The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

Status
Not open for further replies.
Ulikiwa PCB1 OR PCB2??

Kule PCB1 Unamjua Amney?? Yule binti wa Kiarabu??

Memory unamjua??

Evelyn unamjua?

Ester? Josephine? Au nikutajie darasa zima?

Ticha Mjuni wa Physics??

Unawajua hao??

Somehow mkuu HB umeniimpress kwa kuwataja hao watu lakini kwa hilo jina ulilotuambia hapana mayb ulikua unatumia jina jingine
 
Mkuu nakumegea tu Kuna mtu anaitwa Mange Kimambi Nifah alishawahi kuleta thread kumuhusu na alimjibu kwa I D yake halisi kwaiyo jiandae kuchambwa wewe ,mkeo na koo zenu kwa ujumla ukishakuwa verified sijui umejiandaa kisaikolojia na hilo?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] watakan kata.
 
The bold
Kipi ni sahihi kwako kati ya serikali kumiliki fedha nyingi kisha wananchi hawana kitu, au wananchi kuwa na fedha nyingi alafu serikali haina kitu? Why?
(Ningependa ujibu hili swali kitaalamu hasahasa katika kubalance hali ya maisha)
swali jepesi.
unyoya wa kifaraanga cha kuku...ni mzito zaidi...!!..
 
Hizi interview zahitaji moyo na muda kujibu. Maswali mengine ni ngumu kumesaaa
 
Brother, Congrats for the interview but bahati mbaya sana hujamuuliza maswali yeyote kuhusu intellijensia.
ndio interview ilipokosa maana ya muhusika maana... amepata jina ktk misingi ya makala zake kali zenye kusisimua kuhusu intell...
 
Hili swala la Kibiti nimewahi kuilizaa na wahusika wa vyombo vya usalama na nimetoka maoni yangu marefu sana huko...

Sasa najua watu watauliza... Wakuilize wewe kama nani.? Nadhani hili swali wakaulizwe walionifuata, walinifuata mimi kama nani??


Hili la North Korea nimewahi kuandika mpaka uzi kipindi kile mzozo umekole...

1. Nilisema licha ya kwamba japo tunaichukia Marekani, lakini uhalisia ni kwamba NK hawezi kumpiga Marekani abadani... Ni sawa na kusema Stendi United amfunge Barcelona... Miujiza inatokeaga... Ila muujiza huu unaoswa uwe muujiza haswa


2. Nikasema kuwa haiwezi kutokea vita ndani ya miezi minne ijayo kwa kuwa kadiri nilivyofuatikua hakuna mabadiliko yoyote kwenye kiwango cha DefCon ya JCS nchini Marekani.... Watu wakabisha hasa kuwa ndani ya siku chache vita itatokea... Huu mwezi wa pili sasa unaenda wa tatu... Nadhani tumeshajua nani yuko sahihi... Na nakazia kwamba mpaka mwaka huu unaisha usitegemee vita kati ya US vs NK
we jamaa kuhusu kibiti..
mbona umejibu kibabe..??..
 
Pamoja mkuu...

Ingawa nahisi kuna maswali watu walikuwa na kiu nayo haujayauliza...

Tusubiri wadau labda watauliza...
yaani maswali yake kwako...ilikuwa baina ya chai na mkate tuu..embu nijibu hili...
1*kwanini makala,uchambuzi na hadithi zako unazama sana kwenye taaluma ya KIINTELLIJENSIA..lengo lako hasa nini..??. kutuonyesha kwamba intell unaijua sana,unaipenda au umejikuta tu intelligence ndio muongozo wa maisha yako..
2*wewe ni muumini wa imani ipi ktk ulimwengu wa kiimani..??.
3*kabila gani..??..

nianze na hayo kwanza....
 
hongera sana mkuu The bold ....umesema unapenda kuangalia cinema hebu tuambie kati ya wakali hawa wawili wa hollywood rambo vs anord yupi unamkubali zaidi na kwa sababu zipi hasa
Una umri gani dogoo mpaka uulize eti kati ya Rambo na Anord yupi mkali ama anayekubalika zaidi

Wewe ni msukuma eeh...!

Shie.
 
We need to modernise our intelligence machinery... Bado kwa asilimia kubwa haiendani na kasi ya karne ya 21...

Wanausalama wetu they have to work twice as hard kufikia lengo...

Pia majukumu ya TISS yapunguzwe kwa kuundwa Idara dada za Usalama ambazo zinajitegemea...

Kwa sasa Tiss na polisi wanamajukumu mengi mno... Mfano masuala ya counterterrorism hayako sawia ni nani hasa anapaswa kuyatekeleza... Matokea yake Tiss wanabebeshwa mzigo mkubwa ambao muda mwingi unavuka mpaka malengo ya kuanzishwa kwake...

Kuwe na Idara nyingine mahususi za masuala ya Intelijensia...


Kwenye jeshi... Kitengo MI (Military Intelligence) ipewe mikono zaidi ya kufanya mambo bila urasimu wa kiprotokali... Ikiwezekana iwe-rebranded hata ijitegemee na kubadilishwa jina na jeshini wabaki na MI ya kwao (ambayo haitakuwa hii mpya)

Pia ni vyema ikaanzishwa ofisi ya National Director of Intelligence... Simuongelei mkurugenzi wa Tiss... Mkurugenzi wa Tiss abakie vile vile kama DG wa TISS... Huyu ni National Director of Intelligence (Au tunaweza kuita vingine) hii ofisi ndio ambapo masuala yote ya Intelijensia watakuwa wanayachakata na kuyawasilisha mahala husika... (Mfano kwa rais)

Hii itasaidia kuwa na flow na coordination nzuri ya Intelijensia kutoka vyombo vyote... Tiss, polisi, jeshi na vingine ambavyo nahisi ni vyema vianzishwe...

Lakini pia itaondoa hii kasumba ya Rais kuwa Sponsor wa mashushushu wote... Rais ni mwanasiasa na binadamu... Kufanya yeye kuwa Sponsor wa Tiss inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi ya taifa na maslahi yake...

Ni vyema huyu National Director of Intelligence ndio awe anatoa briefing zote za Intelijensia kwa Rais kutoka Idara na vitengo vyoye vya ushushu...


Kuna changamoto kubwa sana ya coordination ya taarifa za Intelijensia kwenye vyombo vyetu! Kila mtu yuko na Lwake... We need a center point... Sehemu mahususi ambayo itachakata hizi Intelijensia na kutoa miongozi mahususi kwa serikali ma vyombo husika... Nadhani tukianzisha ofisi ya National Director of Intelligence inaweza kutupeleka mahala...


(Kumbuka siongelea director wa Tiss)
NAOMBA NAMBA YA KUJIUNGA NA LILE GROUP LAKO LA WHTSAPP....
we jamaa... kuna kitu unacho...kila ninapokusoma naona kuna kitu zaidi unacho kwa ajili maslahi fulani ya jamii...lakini hukimalizi...
embu fanya hivyo...kwanza...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom