Onyo la Bunge lapondwa
2007-08-19 11:09:13
Na John Ngunge na Gaudensia Mngumi
Wahadhiri waandamizi wa sheria wameponda onyo lililotolewa na Bunge kwa wanaharakati kuwa linawatisha Watanzania na kuharatisha uhuru na demokrasia yao na wamesema Bunge halina mamlaka ya kunyamazisha wananchi.
Akitoa maoni yake jijini Dar es Salaam jana, Profesa Issa Shivji, alieleza kusikitishwa na onyo hilo na kwamba limemshangaza kama mwanasheria na kumtisha zaidi kama mwananchi hasa akitafakari hatma ya demokrasia na uhuru wa wananchi.
``Taarifa ya Bunge iliyosainiwa na Katibu Mkuu imenishangaza kidogo kama mwanasheria, lakini?imenitisha zaidi kama mwananchi, hasa nikitafakari hatma ya demokrasia na uhuru wa wananchi kutoa maoni yao na uhuru wa vyombo vya habari kutoa taarifa bila uoga au bila kujali taarifa hizi zinamhusu nani au chombo gani.
Haki zote hizo ni za msingi na zinalindwa? na Katiba ya Jamhuri na Katiba ya Serikali ya Zanzibar,`` alisema.
?Katibu wa Bunge, Bw. Damian Foka, juzi alitoa taarifa ya kuwaonya wanaharakati kuwa makini na matamshi yanayopotosha umma kuhusu uamuzi wa kumsimamisha Bw. Kabwe kufanya kazi za Bunge.
Alisema huko ni kukiuka sheria, madaraka, kinga na haki za Bunge ya mwaka 1988.
``Hivyo basi Bunge halitasita kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria hii,`` ilisema.
Alisema taarifa hiyo haigusii kabisa?jambo lililokuwa ndani ya hoja ya iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Bw. Zitto Kabwe, bali inazungumzia vifungu vya kanuni za Bunge na tafsiri zake katika jitihada?za kuhalalisha uamuzi wa Bunge/Spika wa kumsimamisha Bw. Kabwe na kupinga tafsiri ya ``wanaojiita wanaharakati.``
?Tuachilie mbali maneno haya ya kejeli, tubaki kwenye hoja za msingi,? alisisitiza.
?Alisema, ?kwa maoni yangu, suala la msingi?hapa ni kutofautisha kati ya uhalali wa kisiasa (political legitimacy)??na uhalali wa kisheria (legality) ya?uamuzi wa Bunge,? alisema.
Kuhusu sheria, Profesa Shivji aliongeza kuwa jambo linalobishaniwa ni tafsiri ya Kanuni za Bunge.
?Katika hiyo sitaki kusema mengi isipokuwa tujikumbushe?tu kwamba katika mfumo wetu kauli ya mwisho juu ya tafsiri ya sheria ni ya ?Mahakama na Mahakama peke yake. Kwa hiyo tafsiri inayotolewa na wanaharakati, au mawakili maarufu au hata Katibu Mkuu wa Bunge ni maoni tu,? alisema.
Alisema katika mjadala huo wananchi wana haki ya kutoa maoni yao na hakuna ye yote kati yao mwenye uwezo wa kudai kwamba maoni yake ni sahihi na sahihi tupu na ye yote akitofautiana naye anaupotosha umma na kwamba \'atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria hiyo.
?``Huwezi ukalazimisha maoni yako juu ya tafsiri?ya sheria kwa mabavu na vitisho. Ukifanya hivyo, maana yake ni huna nia ya kuendesha mjadala bali kusudio lako ni kufunga midomo ya wananchi.
Wahenga husema: usimuue mjumbe kwa sababu hupendi ujumbe wake,? alisema na kuongeza anavyoona jambo muhimu, ni suala la uhalali wa kisiasa.
