The Bible Fraud & Secret in the bible...!!!

The Bible Fraud & Secret in the bible...!!!

Ni ukoloni kwani wazungu ndiyo waliotumia ukristu kututawala na kutupumbaza huku wakituibia rasilimali zetu. Walifuata nyayo za waarab.
Ndiyo maana nikasema athari za kutawaliwa na wazungu ndiyo zinazotufanya waafrika tuwahusishe wazungu na ukristo.
 
Mkuu donlucchese hakuna mtu yeyote anayekulazimisha kuamini kile unachotaka kuamini wewe. Hata BWANA MUNGU pia hakulazimishi umwamini, ni hiari yako kuamini utakacho. Kama wewe unawaamini hao walioandika hicho kitabu ulichokiweka hapa na kuona ndiyo wanasema kweli zaidi kuliko NENO la MUNGU ambalo limeandikwa kwenye BIBLIA, basi hiyo ni hiari yako wewe, unao uhuru wa kuamua.

Lakini muda wa kuamua utakapokwisha, ile siku ikifika, ambayo hakika imekaribia sana, hapo ndipo utajua kama ulifanya maamuzi sahihi au ulikosea katika maamuzi yako. Maana amini nakwambia siku hiyo YESU KRISTO atakuja na huku akiwa amezungukwa na jeshi lote la Malaika.

Wakati ule alikuja na akazaliwa kama katoto kadogo na kulazwa kwenye zizi la ng'ombe, lakini safari hii anakuja kama Mfalme mwenye Mamlaka juu ya viumbe vyote. Wakati ule walimkamata na akajitoa ili wamkamate, na wakamtundika juu ya mti, safari hii Yeye ndiye anakuja kukamata, kuhukumu na kutupa ndani ya moto ulao.

Mwenye masikio na asikie, mwenye kusoma na afahamu!
 
Kutoamini Biblia sio kwamba ni atheist, wazee wa zamani hawakuifahamu Biblia lakini walikuwa wacha Mungu. Kukataa ukristu na uislam sio kwamba humwamini Mungu ila una njia zako za imani. Narudia tena kwa confidence kwamba dini zimetengenezwa na watu, ni biashara hivyo zingatia unachoamini. Mimi naamini katiba ya nchi yangu kuliko Biblia kwa sababu tulishirikishwa katika maamuzi, ulikuwepo kwenye maamuzi ya Biblia? Wanasema ni kitabu cha Mungu ni kweli?
 
Biblia sehemu ile ya kwanza yaan maandishi ya kiebrania pamoja na kiaram yamekuepo kwa kwa maelfu ya miaka sehemu ya pili ya maandishi ya kigiriki yamekuepo karibu miaka 2000 sasa na wachimbuzi wengi wa vitu vya kale wanazidi kuchimbua vitu vingi vya zamani sana vyenye habari fulani zinazounga mkono masimulizi ya biblia.kufikia ss kuna uthibitisho mwingi wa usahihi wa masimulizi ya biblia kuliko kitabu kingine chochote cha kale...tunawezaje kuamini kitabu cha juzi tu cha Tony Bushby ambacho masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa pasipo kuacha shaka..kwa kifupi kwa maoni yangu masimulizi ya Tony Bushby ambayo anaaminisha watu kuwa ni sahihi ni hadithi za kutungwa kwa usanii kwa ustadi mkubwa lakn hazina uthibitisho.
Mambo ya kutungwa na madhara yake yakikaa miaka mingi na vizazi kupita watu wenye imani haba wanaingia kwenye huu mtego ila mi sishangai kwani vitabu vya kizushi vipo vingi kama kuna kitabu kimoja kinatambulika kama ''injili ya barnaba'' mwandishi anajifanya ni barnaba yule aliyekua anaongozana na paulo.
 
Mimi natoka nje ya mada makusudi.

