The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Ogah,

Not only Karamagi must go, but all economic looters (CCM) must go.
 
Namkubali kabwe kwa kukubali KUSULUBIWA kwa manufaa ya taifa. Angeitoa hoja yake bungeni leo tungekuwa na hadithi nyingine. Lakini kwa msimamo aliouonesha unapaswa kuigwa na sisi vijana. LAZIMA tulinde maliasili yetu isiwe ni kwa ajili ya manufaa ya wachache....

Nilishasema ktk reply zangu siku za nyuma kuwa huwa napata kizunguzungu pale ambapo wabunge wengi wanaunga mkono hoja asilimia mia kwa mia huku wakiikosoa hoja kwa kiwango cha juu. Huu ni unafiki wa kisiasa unaopaswa kupigwa vita na wapenda mabadiliko na mamendeleo.

Nikiwa kama Mtanzania mpiga Kura ninajutia na kujilaumu kwa kuipigia kura serikali hii. Nadhani ninahitaji ushauri nasaha kwa hilo na pia watanzania mjue kuwa wapinzani (kama mpendavyo kuwaita) ni watanzania wenzetu na ni jirani na ndugu zetu. Wanatetea maslahi ya Taifa.

Heko Kabwe, Heko Slaa, Heko CHADEMA.

KATIKA KUFUMA WAMETUFUMBUA MACHO,
KATIKA KUTAMBA TUMEWATAMBUA KWEUPEE...!
 
Wavutaji wa mashati hawakosi katika jamii. Mrema na Zitto hawalinganishwi kwa vigezo vyovyote vile. Tunachosema hapa ni kwamba times have changed baada ya "chaguo la Mungu" kuonekana mbabaishaji, mwizi (na amezungukwa na wezi) kama waliomtangulia. But cynics will always be there!


You said it all! Yaani watu waone kwa kuwa makosa yalifanyika huko nyuma basi haiwezekani kurekebisha hata pale watu wanapofanya jitihada. Jana nimehudhuria maandamano, nimenyeshewa na mvua kama walala hoi wengie. Walala hai tulikuwa tunahesabika; nilichojifunza ni kuwa bado walala hai (middle class) wanafikiri kwamba shida za nchi hii haziwahusu maadamu wao wanapata kula yao kama kawaida, wananunua escudo na wanaweza kujenga vijumba uchwara kule Tegeta. Lakini kwa jinsi ninavyoliona wimbi la mageuzi, walala hai lazima tutasombwa na mhemuka wa wananchi, mabadiliko yanakuja hata kama watu wemgine kwenye hii JF wanaonekana kwa cynical sana na kinachoendelea!
 
Hotuba ya Kabwe Zitto imeleta mengi mapya masikioni mwa Watanzania,Ambayo hatukuyasikia kwenye hotuba(Hoja) yake kule Dodoma Bungeni,Sio kwamba Mkataba ulisainiwa Hotelini na sio Ubalozini,bali pia Mkuu wa Kaya hakufahamishwa Ukweli kuhusu Mkataba huo.Pamoja na kwamba walikuwa pamoja ktk safari hiyo ya Uk na Japan.

Katika Hotuba yake kwenye sherehe ya Mei Mosi/2006,Jk alisema kwamba Utiaji saini mikataba yote ya madini umesimamishwa na serikali ya awamu ya NNE ili kutoa nafasi kwa Mabingwa wa mikataba kuipitia Upya kwani Mikataba iliyopita ina Utata,Alirudia maelezo hayo ya kusimamisha Utiaji saini Mikataba ya Madini huko Afrika kusini kwenye Seminar ya Madini.Sasa Mkataba huu uliotiwa Saini na Karamagi una utofauti na Mingine?

Kitendo cha Ndg Karamagi(Waziri mfanyabiashara)kutia saini Mkataba wa Uchimbaji Madini huko Kahama kinanipa wasiwasi kuwa kuna Mazingira ya Rushwa.Maelezo ya Zitto ni mwanzo tu wa ukweli mzima wa mambo.Na kama ni kweli Waziri alitia saini Mkataba huo bila Ufahamu wa Rais sioni kwanini Waziri asiwajibike!!

