The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

Status
Not open for further replies.
Japo kuwa STUNTER hajakuuliza maswali ya maana saana hasa deep kwa mtu wa level yako, watu kama nyie mna maswali yenu bwaanaaa, mambo ya kiungo sijui usichokipenda sijui mbuzi kwenye gunia hayo ni ya kina mond na wema, BTW amejitahidi kukuvuta hapa kwakuwa bold alikuwa anaonekana katika makala au andishi lake tu, Leo kujumuika hapa aiseee mungu mkubwa, ni sawa na diamond akafanye show ya bure uwanja wa taifa,
Ok labda mm niulize maswali yangu matatu tu ambayo sijaridhika nayo.

1. Ningependa kujua elimu yako stage kwa stage kama fundi wa tanesco anavopanda ngazi zake kumfungia mteja mpya umeme, [emoji3][emoji3][emoji3] from vidudu- ------++

2. Umesema umeanza kutumikia taifa tangu upo shule, JE KIVIPI? Kuna ukakasi nauona hapa ukizingatia na umri wako sio kivileee hadi tukuweke katka list ya waliosoma kipindi cha mwalimu....
Tungependa utuambie ni kazi gani hiyo najua unaendelea nayo, kazi gani kwa serikali gani ya kukufanya ulale hadi saa 3/4 asubuhi?

3. Hili linaweza tegemeana na swali la pili kiasi fulani, kuhusu kibiti umesema kuwa wahusika walikufuata kukuomba ushauri how? Waache mawaziri wastaafu, wabunge wa upinzani mbali na kufuatwa hawaruhisiwi hata kuzungumzia hiyo kitu. Kwanini wew?

Inatosha kwa sasa nikikumbuka jambo nitauliza tena
Cc The bold
duu unaunganisha Dots haa haah
 
Mmmhh my sista from another mother... Haya maswali kuntu hahaha


1. Nimeeleza kuwa nilipata mchongo kwa serikali kipindi niko chuo Mzumbe... Kuna jamaa flani, Lecturer ndio aliniconnect kwenye hiyo mishe anaitwa Leonard (not his real name, trying to conceal his identity)... Over time dizaini ndio akawa kama 'Mentor' wangu... Nilijifunza a lot of thing from him... Yani nahisi alisaidia kushape my mind and the way I think na personality...

Now ilikuja kipindi akawa anaumwa... Alipata tatizo la kidneys... Alizidiwa sana sana to the point akwa anashindwa kutimiza majukumu yake... So I had to help him kutimiza majukumu yake fulani fulani ya kikazi...

Kuna siku alipata nafuu kabisa tukahisi anapona sasa...

Kulikuwa na trip flani hivi kwenda mwanza alikuwa anatakiwa aende... So nikasema sio kesi ngoja niende kwa niaba yake... But jamaa akawa ananisisitiza kuwa potezea bhana... Pumzika... Live a little, kazi ipo tu... But I was overzealous, too ambitious... Wanted to impress Tue bosses... So I made that trip... But nilipokuwa naondoka akaniambia "..khabib usichelewe mwanangu... There is something real important I need to share with you.!"

Nikiwa mwanza huku nyuma jamaa akazidiwa sana ikabidi mpaka achukuliwe na ambulance kutoka Mzumbe chuo mpaka Muhimbili...

Akiwa muhimbili familia yale wakanipigia... Wanasema "rudi fasta mzee anataka kuongea na wewe!"

Kesho yake nikafunga safari kutoka mwanza to dar... Nikiwa njiani mzee akafariki...

Mpaka leo nikikumbuka hili suala linanipa tabu sana... Alikuwa anataka kuniambia nini??? Kwenye pumzi yake ya mwisho alikuwa na secret ambayo alihisi ni mimi anapaswa kunieleza what was it???

That's my biggest regret kwenye maisha... I should gave made that trip to mwanza... I should have been overzealous namna ile...

Will never get a chance kujua hicho kitu!! Mbaya sana kuishi na feeling ya namna hiyo...
Hii kweli inauma, very sorry bro
Mcheki Mshanajr akupe hata mbinu za kumfata mzee ndotoni akupe ulichomiss
 
Haswaaa mkuu nikupe siri ndogo tu nyie hamumfaidi huyu mtu, najivunia kuwa nae karibu aisee!
True mkuu, i wish i could be you thou, sema japo sina mda mrefu sana tangu nianze kumfahamu na mkumfatilia but ninafahidi sana hiki ninachokipata toka kwake, ubaya zaidi wawezakuta jamii inayomzunguka haitambui na kuelewa kipawa alichonacho
natamani sana kuketi na jamaa walau a single day hopefully nitagain vingi sana toka kwake.
 
True mkuu, i wish i could be you thou, sema japo sina mda mrefu sana tangu nianze kumfahamu na mkumfatilia but ninafahidi sana hiki ninachokipata toka kwake, ubaya zaidi wawezakuta jamii inayomzunguka haitambui na kuelewa kipawa alichonacho
natamani sana kuketi na jamaa walau a single day hopefully nitagain vingi sana toka kwake.
Cc The bold [emoji115]
 
Karibuni members wote wa Jf kwenye haya mahojiano ya moja kwa moja, Yaani ni Mubashara kabisaaaa ambayo yataendeshwa na kusimamiwa na mimi STUNTER !
-
Na kwa siku ya leo tutakuwa na Mbobezi wa masuala ya Intelijensia ambaye si mwingine ni Mr. The bold !!

Hii ni ile siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi
hivyo
naomba kwa pamoja tutege masikio yetu na macho yetu na USIKUCOMMENT CHOCHOTE,
mpaka pale nitakapotoa ruhusa ya kuuliza maswali ya pamoja.
-
N.B
Hautakiwi kucoment chochote, na kama una swali basi subiri mpaka utakaporuhusiwa kuuliza
(maswali yote yatakayoulizwa nje ya utaratibu hayatojibiwa hatakama swali lako ni zuri kama MAKINIKIA).
Ninja naomba zawadi yangu
 
Zimewahi kutokea 'attempts' kadhaa za kunidukua mtandaoni... Tena nyingi nyingine juzi kati tu hapa

Kuna measures kadhaa huwa nazingatia ili kuwa safe mtandaoni ndio maana hackers hawajawahi kufanikiwa asilimia zote! Zinakuwaga attempts tu na kabla hazijaleta madhara zinakuwa contained
Unaweza kutuelezea hizo attacks kutoka kwa hackers zilivyokuwa na jinsi ulivyozicontain ili utusaidie na ss wengine tusiweze kudukuliwa?
Dogo unapenda kutuchoma roho walah[emoji23] [emoji23] [emoji23] nitavunja undugu wetu ohoo.hee kumbe nimeingia nisipotakiwa[emoji125] [emoji125]
 
Mh! Kwa hivyo ww ni mtuzi tu wa makala? Kwa maana watu wengi huwa tunajificha nyuma ya pazia
 
Mkuu The bold unahisi kuna tofauti gani kati ya intelligence ya Tanzania uki compare na za nchi zingine kama USA n.k?
Unahisi nini kinafeli kati shughuli nzima za ki intelijensia za Nchini mwetu?
Kipi kifanyike walau waweze kufikia level ya hao walioendelea mfano FBI n.k
Shukran.

We need to modernise our intelligence machinery... Bado kwa asilimia kubwa haiendani na kasi ya karne ya 21...

Wanausalama wetu they have to work twice as hard kufikia lengo...

Pia majukumu ya TISS yapunguzwe kwa kuundwa Idara dada za Usalama ambazo zinajitegemea...

Kwa sasa Tiss na polisi wanamajukumu mengi mno... Mfano masuala ya counterterrorism hayako sawia ni nani hasa anapaswa kuyatekeleza... Matokea yake Tiss wanabebeshwa mzigo mkubwa ambao muda mwingi unavuka mpaka malengo ya kuanzishwa kwake...

Kuwe na Idara nyingine mahususi za masuala ya Intelijensia...


Kwenye jeshi... Kitengo MI (Military Intelligence) ipewe mikono zaidi ya kufanya mambo bila urasimu wa kiprotokali... Ikiwezekana iwe-rebranded hata ijitegemee na kubadilishwa jina na jeshini wabaki na MI ya kwao (ambayo haitakuwa hii mpya)

Pia ni vyema ikaanzishwa ofisi ya National Director of Intelligence... Simuongelei mkurugenzi wa Tiss... Mkurugenzi wa Tiss abakie vile vile kama DG wa TISS... Huyu ni National Director of Intelligence (Au tunaweza kuita vingine) hii ofisi ndio ambapo masuala yote ya Intelijensia watakuwa wanayachakata na kuyawasilisha mahala husika... (Mfano kwa rais)

Hii itasaidia kuwa na flow na coordination nzuri ya Intelijensia kutoka vyombo vyote... Tiss, polisi, jeshi na vingine ambavyo nahisi ni vyema vianzishwe...

Lakini pia itaondoa hii kasumba ya Rais kuwa Sponsor wa mashushushu wote... Rais ni mwanasiasa na binadamu... Kufanya yeye kuwa Sponsor wa Tiss inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi ya taifa na maslahi yake...

Ni vyema huyu National Director of Intelligence ndio awe anatoa briefing zote za Intelijensia kwa Rais kutoka Idara na vitengo vyoye vya ushushu...


Kuna changamoto kubwa sana ya coordination ya taarifa za Intelijensia kwenye vyombo vyetu! Kila mtu yuko na Lwake... We need a center point... Sehemu mahususi ambayo itachakata hizi Intelijensia na kutoa miongozi mahususi kwa serikali ma vyombo husika... Nadhani tukianzisha ofisi ya National Director of Intelligence inaweza kutupeleka mahala...


(Kumbuka siongelea director wa Tiss)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom