The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

And, how does an opposition "rainball" meeting take place? Help me out.

ukiona mwanamke mzima au mtu mzima kama wewe na heshima zote unaanza kushadadia typing errors as if its an agenda...you know she is almost reduced to ashes..you better feel sorry for our fellow country men even if you are within vigogos who feed from our blood sweat ...u never know one day your offsprings will be beggers wakati huo migodi itakuwa imebaki mashimo..si unajua watoto wa wanaoachiwaga mali ya haramu wanavyotawanya mapema...
 
its rainbow.....macho na vidole vimekosa ushirikiano..i mean its typing error...vipi umeona hilo tu??....yule mbunge wenu eng stella aliwashauri vizuri sana pale alipotoa mfano wa biblia"..pakiwamo wenye haki 9 katika mji wenu nitawasamehe kwa ajili yao..yesu akashuka hadi akauliza kama kuna mwenye haki hata mmoja tu ili aunusuru mji wa sodoma na gomora..." eng stella alimalizia akasema pamoja na mabaya yote ya hoja za zitto kwa ccm "hawaoni hata hija moja ya muhimu??? ili wamsamehe kutokana na hiyo hoja moja nzuri.....wabunge wenzake wa ccm walim boow..hii ina maana wenzako wengi pale bungeni waliona sense kwenye hoja za zitto na kimsingi wanakubali kuwa zinahitaji kufanyiwa kazi..tatizo lipo kwa waitikiaji wa JSM Kama wewe.....

Look, huongei na kina Mnyika hapa. Kuandika "rainball" badala ya "rainbow" sio vidole kuteleza kama unavyodai. Ni kwamba hukuwa unajua a correct spelling ya "rainbow" kwahiyo ukaandika kama inavyotamkwa. Watu wakisema mnaandikiwa makala mnawaona wanaleta fitina...ushahidi gani tena unatakiwa zaidi ya huu! Reminds me of Dan Quayle! Kwi kwi kwi. I have to tell my husband this when I get home!

And who said ujasiri ni kukiri udhaifu?
 
Mida hii, chama cha mhe. Zitto (CHADEMA) kinamfanyia pati ya pongezi..

Hapa ndipo vyama vya upinzani Tanzania vinapochemsha, party ya nini? Huu ndio muda wa Zitto sio kuzungukwa na viongozi wa CHADEMA bali kuwatembelea wananchi wa kawaida na kupeana nao mikono (Clinton style). Inatakiwa Zitto atumie nafasi hii kukutana na wananchi wengi kadri iwezekanavyo.

Hayo ndio mambo yalimponza Mrema. Kura ziko kwa wananchi tena vijijini, haya mambo ya party ni ulaji tu usio na maana.

Nendeni mkamwone Carl Rove awasaidie namna ya kupata ushindi.
 
carl rove .....ameondoka baada ya shutuma nyingi za ushauri aliompa mkubwa wake...na pia ameangalia kwa kina future yake ukizingatia bosi wake kengele ya kuondoka inakaribia ..
 
carl rove .....ameondoka baada ya shutuma nyingi za ushauri aliompa mkubwa wake...na pia ameangalia kwa kina future yake ukizingatia bosi wake kengele ya kuondoka inakaribia ..

Si kaondoka baada ya kushinda safari zote kuanzia Ugavana mpaka urais? Kungelikuwa na kugombea mara nyingine kwa boss wake, asingeondoka.
 
Si kaondoka baada ya kushinda safari zote kuanzia Ugavana mpaka urais? Kungelikuwa na kugombea mara nyingine kwa boss wake, asingeondoka.

huyu jamaa kama mshauri au "the brain"..ni mtaalamu wa strategies..anajua wapi na lini aingie na wapi atoke..inavyoonekana na analysts wengi ni kuwa yeye pia ana ambitions za kugombea political post in next four years ..so asingependa kuporomoka kwa rating ya bush kunakohusishwa na ushauri wake kuje kumuharibie badaye..inaonekana ameshahisi mwisho mbaya kabisa ..bush is likely to become the least popular president[in terms of public ratings] when he steps down from office..kwenye corridor za oval office staffs watakuwa wanasemezana""huyu dudu washa anaondoka lini???

au pia usikute anaenda kujipanga kwa ajuli ya kumleta jeb bush ..[ikiwa republican watapoteza ..jeb anataka kugombea 2012]..si unajua familia ya bush wanavyopenda kushea washauri..wengi walio kwa bush jr pia wali save under bush sr...
 