Inanikumbusha hii habari ya makundi ya wanamtandao ndani ya Chama, wakati Mheshimiwa amekalia tawi, huku chini mti unakatwa!!!
 
Mvua jana ilinyea sana, bahati mbaya sikuweza kumwona huyu Kitila Mkumbo. Sikutarajia maandamano yawe makubwa kiasi kile kwa namna vua lilivyodondoka tena kipindi ambaco si cha mvua hiki!

Hivi hii mvua ya jana ilitoka wapi? Au ndio waliitengeneza ili tusiweze kufanya tulichopanga? Si mchezo... Uzuri wafanyakazi wote hatukwenda makazini Jumamosi hiyo. Hii issue ya JK kutojua kinachoendelea siishangai kwakuwa mengi anazungukwa kama alivyoongea Kabwe hiyo jana. Anazungukwa kuliko anavyodhania... Ni mambo mengi yanaenda mrama!

Maisha mazuri kwa mtanzania HAYATOWEZEKANA KAMWE endapo JK hatabadili attitude! Anawaamini wasio waaminifu. Kazungukwa na wasanii nae anaonekana msanii pia. Watanzania bado wanampenda sana JK lakini kwa mwendo huu wa sheria kupindishwa na inflation ya namna hii basi mkuu JK ajue kakalia kuti kavu kabisaa.

Kipindi Mkapa anatoka madarakani mwaka mmoja unusu uliopita hali ilikuwa hivi:

Mkate wa boflo dukani uliuzwa Tshs 250/= na sasa JK within a short period hata miaka miwili bado mkate huohuo unauzwa Tshs 600/=

Mafuta ya petrol kipindi cha BM yalikuwa kati ya sh 800-900 (Super) lakini sasa ndani ya mwaka mmoja unusu lita moja ni Tshs 1500/=

Nyumba ya uswahilini kipindi cha Mkapa (2005/6) chumba kimoja chenye hadhi ya kawaida kilipangwa kwa sh. 10,000/= na sasa kwa JK chumba hichohicho kimefikia sh. 20,000/=

Kipindi cha BM nauli ya daladala jijini Dar na kwingineko ilikuwa Tshs 150/= na sasa kwa JK ndani ya mwaka mmoja unusu hivi tayari ni Tshs 350/=!

Ni mengi ambayo mwananchi wa chini anazidi kukabiliana nayo na akiisubiri ahadi ya 'Chaguo la Mungu' iweze kumfikisha Kanaani lakini anazidi kukatishwa tamaa. Soko huria limekuwa soko holela. Hakuna udhibiti tena. Hali ni mbaya kuliko maelezo. Viwango vya mishahara ndo hivyo vinapanda kwa sh 5,000 - 10,000/=. Jamani hali ni mbaya! Hata wale tuliokuwa na matumaini na mheshimiwa tunakata tamaa! Wizi unazidi, utapeli wa wazi toka kwa watumishi wa umma...

Amka JK!
 
leteni petition tusaign ili karamagi atoke ofisini...
 
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4554

That's damn right Yebo Yebo!

Ila kuna mambo JK anazungukwa mzee wangu. Utakuja ona soon what people are talking about. Ila hii ya Buzwagi kuna link kubwa zaidi ya hii ninayoona kwenye mitandao. Kuna watu ninaojua wazi kuwa wamo kwenye hiyo connection halafu hawajaandikwa humo na mimi mwenyewe nilikuwa Buzwagi majuzi ambako shughuli za ujenzi zinaendelea kwa kasi ya ajabu na kwa kiwango kizuri tu.
 
Hawa watu wa CCM ngoja waendelee kuwa na jeuri yao na kiburi."THE DAY IS COMING" watalala na kuamka na kujikuta wako nje.Tabia yao inawalazimisha na kuwapeleka Watanzania kwenye point of no return.Tusisahau kila kilicho na mwanzo kina mwisho.
 

