The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Kuna mtu hapa JF anayeweza kuelezea hii "..........15% additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expedicture,........" kwa lugha nyepesi kidogo what does it mean in real terms........ maana wananchi tunahitaji lugha nyepesi ati!!

Hii ni deduction ya tax burden kwa mlipa kodi; formula yake siifahamu, ila wakati wa kumpigia hesabu ya kodi yake, wanachukua tofauti ya matumizi na mapato ili kutafuta faida aliopata. Sasa katika hiyo faida wanapiga factor fulani kupunguza ukubwa wa faida kwa kuweka gharama za vitendea kazi alivyonunua kwa bei mbaya na gharama yake haiwezi kurudishwa kwa muda mfupi. Ile sheria ya kodi ya mwaka 1973 ilikuwa inamruhusu mlipa kodi kumwomba kamishna afikirie gharama alizoninga kununua vitendea kazi ambavyo gharama yake ni kubwa sana haiwezi kurudishwa kwa muda mfupi; kwa hiyo kamishina alikuwa na uhuru wa kuamua afidie gharama hizo kwa kiasi gani. Sheria ya madini ya mwaka 1998 iliweka fixed rate kuwa wawekezaji katika madini watapewa punguzo zaidi la asilimia 15 ya gharama waliozingia kununua vitendeakazi badala ya kuomba huruma ya kamishna. Ni kipengele ambacho kilileta utata kwa vile kuna makampuni mengine yaliyotumia hiyo asilimia kumi na tano kuwafanya wasilipe kodi kabisa kwa vile ilikuwa inafuta kabisa tax burden yao.

Swali la Zitto ni kuwa kipengele hicho hakijaondolewa rasmi na bunge kwa vile bado wanapitia tena sheria ile ya madini ya mwaka 1998. Swali hili lilikuwa limelenga kuwa serikali isijifanyie mambo bila kufuata sheria za bunge kwa vile bunge halijabadili sheria ya madini ya mwaka 1998. Waziri anadai kuwa kiliondolewa na bunge kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2001 na wala siyo sheria ya madini; mimi jana nimepitia sheria zetu zote sikuona mahali kilipoondolewa. Kilichoondolewa ni tafsiri ya maneno kadhaa ambayo zamani yalikuwa yakichukulia kuwa gharama za mining ni kwenye migodi tu, bila kuchukulia kuwa mining company inaweza kuwa na ofisi au laboratory sehemu kama Dar es Salaama ambapo hakuna mgodi. Kwa hiyo wakaondoa tafsiri hiyo ya mgodi kusudi gharama za kampuni kwa ajili ya kodi ziwe ni zote za mgodini na zile zisizokuwa za mgodini.

Tatizo nililogundua ni kuwa sheria zetu hazikuwandikwa makini kwa hiyo zinaleta confusion isyokuwa ya lazima. Inawezekana zamani zilikuwa zimeandikwa vizuri lakini walipoanza kuziscan mechanically kwa kutumia OCR software zimevurugika na wala hawakufanya effort ya ku-proof read kuona kama ziko sahihi. Kampuni iliyopewa tenda hiyo imeshachukua chake na kuondoka. Ili kufanya research nzuri kutumia sheria zetu inabidi mtu upate print copies za sheria zile baada ya kutumia zile zilizoko pale kwenye tovuti ya bunge ambazo ni bure kabisa.
 
Akizungumza katika mkutano huo, wakili maarufu aliyepata kuwa mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano (1995-2000) na Mbunge wa Afrika Mashariki, Mabere Marando, alisema kuwa, kifungu kilichotumika kumhukumu Zitto hakikuwa sahihi.

Alisema anachojua yeye ni kwamba, kisheria inapotokea kuwa mkataba ukasainiwa nje ya nchi, basi sheria zinazotumika ni za nchi hiyo ilikosainiwa, akimaanisha mkataba kati ya serikali na Barrick umesainiwa chini ya sheria za Uingereza.
Huyu Marando ni mwanasheria maarufu sana na nina imani kuwa anajua mambo ya mikataba sawasawa. Bado nina imani kuwa kama rais atalazimika kusaini mkataba ambao ni binding akiwa nje ya nchi, atafanya hivyo akiwa kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania ambayo ni sehemu ya Tanzania.

Kidogo kidogo, wanasheria watatufahamisha vizuri kuhusu hilo la mahali mkataba unaposainiwa. Kumbukeni kuwa huu siyo mkataba wa offer-acceptance ambapo offerer atakuwa kwenye nchi ambayo sheria zake zitagovern mkataba ule na offeree anaweza kuwa popote.
 
Labda tukuulize wewe Je, hii sera na sheria ya madini zimekwisha rekebishwa?

Mkandara,

It is open kwamba sheria hazijabadilishwa,,, lakini mathematically (proof by contradiction) haijadhihirika bado, hakuna sehemu mpaka sasa aidha imeletwa hapa JF au tumesoma mahali iliyosema "Serikali haitaingia mkataba mwingine na mwekezaji wowote wa madini hadi hapo sheria itakapobadilika"

Mimi ndio natafuta kipengele hicho ili nijui mkweli nani!!! unajua watu wengine hatubebwi juu juu kirahisi kama madodoki.

Wachanngiaji wengi walisema rais alisema hayo Shinyanga kwenye Mei Mosi 2007... Kitu ambacho sio kweli.! Kama tulivyoonyesha kwenye hotuba yake ya Shinyanga.

Issue ya sheria inaangalia mahali iliposainiwa!!! mmmhhhh... sijui, lakini ninalofahamu mimi makubaliano/agreement is btn two parties [Serikali ya Jamhuri] na huyo Mwekezaji... Sheria zinazoapply hapa ni Za serikali ya Jamhuri... na nina uhakika bila hata kuona kwamba kwenye huyo mkataba kuna quote chache za sheria za nchini kwetu.
 
Kinacho nisikitisha ni spika na wapambe wake kuona watu wote hawajui kitu kwa makundi yote yaani wanachi wakawaida,wanasheria,na wasomi wa nyanza zote, na spika na wapambe kuona wao ndio wanasema ukweli na makundi mengine yana zusha uwongo.

Spika kama akitaka achukue ile video aone njinsi alivyo ongoza bunge siku hiyo hata yeye atakiri kuwa alichemsha sana na pia ataona njinsi alivyo wakatisha tamaa wabunge wote waliojaribu kujenga hoja ya kutetea hoja ya Zitto na kuona wanayoyasema sio ya maana na hata kupelekea kusema michango ya mbunge mmoja inafurhisha tu na haina mwelekeo wa hoja yenyewe.

Kwa hiyo mwongozo wake ndio uliyopelekea maamuzi haya yanayopigiwa kelele na watu wengi na ilionyesha kuwa maamuzi haya ndio hasa alikuwa akiyapendelea sana yeye spika na pia alionyesha pia kama alikuwa na bifu na mheshimiwa Zitto.

Tunamwomba spika,Jk na wengine wote watakaopenda wairudie hiyo video yote na wahakikishe wanaiona yote na nafikiri watabaini nini kinapigiwa kelele na wanachi wengi na namshauri spika aige mfano wa mzee makamba alipobanwa akasema mtuu mzima akikosa na akiguna inamanisha amekiri kosa kwahiyo atarekebisha hayo makosa.

TVT Nayo pia inaleta mtindo mchafu kwani wakati ikirudia kuonyesha huo mjadala huo ulioleta utata nao wanakata sehemu ambazo ziliibana serekali na kuonyesha sehemu kidogo tu na kuwafanya wanachi waamini huo ndio mjadala mzima,Jamani TVT tunawaheshimu sana kama kunakitu kimewakera ni afadhali msikionyeshe na kumbukeni kuwa ni wananchi ndio wajiri wenu na ni tabia mbaya kumdanganya mwajiri wako.
 
Hii katuni itazua mambo mengine muda si mrefu! Yaani pamoja na KAtibu wa Bunge Bwana Foka kufoka bado magazeti yanaendelea kuliandama Bunge!

Muda si muda ya Mwanahalisi yatalikuta hili gazeti pia; tumsubiri Mhe. Khatibu.
 
Halafu tu-stick na ishu, hummer sio tija na wala hatuko tena kwenye siasa ya uajamaa na kujitegemea, kwa hiyo ni rukhsa kuwa na gari lolote, kuwatetea wanyonge sio lazima na wewe uwe masikini masikini, na kiongozi safi sio lazima awe masikini masikini, hizo ndio zilikuwa zidumu fikra za mwenyekiti!

Hapo umesema kweli! Ukiwa mtetezi wa wanyonge si lazima na we uwe hohe hae kama wao! Utapimwa kwa dhati yako, ukweli wako na nia yako ya ndani ikiambatana na maneno yako. Pia vitendo vyako vinavyoshabihiana na kauli zako! Zaidi ya hayo ukiwa na rasilimali pesa una added advantage ya kuwatetea watu kuliko wale wenye rasilimali chache!
 
1. Jana kwenye data zetu tulisema hivi,

Quote

1."Okay wazee niko njiani ninaendesha, lakini kewa hraka haraka, nilizozipata,

1. Mbunge wa Same East, alifikisha hoja ya madini bungeni, Zitto wakati wa break time akamwambia umeanzisha moto, subiri tukirudi uone nitakavyoiweka vizuri hoja ya madini!

2. Zitto, akaiweka inavyotakiwa kuwa Karimagi, amesaini mkataba na Barrick, London tena hotelini, hakuifahamisha kamati ya bunge ya uwekezaji, wala bunge zima kwa ujumla! hiyo mikataba ina utata!

3. Wabunge wote wakapigwa na shock ya umeme kusikia hayo maana waklikuwa hawajui kuhusu huo mkataba!"

2.Leo Mbunge Zitto, kwenye maandamano amesema hivi:

"Niwaambieni tu ndugu zangu, hiki ni kitu ambacho sikukisema hapo mwanzo lakini kama kamati ingeundwa ingegundua kuwa mkataba huo ulisainiwa hotelini na hoteli yenyewe inaitwa hoteli ya Churchill iliyoko jijini London," alisema Kabwe.


Je kuna mahali popote kwenye media zetu mlipoiona hii habari? Au kwenye hiyo kitu inaitwa ansard? Sasa haya maneno yalienda wapi na Zitto aliyasema ndani ya bunge? Ndio maana tunasema vijana muwe macho na data, na usanii wa serikali!

Wana JF, me nilifanikiwa kuwa miongoni mwa wasikilizaji wa hotuba ya Shujaa Zitto, alisema hivi na kama nitakosea nipo tayari kusahihishwa na sio kwamba nanukuu, najaribu kueleza tu kuwa suala la kuwa mkataba ulisainiwa hotelini hakulizungumza Bungeni (yaani ndani ya Bunge wakati wa kutoa na kujibu hoja yake), so haiwezekani likawemo kwenye taarifa zao za Kibunge.
 
...CCM wana-survive kashfa kama hizi kwasababu wananchi hawajaelimishwa jinsi gani mikataba mibovu inavyotumika kuiba rasilimali zao.

...infact karibuni JK atatembelea Buzwagi na utasikia mapokezi mazuri/makubwa/yanayostahili nabii wa mungu atakayoyapata.

...labda Zito,Mtikila,Mbatia,Lipumba,Seif Sharrif....ndiyo Maalimu Seif, waende wakapige kambi Buzwagi wakiwaelimisha wananchi kabla ya ziara ya Raisi.
 
Mkandara,

It is open kwamba sheria hazijabadilishwa,,, lakini mathematically (proof by contradiction) haijadhihirika bado, hakuna sehemu mpaka sasa aidha imeletwa hapa JF au tumesoma mahali iliyosema "Serikali haitaingia mkataba mwingine na mwekezaji wowote wa madini hadi hapo sheria itakapobadilika"

Mimi ndio natafuta kipengele hicho ili nijui mkweli nani!!! unajua watu wengine hatubebwi juu juu kirahisi kama madodoki.

Katika hotuba yake ya Bajeti ya 2006/2007 ya Wizara wa Nishati na Madini waziri wa wakati huo Dr. Ibrahim Msabaha alisema hivi kuhusu kupitia mikataba ya madini.

47. Mheshimiwa Spika, kufuatia hotuba ya Mheshimiwa
Rais aliyoitoa Mei Mosi, 2006, Kamati Maalumu imeundwa
kudurusu mikataba ya madini kwa lengo la kuona uwezekano
wa sekta ya madini kuongeza mchango wake kwenye Pato la
Taifa. Kamati hiyo imekwishawasilisha taarifa ya awali ambayo
kwa sasa inafanyiwa kazi. Aidha, wakati zoezi la kudurusu
mikataba hiyo likiendelea,
Wizara ilisimamisha utoaji leseni kwa
wawekezaji wakubwa waliotaka kuanza uzalishaji katika migodi
mipya.
Mojawapo ya mafanikio yaliyofikiwa katika zoezi la
upitiaji upya wa mikataba ya madini ni pamoja na makubaliano
yaliyofikiwa baina ya Serikali na Kampuni za uchimbaji mkubwa
wa madini kukubali kuanza kulipa Dola za Marekani 200,000
14
kwa mwaka kwa halmashauri husika kama kodi. Malipo ya kodi
hiyo kwa halmashauri yamekuwa hayafanyiki kwa kipindi kirefu
kutokana na utata wa kisheria uliosababishwa na kupingana
kwa mikataba ya madini na Sheria ya Serikali za Mitaa ya
mwaka 1982. Majadiliano yaliyofikiwa baina ya Serikali ya
Awamu ya Nne na kampuni hizo yalifanikisha kupatikana kwa
ufumbuzi wa utata wa kisheria uliokuwepo na hivyo kuruhusu
malipo hayo ya kodi kwa halmashauri husika kuanza kufanyika.
Hadi sasa, Kampuni ya Barrick Gold Tanzania inayomiliki
migodi ya Bulyanhulu, Tulawaka na North Mara imelipa jumla
ya shilingi 734,999,999 kwa wilaya za Kahama, Biharamulo na
Tarime. Kampuni ya Resolute itaanza kulipa kodi kwa
Halmashauri ya Nzega kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Aidha, mashauriano kati ya Serikali na kampuni za madini
yameanza katika zoezi la kudurusu mikataba ya madini kwa
lengo Ia kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika ipasavyo.

angalia maneno hayo kuwa "wakati zoezi la kudurusu mikataba hiyo likiendelea".. Sasa tuangalie majibu ya Karamagi kwenye hoja za Zitto.

Sasa Karamagi kwanza anakanusha kuwa zoezi la kudurusu (kupitia) mikataba linaendelea:

"Mheshimiwa Spika, hivyo, si kweli kuwa zoezi la kudurusu mikataba ya madini bado linaendelea."

Kwa maneno mengine (ukitumia mwanga wa hotuba ya Msabaha) ni kuwa sasa hivi leseni za madini zinaweza kutolewa kwani zoezi la kudurusu mikataba yote "limekamilika".

Hata hivyo, sentensi chache kabla ya hapo akizungumzia matokeo ya kupitia mikataba hiyo Karamagi anasema hivi kuhusu Anglo Ashanti Gold:

Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki mgodi wa Geita imekubali kulipa kiasi cha Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Aidha, majadiliano katika maeneo mengine ya mkataba wake, yanaendelea.

STOP...!!! and Scream... whaaaat?

Ina maana kupitia mikataba ya madini na makampuni yote kumekamilika hivyo Zitto anasema Uongo anaposema kuwa kunaendelea, lakini wakati huo huo kudurusu mkataba wa Ashanti Gold bado kunaendelea? Nani kati yao kasema Uongo?

Angalia maneno ya Msabaha mwaka mmoja uliopita kuhusu kampuni ya Resolute, anasema:

Kampuni ya Resolute itaanza kulipa kodi kwa
Halmashauri ya Nzega kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.

Kutokana na majadiliano na Resolute basi Resolute wamekubalia kulipa Halmashauri ya Nzega. Lakini kutokana na majibu ya hapa chini ya Karamagi, suala la Nzega si mojawapo ya vilivyokubaliwa na Resolute.

Kampuni ya Resolute (Tanzania) Limited imeondoa kipengele kwenye mkataba wake kilichokuwa kinairuhusu kutokulipa kodi ya mapato kwa wafanyakazi wake wa kigeni. Kuondolewa kwa kipengele hiki kutailazimu kampuni hii kulipa takriban Dola za Marekani milioni 2.2 kila mwaka kama malipo ya kodi ya mapato. Katika mwaka 2006/07 kampuni hiyo imelipa Dola za Marekani milioni 2.3.

Swali hapa ni dhahiri: Kampuni ya Resolute imeishailipa halmashauri ya Nzega kiasi chochote? Inawezekana bado wanajadiliana (kitu ambacho kitaivunja kauli kuwa kudurusu kumekoma) na kama wamemaliza na ikawa ni "lose win" situation bado watakuwa hawajatimiza agizo la Rais.

Sheria gani imebadilishwa?

Hili nalo ni swali la Msingi kama Kichuguu alivyoonesha kwa werevu hapo juu. Wakati Mramba akizungumzia suala hili alisema kipengele hicho kimeondolewa. Ukweli ni kuwa huwezi kufuta sheria kwa kubadili maana ya maneno. Kama kuna majibu ya kihuni hili linastahili tuzo. Kipengele anachonukuu kinasema hivi kwa kuanzia "By deleting the definitions of the words.." na sehemu yake ya pili inasema "by deleting the definition of the word". Sasa, sheria ya fedha ya 2001 ilichofanyia mabadiliko siyo sheria yenyewe ya 1973 bali maana ya maneno yaliyotumika kuelezea subject matter which is "15% ya additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure".

Sasa hapa ndio Mgogoro na Zitto unapotokea. Wakati Mramba alipoleta bajeti yake 2002 (akiwa waziri wa fedha) alisema hivi kuhusu kurejesha kifungu hicho:

“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures: (v) I propose to reinstate (Naomba kurudia) the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998”

Sasa, Karamagi anapojibu hoja ya Zitto anasema kuwa kifungu hicho si cha sheria ya madini ya 1998 bali ya 1973. Haya ni maneno yake:

Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko haya ni kwamba fungu la 18 (1) la Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 linaloweka masharti ya kipengele cha nyongeza ya asilimia 15% kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa liliondolewa.

Sasa hili ni rahisi kuliangalia. Kama sheria iliyofanyiwa mabadiliko ni ile ya 1973 basi Mramba alisema Uongo Bungeni na anastahili kufungiwa. Kama sheria iliyofanyiwa mabadiliko ni ile ya madini ya 1998 basi Karamagi kasema uongo. Jambo moja zaidi kuhusu hili, anapofafanua kuhusu hili Karamagi anaanza kwa kusema:

"Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko haya ni kwamba fungu la 18 (1) la Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 linaloweka masharti ya kipengele cha nyongeza ya asilimia 15% kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa liliondolewa."

Hivi Karamagi alianza kuwa Mwanasheria lini? Alijuaje kuwa mabadiliko hayo yalimaanisha nini? Tafsiri ya sheria na maana yake haitolewi Bungeni. Katika mfumo wetu wa serikali chombo pekee ambacho kina mabadaraka ya kutoa tafsiri ya sheria zetu siyo Bunge bali ni Mahakama. Kwa vile umetokea mgongano kati ya tafsiri binafsi ya Zitto na ya Karamagi, ambayo imechangiwa na maelezo ya Mramba, basi haja ya chombo huru (Mahakama au Kamati Teule) ndio inakuwa nzito zaidi.

Maana yake ni kuwa, endapo kipengele kinachodaiwa kurejeshwa kwa kauli ya Mramba hakikufutwa kama anavyodai Karamagi, basi Zitto ana point kubwa zaidi ya kuelezea ilikuwaje Mramba arejeshe kifungu ambacho hakikufutwa kisheria? Chombo pekee chenye mamlaka ya kufuta sheria na kutunga nyingine ni Bunge. HAKUNA mahali popote ambapo sheria iliyoweka hiyo 15% (ya mwaka 1973) ilibadilishwa. Siyo kwenye sheria ya fedha ya 2001 au sheria mpya ya mapato ya 2004.

Maana yake ni kuwa inawezekana kabisa aliyesema uongo Bungeni ni Karamagi na Mudhihir kwa kudai Zitto kadanganya. Kwa Mudhihir kudai kuwa Zitto kadanganya, na akaliambia kuwa Zitto amedanganya, basi yeye mwenyewe naye kadanganya kwa kushuhudia uongo usiokuwapo.

Nitaendelea baadaye kuangalia tena majibu ya Karamagi na kuonesha ni kwanini Wamemfungia mtu asiye sahihi.
 
Maana yake ni kuwa inawezekana kabisa aliyesema uongo Bungeni ni Karamagi na Mudhihir kwa kudai Zitto kadanganya. Kwa Mudhihir kudai kuwa Zitto kadanganya, na akaliambia kuwa Zitto amedanganya, basi yeye mwenyewe naye kadanganya kwa kushuhudia uongo usiokuwapo

Mudhihiri yeye msamehe tuu nadhani hata hailewi unaposema sheria ya mwaka .... iliyofanyiwa mabadiliko... Yeye ni mtu wa mipasho ndio maana alishabikia kusimamishwa kwa ZK.

Ila mkuu nakupa salute kwa uchambuzi keep it up Mwkjj. Tupe nondo.
 
Hamna maneno, nitaendelea kuchambua pale wenzangu humu walipoachia kuonesha kuwa alichosema Dr. Slaa kuwa kilichofanyika ni "kichekesho cha demokrasia" ni kweli.
 
Kabla ya Zitto kuibua hoja ya Karamagi kusaini mkataba wa Buzwagi, Mbunge wa Jimbo la Kahama kupitia CCM, James Lembeli, aliibua hoja hiyo ndani ya Bunge wakati akijadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini siku hiyo ilikua ndio siku mpendwa wetu, Marehemu Amina Chifupa, aliaga dunia. Lakini jambo la kusikitisha siku Zitto alipoiboresha hoja hiyo na kuiweka hadharani, wabunge wa CCM waliikimbia na kumsulubu.. hii ni dalili ya wazi ya UNAFIKI wa WABUNGE wa CCM. hapa chini naambatanisha sehemu ya maelezo ya Lembeli:

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Madini. Wilaya ya Kahama ni miongoni mwa Wilaya hapa nchini ambazo zina madini mengi na hususan dhahabu. Kahama dhahabu inapatikana karibu kila mahali . Hivi karibuni nimesikia redioni kwamba mgodi mpya wa madini ya dhahabu unaitwa Buzwagi utaanza kujengwa nje kidogo ya mji wa Kahama kilomita kama tano. Kwa kutumia Ilani ya Uchaguzi mimi nimeshiriki kikamilifu kuhamasisha wananchi kujiandaa na ujio wa mgodi huu.

Kinachosikitisha ni kwamba nimesikia tayari mkataba baina ya Serikali na Kampuni itakayochimba dhahabu hiyo tayari umeshawekwa. Lakini wananchi wa Kahama wamekuwa wakipiga kelele husasan wale wa maeneo ambako mgodi huu unajengwa hivi sasa wananchi wa Mwendakulima, Mweme na Chapulwa. Kila siku wanalalamikia juu ya fidia zao, hakuna mtu anaweza kuwaeleza kikamilifu kwamba Serikali inasema nini watalipwa kiasi gani na kadhalika. Matokeo yake sasa hivi ni vurugu tupu mpaka inalazimika Mkuu wa Wilaya anakwenda na Polisi kuwajaribu kuwazuia wananchi wenye hamaki wasiwashambulie wale ndugu zangu wa Barricks.

Sasa hili naliona ni tatizo kubwa. Mimi niliamini wazi kuwa Mkataba huu utakuwa tofauti na mikataba ile ya nyuma; na kama umefanyika kwa nini umefanyika kwa siri siri hata mwakilishi wa wananchi wa eneo hilo Mbunge, hana habari. Kinachosikitisha zaidi nimewahi zaidi ya mara mbili kuomba Waziri wa Nishati au Naibu wake aje Kahama azungumze na wananchi wa eneo hilo Kata ya Mwendakulima kuhusu haki zao baada ya mgodi huu kuanza kufanya kazi. Mpaka hii leo hakuna na wanategemea mimi Mbunge niende pale nizomewe halafu ndiyo waje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili ni hatari sana kwa nchi yetu, ninamwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu ahakikishe kwamba Waziri wa Nishati anafika Kahama na si kwenda Blyanhulu, anakuja Buzwagi kuzungumza na wananchi wa Kata ya Mwendakulima.

Lipo tatizo, bado makampuni haya pamoja na kuahidi kwamba yatalipa dola laki mbili kwa Halmashauri ambako wanafanya kazi, nasikitika mpaka jana Barricks walikuwa hawajailipa Halmashauri ya Kahama dola laki mbili. Na sasa wameanza ujanja, barua na maulizo mbalimbali wakati jambo hili ni lipo wazi. Hela hizi zilitakiwa zitumike kwa maendeleo ya wananchi wa Kahama katika mwaka huu wa Fedha unaokwisha, mpaka leo pesa hizo hawajalipa.
 
#12 21st April 2007, 04:20 AM
Augustine Moshi
JF Senior Expert Member Join Date: Sat Apr 2006
Posts: 397
Rep Power: 22

Thanks: 0
Thanked 46 Times in 25 Posts



--------------------------------------------------------------------------------

Mzee Mwanakijiji,

Umewafafanulia vizuri sana wabunge namna walivyopashwa kumjibu Gaudence Kayombo. Kayombo alidanganya (labda bila kujua) aliposema separation of powers hairuhusu wabunge kuridhia mikataba ya kiserikali kabla haijawa sheria. Ni wazi kabisa toka kwenye ibara za katiba ulizotaja (IBARA 63(2) (E)) kwamba Wabunge wana haki na uwezo wa kuhakiki mikataba kati ya Jamhuri ya Muungano na mtu yeyote.

Inabidi wabunge wawe wanaifahamu vizuri Katiba. Wanaapaje kuilinda kama hata hawaifahamu? Kama wangekuwa wanaifahamu, wangejibu huo uongo wa Gaudence Kayombo hapo hapo, kwa njia ya swali la ziada.

Gaudence Kayombo amejichanganya aliposema wabunge wana uwezo wa kusimamia serikali inavyotekeleza mikataba, na huku anasema hawana uwezo wa kudai kuiona mikataba yenyewe. Kuna level mbili za kuona mkataba. Kuna kuuona kabla haujasainiwa na kuwa wa kisheria, na kuna kuuona wakati umeshasainiwa. Inaelekea kwa sasa wabunge wananyimwa kuona mikataba hata baada ya kusainiwa. Watasimamiaje utekelezaji wake?

Wabunge watumie Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulazimisha serikali isisaini mkataba wowote bila ridhaa ya Bunge.

Wanaong'ang'ania mikataba iwe siri na isiridhiwe na wabunge wana lao!

Augustine Moshi
__________________
Time has a history. It was not there before the beginning and it will cease to exist
Na huyu basi asimamishwe uwaziri/Ubunge kwa kulipotosha Bunge
 
Mwanakijiji,

Mbunge gani angechangia? Waliambiwa ambaye anamuunga mkono Zitto asizungumze akae kimya... wengine walikasirika wakatoka nje aliposimama Mudhihir...walikuwapo Mawaziri, Zakia Meghji (alisimama akatembea kidogo, akarudi kukaa, halafu akainuka tena akatoka moja kwa moja), Anthony Dialo, (alisimama na kutoka kabisa nje) wabunge waliotoka walikua Anna Kilango Malecela, Victor Mwambalaswa na Harrison Mwakyembe. MWandosya, Mwakyusa na Mungai, wao walibaki kushika vichwa wakionekana kukerwa, nyuso zao zilionyesha wazi kusikitika..... Hiyo ndio CCM.

Wakati huo huo, Mudhihir na Adam Malima wameomba ulinzi kwa Waziri Mkuu baada ya kupokea simu kibao za kuwataka wasitembee mitaani ambako watazomewa na kupigwa mawe ama kumwagiwa uchafu... wameambiwa hawana UZALENDO na ni WALAFI,
 
Hivi mlimuona Mudhir alivyokuwa anazungumza... ni wazi alikuwa anaomba cheo mahali fulani..
 
Hivi mlimuona Mudhir alivyokuwa anazungumza... ni wazi alikuwa anaomba cheo mahali fulani..

That guy Mudhir is a real fool,but this time he is in for it,He is always trying to make out that he is a do or die CCM stalwart. But MKJJ are not all the CCM mbunges imagining or seeing themselves as Ministers in waiting.!!
 
Back
Top Bottom