Hivi kama lengo la biblia ni kufundisha upendo na imani. Kwanini hao walioileta biblia wasiwafundishe na kuwaachia hayo mafundisho hao wanao wafunsha ili wakafanye sawa na mapenzi yao? Kwanini ujenge nyumba uwakusanye kila siku? Kwanini uwawekee utaratibu na kuwaongoza? Je binadamu hushurutishwa kuzaliwa? Je binadamu hushurutushwa kuishi? Nini maana ya maisha? Je maisha sio kua huru na kufanya utakacho? Je kunamtu mwenye maamuzi juu ya mwisho wa mwenzake kama ni hivyo kwanini watu hufa wakiwa huru?

Hii ina maana maisha ni uhuru hadi mwisho wake ni uhuru pia. Sasa basi kwanini uwalazimishe watu na kuwamonitor? Kwakuwajengea "kanisa" na kuawapa miongozo ya kuishi?

Mwenye hoja anipinge kwa hoja, usilete hisia hapa.
Hoja zako zinaitaji akili kubwa sio ki 00 tu
 
Uko sahihi kuhusu idadi ya vitabu vinavyotokeza biblia ila hauko sahihi kuhusu walioandika vitabu hivyo kitabu cha Mathayo kimeandikwa na mathayo mwaka 41AD, marko kimeandikwa na marko 65AD, Yohana kimeandikwa na Yohana 98AD, matendo kimeandikwa na luka mwaka 61AD na vile vitabu vya kwanza vya biblia viliandikwa na musa kuanzia mwaka 1513BC hadi1473bc...hiyo dhana kuwa vitabu viliandikwa miaka 600 baada ya Yesu kufa sio kweli kwa maana Yesu au Issa alikufa mwaka wa 33AD miaka 8 baadae Mathayo anakamilisha kitabu chake yaan mwaka 41AD.
Mkuu ukisoma matthew(Matayo) 9:9, ni kisa cha Yesu alipomuana Matayo(Mathew) kakaa katika offisi ya mkusanya kodi,utaona kuwa alieandika hii stori sio Matayo(Mathew)

Matayo 9:9
inasema -"Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata"

Kama Matayo ndie alieandika biblia ya matayo angeliandika "Yesu aliponiona mimi,nimeketi katika ofisi ya kukusanyia kodi,akanambia "“Nifuate”,na mimi nikainuka,nikamfuata""... sio alipomuona mtu mmoja anaitwa Matayo(Mathew),..

Hii inaonyesha sop Mayato ni mtu mwengine alieandika stori,na ndio maana ukisoma biblia inasema "kutokana na Luka au Matayo..nk", "bible according to Mark or John... etc...."

Ukweli wenyewe haijulikana ni mwaka gani hivi vitabu vimeandikwa na nani kaandika,isiposipokuwa biblia ya "King James" hii inajulikana mwaka gani imeandikwa..

Unasema dhana ya kuwa biblia imeandikwa miaka 600 baada ya yesu sio kweli,basi lete ushahidi wako kuwa hiyo miaka uliyoiandika wewe ni kweli..
 
Unafikiri waafrika hatukuandika historia kwa sababu gani?
Ustaarabu umeanza Egypt, wafrika wa Egypt wameandika historia kwa kila walichokifanya,kila kitu kimeandikwa,Wazungu wanasema wagiriki ndio waliowaletea ustaarabu ulaya,Mgiriki kaiga kila kitu kutoka Egypt hao wanafilosofi wa Kihiriki wote wameiga kila kitu kutoka Egypt..

Kumbuka kuwa warumi(Roman empire) wametawala Egypt miaka mingi,wagiriki wamekaa hiyo nchi miaka mingi,watu wa mwanzo kuitafsiri biblia kutoa kihibrania(Arameic) lugha ya Isa(yesu) kwenda lugha nyengine ni wagiriki,Armenic na Kigiriki ni lugha zenye mfumo tafauti,akosa mengi yametokea katika tafsiri

Kuna watu,baadhi ya wazungu wanafikri yesu(Isa) alikuwa anazungumza kigiriki,...Mkuu sio kama waafrika hawajaandika historia,ukweli ni wazungu wamepindisha historia ya mwafrika,...
 
Naona umeizungumzia Egypt tu,kwanini iwe Egypt tu?
 
Nilikuwa nauliza hivyo tu kama madawa tunayotumia yana majina yenye asili na afrika basi sikuwa na lengine.
kama ulitaka hivyo yapo ya kwetu yenye majina yetu, kwani hujawahi kusikia kiboko ya chausiku? Au mshana? Sio wa jf Hiyo ni Dawa ya kihaya
 
Mkuu ukisema kitu fulani ni feki maana yake kuna original na ndiyo maana ukaweza kugundua feki yake,sasa unaweza kutuambia dini ya kweli ambayo ndiyo halisi ipo wapi au ilipotelea wapi?
nitajie criteria za kuipima dini ya ukweli mimi ninakwambia dini hizi ni feki sababu zimebeba visa vya uongo na kutungwa vingine havi make sense hata kwa akiri ya kawaida stori za wanyama kuongea si hadith za kawaida tu hizo lakini kwenye vitabu vya dini tunaona kama visa vya ukweli
 
Mkuu dini ya ukweli(original) ni wazi utakuwa unaijua na ndiyo maana ukaweza kutambua dini feki,ndiyo mie nikakuomba unitajie hiyo dini halisi ili tuache hizi feki.

Wewe ndiyo uliyesema dini zote feki sio mie,na ndiyo nikataka kujua dini ya ukweli ilipotelea wapi hadi zikabaki feki tupu?
 
Wazungu nao wanaiga lakini ni wazuri wa kujifanya kila kitu wamegundua wao,ustaarabu wa wanzo duniani,kuanzia dini na mambo mengine umeanzia Egypt,wazungu mpaka leo hii wanapinga kuwa yale magofu ya Pyramid yamejengwa na mtu mweusi..

Ukiangalia na kutafakari,Nabii Musa ambae alizaliwa Egypt nae alikuwa mweusi,Nabii Ibrahim alikwenda Egypt na kupewa mke Hahar(Hajir) mke nae alikuwa mweusi,Hagar aliezaa na nabii Ibrahimu wakamzaa Ismael,.Isa(Yesu) alikuwa mweusi,ukisoma biblia wasifu wa Isa(Yesu) ni kama wasifu wahabeshi(Waithiopa),nikisema weusi hapa namanisha na wasifu wa wahabeshi au wasomali,hawa watu ni weusi lakini wana nywele kama za manyoya ya kondoo...

Historia ya dunia kaandika mzungu kwa kujipendela yeye ili binaadamu wengine wamuone yeye bora,tafakari
Mkuu usiropoke nani kakwambia ustaarabu umeanzia misri?!,b4 egypt was sumerian ni after 4000 years ndo wakaja wamisri napo ni kwa sababu ya migration tu ya wale wamesopotomian,usikalili na kujipendekeza.
 
Sumarian ndio akina nani hao mkuu,Ustaarabu umeanza Egypt,Wagiriki ndio wakapeleka ustaarabu waliouona Egpt Ulaya..

Mkuu kwa ufupi Sumerians ni watu walioishi kusini mwa "Mesopotamia" kwa sasa hiyo nchi inaitwa Iraq,,walijenga miji mingi sehemu ya kusini mwa Iraq(Mesopotamia)mpaka kufikia miaka ya 1700 BC,walipofukuzwa na "Babylonian"..

Inasemekana Nabii Abraham(Ibrahim) alikuwa Sumarien alizaliwa sehemu inaitwa Ur, lakini hata hivyo Ibrahim alihama na mkewe Sarai na Mpwa wake Lot,walichokuwa na kila walichonacho na kuhamia Cannan(Lebanon/Israel)

Vilevile historia inasema Ibrahim alikwenda kushangaa Egypt na akapewa mke huko alieitwa Hagar

Sasa mkuu hiyo miji ya hawa "Sumerians" je bado iko Iraq,!??Ustaarabu gani walioleta duniani!??Kama hujui kabla ya hawa "Sumerians" kulikuwa na watu wengine na ustaarabu wao wa sehemu zao tu,..Mkuu watu walioleta ustaarabu duniani ni watu wa Egypt..

