The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

Status
Not open for further replies.
duu unaunganisha Dots haa haah
 
Hii kweli inauma, very sorry bro
Mcheki Mshanajr akupe hata mbinu za kumfata mzee ndotoni akupe ulichomiss
 
Haswaaa mkuu nikupe siri ndogo tu nyie hamumfaidi huyu mtu, najivunia kuwa nae karibu aisee!
True mkuu, i wish i could be you thou, sema japo sina mda mrefu sana tangu nianze kumfahamu na mkumfatilia but ninafahidi sana hiki ninachokipata toka kwake, ubaya zaidi wawezakuta jamii inayomzunguka haitambui na kuelewa kipawa alichonacho
natamani sana kuketi na jamaa walau a single day hopefully nitagain vingi sana toka kwake.
 
Cc The bold [emoji115]
 
Ninja naomba zawadi yangu
 
Unaweza kutuelezea hizo attacks kutoka kwa hackers zilivyokuwa na jinsi ulivyozicontain ili utusaidie na ss wengine tusiweze kudukuliwa?
Dogo unapenda kutuchoma roho walah[emoji23] [emoji23] [emoji23] nitavunja undugu wetu ohoo.hee kumbe nimeingia nisipotakiwa[emoji125] [emoji125]
 
Mh! Kwa hivyo ww ni mtuzi tu wa makala? Kwa maana watu wengi huwa tunajificha nyuma ya pazia
 

We need to modernise our intelligence machinery... Bado kwa asilimia kubwa haiendani na kasi ya karne ya 21...

Wanausalama wetu they have to work twice as hard kufikia lengo...

Pia majukumu ya TISS yapunguzwe kwa kuundwa Idara dada za Usalama ambazo zinajitegemea...

Kwa sasa Tiss na polisi wanamajukumu mengi mno... Mfano masuala ya counterterrorism hayako sawia ni nani hasa anapaswa kuyatekeleza... Matokea yake Tiss wanabebeshwa mzigo mkubwa ambao muda mwingi unavuka mpaka malengo ya kuanzishwa kwake...

Kuwe na Idara nyingine mahususi za masuala ya Intelijensia...


Kwenye jeshi... Kitengo MI (Military Intelligence) ipewe mikono zaidi ya kufanya mambo bila urasimu wa kiprotokali... Ikiwezekana iwe-rebranded hata ijitegemee na kubadilishwa jina na jeshini wabaki na MI ya kwao (ambayo haitakuwa hii mpya)

Pia ni vyema ikaanzishwa ofisi ya National Director of Intelligence... Simuongelei mkurugenzi wa Tiss... Mkurugenzi wa Tiss abakie vile vile kama DG wa TISS... Huyu ni National Director of Intelligence (Au tunaweza kuita vingine) hii ofisi ndio ambapo masuala yote ya Intelijensia watakuwa wanayachakata na kuyawasilisha mahala husika... (Mfano kwa rais)

Hii itasaidia kuwa na flow na coordination nzuri ya Intelijensia kutoka vyombo vyote... Tiss, polisi, jeshi na vingine ambavyo nahisi ni vyema vianzishwe...

Lakini pia itaondoa hii kasumba ya Rais kuwa Sponsor wa mashushushu wote... Rais ni mwanasiasa na binadamu... Kufanya yeye kuwa Sponsor wa Tiss inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi ya taifa na maslahi yake...

Ni vyema huyu National Director of Intelligence ndio awe anatoa briefing zote za Intelijensia kwa Rais kutoka Idara na vitengo vyoye vya ushushu...


Kuna changamoto kubwa sana ya coordination ya taarifa za Intelijensia kwenye vyombo vyetu! Kila mtu yuko na Lwake... We need a center point... Sehemu mahususi ambayo itachakata hizi Intelijensia na kutoa miongozi mahususi kwa serikali ma vyombo husika... Nadhani tukianzisha ofisi ya National Director of Intelligence inaweza kutupeleka mahala...


(Kumbuka siongelea director wa Tiss)
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…