The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Lesson: tolerance of other people's views and beliefs ain't that easy...so, mnapolaani na nyie mjitazame ni kwa kiasi mnaweza kuvumilia beliefs tofauti na za kwenu. Haya sasa tunaanza kutishana kisa tumetofautiana kwenye JF. For me, the point is made.
 
1. Hivi tunaweza kupata Hoja hizo 11 za Zitto na hayo majibu ya Karamagi? Sikupata nafasi kuona TV- nina habari tu za magazeti.
2. Kama Zitto alitoa tuhuma na Kamaraj akazijibu kuwa serikali haikufanya kosa- kama Zitto hakuwa na ushahidi wa kutosha- basi hakukuwa na haja na kuunda tume. Si wabunge wengi tu wa CCM na upinzani wanatuhumu mengi wakiwa bungeni? tutaunda tume ngapi?
3. Kumfungia Zitto hadi Jan. Bunge has gone too far! Haikuwa na haja- mimi nadhani majibu ya Karamaj yalikuwa yanatosha.
4. Zitto na CHADEMA wasikate tamaa- wajipange tu upya- na kuwa na ushahidi tosha wakati wakitoa tuhuma- na kujiandaa vyema kujitetea hoja!
 
Lesson: tolerance of other people's views and beliefs ain't that easy...so, mnapolaani na nyie mjitazame ni kwa kiasi mnaweza kuvumilia beliefs tofauti na za kwenu. Haya sasa tunaanza kutishana kisa tumetofautiana kwenye JF. For me, the point is made.


Unatumia wingi kwa kumaanisha kuwa....

Ama kweli the same muongo.... umeanza kuishiwa na kudai kuwa unatishiwa...

Naona unatumia the same defense uliyotumia wakati wa skendo yako ya wizi wa mitihani kuwa adui zako ndio waliiweka kwenye mikoba yako ya shule...

tiht thit htitttt ti iiiii
 
Comimg to the issue of not doing research. Hivi ni mbunge gani anayeweza kusimama kifua mbele kujinadi kuwa yeye anafanya research zaidi ya ZITTO KABWE. Zitto sio mbunge kasuku kama tuliowazoea. Kama kuna kitu kinachompa nguvu kifikira ni hili la kujisomea na kufanya research. Actually researching ndio hobby yake kubwa zaidi ya siasa.

Wajanjawajanja ndio wanapenda kutumia neno la research kupunguza uhalali wa hoja makini wakati wao ndio mabingwa wa kutoa hoja za kikasuku.

Ni ajabu kwa wabunge waliokimbilia kudai kuwa KARAMAGI hajadanganya kuhusu maslahi ya taifa katika mkataba wakati hata huo mkataba wenyewe hawajauona. Halafu wana guts za kumhukumu Zitto kuwa hajafanya research.

Nina wasiwasi hii yote ya kumsimamisha Zitto ubunge inaweza ikawa mbinu ya maadui wa MTANDAO ndani ya CCM kusabotage legitimacy ya JK kwa wananchi. Kama wamefanya hilo kwa mpango maalum ama bahati mbaya lakini ni wazi wamefanikisha hilo. Wametumia mbinu ya kuua ndege wawili Zitto na JK kwa jiwe moja.

Sijui nini kitakachofuata dhidi ya Zitto lakini ni wazi kwa JK wameshafanikiwa.

Tanzanianjema
 
1. Hivi tunaweza kupata Hoja hizo 11 za Zitto na hayo majibu ya Karamagi? Sikupata nafasi kuona TV- nina habari tu za magazeti.
2. Kama Zitto alitoa tuhuma na Kamaraj akazijibu kuwa serikali haikufanya kosa- kama Zitto hakuwa na ushahidi wa kutosha- basi hakukuwa na haja na kuunda tume. Si wabunge wengi tu wa CCM na upinzani wanatuhumu mengi wakiwa bungeni? tutaunda tume ngapi?
3. Kumfungia Zitto hadi Jan. Bunge has gone too far! Haikuwa na haja- mimi nadhani majibu ya Karamaj yalikuwa yanatosha.
4. Zitto na CHADEMA wasikate tamaa- wajipange tu upya- na kuwa na ushahidi tosha wakati wakitoa tuhuma- na kujiandaa vyema kujitetea hoja!

Mimi ninazo hard copies tu. I am organising electronic versions, and should have them in the next 24 hours, tupate nafasi ya kuchambua pumba za Zitto Kabwe na mchele wa Karamagi. Kwi kwi kwi!
 
Mwafrika wa kike mwambie huyo dada::,kama ameshindwa kukubali ukweli wa zitto kwa kufukuza sababu wako wengi,,basi na sisi hatukubali upuuzi kwenye blog wadau tumpigie kura huyu tafadhali
pili,,wewe mgongo mgongo kwa kweli nina wasiwasi sana na elimu yako,,majibu kama haya wanajibu wasioenda shule ndio maan nakupa muda utaona,,,huyu bwana atakaa hapo kwenye hiyo wizara,,haya ndio matatizo ya kupeana vyeo kisa kulindana,,
 
Mwafrika wa kike mwambie huyo dada::,kama ameshindwa kukubali ukweli wa zitto kwa kufukuza sababu wako wengi,,basi na sisi hatukubali upuuzi kwenye blog wadau tumpigie kura huyu tafadhali
pili,,wewe mgongo mgongo kwa kweli nina wasiwasi sana na elimu yako,,majibu kama haya wanajibu wasioenda shule ndio maan nakupa muda utaona,,,huyu bwana atakaa hapo kwenye hiyo wizara,,haya ndio matatizo ya kupeana vyeo kisa kulindana,,

Elimu ya muongo kama inavyoonekana kwenye karatasi ni nzuri na wala sio kidogo.... issue kubwa kwake ni skendo ya wizi wa mitihani ambayo alisaidiwa na kigogo fulani kuifunika...

Sidhani kuwa ni idea nzuri kum-vote out. Mwache awepo ili nipate sababu moja zaidi ya kuchangia mijadala hapa
 
mzalendo halisi nadhani utapata kwenye gazeti la majira la leo ,,tatizo tunaloliongolea hpa jamani ni "uongo wa bwana zitto""sasa kama hoja ilikuwa ni ya uongo iweje nikimnukuu karamagi"nilisaini mkataba wa B***** kwasababu ya maslahi ya taifa,,jamani uo uongo mnaosema nyie ni upi,,pili huyo bwana
anataka turudushe swala la mitihani uku,,kuweza kumowonyesha upumbavu wake,,??
 
zittoaadhibiwa.jpg

Kigoma North legislator Zitto Kabwe makes a submission in the National Assembly in Dodoma yesterday. (Photo: Moshy Kiyungi)
 
Asalamu alaykum.

Kwanza nampongeza kwa dhati kijana mdogo kama yeye ambaye amejiamini katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kupeleka hoja nzito kama ile kwa hilo anastahili pongezi.

la pili Zitto kwa mujibu wa hoja yake alikuwa alikuwa anahoji namna ya mkataba uliosainiwa nje ya nchi na akaeleza alitoeleza ambayo sina haja ya kuyataja hapa kwa vile wengi tumesikiliza mjadala wa bunge mimi mimi nilikaa mpaka umemalizika maana Star TV walirekodi kwa hivyo niliangalia usiku mkubwa.

Cha msingi Zitto alitaka kuundwe tume kuchunguza suala hilo kwa hivyo Bunge lilikuwa liridhie kuundwa kwa tume then hapo atajulikana mkweli na muongo lakini kutaka Zitto afungiwe mwaka mzima na kwanza ukweli hautopatikana na hilo linawafanya wengine nikiwemo mimi kuona hapa lazima kuna udanganyifu wa mikataba na kuna ubadhirifu wa wazi wazi na pia kufungiwa Zitto ni kuzorotesha demokrasi nchini na kuwafanya wabunge wengine waogope kuhoji mambo mazito ya serikali.

kitendo alichofanyiwa Zitto Kambwe nhakina tofauti yoyote na alichofanyiwa Abass Juma Mhunzi, Mwakilishi wa Chambani Pemba ambaye pia ni waziri kivuli wa fedha na uchumi zanzibar aliwahi kuhoji kampuni ya mafuta ya GAPCO na akasema biashara ya mafuta ni ya vigogo wa ikulu na bei zake hupangwa ikulu pia na mengi mengineyo jambo ambalo alitaka kuungwe tume ya baraza la wawakilishi kufanya uchunguzi lakini Spika wa baraza hilo Pandu Ameir Kificho ambaye ni mjumbe wa (NEC)kutokana na ukereketwa aliwasikiliza wajumeb wa CCM waliotaka aombe radhi baraza naye alikataa kuomba radhi kwa madai kwamba shutuma alizotoa zina ukweli na alikuja na vithibitisho vyake vyote lakini Spika aliziba mashikio na akakataa asiwasilishe na alimuamuru akae chini.

hatimae alipewa adhabu ya mwaka mmoja katika kikao cha bajeti hadi kikao changine cha bajeti lakini Mwakilishi huyo hakuishia hapo alikwenda mahakamani na alishinda kesi yake akatakiwa arudi barazani na alipwe posho zake zote lakini kama mnavyojua SMZ imepindua na baraza la lake ikawa inazorotesha zorotesha mpaka ilipofika kikaoc ha bejeti cha pili ndio akaingia barazani.

sisi wananchi tunaowakilishwa tulimuona Mwakilishi wa Chambani kama ni mtu shujaa aliyejitolea kwa hali na mali kutetea wananchi wake na wazanzibari kwa ujumla na pia Zitto Kabwe tunamhesabu ni kijana jasiri, hodari asiyetetereka na ameandika historia ya tanzania kwamba haitaki kukosolewa wala kukubali kosa lake.

Tunahitaji wabunge na wawakilishi kama Zitto na Mhunzi ili watuwakilishe katika vikao kwa kutetea maslahi ya wanyonge na hatutaki kuwakilishwa na watu wenye kupiga makofi na kuunga mkono kila linalosemwa na serikali.

stonetowner
 
Hivi pale mwisho Zitto alipopewa nafasi ya kujitetea kipi kilikuwa bora? Kama alivyofanya au angetumia nafasi hiyo kurusha madongo zaidi?

Sijui ipi ni strategy nzuri, ila wakali wengi ninaowajua mimi, wangetumia hiyo nafasi kurusha madongo ya nguvu. Lakini wakati mwingine unaweza kumuumbua mbaya wako kwa kukubali adhabu isiyo halali with humility. "It was pride that changed angels into devils; it is humility that makes men as angels." - St. Augustine
 
ndugu yangu stone town nnaikumbuka kesi hiyo, iliihusisha kupokonywa leseni ECOTEC na kupewa GAPCO, hali ambayo ilisababisha kupanda na kutokuwepo vituoni. hali ambayo haijawahi kutokea kwa ECOTEC.

ila nnalumbuka iliundwa kamati na Mh Shamhuna alikuwa mwenyekiti wa kufuatilia, kwa kabwe hata kamati haijaundwa.

sasa si wazo baya kumshauri Mr kabwe akimbilie mahakamani.

ila kesi hizi mbili tofauti, kule Mzee Muhunzi hakukurupuka tu, na alitinga na data za kikweli kweli kiasi ambacho kuupinda ukweli ilikuwa shughuli na ikabidi bwana mashurubu kutumia sharabu zake kumuadhibu lkn mahakama ikashindwa maana hoja zinasema. ila huyu Kabwe mkurukupaji hana lolote.

