The bold: Waraka

The bold: Waraka

Flola alikubali kuolewa na Mbasha akiwa hana kitu kwanini leo afanye hivyi kuna vitu ambavyo mumewe katenda sasa amefikia kusema mwisho/amechoka.Na imefikia hapo sababu Mbasha ni king'ang'anizi hataki kumuacha Flola sababu ya umarioo wake.
Mwanaume anayejielewa hawezi kulazimisha kuishi na mwanamke ambaye ni mzinzi, na kama alijua mchungaji anadhini na mkewe kwanini aliendelea kusali hapo? Mbasha anatafuta tu huruma kama ni unzinzi wote ni wanzinzi sema mwanamke kawa smart kamzidi ujanja.
Maana ktk mahojiano yote na waandishi sijasikia Mbasha akikana tuhuma za kutembea na hao mabinti/kubaka.

Maisha Mbasha aliyakosea mwenyewe kijana mzima badala ya kufanya kazi unakaa kuruka ruka jukwaani na mkeo. ndio matokeo yake hayo mwanamke anakuchoka anaona umekuwa mzigo anakulisha, kukuvisha na unalala kwa jasho lake.,akipata mwanaume wa kumtunza tu anakushiti. Hela ya mwanaume ina raha yake jamani

siamini kama Mbasha alibaka lakini naamini alikuwa na uhusiano na hao wasichana sasa mrs amechoka na vitendo vyake kaamua kumkomesha.
 
Unajuaje kama alivyogundua na kutaka kuchukua hatua ndio wakambambika kesi? Nyie misukule ya Gwajima mmeshikiwa akili hamtaki hata kufikiria nje ya box. Endeleeni na ufufuo wa misukule na uzinzi lakini kijana amegoma kuendelea kuishi huku amepiga magoti.


Yeye mwenyewe anasema huu mchezo ni wa mda mrefu halafu wwe unasema tofauti tukuamini wewe au mhusika mkuu.
 
Ila Frola ni mkatili sanaaa
Kuna kitu nyuma ya huu ukatili,hawezi kua katili hivi hivi,huwezi jua Imma kamtenda mara ngapi tena kwa ktembea na mdogo wake,bora yeye anatembea na Gwajima ambae hana uhusiano wowowte wa ki DNA na Imma.
 
Tafadhali: mods nimejitahidi kadili niwezavyo kutotaja majin ya watu kuepuka kuviolate sheria za jf, naomba muache huu uzi!!


Wakuu,

Kwa makusudi kabisa nimekuwa nikiliepuka kujibu swali kaka mimi ni mme wake dada yetu muimbaji ama la, laiti ningekuwa ndiye ningependa yeye na mchungaji wasome hapa;

“ mchungaji, ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako.

Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!

Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha?? Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo?????

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa! Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!! Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!! Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!! Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani??? Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!! Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!

Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako??? How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje??? Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea??? Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda???

Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu??? Fedha??? Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe???

Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii??? Ni nini kilichokuoata mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!

Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!! Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!! Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!! Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti! Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."


- The bold

Hapo ni lazima Mungu asimame vinginevyo shetani atapata nafasi zaidi
 
Kuna kitu nyuma ya huu ukatili,hawezi kua katili hivi hivi,huwezi jua Imma kamtenda mara ngapi tena kwa ktembea na mdogo wake,bora yeye anatembea na Gwajima ambae hana uhusiano wowowte wa ki DNA na Imma.

Pamoja na hayoo ni mmewe amezaa nae hautakiwi kulipiza kisasii na basi kama umechoka muachane tu kwa amani sio kivitaa, na huwez shindana na mwanaume, kwa hili frola ni mkosajiii hakuwah kumtembelea kule jela hata tu kutuma ndugu zake kama ye hatakii bado hujaona frola ana matatizoo, mwanaume ni mwanaume tu
 
mi nahisi the bold ndo mbasha by the way kaka wanawake sisi UTUONAVYO SIVYO UTUFIKIRIAVYO NA UTUFIKIRIAVYO SIVYO UTUONAVYO we are more than we are.Mwanamke akikuchukia ujue ht ufanyeje ndo imekula kwako.My advice futa vumbi futa machozi lia na mungu wako tu hapo hakuna ndoa tena ninyi s wa kwanza kutengana ktk hii dunia.ULIPOAMBIWA KUA UYAONE SIO MAGHOROFA KAKAAA......HUO NDO UKUBWA FUNGA MKAJA KM ULIBAKA KWELI AU SI KWELI HEBU LIA NA MUNGU AKUPIGANIE KTK UNACHOKIAMINI.