Unasoma biblia vipande vipande,soma uunganishe "dots" ili upate kufahamu
 
Mkuu ukisoma matthew(Matayo) 9:9, ni kisa cha Yesu alipomuana Matayo(Mathew) kakaa katika offisi ya mkusanya kodi,utaona kuwa alieandika hii stori sio Matayo(Mathew)

Matayo 9:9
inasema -"Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata"

Kama Matayo ndie alieandika biblia ya matayo angeliandika "Yesu aliponiona mimi,nimeketi katika ofisi ya kukusanyia kodi,akanambia "“Nifuate”,na mimi nikainuka,nikamfuata""... sio alipomuona mtu mmoja anaitwa Matayo(Mathew),..

Hii inaonyesha sop Mayato ni mtu mwengine alieandika stori,na ndio maana ukisoma biblia inasema "kutokana na Luka au Matayo..nk", "bible according to Mark or John... etc...."

Ukweli wenyewe haijulikana ni mwaka gani hivi vitabu vimeandikwa na nani kaandika,isiposipokuwa biblia ya "King James" hii inajulikana mwaka gani imeandikwa..

Unasema dhana ya kuwa biblia imeandikwa miaka 600 baada ya yesu sio kweli,basi lete ushahidi wako kuwa hiyo miaka uliyoiandika wewe ni kweli..
Sawa nitakupa ushahidi wa vitabu vya kihistoria uende ukasome uongeze uelewa wa mambo ingawa ww pia umesema tu hiyo miaka 600 hujaleta ushahidi,kwa upande wa kwanini inasemwa kama ilivyoandika na Mathayo etc ni kwasababu biblia hizi tulizonaxo leo ni tafsiri hivyo watafsiri wao si mathayo ndio sababu wanakwambia kama alivyo...... sio kama nilivyo...hapo kinachokuchanganya unashindwa kutofautisha kilichotafsiriwa na original version.....tena kuhusu biblia ya king James hiyo ni tasfiri sio original version so kinachojulikana ni mwaka waliomaliza kutafsiri maandishi ya awali yaliokuwa na lugha ya kiebrania na kigiriki kwenda ktk kiingereza.
 
Mkuu hakuna asiejua kuwa Yesu alikuwa anazungumza lugha inayoitwa"Aramaic"unatakiwa ujue kuwa kiyahudi ni lugha yenye lafdhi("dialet") tafauti kama lugha nyengine,Yesu alikuwa anazumngumza kiyahudi (Jewish Palestinian Aramaic),

Yesu hakuandika kitabu,alikuwa anahubiri mafundisho yake kwa wanafunzi wake na kwa wanaemfata wa Israel,,,Hakuna biblia iliyondikwa kwa lugha ya Yesu(Aramic),katika karne ya kwanza watu walianza kukusanya na kuandika yale aliyohubiriwa Yesu..

kwanza mkuu nafikiri unajua kuwa hizi biblia ziko tafauti,biblia ya King james ina vitabu 66,biblia ya RC ina itaby 73,..

china nakuwekea copy and paste ya historia ya uandishi wa biblia:-

"The Bible was written over a period of 1400 to 1800 years by more than 40 different authors. The Bible is a compilation of 66 separate books, divided into two primary divisions: the Old Testament (containing 39 books) and the New Testament (containing 27 books). It is believed that all of the books of the Bible were written under inspiration of the Holy Spirit."..

kwa kiswahili cha kwaida:-
"Biblia iliandikwa katika miaka ya 1400 mpaka 1800 na zaidi ya waandishi 40,bibilia ni mkusanyiko wa vitabu zaidi ya 66,ambavyo vimegawika katika makundi mawili;Agano la kale(Taurat) lenye vitabu 39 na Agano jipya lenye lenye vitabu 27.,inasadikia kuwa vitabu vyote vya biblia vimeandikwa kwa mujibu wa roho mtakatifu"

Sasa Mkuu hii sentensi ""inasadikia kuwa vitabu vyote vya biblia vimeandikwa kwa mujibu wa roho mtakatifu", ndio utagundua kuwa sio kila kitu kilichiandikwa kwenye biblia ni maneno au mafundisho ya Yesu,ni mawazo ya watu

Mandiko ya mwanzo ya biblia ni barua aliyoandika Paulo kupeleka sehemu mbali mbali kwa waumini wa kikristo,..