ndugu yangu stone town kuwa muelewa
 
Wananchi wamlilia Kabwe, wadai haki haikutendeka

*Wakosoa jibu la Waziri kuondoa shutuma
*Wanasiasa wasema Zitto ameibuka shujaa

*Mwenyewe asema hatakubali, atakata rufaa


Na Waandishi Wetu

SIKU moja tu baada ya kukabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kuhuduria vikao vya Bunge kwa takribani miezi mitano, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) amejizolea umaarufu mkubwa na baadhi ya wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaifa wamemchukulia kama shujaa kutokana na msimamo wake.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wananchi mbalimbali, mmoja mmoja, taasisi na vyama vya siasa, wameelezea kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa dhidi ya mbunge huyo na kusema hatua hiyo haikuwa ya haki na inakandamiza uhuru na demokrasia Tanzania.

Profesa Mwesiga Baregu, mhadhiri mwandamizi wa masuala ya siasa na ushirikiano wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema uamuzi wa Bunge kumsimamisha Kabwe kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge haujamtendea haki.

Akizungumza na Mwananchi, ofisini kwake jana, Profesa Baregu alisema kwa kitendo hicho, Bunge halikumtendea haki Kabwe, halikutenda haki kwa demokrasia na pia halikutenda haki kwa wananchi.

Alisema kumwadhibu mbunge huyo hakujaweza kuondoa ukweli kwamba kuna mikataba mibovu inayoingiwa na serikali na suala la Buzwagi ni mfano tu kati ya mikataba mingi mibovu iliyoingiwa, hasa ya madini.

?Wabunge wengi wanaonyesha kuwa hawana utashi wa kulinda maslahi ya wananchi na ndiyo maana wakakataa kuunda kamati kujadili suala lile muhimu,? alisema Profesa Baregu.

Alisema kuzimwa kwa jambo lile bungeni si dawa na wala kumuadhibu Kabwe kwa kuonyesha uzalendo wake hakusaidii kuliziba tatizo bali kilichofanyika ni kudhihirisha tu kwamba Bunge limetumika kuisigina demokrasia.

Profesa Baregu alisema kimsingi maswali ya Kabwe hayajajibiwa kwani jibu la kuwa kulikuwa na ulazima wa kuharakisha mkataba si jibu lenye mantiki.

Naye Dk Mohamed Bakari wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema alichofanya Kabwe ni kutoa shutuma na njia muafaka ni anayeshutumiwa kutoa hoja mbadala na kuonyesha kwamba shutuma zilizotolewa si za kweli.

Alisema hilo ni jambo la kawaida hata katika uvumbuzi wa kisayansi, kinachoanza ni kuwa na wasiwasi na kitu, dhana ndiyo huzaa ukweli, sasa hakukuwa na ubaya wowote kuiacha dhana kujadiliwa ili hatimaye ukweli upatikane.

?Jibu la Waziri peke yake halijatosha kuondoa shutuma na kwa kweli kilichotendeka ni sawa na kuwazuia watu kusema. Kitendo kilichotendwa dhidi ya Kabwe ni cha aibu kwa Spika na hata kwa Bunge,? alisema Dk Bakari.

Umoja wa vyama vya upinzani mkoa wa Arusha, umempongeza Kabwe kwa kutoa hoja binafsi ya kutaka kuundwa kamati ya kuchunguza kusainiwa mkataba wa mradi wa madini ya Buzwagi wilayani Kahama na umemkaribisha mkoani Arusha kuzungumza na wananchi.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amepinga hatua iliyochukuliwa na Bunge kumsimamisha Kabwe na kudai kuwa adhabu hiyo ni ya ukandamizaji wa demokrasia nchini.

Mbatia alisema pia kuwa hiyo ni picha halisi kuwa Bunge chini ya Spika Samwel Sitta, limekuwa ni la kuwaburuza wapinzani na pia kumlaumu Spika kwa kuruhusu kuingiza mjadala wa kiitikadi katika Bunge, suala ambalo alisema si sahihi.

