Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
And, how does an opposition "rainball" meeting take place? Help me out.
its rainbow.....macho na vidole vimekosa ushirikiano..i mean its typing error...vipi umeona hilo tu??....yule mbunge wenu eng stella aliwashauri vizuri sana pale alipotoa mfano wa biblia"..pakiwamo wenye haki 9 katika mji wenu nitawasamehe kwa ajili yao..yesu akashuka hadi akauliza kama kuna mwenye haki hata mmoja tu ili aunusuru mji wa sodoma na gomora..." eng stella alimalizia akasema pamoja na mabaya yote ya hoja za zitto kwa ccm "hawaoni hata hija moja ya muhimu??? ili wamsamehe kutokana na hiyo hoja moja nzuri.....wabunge wenzake wa ccm walim boow..hii ina maana wenzako wengi pale bungeni waliona sense kwenye hoja za zitto na kimsingi wanakubali kuwa zinahitaji kufanyiwa kazi..tatizo lipo kwa waitikiaji wa JSM Kama wewe.....
Mida hii, chama cha mhe. Zitto (CHADEMA) kinamfanyia pati ya pongezi..
carl rove .....ameondoka baada ya shutuma nyingi za ushauri aliompa mkubwa wake...na pia ameangalia kwa kina future yake ukizingatia bosi wake kengele ya kuondoka inakaribia ..
Si kaondoka baada ya kushinda safari zote kuanzia Ugavana mpaka urais? Kungelikuwa na kugombea mara nyingine kwa boss wake, asingeondoka.
Look, huongei na kina Mnyika hapa. Kuandika "rainball" badala ya "rainbow" sio vidole kuteleza kama unavyodai. Ni kwamba hukuwa unajua a correct spelling ya "rainbow" kwahiyo ukaandika kama inavyotamkwa. Watu wakisema mnaandikiwa makala mnawaona wanaleta fitina...ushahidi gani tena unatakiwa zaidi ya huu! Reminds me of Dan Quayle! Kwi kwi kwi. I have to tell my husband this when I get home!
And who said ujasiri ni kukiri udhaifu?
Hapa ndipo vyama vya upinzani Tanzania vinapochemsha, party ya nini? Huu ndio muda wa Zitto sio kuzungukwa na viongozi wa CHADEMA bali kuwatembelea wananchi wa kawaida na kupeana nao mikono (Clinton style). Inatakiwa Zitto atumie nafasi hii kukutana na wananchi wengi kadri iwezekanavyo.
Hayo ndio mambo yalimponza Mrema. Kura ziko kwa wananchi tena vijijini, haya mambo ya party ni ulaji tu usio na maana.
Nendeni mkamwone Carl Rove awasaidie namna ya kupata ushindi.
Ndio tatizo la kukurupuka. Siku Zitto alipomtuhumu Karamagi na kuahidi kuleta hoja binafsi...ndio akawa amejifunga kitanzi. Baada ya kutoa hoja ndio akaanza research...iliyo-lead kwenye ukweli kwamba alikurupuka...kuna wakati alikwishaamua asiwasilishe hoja hiyo baada ya kukosa data. Lakini kwakuwa aliahidi kwa mbwembwe hakukuwa na njia zaidi ya kuwasilisha hoja dhaifu....baada ya Karamagi kujibu, ikaonekana kwamba huyu Mheshimiwa aliongopa na wenzake sasa ndio wanamtwanga kwa hoja ya kusimamishwa Ubunge kwa kusema uongo. Hata hivyo, mimi nadhani ni hoja ya kipuuzi ya kutaka asimamishwe Ubunge. Mimi nadhani wamuache aumbuke na uongo wake manake hii ni tabia yake ya kusema uongo kutafuta umaarufu.
kama mtikila amesema anafungua kesi mahakama kuu kupinga adhabu ya zitto....i think it is strategically right..CHADEMA wamuunge mtikila mkono..kwani inapendeza kama kesi hiyo inafunguliwa na mtanzania yoyote aliyeona haki haikutendeka.........utakuwa mtihani wa kwanza kwa augustino ramadhan..ili tujue na yeye muhimili wake umeshatekwa kama ule wa sitta au la..
Ha ha ha! You have been provoked, sio? And you want to take it outside. Hoja hujibiwa kwa hoja, si ndio msemo wenu?
Acheni kujidanganya...Mtikila sio mtu wa kumwamini hata chembe...
Ushauri Zitto atulie tu atumie muda huo kujijenga jimboni.[/B] Na hivi vipati na hao wanasiasa matumbo waliomzunguka ni kupoteza muda tu aende akale bushpati na wapiga kura wake jimboni.
ZITTO ondoka mjini hakuna wa kumwamini huko. Umesahau mambo ya wanafunzi wa mlimani ukishalimwa suspension wanavyokuaga wanafiki?
Tanzanianjema
Ccm Acheni Mambo Ya "'nani Kashika Mpini"" Yamepitwa Na Wakati Hivi Sasa Bwana Jakaya Embu Tuonyeshe Uko Serius Na Maisha Ya Watanzania,,nilijua Ben Pekee Mwenye Kucheza Na Maisha Yetu Kumbe Nyie Mmeamua Kutupiga Mchanga Wa Macho Mpaka Wakina Mgongomgongo Wanaandika Pumba Badala Ya Mchele Wenye Kulika
Zitto Baba Tuko Nyuma Yako Tunakusubiri Dar,,tuanataka Watu Wenye Kujitoa Na Kujua Umuhimu Wa Wananchi Kama Wewe, Si Washenzi Kama Mgongomgongo Na Inviscible,,leo Hii Watu Kama Hawa Tukiwapa Madaraka Wanaweza Kutusaini Mkataba Wa Kuuza Ikulu Hata Wakiwa Chooni Cha Ikulu Yenyewe,,
hapa nakuunga mkono,
nenda katulie ujipange usome makosa yako, wala usikurupuke tena. tatizo lako mkurupukaji na kiromo romo sasa siasa ni ujanja hadaa, tectiki na mengineyo, maadam umeingia kwenye siasa unatakiwa uwe makini. na ushauri huu ni kwa wote walioingia na wanaotegemewa kuingia kwenye siasa.
kijana ulitegwa na hukuiona mitego ukaingia kichwa kichwa kwa hio leo umelala lkn usikate tamaa kubali hili umeteleza acha misifa jipange kimya kimya.
Hivi wabunge wanaweza kumsimamisha mbunge aliyechaguliwa na wananchi kwa sababu ya Hoja yake?... I mean hao wananchi wa Kigoma leo hii wanawakilishwa na nani - on his behalf! Je, ndio kusema jimbo la Kabwe limesimamisha Uraia wake hadi hapo January?.Mzee Mkandara, heshima yako na pole sana na hiki kisanga!
Binafsi, nitaandika makala kuhusu haki za Zitto na ikiwezekana niombe ichapishwe na gazeti lolote. Hata hivyo, ni vigumu sana kumtetea Zitto kwasababu dhamiri zetu zinatusuta. Mzee Mkandara, swali lako jibu ni hapana. Hili Bunge halina haki ya kumsimamisha Mbunge aliyechaguliwa na wananchi. Lingekuwa Bunge ambalo wabunge wote wamechaguliwa na wananchi, jibu lake lingekuwa ndiyo wanaweza.
Jamani, hili Bunge sio halali, kikatiba na kiutendaji, hivyo maamuzi yote yanayofanywa na hili Bunge sio halali. Utangulizi wa katiba ya nchi yetu umeweka msingi kwamba tunajenga jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, undugu na amani. Katiba inaendelea kusema kuwa misingi hiyo itasimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi. Hili Bunge lina wabunge ambao hawakuchaguliwa na wananchi hivyo hawawakilishi wananchi.
Leo hii tunajiuliza kwamba inakuwaje Bunge la namna hii limsimamishe Mbunge aliyechaguliwa na wananchi? Lakini tumewahi kujiuliza kwamba inakuwaje katiba ya nchi yetu inatoa mamlaka kwa vyama vya siasa kumfuta kabisa Mbunge aliyechaguliwa na wananchi? Yaani kamati kuu ya CCM ikimfukuzuza uanachama Mbunge yeyote, basi na Ubunge wake unakoma palepale. CHADEMA ikimfukuza uanachama Mbunge yeyote, basi na Ubunge wake unakoma papo kwa papo bila kujali amechaguliwa na wananchi au la. Haya yote yako kwenye maandishi na wabunge walichokifanya ni kuweka mojawapo kwenye matendo.
Leo hii tunaweza kuhoji uhalali wa Bunge kumfukuza mbunge bila kuhoji uhalali wa vyama vya siasa kumfukuza Mbunge? Yote tisa, kumi ni je, haki ya Mbunge inaweza kutenganishwa na haki ya wananchi? Jibu ni hapana. Je haki ya mwananchi inaweza kutenganishwa na haki ya Mbunge? Jibu ni ndiyo kwasababu viraka katika Katiba yetu vimeweka masharti katika haki ya mtu kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa wananchi. Nyerere alituasa kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukisha kuitenda hautakoma.
Ndiyo maana ni vigumu sana kumtetea Zitto kwasababu yuko ndani ya Bunge linalowanyanganya watu haki zao kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa. Ubaguzi kumbe haukukoma kwa wananchi ambao sio wanasiasa bali umeanza kuwatafuna wanasiasa wenyewe ambao wako ndani ya Bunge. Wengine wanasema kuwa leo ni siku ya giza kwa taifa letu kwasababu Zitto amenyanganywa haki yake. Well, binafsi nadhani siku ya giza ilikuwa pale Bunge lilipo wanyanganya wananchi haki yao ya kuwawakilisha wenzao. Leo ni matokeo ya ile siku.
Sasa Zitto afanye nini? aende kwa wananchi katika jimbo lake? Atawambia nini? Aseme tuungane kudai haki yangu niliyopokonywa na Bunge? Akitoka mtu akamuuliza swali kuwa unasemaje kuhusu haki zetu ambazo hazikusimamishwa kwa muda bali zilifutwa kabisa ndani ya katiba na Bunge hilohilo ambalo wewe ni mjumbe, atasema nini? Je haki ya Mbunge ni bora kuliko haki za wananchi?
Tutafika mahala tutambue kuwa hakuna kitu kinaitwa maslahi ya taifa, hakuna kitu kinaitwa mgombea binafsi, hakuna kitu kinaitwa Mbunge, hakuna kitu kinaitwa nchi. Kuna kitu kinaitwa watu ambao wana haki zao za msingi walizozaliwa nazo. Hizi haki wamepewa na Mungu hivyo hakuna kiumbe yeyote mwenye haki ya kuzifuta. Watu ndio wanaunda Bunge, nchi, Taifa, n.k. Unapofuta haki za watu unakuwa umefuta maslahi yao ambayo ndio maslahi ya Bunge, nchi, na taifa. Huwezi kutenganisha maslahi ya watu na maslahi ya taifa.
Kwa mara nyingine, natoa wito kwa wabunge wenye nia njema kujiuzulu ubunge wao ili tuungane na wananchi kudai haki zetu ambazo zitaandikwa ndani ya katiba mpya. Juhudi zote za kulitoa Bunge mikononi mwa wanasiasa na kulirudisha mikononi mwa wananchi lazima ziungwe mkono na zisichukuliwe kiushabiki.