Look, huongei na kina Mnyika hapa. Kuandika "rainball" badala ya "rainbow" sio vidole kuteleza kama unavyodai. Ni kwamba hukuwa unajua a correct spelling ya "rainbow" kwahiyo ukaandika kama inavyotamkwa. Watu wakisema mnaandikiwa makala mnawaona wanaleta fitina...ushahidi gani tena unatakiwa zaidi ya huu! Reminds me of Dan Quayle! Kwi kwi kwi. I have to tell my husband this when I get home!

And who said ujasiri ni kukiri udhaifu?

Mnyika anahusiana vipi na michael....
wewe nawe huchoki kuongelea watu kwa kila postings zako
inaonekana kazi ya u-groupie huko CCM itakushinda sasa na unawataka kuwa groupie wa vyama vyote viwili!
 
Hapa ndipo vyama vya upinzani Tanzania vinapochemsha, party ya nini? Huu ndio muda wa Zitto sio kuzungukwa na viongozi wa CHADEMA bali kuwatembelea wananchi wa kawaida na kupeana nao mikono (Clinton style). Inatakiwa Zitto atumie nafasi hii kukutana na wananchi wengi kadri iwezekanavyo.

Hayo ndio mambo yalimponza Mrema. Kura ziko kwa wananchi tena vijijini, haya mambo ya party ni ulaji tu usio na maana.

Nendeni mkamwone Carl Rove awasaidie namna ya kupata ushindi.

Kila kitu kina wakati wake ila pia nakiri kuwa ushauri wako ni mzuri zaidi. Hata hivyo kumbuka kuwa politics haina formula na hivyo chochote chaweza kutokea na kufanywa anytime.

Suala la Zito ni la kitaifa na kimataifa. Serikali ya Tz iko Dar au Dodoma. Kwa sasa Zito anahitaji media exposure ya kutosha ili kumake his case. Akienda Kigoma media itamtosa na kum-maginalize.

Kuhusu Carl Rove..... kuna mengi zaidi ya Carl Rove na Bush ambayo wengi hawajui hivyo ni bora wapinzani wasipoteze muda wao kwa this guy
 
Mzee Mpaka Kieleweke, heshima yako!

Shukurani kwa kutupeperushia hoja kamili ya Mzee Zitto Kabwe aliyoiwasilisha Bungeni. Binafsi imeniwia vigumu kuchangia huu mjadala kwasababu nimeshindwa kupata hoja ya Waziri Karamagi iliyoipiku hoja ya Zitto na kumfanya Zitto aonekane amejenga hoja ya uongo. Ombi langu kwako au kwa mdau yeyote mwenye hoja kamili ya Waziri Karamagi aipeperushe hapa JF ili zote mbili zitendewe haki ya kupitishwa kwenye darubini.

Nakiri hata kabla ya kusoma hoja kamili ya Waziri Karamagi kuwa itakuwa vigumu kupingana na baadhi ya vipengere katika majibu ya Waziri kwasababu mazingira yenyewe ya mikataba ni ya usiri mkubwa. Huwezi kuwa na ushahidi wa mambo yanayofanyika sirini. Hata hivyo, mambo yanayofanyika sirini sio tatizo sana kwa watu wenye akili timamu, kwani waswahili walisema “njia ya mwongo ni fupi”.

Mfano, ngoja ninukuu gazeti la Majira kuhusu mojawapo ya majibu ya Waziri kwa hoja ya Zitto. “Aidha, Karamagi alisema si kweli kama anavyodai Bw. Zitto kwamba kazi ya kudurusu mikataba ya madini nchini bado inaendelea. Alisema udurusu wa mikataba umekamilika na vipengere kadhaa vimeboreshwa katika mikataba ya zamani kwa ajili ya maslahi ya Taifa.”

Lakini tarehe 1 August 2007, Rais Kikwete akihojiwa na Bw. Shaka Ssali wa Voice of America's (VOA) Straight Talk Africa program,alisema kuwa suala la udurusu wa mikataba bado halijakamilika kwa makampuni ya uchimbaji wa madini nchini kwetu. Alisema Serikali ilifanikiwa kuishawishi kampuni moja tu ya Barrick Gold kufuta kipengere kinachotoa mwanya kwa makampuni ya uchimbaji madini nchini kulipa corporate tax kwa increment kwa jinsi makampuni yanavyopenda (Refer to http://www.voanews.com/english/Afric...TalkAfrica.cfm).

Waziri Karamagi katika hoja yake anasema alisaini huo mkataba February 2007. Tafsiri yangu ya hoja ya Zitto ni kuwa wakati Waziri Karamagi anasaini huu mkataba February 2007, zoezi la kudurusu mikataba ya madini lilikuwa bado linaendelea. Akimjibu Zitto, Waziri Karamagi analiambia Bunge kuwa zoezi la kudurusu mikataba ya zamani ya madini limekamilika, ingawa hakuna maelezo yanayoonyesha tarehe ya kukamilika kwa zoezi lenyewe. Hata hivyo, Rais wa taifa ambalo maslahi yake yako mezani Mheshimiwa Kikwete ameiambia VOA siku 14 zilizopita kuwa zoezi la kudurusu mikataba halijakamilika. Katika suala la kudurusu mikataba ya madini, maelezo ya Zitto yanafanana na maelezo ya Rais Kikwete. Kama hivi ndivyo, nani anasema uongo?

Mtafaruku wa Zitto na Bunge unazidi kuibua maswali mengi yasiyo na majibu. Ahaa! No wonder! Nilishangaa kwanini Rais Kikwete aliiambia VOA kwamba Serikali imeshawishi kampuni moja tu ya Barrick Gold kufuta kipengere cha kulipa corporate tax kwa increment. Na akaongeza kuwa baada ya miaka mitatu au minne, ndipo hiyo kampuni itaanza kulipa corporate tax.

Kumbuka Barrick Gold ilikuwa inamalizia muda wake wa “tax holiday arrangements” kutokana na sheria ya uwekezaji “act No. 26 of 1997” ambayo inatoa muda wa miaka mitano kwa mwekezaji kurudisha gharama za uwekezaji kabla ya kuanza kulipa kodi. Muda huo kwa Barrick ulikuwa umeyoyoma. Hivyo walitakiwa waanze kulipa 30% corporate tax lakini kwa increment na kwa jinsi wanavyoona wao na wanavyopata faida. Rais Kikwete ameiambia VOA kuwa kipengere hicho kimefutwa na Barrick gold wataanza kulipa 30% Corporate tax baada ya miaka mitatu au minne.

Mantiki hii ina maana kwamba Barrick Gold has 3 to 4 more years of paying no tax at all. Anyway, tuleteeni majibu ya Waziri ili tujadili vizuri.
 
Ndio tatizo la kukurupuka. Siku Zitto alipomtuhumu Karamagi na kuahidi kuleta hoja binafsi...ndio akawa amejifunga kitanzi. Baada ya kutoa hoja ndio akaanza research...iliyo-lead kwenye ukweli kwamba alikurupuka...kuna wakati alikwishaamua asiwasilishe hoja hiyo baada ya kukosa data. Lakini kwakuwa aliahidi kwa mbwembwe hakukuwa na njia zaidi ya kuwasilisha hoja dhaifu....baada ya Karamagi kujibu, ikaonekana kwamba huyu Mheshimiwa aliongopa na wenzake sasa ndio wanamtwanga kwa hoja ya kusimamishwa Ubunge kwa kusema uongo. Hata hivyo, mimi nadhani ni hoja ya kipuuzi ya kutaka asimamishwe Ubunge. Mimi nadhani wamuache aumbuke na uongo wake manake hii ni tabia yake ya kusema uongo kutafuta umaarufu.

Wewe unaonekana umepandikizwa na CCM na hauitakii mema Tanzania maana unatetea hata ambapo hakuna cha kutetea au utalaumu hata pale ambapo hakuna cha kulaumu. Hivi kweli huoni kasoro chungu nzima ndani ya siri kali na CCM ambazo zinaiangamiza Tanzania!? Hivi huoni mali ya Tanzania (rasilimali) inachukuliwa bila Watanzania kufaidika chochote!? Wewe una cheo ngani ndani ya CCM kinachokufanya ufumbie macho rushwa na dhuluma nyingi tu dhidi ya Watanzania!? Umeona juzi kulikuwa na article inayoonyesha tunapoteza madaktari wetu kwa kulipwa ujira mdogo hilo pia hulioni!? Hebu fungua macho nawe mkweli kwa nafsi yako ili uone maovu yanayofanyika ndani ya nchi yetu na wahusika wakuu wakiachwa bila kufanya lolote! Fungua macho kaka acha kuyafumbia maovu ndani ya Tanzania
 
