Mkandara,
It is open kwamba sheria hazijabadilishwa,,, lakini mathematically (proof by contradiction) haijadhihirika bado, hakuna sehemu mpaka sasa aidha imeletwa hapa JF au tumesoma mahali iliyosema "Serikali haitaingia mkataba mwingine na mwekezaji wowote wa madini hadi hapo sheria itakapobadilika"
Mimi ndio natafuta kipengele hicho ili nijui mkweli nani!!! unajua watu wengine hatubebwi juu juu kirahisi kama madodoki.
Katika hotuba yake ya Bajeti ya 2006/2007 ya Wizara wa Nishati na Madini waziri wa wakati huo Dr. Ibrahim Msabaha alisema hivi kuhusu kupitia mikataba ya madini.
47. Mheshimiwa Spika, kufuatia hotuba ya Mheshimiwa
Rais aliyoitoa Mei Mosi, 2006, Kamati Maalumu imeundwa
kudurusu mikataba ya madini kwa lengo la kuona uwezekano
wa sekta ya madini kuongeza mchango wake kwenye Pato la
Taifa. Kamati hiyo imekwishawasilisha taarifa ya awali ambayo
kwa sasa inafanyiwa kazi.
Aidha, wakati zoezi la kudurusu
mikataba hiyo likiendelea, Wizara ilisimamisha utoaji leseni kwa
wawekezaji wakubwa waliotaka kuanza uzalishaji katika migodi
mipya. Mojawapo ya mafanikio yaliyofikiwa katika zoezi la
upitiaji upya wa mikataba ya madini ni pamoja na makubaliano
yaliyofikiwa baina ya Serikali na Kampuni za uchimbaji mkubwa
wa madini kukubali kuanza kulipa Dola za Marekani 200,000
14
kwa mwaka kwa halmashauri husika kama kodi. Malipo ya kodi
hiyo kwa halmashauri yamekuwa hayafanyiki kwa kipindi kirefu
kutokana na utata wa kisheria uliosababishwa na kupingana
kwa mikataba ya madini na Sheria ya Serikali za Mitaa ya
mwaka 1982. Majadiliano yaliyofikiwa baina ya Serikali ya
Awamu ya Nne na kampuni hizo yalifanikisha kupatikana kwa
ufumbuzi wa utata wa kisheria uliokuwepo na hivyo kuruhusu
malipo hayo ya kodi kwa halmashauri husika kuanza kufanyika.
Hadi sasa, Kampuni ya Barrick Gold Tanzania inayomiliki
migodi ya Bulyanhulu, Tulawaka na North Mara imelipa jumla
ya shilingi 734,999,999 kwa wilaya za Kahama, Biharamulo na
Tarime. Kampuni ya Resolute itaanza kulipa kodi kwa
Halmashauri ya Nzega kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Aidha, mashauriano kati ya Serikali na kampuni za madini
yameanza katika zoezi la kudurusu mikataba ya madini kwa
lengo Ia kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika ipasavyo.
angalia maneno hayo kuwa "wakati zoezi la kudurusu mikataba hiyo likiendelea".. Sasa tuangalie majibu ya Karamagi kwenye hoja za Zitto.
Sasa Karamagi kwanza anakanusha kuwa zoezi la kudurusu (kupitia) mikataba linaendelea:
"Mheshimiwa Spika, hivyo, si kweli kuwa zoezi la kudurusu mikataba ya madini bado linaendelea."
Kwa maneno mengine (ukitumia mwanga wa hotuba ya Msabaha) ni kuwa sasa hivi leseni za madini zinaweza kutolewa kwani zoezi la kudurusu mikataba yote "limekamilika".
Hata hivyo, sentensi chache kabla ya hapo akizungumzia matokeo ya kupitia mikataba hiyo Karamagi anasema hivi kuhusu Anglo Ashanti Gold:
Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki mgodi wa Geita imekubali kulipa kiasi cha Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Aidha, majadiliano katika maeneo mengine ya mkataba wake, yanaendelea.
STOP...!!! and Scream... whaaaat?
Ina maana kupitia mikataba ya madini na makampuni yote kumekamilika hivyo Zitto anasema Uongo anaposema kuwa kunaendelea, lakini wakati huo huo kudurusu mkataba wa Ashanti Gold bado kunaendelea? Nani kati yao kasema Uongo?
Angalia maneno ya Msabaha mwaka mmoja uliopita kuhusu kampuni ya Resolute, anasema:
Kampuni ya Resolute itaanza kulipa kodi kwa
Halmashauri ya Nzega kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Kutokana na majadiliano na Resolute basi Resolute wamekubalia kulipa Halmashauri ya Nzega. Lakini kutokana na majibu ya hapa chini ya Karamagi, suala la Nzega si mojawapo ya vilivyokubaliwa na Resolute.
Kampuni ya Resolute (Tanzania) Limited imeondoa kipengele kwenye mkataba wake kilichokuwa kinairuhusu kutokulipa kodi ya mapato kwa wafanyakazi wake wa kigeni. Kuondolewa kwa kipengele hiki kutailazimu kampuni hii kulipa takriban Dola za Marekani milioni 2.2 kila mwaka kama malipo ya kodi ya mapato. Katika mwaka 2006/07 kampuni hiyo imelipa Dola za Marekani milioni 2.3.
Swali hapa ni dhahiri: Kampuni ya Resolute imeishailipa halmashauri ya Nzega kiasi chochote? Inawezekana bado wanajadiliana (kitu ambacho kitaivunja kauli kuwa kudurusu kumekoma) na kama wamemaliza na ikawa ni "lose win" situation bado watakuwa hawajatimiza agizo la Rais.
Sheria gani imebadilishwa?
Hili nalo ni swali la Msingi kama Kichuguu alivyoonesha kwa werevu hapo juu. Wakati Mramba akizungumzia suala hili alisema kipengele hicho kimeondolewa. Ukweli ni kuwa huwezi kufuta sheria kwa kubadili maana ya maneno. Kama kuna majibu ya kihuni hili linastahili tuzo. Kipengele anachonukuu kinasema hivi kwa kuanzia "By deleting the definitions of the words.." na sehemu yake ya pili inasema "by deleting the definition of the word". Sasa, sheria ya fedha ya 2001 ilichofanyia mabadiliko siyo sheria yenyewe ya 1973 bali maana ya maneno yaliyotumika kuelezea subject matter which is "15% ya additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure".
Sasa hapa ndio Mgogoro na Zitto unapotokea. Wakati Mramba alipoleta bajeti yake 2002 (akiwa waziri wa fedha) alisema hivi kuhusu kurejesha kifungu hicho:
Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures: (v) I propose to reinstate (Naomba kurudia) the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998
Sasa, Karamagi anapojibu hoja ya Zitto anasema kuwa kifungu hicho si cha sheria ya madini ya 1998 bali ya 1973. Haya ni maneno yake:
Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko haya ni kwamba fungu la 18 (1) la Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 linaloweka masharti ya kipengele cha nyongeza ya asilimia 15% kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa liliondolewa.
Sasa hili ni rahisi kuliangalia. Kama sheria iliyofanyiwa mabadiliko ni ile ya 1973 basi Mramba alisema Uongo Bungeni na anastahili kufungiwa. Kama sheria iliyofanyiwa mabadiliko ni ile ya madini ya 1998 basi Karamagi kasema uongo. Jambo moja zaidi kuhusu hili, anapofafanua kuhusu hili Karamagi anaanza kwa kusema:
"Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko haya ni kwamba fungu la 18 (1) la Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 linaloweka masharti ya kipengele cha nyongeza ya asilimia 15% kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa liliondolewa."
Hivi Karamagi alianza kuwa Mwanasheria lini? Alijuaje kuwa mabadiliko hayo yalimaanisha nini? Tafsiri ya sheria na maana yake
haitolewi Bungeni. Katika mfumo wetu wa serikali chombo pekee ambacho kina mabadaraka ya kutoa tafsiri ya sheria zetu siyo Bunge bali ni Mahakama. Kwa vile umetokea mgongano kati ya tafsiri binafsi ya Zitto na ya Karamagi, ambayo imechangiwa na maelezo ya Mramba, basi haja ya chombo huru (Mahakama au Kamati Teule) ndio inakuwa nzito zaidi.
Maana yake ni kuwa, endapo kipengele kinachodaiwa kurejeshwa kwa kauli ya Mramba hakikufutwa kama anavyodai Karamagi, basi Zitto ana point kubwa zaidi ya kuelezea ilikuwaje Mramba arejeshe kifungu ambacho hakikufutwa kisheria? Chombo pekee chenye mamlaka ya kufuta sheria na kutunga nyingine ni Bunge.
HAKUNA mahali popote ambapo sheria iliyoweka hiyo 15% (ya mwaka 1973) ilibadilishwa. Siyo kwenye sheria ya fedha ya 2001 au sheria mpya ya mapato ya 2004.
Maana yake ni kuwa inawezekana kabisa aliyesema uongo Bungeni ni Karamagi na Mudhihir kwa kudai Zitto kadanganya. Kwa Mudhihir kudai kuwa Zitto kadanganya, na akaliambia kuwa Zitto amedanganya, basi yeye mwenyewe naye kadanganya kwa kushuhudia uongo usiokuwapo.
Nitaendelea baadaye kuangalia tena majibu ya Karamagi na kuonesha ni kwanini Wamemfungia mtu asiye sahihi.