"Zitto Kabwe ni shujaa, ninavyomjua mimi si mropokaji hata siku moja, lakini amedhihirisha pia ushujaa kwa kusimamia lile analoliamini mpaka dakika ya mwisho, adhabu aliyopewa haikufuata kanuni na misingi ya haki za binadamu kujitetea, ni maonevu ambayo yameweka kovu lisilofutika kwa makundi ya demokrasia," alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila pia ameungana na wenzake akisema Zitto hana kosa, adhabu aliyopewa ni uharamia wa demokrasia na suala ambalo kila Mtanzania anatakiwa kulitambua na kutotakubali kukaa kimya.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutokea Mwanza, Mchungaji Mtikila alisema tayari ameshazungumza na mwanasheria wake aliyeko Dar es Salaam ambaye anaandaa kusudio la kupinga adhabu hiyo ili kulifikisha Mahakama Kuu mapema iwezekanavyo.

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Wilaya ya Arusha, Calist Lazaro, alisema licha ya kumwalika Kabwe kwenda Arusha kuzungumza na wananchi, juu ya hoja hiyo na watamuandalia mapokezi makubwa. ?Tayari tunajipanga kumpokea aje Arusha kwani wabunge wa CCM hawajamvua ubunge, sisi tutaendelea kumpa heshma yake.?

Kwa upande wa Asasi za kiraia zimesema utaratibu uliotumika kumwadhibu Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ni batili kwa maelezo kuwa haukufuata maadili wala kanuni za Bunge.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa taasisi hizo jana, Wakili wa Kujitegemea, Tundu Lissu, alisema adhabu iliyotolewa kwa Kabwe sio halali, huku akitaka mbunge huyo aruhusiwe kuendelea na vikao vyote vya Bunge.

Lissu alisema ni bora Bunge likaeleza mbunge huyo amepewa adhabu ya ngapi ili wananchi walinganishe na kufahamu adhabu ambayo ilikuwa inastahili kulingana na kosa, kama analo.

Naye Gema Akilimali wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), alisema Bunge sasa limegeuka kuwa serikali na siyo mhimili wa tatu wa serikali kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

?Spika aueleze umma, je Bunge lipo au halipo kwani, linatetea serikali badala ya wananchi hii ni ajabu!? alisema Akilimali.

Pia alipendekeza Bunge lielewe kuwa adhabu ya Zitto ni dhidi ya wananchi wa Kigoma Kaskazini kwani, kutokuwa na mwakilishi katika vikao viwili vya bunge ni hasara kubwa kwao.

Mbali na mahojiano na makundi hayo ya wanazuoni na viongozi wa kisiasa, wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, wametuma barua pepe na wengine kupiga simu chumba cha habari, wote wakilaani kusimamishwa kwa Mbunge huyo.

Wakati huo huo Kabwe ametangaza azma ya kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga adhabu ya kusimamishwa kujishughulisha na shughuli zote za Bunge hadi Januari mwakani kwa madai kwamba ameonewa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Zitto alisema anawasiliana na mwanasheria wa chama chake, Tundu Lissu, pamoja na wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuiomba mahakama uwezekano wa kuipitia upya hukumu aliyopewa na Bunge.

Alisema adhabu aliyopewa ni ya uonevu kwa kuwa kanuni ya Bunge namba 59 iliyotumiwa kumpa adhabu hiyo, haihusiani na masuala ya adhabu, badala yake ilipindishwa makusudi ili kumkomoa.

Zitto alisema kanuni hiyo inahusu masuala ya amani na usalama bungeni tofauti na ilivyotumiwa na Bunge kumuadhibu.

"Walipindisha kanuni kunikomoa, wameshindwa kuthibitisha uongo wangu, najua nafsi zao zimejuta kwa sababu nimeibua uozo unaofanywa. Nitashtaki pia kwa wananchi, waamue la kufanya," alisema Zitto.

