Wakuu nimefuatilia hii mambo, bado najiuliza maswali kadha wa kadha!!
1. Thebold ambae ni Mbasha au mtu aliekaribu na Mbasha, pamoja na mambo mengine anatuhum Gwajima kujihusisha na sembe, pesa chafu, usanii kwenye hiyo ministry yake nk.
Kama ndivyo mbona utetezi wa hizi tuhuma haupewi uzito unaostahili??
2. Msemaji wa huduma aliejitambulisha kwa jina la injinia Bihagize alikuja humu kujibu hoja zinazoelekezwa kwenye ministry yao, cha ajabu hakuna alichofanya zaid ya kukimbia uzi alionzisha mwenyewe baada ya kuzidiwa hoja,,, najiuliza kwa nn hakutolea ufafanuzi wa kina uhusika au kutokuhusika kwa gwajima kwenye hili sakata??
3. Baadhi ya memba wanaotetea Gwajima mfano davidm, huyu ndugu ilifika mahala akaliambia jamvi kuwa thebold ndo mbasha mwenyewe, na akadai huyu thebold hawezi endelea kuandika coz yote alioandika awali ni uongo, yet Thebold amerudi na safari hii amekuja kivingine, najiuliza kwa nn davidm na wenzie hawataki, au kwa namna yeyote ile kubeza thebold na kumuita muongo, mbakaji, nk,,
Kwa nn wamechagua kuegemea upande mmoja????
4. Tangu mwanzo wa hii scandal thebold amekuja na hoja nzito kiasi kwamba ukisoma unapata shida kuamini kuwa ni cooked story,,, sasa kama ndivyo kwa nn thebold hakuchukua hatua mapema??? Au ndo aliamua kufa na tai shingoni,,!!
5. Najaribu kupata taswira nzima ya makanisa haya ya kiroho juu ya nini kinachofanyika nyuma ya pazia; mathalani, kwa kipindi chooote mbasha na mkewe walijua nini kinachofanyika huko kwenye huduma yao,, kwa gwajima,, mambo ya ufufuzi wa misukule feki, dawa za kulevya nk, jiulize kwa nn hawakusema hili???
Na endapo hiz tuhuma za ubakaji zisingekuwepo ina maana mbasha angeendelea kukaa kimya? Iweje Leo atuhum gwajima kwa dawa za kulevya, uzinzi, na usanii ilihali amekuwa akitambua hayo toka awali?
6. Mengi yameandikwa kuhusu umario wa mbasha,, yawezekana kweli alikosea kama ni kweli alikuwa Mario, itoshe kusema mbasha atake amani na frola basi. Hizi mambo za kutaka kurudiana na mwanamke ambae ameonesha kila dalili za kukukataa afu ww bado unakomaa sio mpango kbs...
Kuna mahali kwenye hili tamko thebold amekiri kumkosea frola lkn pia frola nae kwa nyakati tofauti amemkosea mbasha,,maana yake wamekuwa wakikoseana,,, sasa iweje thebold utake kulazimisha suluhu kwa mtu ambae hataki yan yeye aone makosa yako makubwa kuliko yake???
Kama nilivyosema cha msingi omba amani na maelewano kati yenu tu,, usilazimishe kutaka kurudiana nae hiyo ni weakness na wanamme hatuko hivyo, be strong!!
7. Thebold achana na hii style ya kuvizia vizia na kusoma upepo unaendaje kwangu mm naona sio, ukiamua jambo fanya uamuzi mgum, inaonekana unatikisika na kila hatua anayochukua frola, hapa katikati ulikuwa mafichoni baada ya kutikiswa na frola umetoka mafichoni,,, kwa nn usiakae kimya au kutoa tamko la kueleweka kuliko kufuata upepo?
8. Na kwa nini bado unakuja na story nusu nusu, Mkuu just one big blow inatosha,,,, achana na hizi mambo nusu nusu!!!
Na mwisho niseme Mungu aonaye sirini atahukum kwa haki na awape amani ya kweli mioyoni mwenu,,!!!
Ova!!