``Unaweza ukawa na uhalali wa kisheria ni papo hapo ukakosa uhalali wa kisiasa. Jambo la mikataba ya madini - na mikataba mingine ya ubinafsishaji na inayohusu rasilimali za wananchi - limezungumziwa sana na wananchi katika mabaraza yao, vijiwe vyao na hata katika Bunge Tukufu na katika magazeti, kiasi kwamba Rais Kikwete mwenyewe alitamka wazi kwamba mikataba hiyo itaangaliwa,? alisema.
Profesa Shivji alifafanua kuwa Bw. Kabwe alipoleta hoja zake binafsi aligusia kwa karibu sana hisia za wananchi, na alikuwa anaweka wazi madukuduku ya wananchi kwa ujumla na walikuwa wanasubiri kwa hamu taarifa kuhusu ukweli wa mambo yaliyoko ndani ya mikataba hiyo.
Aliongeza kuwa badala ya kujadili na kukubali kufanya uchunguzi wa kina juu ya suala hili,?wawakilishi wetu na watumushi wa umma, wakaamua?kumziba mdomo Bw. Kabwe.
``Mara moja, ikaamsha, siyo hisia tu bali hasira za wananchi wa hali na hadhi tofauti.?Kwa mantiki hiyo, hoja za Bw. Kabwe zilikuwa na uhalali wa kisiasa kwa kiasi kikubwa, wakati?hatua za Bunge zikakosa uhalali huo.
Na uhalali wa kisiasa huwezi ukaulazimisha. Naam, unaweza ukafunga midomo ya watu kwa mabavu na vitisho lakini kamwe huwezi kuuwa hisia zao,? alisisitiza.?
Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi , amepuuza onyo hilo la kuwakataza wananchi kuzungumzia kusimamishwa kazi kwa mbunge huyo kwani halina mamlaka ya kunyamazisha watu.
?Bunge halina mamlaka ya kuingilia uhuru wa jamii kujadili hoja yoyote hata kama imejadiliwa ndani ya bunge na haijatolewa maamuzi, mamlaka ya kunyamazisha watu wasijadili kesi iliyo mahakamani ni ya mahakama pekee,? alisema.
Dk. Mvungi ambaye ni mhadhiri wa Kituo cha Sheria alisema hata mahakama yenyewe haina mamlaka ya kunyamazisha jamii isijadili kesi iliyokwishaamuliwa.
?Iweje Bunge liwanyamazishe wapiga kura kujadili suala la Bw. Zitto ambalo limekwishaamuliwa na Bunge,? alihoji.
Akikariri taarifa ya Bw. Foka iliyosema mbunge huyo alisimamishwa baada ya Bunge kuona kuwa uongo aliousema ni mkubwa na umeathiri heshima ya Bunge, Dk. Mvungi alisema, ?hajui anachozungumza, suala la Kabwe limekwishaamuliwa na Bunge na wananchi wanajadili uamuzi huo?hajui mamlaka ya Bunge na Bunge ni kitu gani.?
?Zama za kuburuzana zimekwisha, sasa kama hawaujui huu mchezo tutawafundisha unaovyochezwa, Bunge haliwezi kuburuzwa na kamati ya CCM,? aliongeza.
Dk. Mvungi ambaye ni mtaalamu wa sheria ya katiba, alisema Katibu wa Bunge ni mtumishi wa chombo hicho wakati Spika ni mtumishi na mwakilishi wa wapiga kura wake.
?Pia bosi wa Bunge ni wananchi-wapiga kura wenyewe, wewe ni mtumishi/mwakilishi wa wananchi bado hajui mamlaka ya Bunge na haelewi ni kitu gani,? alifafanua Dk.Mvungi.
Kuhusu kamati ya chama kiliburuza Bunge alifafanua kuwa wabunge wa CCM walikaa kama kamati na kuamua kumuadhibu Bw. Kabwe, waligeuza hoja ya kawaida ya Bunge kuwa suala la chama chao.
?Bunge lilikubali kuburuzwa na CCM, tena aliyehitimisha hoja ya chama ni Mbunge wa Mtera (CCM) , Bw. John Malecela, ?huu ni mwiba lazima uondoke,? alihoji, Kabwe kuitwa mwiba.