Mkuu Paulo ndie muazilishi wa dini ya Kikristo,Yesu hakuhubiri kuwa aabudiwe,Yesu hakuhubiri kuwa yeye ni mtoto wa mungu,Yesu hakuhubiri kuwa atakufa kwa dhambi za binadamu,haya yote kayaleta Soul aka Paul,Asilimia 70% ya aliyokuwemo kwenye Biblia ni maneno ya Paulo
 
Mimi natoka nje ya mada makusudi.

Hivi kama lengo la biblia ni kufundisha upendo na imani. Kwanini hao walioileta biblia wasiwafundishe na kuwaachia hayo mafundisho hao wanao wafunsha ili wakafanye sawa na mapenzi yao? Kwanini ujenge nyumba uwakusanye kila siku? Kwanini uwawekee utaratibu na kuwaongoza? Je binadamu hushurutishwa kuzaliwa? Je binadamu hushurutushwa kuishi? Nini maana ya maisha? Je maisha sio kua huru na kufanya utakacho? Je kunamtu mwenye maamuzi juu ya mwisho wa mwenzake kama ni hivyo kwanini watu hufa wakiwa huru?

Hii ina maana maisha ni uhuru hadi mwisho wake ni uhuru pia. Sasa basi kwanini uwalazimishe watu na kuwamonitor? Kwakuwajengea "kanisa" na kuawapa miongozo ya kuishi?

Mwenye hoja anipinge kwa hoja, usilete hisia hapa.

Kwa Biblia hayo ndiyo maagizo. " Msiache kukusanyika...". Tangu mwanzo waumini "walikutana....". Kukutana kuna faida yake. Mnajengana, mnahudumiana kwa huduma mbalimbali. Mbinguni wanadamu watakuwa na maskani yso pamoja na Mungu. Ibada ni ya pamoja na wengine siyo ya mtu mmoja.
 
Kabla ya kuletewa kitabu cha biblia waafrika walikua hawakusanyiki? Una ushahidi kama unao uweke hapa.
Kabla ya kuletewa dini waafrika walikua hawaishi? walikua hawapendani? walikua hawasaidiani?Je hawakupata mahitaji yao ya msingi?

Kabla ya kuja kwa wageni weupe walio beba kitabu cha biblia na nia ovu ya kuwagawanya na kuwatawala waafrika ambao tayari waliishi maisha yao mazuri, waafrika hawakuhitaji chochote juu ya dini wala imani. Kwani kabla ya hapi waliishi miaka mingi ya furaha bila ya uhitaji wa msaada unaowadumbukiza katika mgawanyiko wa kidini,magonjwa,madawa feki yenye sumu na kudharauliwa(racism).

Maswali mengine ya msingi.
Kama hicho kitabu cha biblia kinatangaza "yajayo",imani na upendo. Niambie nini hatma ya waafrika waliokufa miaka mingi kabla ya kuja kwa biblia? Nini hatma ya wenzetu wa mfano (wamang'ati ) na jamii zinazoishi maisha yao mazuri porini na hazifahamu bibilia? Je kwamba hawa si binadamu? Nini hatma yao kama wanadamu? Je utamlaumu mzungu kutowapa biblia? Au tuilamu mother nature kwa kuwapa hayo mazingira?
 
Sasa huyo twin brother wa YESU ametokea wapi?
Na kufa kwa kupigwa mawe haiendani na mafundisho ya "ufufuko" wa YESU... Kuna maana ya kibiblia kwa nini alisulubishwa.. Na kwa nini alifufuka..

Na hapo ndio ulipo msingi au chimbuko la ukristo.
Juhudi kubwa ya kufifisha hilo tukio ni kuvunja na kuonyesha ukristo hauna maana.
 
Back
Top Bottom