Hotuba ya Kabwe Zitto imeleta mengi mapya masikioni mwa Watanzania,Ambayo hatukuyasikia kwenye hotuba(Hoja) yake kule Dodoma Bungeni,Sio kwamba Mkataba ulisainiwa Hotelini na sio Ubalozini,bali pia Mkuu wa Kaya hakufahamishwa Ukweli kuhusu Mkataba huo.Pamoja na kwamba walikuwa pamoja ktk safari hiyo ya Uk na Japan.
Katika Hotuba yake kwenye sherehe ya Mei Mosi/2006,Jk alisema kwamba Utiaji saini mikataba yote ya madini umesimamishwa na serikali ya awamu ya NNE ili kutoa nafasi kwa Mabingwa wa mikataba kuipitia Upya kwani Mikataba iliyopita ina Utata,Alirudia maelezo hayo ya kusimamisha Utiaji saini Mikataba ya Madini huko Afrika kusini kwenye Seminar ya Madini.Sasa Mkataba huu uliotiwa Saini na Karamagi una utofauti na Mingine?
Kitendo cha Ndg Karamagi(Waziri mfanyabiashara)kutia saini Mkataba wa Uchimbaji Madini huko Kahama kinanipa wasiwasi kuwa kuna Mazingira ya Rushwa.Maelezo ya Zitto ni mwanzo tu wa ukweli mzima wa mambo.Na kama ni kweli Waziri alitia saini Mkataba huo bila Ufahamu wa Rais sioni kwanini Waziri asiwajibike!!