geniveros, ulichoandika hapa ndo sahihi: hata wakirudiana hawataweza kuaminiana tena. Na hawa watu wa "SYSTEM" watammaliza huyu Jamaa - ama kwa kumfunga miaka 30jela, au atapotea kiana "kwa maombi".. Jambo jema kwa yeye ajue tu kwamba mke wake yuko under dures kumfanyia hicho anachofanya : ni ama ahakikishe mumewe anapotea au apotee yeye. Keshakula pesa za "SYSTEM" asitegemee huruma yoyote ile. Tena The bold ameandika na maswala ya kuuza sembe , anategemea nini? Yuko wapi Amina (Mbunge kijana) na Mumewe? huwezi kuwagusa hawa mafiosi halafu utegemee huruma, ni lazima wakumalize. Mimi ningekuwa yeye, ningekusanya kilichochangu na kutokomea kusikojulikana, hata nikawe kibarua nchi jirani. Hao lazima wamfunge, au wamwondoe duniani, ni swala la muda tu!!
Huyo mama ameshaonja hela, huyo mama ameshaonja heshima, huyo mama ameshaingia jikoni kwa "mchungaji"...sasa hii maana yake ni kuwa ameshaona "siri" na ni hiyo "siri" na wala si kumchukia mume wake, kinachomfanya asiwe na huruma kiasi hicho. Ngoma nzito hapa ni kuwa " je atoe siri au amtelekeze mume wake?" jibu hapa ni rahisi...atamtelekeza mume wake!
 
kweli watu tuna roho tofauti, hii ingekuwa kwa upande wangu lazima ninge geuka kubwa boko haram
 
Flola alikubali kuolewa na Mbasha akiwa hana kitu kwanini leo afanye hivyi kuna vitu ambavyo mumewe katenda sasa amefikia kusema mwisho/amechoka.Na imefikia hapo sababu Mbasha ni king'ang'anizi hataki kumuacha Flola sababu ya umarioo wake.
Mwanaume anayejielewa hawezi kulazimisha kuishi na mwanamke ambaye ni mzinzi, na kama alijua mchungaji anadhini na mkewe kwanini aliendelea kusali hapo? Mbasha anatafuta tu huruma kama ni unzinzi wote ni wanzinzi sema mwanamke kawa smart kamzidi ujanja.
Maana ktk mahojiano yote na waandishi sijasikia Mbasha akikana tuhuma za kutembea na hao mabinti/kubaka.

Maisha Mbasha aliyakosea mwenyewe kijana mzima badala ya kufanya kazi unakaa kuruka ruka jukwaani na mkeo. ndio matokeo yake hayo mwanamke anakuchoka anaona umekuwa mzigo anakulisha, kukuvisha na unalala kwa jasho lake.,akipata mwanaume wa kumtunza tu anakushiti. Hela ya mwanaume ina raha yake jamani

siamini kama Mbasha alibaka lakini naamini alikuwa na uhusiano na hao wasichana sasa mrs amechoka na vitendo vyake kaamua kumkomesha.

Umemaliza kila kitu hapo kwenye bold zavi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu The Bold, kwanza pole dana kwa yote!.
Kiukweli nimeguswa sana!, and I think I can help somewhere somehow!.

Kwa wenye mashaka, naomba niwathibitishie "this is bonafide genuine!".

Naomba kutoa usaidizi mfupi namna ya kuipambanua "bonafide genuine" from "fake"
Unaweza kuijua tuu kwa kuusikiliza moyo wako!, listen from your heart!.
Pasco.

Mkuu Pasco, huwa naipenda sana hii "this is bonafide genuine!"
 
Last edited by a moderator:
Nimefurahi kweli ulipomuita Gwajima MBWA..., hahahahahah...! pole bhana unajua yule mke wako nae tatizo anakua kama wale mbwa walio kwenye joto bhana..., aaaghhh..., pole bwana..
 
Mkuu The Bold, kwanza pole dana kwa yote!.
Kiukweli nimeguswa sana!, and I think I can help somewhere somehow!.

Kwa wenye mashaka, naomba niwathibitishie "this is bonafide genuine!".

Naomba kutoa usaidizi mfupi namna ya kuipambanua "bonafide genuine" from "fake"
Unaweza kuijua tuu kwa kuusikiliza moyo wako!, listen from your heart!.
Pasco.

