa mwaka Simba alikuwa anaingiza Bilion 1 bila kutegemea soko la mauzo.
Mashabiki wa Yanga mnapaswa kuwa wachambuzi wa takwimu, si wapiga kelele wa makadirio ya kufikirika.