Habari za wakati huu wakuu,
Kwanza kabla yayote labda nitamke tu rasmi kwamba mimi ni muumini wa dini ya kikristu na dhima ya uzi huu sio ku-criticize our faith (for those Christians) Bali ningependa tuweze kushare mawazo kusudi kung'amua hasa kweli ni ipi. Baada ya kusoma nyuzi kadhaa za mkuu Likud na na comments za mkuu Kiranga, nilijaribu kutafuta vitabu kadhaa niweze japo basi kupata mwanga kidogo kuhusu ni ipi ni kweli. Kitabu cha The bible fraud (hivi vyote vimeandikwa na Tony Bushby) sikufanikiwa kukipata ila hiki cha secret in the bible nimefanikiwa kukipata na ndio niko mbioni kumalizia. Aisee,
Ukisoma hiki kitabu kuna shocking facts (truth) ambazo kiukweli zimenishtua hadi sasa moyo wangu hauna amani. Imagine what you have been made to believe turns out to be fake. Kwenye biblia kuna siri nyingi sana na according to bwana bushby, mtu aliyeitwa Francis Bacon ambae ni moja ya magenius waliowahi kutokea duniani, ambae pia ni among the earliest initiates (masonry) ndie aliyepewa jukumu LA kuandika biblia ya kwanza na king jes ambapo humo aliencode siri nyingi sana ambazo inabidi uwe enlightened kuweza kuzifahamu. Pia anasema Jesup christ had a twin brother na hakuuliwa kwa crucifixion bali he was stoned to death baada ya kukamatwa na hatia ya kuiba the ancient secrets from Egypt na ndipo alipoanza kuperform MIUJIZA. hizi ni baadhi ya screenshots za baadhi ya pages Kwenye kitabu hiko...
View attachment 775699
View attachment 775704
View attachment 775706
Naomba tuweze kujadili swala hili kwa marefu na mapana wakuu lengo ni kugain knowledge wala sio kukashifiana kiimani. Mods pls Naomba msiuunganishe huu uzi na nyuzi zingine na kwa atakae hitaji hiki kitabu nitampatia.
Labda nianze kwa kukushukuru kuleta hoja yenye vielelezo vya kihistoria inayojaribu kuaminisha kuwa habari za Biblia ni hadithi za Wazungu zilizo na makosa mengi na kwamba sio za kuaminika! (HABARI ZA UONGO).
Ukweli ni Upi sasa?
Ukweli ni kwamba iwapo IMANI haikujaribiwa haiwezi kuwa thabiti na imara.
Kuna imani nyingi sana ambazo hazijawahi jaribiwa na bado zipo na watu wanazidi kuziamini imani hizo
.(IMANI ZA UPOFU - Ukiihoji tu unaacha kuiamini siku hiyohiyo).
Naomba Nieleze Kidogo kuhusu Ukristo na Kitabu chake kikuu rejea ambacho ni BIBLIA.
Ni Dini pekee ambayo Kitabu chake cha Maarifa na Imani ni kimoja tu.
Dini zingine kwa mfano Dini ya Wayahudi ina kitabu zaidi ya kimoja -
TORAH na
TALMUD. Huezi kushiba maarifa ya imani hiyo bila kusoma kitabu cha ziada.
Hivo hivyo Uislam -
Quran na
HADITH.
Ukristo umepigwa vita na Watu wengi sana katika historia;Watawala(mfano NERO),Imani zilizokinyume chake,Kuchomwa kwa nakala za biblia,Kubanikwa kwa wote waliojiita Wakristo (Wafia dini ulimweguni kote - Hawa waliuwawa kwa kukiri kuwa wao ni wafuasi wa Yesu Kristo - Kanisa la kwanza) Kukatazwa kuabudu na mambo kadha wa kadha yanayofanana na hayo. Lakini mpaka leo bado ukristo ni imani pekee ambayo mafundisho yake yasipopotoshwa yanaleta Uzima na Amani sana.
Nafurahi kwa sababu Ukristo Umesemwa vibaya sana! Umetukanwa mno! Umebezwa sana! Umedharauliwa sana!
Naomba niwataje baaadhi ya waandishi maarufu sana ambao iwapo maandishi yangekuwa na nguvu yangesha uuwa Ukristo Duniani.
1. Bertrand Russel
2.Richard Dawkins
3.George Bernard Shaw
4.Karl Marx
5.C.S Lewis
6.Lee Strobel
7.Malcom Muggeridge
LIST NI NDEFU!....
Lakini cha ajabu sasa baadhi ya hawa waandishi walibadili gia angani na kuukubali Ukristo kwa Mikono Miwili.
HOJA NINI BASI JUU YA UKRISTO.
Hoja ni Ndogo sana "Kubwa sanaaaa' -
YESU.
Shida ni Huyu Bwana Mkubwa - YESU.
Iwapo wangeweza Kumdiscredit YESU basi Imani ya Wakristo ingekuwa ni Bureeeeeeeeeeee.
Wanatumia Makosa madogo madogo sanaa ya Watafsiri wa Biblia - (Trivial errors and innocuous one) toka Lugha moja hadi nyingine = Kiebrania (Hebrew) - Kiyunani (Greek Septuagint) - Kilatini (Latini Vulgate) mpaka kwenye versions za kiingereza Kama vile NIV,KJV,SV na nk.
Pseudo Historical Narratives.
Ooh sijui Hadithi za Wamisri wa kale - Kabala na uongo mwingine.
Na hoja zingine nyingi ambazo kisomi "zinamashiko ya Kishule" Welevu wa kidunia sio wa kiimani( Research is only refuted by another research).
Iwapo wewe ni Mkristo wau Mwislam swali ni moja tu! Je Imani yangu inafanya unachokiamini?
-
kama hamniamini Mimi basi aminini kwa kazi ninazofanya -Yesu Kristo
Faith is all about experience and revelations.
Kwa sababu binadamu wamekuwa na masikio ya kuwasha sana! hawataki kuamini Biblia basi aminini kwa kusoma Habari toka kwa Wasioamini Kristo ambao walikutana na Experience ya ajabu wakakubali.