kama mtikila amesema anafungua kesi mahakama kuu kupinga adhabu ya zitto....i think it is strategically right..CHADEMA wamuunge mtikila mkono..kwani inapendeza kama kesi hiyo inafunguliwa na mtanzania yoyote aliyeona haki haikutendeka.........utakuwa mtihani wa kwanza kwa augustino ramadhan..ili tujue na yeye muhimili wake umeshatekwa kama ule wa sitta au la..

Acheni kujidanganya...Mtikila sio mtu wa kumwamini hata chembe...

Ushauri Zitto atulie tu atumie muda huo kujijenga jimboni. Na hivi vipati na hao wanasiasa matumbo waliomzunguka ni kupoteza muda tu aende akale bushpati na wapiga kura wake jimboni.

ZITTO ondoka mjini hakuna wa kumwamini huko. Umesahau mambo ya wanafunzi wa mlimani ukishalimwa suspension wanavyokuaga wanafiki?

Tanzanianjema
 
Ha ha ha! You have been provoked, sio? And you want to take it outside. Hoja hujibiwa kwa hoja, si ndio msemo wenu?

Na hii ndio hoja....kwa faida yako bado una miaka mingi ya kuwa machoni mwa wanaosulubiwa na madhila unayoyafanyia kejeli..


MUONGOMUONGO HAUNA MAWAZO TOFAUTI. TATIZO LAKO UNAKEJELI UTU WA WATANZANIA. NAKUHAKIKISHIA KAMA UNAONA NI MCHEZO HUU VERY SOON UTAJUTIA HAYA UNAYOYAFANYA HAPA. USIDHANI KUWA YATAISHIA HUMU KWENYE FORUM TU. WENGI WALIKUWEPO KAMA WEWE NA WENGI WATAKUJA LAKINI KUMBUKA TANZANIA HAITAKUWA HII HII AMBAYO UNAJIONA UPO KATIKA TIMU YA USHINDI. LAKINI VILEVILE LEO KIJANA KESHO MTU MZIMA NA MTONDOGOO UTAKUWA MZEE. KAULI ZAKO HAPA HAZITAFUTIKA KATIKA HISTORIA.

Tanzanianjema
 
Ndugu zangu wanaJF
Kitu kimoja ni lazima mjue kuwa sasa hivi tuna serikali ya ovyo. Pamoja na kwamba mkapa mwishoni wa uongozi wake alitufanya sisi wajinga, lakini uongozi wake ulikuwa ni much much better than uliopo sasa. Member mmoja amesema vizuri alikotoka Mudhihir na kufika alipo sasa. Huyo Kamaragi sijui kama ndio yeye alikuwa huko Bandari Tanscan au wapi, lakini kilichomuingiza madarakani hakitofautiani sana na Mudhihir. Hii ndio Tanzania ya sasa, no hope. Yeye Kamaragi anasema "BUZWAGI NI KAMGODI KADOGO KWA HIYO HAKUPASWA KUSUBIRI UTARATIBU MPYA" sasa hii na aliyosema Zitto tofauti iko wapi? Zitto amedanganya nini? Sasa hata bunge limekuwa bunge la usanii!! WHERE ARE SPEED AND STANDARDS
 
Acheni kujidanganya...Mtikila sio mtu wa kumwamini hata chembe...

Ushauri Zitto atulie tu atumie muda huo kujijenga jimboni.[/B] Na hivi vipati na hao wanasiasa matumbo waliomzunguka ni kupoteza muda tu aende akale bushpati na wapiga kura wake jimboni.
ZITTO ondoka mjini hakuna wa kumwamini huko. Umesahau mambo ya wanafunzi wa mlimani ukishalimwa suspension wanavyokuaga wanafiki?