Attachments

  • leo.jpg
    leo.jpg
    220.2 KB · Views: 51
I have fond memories of CHURCHILL HOTEL, LONDON
Kaazi kweleikweli..
Church Hill Hotel kama ni ile ya pale Marble Arch, hii ina Presidential Suit, ni kilometa chache mno kutoka Bond Street zilipo ofisi za Balozi yetu..ni less than 7 minutes walk! Lakini hoja kama hata mkuu wa Kaya hakuwa akifahamu utiaji wa saini pia inashangaza..kama kweli hoja yenyewe ina mashiko, JK katika msafara ule alikuwa pale Hotelini Chruch Hill na ndipo msafara wa Raisi ulipofikia.
logically, wajasiriamali wale wa Barick ndio waliomfuata Waziri pale Hotelini..hili la kama Raisi hakuwa akijuwa kama kuna mkataba unasainiwa inawia vigumu kuitetea SANA maana kama nilivyokariri mwanzo Raisi alikuwepo pale Hotelini.
Nilibahatika kuwepo kwenye viwanja vile vya Jangwani jana..tathmini yangu wananchi wana mwamko mkubwa na ni kweli wanafuatilia kwa karibu mwenendo na mustakbali wa nchi yao.
Kaazi kweli kweli,
Kingwele wa kingwele.
Kijijini Kwegole.
 
mwanzo wa mabadiliko unakaribia,
vijana nyuso zao zimekosa matumaini,
wanahitaji kuonyeshwa njia iliyo sahihi nao wako tayari kufuata.
tusiishie Dar peke yake
moto uliowashwa cheche zake zisambae nchi nzima.
Na hapo kutakuwa na nuru ya ushindi.
 
mwanzo wa mabadiliko unakaribia,
vijana nyuso zao zimekosa matumaini,
wanahitaji kuonyeshwa njia iliyo sahihi nao wako tayari kufuata.
tusiishie Dar peke yake
moto uliowashwa cheche zake zisambae nchi nzima.
Na hapo kutakuwa na nuru ya ushindi.


Huo ndio ungekuwa wakati muafaka wa kutumia ile Helkopta...
 

Huo ndio ungekuwa wakati muafaka wa kutumia ile Helkopta...

Yebo Yebo,

Dr. Sla ameipa serikali mpaka tarehe 15 September iwe tayari imeshashulikia mambo ya BOT.

Mbowe kasema kasema watazunguka na helikopta kuwaeleza wananchi kuhusu hilo swala la BOT na Zitto
 
Sasa kwa mbaaali naanza kumwona Karl Marx hapa Tz - 'State Dictatorship' in the form of Party Dictatorship
 
Daaamn. Yani Zitto ali-rise on HUMMER?


Mzee niliona hilo ila nikaona niuchune kwanza...sijui kama ni la chama au mtu binafsi lakini either way nilijiuliza; Hivi kuna watu wana visima vyao vya petrol/disel hapo Tanzania...!!!
 
Yebo Yebo,

Dr. Sla ameipa serikali mpaka tarehe 15 September iwe tayari imeshashulikia mambo ya BOT.

Mbowe kasema kasema watazunguka na helikopta kuwaeleza wananchi kuhusu hilo swala la BOT na Zitto


Good move..I hope hawatapoteza Momentum iliyopo...ningependa nisikie Zitto ameongea na wananchi waliompeleka Bungeni.
 
Yebo Yebo nakupa uhakika wa habari kwamba Zitto ataunguruma next week J5 huko Kigoma jimboni kwake . Kama hapatakuwa na Changes wale vijana wa Merereni walioamua kulipa mshahara wa ndugu Zitto watamuona Live J4 Mjini Arusha ambako atakuwa anawapa somo zito juu ya madini yao. Jana mimi na Lunyungu we bumped into each other na tukawa tumepoa tu na kula maneno mazito. Nilimuona pale Masanja na kundi lake na nadhani next week utasikia mambo on the Ze Comedy .Lakini kuna tetesi kwamba hata mawaziri wa CCM ukiachilia akina Malecela wanafurahi Zitto kusimamia hoja .Wale mawaziri wenye busara zao majina tunayo lakini si Buriani kwenye kiburi na ujinga mwingi .

Jana ilikuwa jana na Hongera sana Zitto endeleeni kukandamiza kwa ajili ya Tanzania yetu .
 
Back
Top Bottom