Ningekuwa The bold ningekuwa macho sana na watu wanaojitolea kutoa msaada kama huu wa Pasco.
Ni Pasco huyu huyu alisema mkanda wa Lwakatare ni "Bonafide Genuine" na sasa hii habari ya The bold anaiona "Bonafide Genuine! Kwa kuwa huyu The Bold ameamua kupambana na huu unafiki wa hawa "maprophet", ajiandae kupata watu wengi "wa kumsaidia" lakini nyuma ya pazia wanammaliza. The Bold asifikiri anapambana na huyu "mchngaji" peke , la hasha, kuna "wachungaji" wengi amewaanika kwenye hii habari. Wapo Ngurumo , wapo Mzee wa Upako, wapo Ephata, wapo na yule mbunge wa viti maalumu aka Mama wa mlima wa moto....ni wengi mno. Kwa hiyo The bold , pambana hii vita bila kutegemea mteremko, umegusa watu hatari sana , tena sana. Yaani umegusa System. Mbaya zaidi, kuna hao waumini wao ambao wako tayari kufa wakiwatete, bila kujali kashfa yoyote ile. Kumbuka hata wewe The bold, ulikuwa unajua uchafu wa "mchungaji wako, lakini kwa kuwa na wewe ni mchafu mwenziwe, na wote mlikuwa mnafaidi kwa namna mke wako alivyokuwa anapiga cash za ajabu ajabu, ukaamua kunyamaza ili uendelee kufaidi. Sasa timing imekuwa mbaya, mama kakuwahi kabla ya mipango yako, ndo manataka kutona roho sasa. ANd unfortunately, The bold uko on a losing side!!! So jitahadhari na misaada ya kina Pasco weye!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu The Bold inafaa sasa uelewe utendaji kazi Bwn Mungu!!
Mungu anakutaka wewe Imma umtumikie!!
Wewe binafsi Mungu anakutaka, wacha jazba na hasira,
Angalia masaibu yako kwa jicho la kiroho, umefunuliwa haya ili ujue unaishi na watu wa aina gani!!
Mtumishi achana na vita ya kimwili rudi kiroho, unyanyasike uteswe ili Bwn Yesu akupe direction ya maisha yako!!
Mrudie Bwn wacha mihemuko na lugha za vitisho ili Bwn akupiganie jinsi ajuvyo yeye!!
Mpe Bwn nafasi akupiganie, shuka kwake kiroho kwa maombi akupe Amani ya moyo utulie!!
Ubarikiwe!!
 
Pamoja na hayoo ni mmewe amezaa nae hautakiwi kulipiza kisasii na basi kama umechoka muachane tu kwa amani sio kivitaa, na huwez shindana na mwanaume, kwa hili frola ni mkosajiii hakuwah kumtembelea kule jela hata tu kutuma ndugu zake kama ye hatakii bado hujaona frola ana matatizoo, mwanaume ni mwanaume tu
My dear,yes mwanaume ni mwanaume tu,kumbuka mwanamke nae ni mwanamke,Nadhani ni ngumu sana kwenda kumtembelea mtu alietembea na mdogo wake.Ingekuwa katembea na mtu baki labda angeenda,Mimi pia mwanzoni nilikwa namlaumu sana Flora,lakini kwa sasa nimejaribu kufikiria,na baada ya kuona video ya Mbasha anavyoomba msamaha,nimejua kuwa Flora alichoka,labda anahitaji muda.Any way Mungu awasaidie warudiane.
 
My dear,yes mwanaume ni mwanaume tu,kumbuka mwanamke nae ni mwanamke,Nadhani ni ngumu sana kwenda kumtembelea mtu alietembea na mdogo wake.Ingekuwa katembea na mtu baki labda angeenda,Mimi pia mwanzoni nilikwa namlaumu sana Flora,lakini kwa sasa nimejaribu kufikiria,na baada ya kuona video ya Mbasha anavyoomba msamaha,nimejua kuwa Flora alichoka,labda anahitaji muda.Any way Mungu awasaidie warudiane.
Kwa hiyo ukimchoka mwanaume, unaamua kumfunga kabisa?
 
tatizo kubwa hapa ni watoto, watapata picha gani? Hii ni fedheha sana kubwa kwa familia na kanisa kwa ujumla wake, Emma piga moyo konde uanze maisha mapya, flora achana nae, hata akirudi hakutakua na maelewano kama zamani.
 
Back
Top Bottom