Tanzanianjema


hapa nakuunga mkono,

unapoanguka simama kama mnazi
ulipochnika tia dawa kwa ujuzi
simama kijana wetu uchape kazi

nenda katulie ujipange usome makosa yako, wala usikurupuke tena. tatizo lako mkurupukaji na kiromo romo sasa siasa ni ujanja hadaa, tectiki na mengineyo, maadam umeingia kwenye siasa unatakiwa uwe makini. na ushauri huu ni kwa wote walioingia na wanaotegemewa kuingia kwenye siasa.

kijana ulitegwa na hukuiona mitego ukaingia kichwa kichwa kwa hio leo umelala lkn usikate tamaa kubali hili umeteleza acha misifa jipange kimya kimya.

na pia nnakwambia watu wa pwani husema "kubwa lijalo"[/B]"kunyamza si kushindwa ni werevu wa kutosha"
 
Ccm Acheni Mambo Ya "'nani Kashika Mpini"" Yamepitwa Na Wakati Hivi Sasa Bwana Jakaya Embu Tuonyeshe Uko Serius Na Maisha Ya Watanzania,,nilijua Ben Pekee Mwenye Kucheza Na Maisha Yetu Kumbe Nyie Mmeamua Kutupiga Mchanga Wa Macho Mpaka Wakina Mgongomgongo Wanaandika Pumba Badala Ya Mchele Wenye Kulika
Zitto Baba Tuko Nyuma Yako Tunakusubiri Dar,,tuanataka Watu Wenye Kujitoa Na Kujua Umuhimu Wa Wananchi Kama Wewe, Si Washenzi Kama Mgongomgongo Na Inviscible,,leo Hii Watu Kama Hawa Tukiwapa Madaraka Wanaweza Kutusaini Mkataba Wa Kuuza Ikulu Hata Wakiwa Chooni Cha Ikulu Yenyewe,,

zitto watu hawa wenye kupenda kukaa nyuma yako waogope, si wema, machoni kama watu nyoyoni hawana kitu, imani imetoweka...
 
hapa nakuunga mkono,

nenda katulie ujipange usome makosa yako, wala usikurupuke tena. tatizo lako mkurupukaji na kiromo romo sasa siasa ni ujanja hadaa, tectiki na mengineyo, maadam umeingia kwenye siasa unatakiwa uwe makini. na ushauri huu ni kwa wote walioingia na wanaotegemewa kuingia kwenye siasa.

kijana ulitegwa na hukuiona mitego ukaingia kichwa kichwa kwa hio leo umelala lkn usikate tamaa kubali hili umeteleza acha misifa jipange kimya kimya.


Yakhe mie napenda kutofautina na weye..

Aliyetegwa na kutegeka hapa ni CCM na haswa wale waliojifanya kutoka vifua mbele kuhalalisha kuwa maslahi ya taifa yamezingatiwa wakati popular sentiments zimeshaamua kuwa wanaibiwa madini yao. Kumfungia ndio wamejifunga bao la kisigino.

Jitahidi kuepuka hizi propaganda za kizamani za kutumia maneno kama kukurupuka ama kutofanya reserach. Zitto hakukurupuka. Alijua anachokifanya na amefanikiwa.


Tanzanianjema
 
Mzee Mpaka kieleweke heshima mbele,

Tumeshapitia hoja ya Zitto, tuwekee hoja/majibu ya Karamagi tupate kuchambua pumba na mchele.........
 
Ogah,
Sure na vilevile tumechoka na personal attacks humu. Wekeni hoja mliyoombwa!

Mgongo ulihaidi lete vitu.

FD
 
Je Kuna Mtu ana Nakala ya Mkataba ambao Bwana Mkubwa Karamagi amepiga Sahihi yake huku London maana wengi tunashindwa kuelewa licha ya kwamba tunajua kwa kusikia sasa tutataka Ushahidi maana najua JF chimba chimba wa ukweli na Haki. Leteni nasi tupate Ushuhuda.
 
Hivi wabunge wanaweza kumsimamisha mbunge aliyechaguliwa na wananchi kwa sababu ya Hoja yake?... I mean hao wananchi wa Kigoma leo hii wanawakilishwa na nani - on his behalf! Je, ndio kusema jimbo la Kabwe limesimamisha Uraia wake hadi hapo January?.
Mzee Mkandara, heshima yako na pole sana na hiki kisanga!

Binafsi, nitaandika makala kuhusu haki za Zitto na ikiwezekana niombe ichapishwe na gazeti lolote. Hata hivyo, ni vigumu sana kumtetea Zitto kwasababu dhamiri zetu zinatusuta. Mzee Mkandara, swali lako jibu ni hapana. Hili Bunge halina haki ya kumsimamisha Mbunge aliyechaguliwa na wananchi. Lingekuwa Bunge ambalo wabunge wote wamechaguliwa na wananchi, jibu lake lingekuwa ndiyo wanaweza.