Aliendelea kueleza, ?nikitafakari mchango wa Malecela niliona kwamba hoja ya kumwadhibu ambayo inalindwa na Katiba iligeuzwa kuwa hoja ya chama na hivyo kumwadhibu Bw. Kabwe.
?Kwa mujibu wa kanuni za Bunge mbunge huyu hakutakiwa kuthibitisha kauli zake, mbunge aliona shaka akaliomba Bunge liunde tume ya kuchunguza, anayetakiwa kuthibitisha ni hiyo tume.?
Kuhusu heshima ya Bunge, alisema Bw. Kabwe analindwa na Katiba ya nchi hivyo hawezi kumtukana Waziri na hajalivunjia Bunge hadhi yo yote wala mtu ye yote, ametekeleza kile ambacho Katiba inamtaka kufanya.
?Hakuna lugha mbaya au nzuri inayoanishwa na kanuni au Katiba ila kiustaarabu huwezi kutumia maneno kama ******** au mshenzi lakini ukisema mathalani Waziri alichosema si kweli, au amedanganya Bunge ni kitu kile kile? alifafanua.
Mwanaharakati na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Hellen Kijo-Bisimba amesema Bunge kutoa matamshi kama hayo limekwenda mbali.
Alisema kama raia wana uhuru wa kujadili na wanajua wanachoongea.
?Tunapoongea hatuingilii uhuru wa Bunge, tunajua kwamba Bunge lina uhuru wake na hatuwezi kuingilia,? alisema.
Hata hivyo, Bi. Kijo-Bisimba alisema Bunge haliwezi kuwafunga mdomo wanaharakati.
Alisema wanaharakati wanao uelewa kuhusu kanuni na Katiba na hivyo katika mjadala huu hawalivunjii heshima Bunge na wala hawawezi kutoa matamshi yanayopotosha.
Alisema wanasubiri kuona Bunge litawashitaki kwa kutumia sheria ipi na kuthibitisha kile wanachoita kwamba wanaharakati wanatoa madai ya kupotosha umma.
?Msimamo wetu ni kwamba Bw. Kabwe aliwasilisha hoja yake Bungeni na hakutakiwa kuthibitisha isipokuwa Kamati ya Bunge ilitakiwa ilithibitishie Bunge, ndio maana sisi wanaharakati tunasema kwamba ameonewa.?
Mshauri wa masuala ya kiuchumi Bw. John Kimbute, alisema hatua ya Bunge ya kukemea wana harakati inadhihirisha namna serikali inavyojificha nyuma ya kivuli cha sheria inapoulizwa juu ya mambo yanayoonyesha kuwa na kasoro.
? Hivi karibuni imeingiza kipengele cha sheria ya 37 (1) kukataza kuhoji masuala yanayochunguzwa na Tume Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) . ?Hatua hiyo inalenga kuzima na kuzuia suala la rada kuendelea kuchunguzwa na vyombo vya habari.?
Kwa wa mbunge Kabwe, alisema kwanini mbunge anapohoji kanuni mahsusi ya mikataba muhimu kusainiwa nje ya nchi na kuonyesha kutokuridhishwa na maelezo kuwa ni mkataba huo una pesa na ajira nyingi, kundi la CCM Bungeni linaharakisha kuridhika na maelezo ya Waziri na kukimbilia kutoa adhabu kwa mbunge ili masuala kama hayo yasiulizwe bungeni.
?Matokeo yake ni kuwa mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk, Wilbrod Slaa, ameondoa suala la kupeleka hoja binfsi ya kuunda kamati ya kuchunguza ujenzi wa majengo pacha ya benki kuu ,?
``Wakweli hawahofu jambo, kukimbilia kwenye sheria na kutisha wananchi kila siku inapoonekana serikali imekosea, kunaonyesha serikali ina hofu mambo yake yasijulikane, hali hii inaondoa imani kwa umma na inaathiri mshikamano miongoni mwa wananchi.``
SOURCE: Nipashe
Tuma Maoni Yako