Alisema adhabu hiyo pia haikutokana na Spika bali na Bunge, kinyume na kanuni za Bunge.

Hata hivyo, Zitto alisema pamoja na adhabu aliyopewa, moyo wake ni mweupe kwa kuwa ametimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuhakikisha analinda raslimali za nchi.

"Nimefanya kazi ambayo Mbunge anatakiwa kuifanya. Wengi walikuwa hawajui kama kuna mkataba uliosainiwa kimya kimya na serikali London. Hata wabunge walioshinikiza niadhibiwe pia walikuwa hawajui hilo," alisema Zitto.


Source: Mwananchi Agosti 16, 2007
 
Huo ndio unafiki wa Wana-CHADEMA ninaousema. Wanalaani Zitto kufungiwa Bungeni, wakati huo huo wanataka watu wengine nao wafungiwe kutoa mawazo yao kisa tu hayafanani na ya kwao. Your true colours ndio zinajionyesha mnapozidiwa hoja.

Kwa nini mugongo afungiwe? Uwepo wake hapa una umuhimu wa kinamna...comedian kama Mr Bean....kiharage.
 
Hiyo makala ya mwananchi inaleta utam!

Hapo CCM walidhani wamemmaliza Zitto kumbe wamejimaliza wenyewe
kwikwi kwi.. Kama ni kupanda Chati wamemtoa 40 wakamfikisha 99%

Walidhani Zitto kakurupuka wakapanga mkakati wammalize kumbe wao ndo wamekurupuka kujimaliza kwa mikakati yao ya U CCM!
Na Bado...
 
nyie wana ilongo nafikirimnaitaji sana msaada wa roho mtakatifu,,maana najua hamjui mnachoongea ama hamjui kilichotekea
tuelewesheni hoja halisi iliyomuondoa mh ZITTO ni nini na sikitika muda si mrefu anakwenda kuwaitwa kizitto kwa hoja ya kumsimamisha,,,kuweni na uadilifu kujibu hoja
 
1.) Hili swala ni kubwa kuliko jinsi tunavyoliona hapa. Ukiangalia kwa undani utaona serikali ya JK wanatumia ujanja (upumbavu) kuficha mikataba kwa wabunge na hivyo unapohoji hiyo mikataba wanaweza kukwambia chochote wanachopenda na huwezi kutetea hoja wakati hujauona huo mkataba.

2.) Sheria na kanuni za bunge zimepitwa na wakati na ni lazima zichambuliwe upya ili kukidhi mahitaji ya sasa. (Huwezi kumfukuza mbunge ambaye hukumchagua na wawakilishi wake wanakosa uwakilishi kwa jambo ambalo sio kosa lao).

3.) Zito amesimamishwa kwa kanuni ipi? Nimeangalia lakini sijaona hicho kifungu ambacho wamekitumia. Kwa mwenye taarifa naomba aweke hapa.

Mwanakijiji

Shukran kwa kuweka PDF.
 
Ccm Acheni Mambo Ya "'nani Kashika Mpini"" Yamepitwa Na Wakati Hivi Sasa Bwana Jakaya Embu Tuonyeshe Uko Serius Na Maisha Ya Watanzania,,nilijua Ben Pekee Mwenye Kucheza Na Maisha Yetu Kumbe Nyie Mmeamua Kutupiga Mchanga Wa Macho Mpaka Wakina Mgongomgongo Wanaandika Pumba Badala Ya Mchele Wenye Kulika
Zitto Baba Tuko Nyuma Yako Tunakusubiri Dar,,tuanataka Watu Wenye Kujitoa Na Kujua Umuhimu Wa Wananchi Kama Wewe, Si Washenzi Kama Mgongomgongo Na Inviscible,,leo Hii Watu Kama Hawa Tukiwapa Madaraka Wanaweza Kutusaini Mkataba Wa Kuuza Ikulu Hata Wakiwa Chooni Cha Ikulu Yenyewe,,
 
Back
Top Bottom