Jamani, hili Bunge sio halali, kikatiba na kiutendaji, hivyo maamuzi yote yanayofanywa na hili Bunge sio halali. Utangulizi wa katiba ya nchi yetu umeweka msingi kwamba tunajenga jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, undugu na amani. Katiba inaendelea kusema kuwa misingi hiyo itasimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi. Hili Bunge lina wabunge ambao hawakuchaguliwa na wananchi hivyo hawawakilishi wananchi.

Leo hii tunajiuliza kwamba inakuwaje Bunge la namna hii limsimamishe Mbunge aliyechaguliwa na wananchi? Lakini tumewahi kujiuliza kwamba inakuwaje katiba ya nchi yetu inatoa mamlaka kwa vyama vya siasa kumfuta kabisa Mbunge aliyechaguliwa na wananchi? Yaani kamati kuu ya CCM ikimfukuzuza uanachama Mbunge yeyote, basi na Ubunge wake unakoma palepale. CHADEMA ikimfukuza uanachama Mbunge yeyote, basi na Ubunge wake unakoma papo kwa papo bila kujali amechaguliwa na wananchi au la. Haya yote yako kwenye maandishi na wabunge walichokifanya ni kuweka mojawapo kwenye matendo.

Leo hii tunaweza kuhoji uhalali wa Bunge kumfukuza mbunge bila kuhoji uhalali wa vyama vya siasa kumfukuza Mbunge? Yote tisa, kumi ni je, haki ya Mbunge inaweza kutenganishwa na haki ya wananchi? Jibu ni hapana. Je haki ya mwananchi inaweza kutenganishwa na haki ya Mbunge? Jibu ni ndiyo kwasababu viraka katika Katiba yetu vimeweka masharti katika haki ya mtu kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa wananchi. Nyerere alituasa kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukisha kuitenda hautakoma.

Ndiyo maana ni vigumu sana kumtetea Zitto kwasababu yuko ndani ya Bunge linalowanyanganya watu haki zao kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa. Ubaguzi kumbe haukukoma kwa wananchi ambao sio wanasiasa bali umeanza kuwatafuna wanasiasa wenyewe ambao wako ndani ya Bunge. Wengine wanasema kuwa leo ni siku ya giza kwa taifa letu kwasababu Zitto amenyanganywa haki yake. Well, binafsi nadhani siku ya giza ilikuwa pale Bunge lilipo wanyanganya wananchi haki yao ya kuwawakilisha wenzao. Leo ni matokeo ya ile siku.

Sasa Zitto afanye nini? aende kwa wananchi katika jimbo lake? Atawambia nini? Aseme tuungane kudai haki yangu niliyopokonywa na Bunge? Akitoka mtu akamuuliza swali kuwa unasemaje kuhusu haki zetu ambazo hazikusimamishwa kwa muda bali zilifutwa kabisa ndani ya katiba na Bunge hilohilo ambalo wewe ni mjumbe, atasema nini? Je haki ya Mbunge ni bora kuliko haki za wananchi?

Tutafika mahala tutambue kuwa hakuna kitu kinaitwa maslahi ya taifa, hakuna kitu kinaitwa mgombea binafsi, hakuna kitu kinaitwa Mbunge, hakuna kitu kinaitwa nchi. Kuna kitu kinaitwa watu ambao wana haki zao za msingi walizozaliwa nazo. Hizi haki wamepewa na Mungu hivyo hakuna kiumbe yeyote mwenye haki ya kuzifuta. Watu ndio wanaunda Bunge, nchi, Taifa, n.k. Unapofuta haki za watu unakuwa umefuta maslahi yao ambayo ndio maslahi ya Bunge, nchi, na taifa. Huwezi kutenganisha maslahi ya watu na maslahi ya taifa.

Kwa mara nyingine, natoa wito kwa wabunge wenye nia njema kujiuzulu ubunge wao ili tuungane na wananchi kudai haki zetu ambazo zitaandikwa ndani ya katiba mpya. Juhudi zote za kulitoa Bunge mikononi mwa wanasiasa na kulirudisha mikononi mwa wananchi lazima ziungwe mkono na zisichukuliwe kiushabiki.
 
Back
Top Bottom