The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Kilitime,
Mkandara,

It is open kwamba sheria hazijabadilishwa,,, lakini mathematically (proof by contradiction) haijadhihirika bado, hakuna sehemu mpaka sasa aidha imeletwa hapa JF au tumesoma mahali iliyosema "Serikali haitaingia mkataba mwingine na mwekezaji wowote wa madini hadi hapo sheria itakapobadilika"
Ndugu yangu naona hapa umerukia hili bus bila kuangalia liendako!.. hivi uliyasoma vizuri hoja za ndugu Zitto?..
Je, katika hoja yake yake kipengele cha saba Nd. Zitto hakusema hivi:-

Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa Rais alikwishapiga marufuku kusainiwa kwa mikataba mipya ya Madini mpaka hapo sheria za madini zitakarekebishwa. Akisoma hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mnamo tarehe 17/7/2006, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Ibrahim Msabaha alilitaarifu Bunge kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezuia kusainiwa kwa Mikataba mipya ya Madini. Nimeambatanisha Hansard ya siku hiyo kama uthibitisho wa kauli hiyo. Sasa inakuwaje Waziri wa Nishati na Madini kwenda kinyume na maagizo ya Rais? Tena nje ya Nchi?

Kilitime,
Mimi nakushauri hivi, maadam majibu mengi ya Karamage unayakubali basi tafadhali ebu rudi nyuma utafute maelezo ya Mkapa Kieleweke ambaye akliyaweka maswali ya ndugu Zitto kisha jabiru kutafuta taratibu majibu ya Waziri yanayolingana na swali.. kama hutaona kwamba Waziri alikuwa akichukua sheria hii na kuibandika kilaka mahala ambapo hakutakiwa. Na kila mmoja wao anadai anao mshahidi na kuambatanisha Hansard lakini wenezetu mnachagua hiyo ya Karamage!.. Kikao ndicho pekee kingeweza kutupa UWAZI wa swala hili... siwezi kutumia ukweli ama Uahihi maanake Wadanganyika mnaweza niweka katika kundi la Kabwe!http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4468&page=12

Labda niweke maswali machache hapa na aribu kuyajibu kutokana na Karamage! maswali in BOLD
24. Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha Mhe. Basili Mramba.
"Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
(v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998"….. Mwisho wa kunukuu.

25. Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002 nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya Madini haitajwi.

26. Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?

27. Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya Waziri ni ya kweli. Je kwa nini makampuni ya Madini ambayo yameingia Mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?

28. Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya Serikali na ufisadi.

Mwisho wa kunukuu!
 
Napenda kuwataarifu tu kuwa hicho kipindi kilisha isha sasa...labda kama unataka kuangalia vipindi vinginevyo endelea... marudio ya kipindi hicho cha 'Jarida Maridhawa' kipo saa 1 ya jioni masaa ya nyumbani.

SteveD.
 
Napenda kuwataarifu tu kuwa hicho kipindi kilisha isha sasa...labda kama unataka kuangalia vipindi vinginevyo endelea... marudio ya kipindi hicho cha 'Jarida Maridhawa' kipo saa 1 ya jioni masaa ya nyumbani.

SteveD.
Kilionyeshwa jana jioni, leo ilikuwa marudio!
 
Kilionyeshwa jana jioni, leo ilikuwa marudio!

Kakalende,
Poa tu, ahsante kwa ku-point hilo, ni kipindi muhimu nilivyo kiona mimi, na leo tena Star TV watakuwa wanakinarudia basi masaa hayo ya jioni, labda watoe kipya. Ningelifurahi kama wale ambao hawajabahatika kukiona wakiangalie, hasa walio mbali na nyumbani na wenye internet zenye spidi kubwa.

SteveD.
 
Habari ambazo zinanijia toka mbali ni kuwa Rais Kikwete anatarajiwa kutembelea eneo la Buzwagi ambako kunatarajiwa kujengwa Mgodi mpya wa dhahabu na kampuni ya Barrick Gold. Hata hivyo habari zinazoingia pole pole sana ni kuwa wananchi wa eneo la Buzwagi na wakesha hoi wengine, wameudindia msafara wa RAis wakitaka maelezo ya kina? Kama Rais atapokewa kwa shangwe au kwa mabango ya maswali tunasubiri kusikiliza.... kwa wenye uwezo tegeni masikio VOA....

Still monitoring....

M. M.
 
Ndiyooooooooooooooo habari toka hapa Shy ni hizo bwana . Kwa bahati nzuri ziara ya mkuu huyu imekumbana na ziara yangu binafsi ni raha tupu .Ukitaka kuujua ukweli angalieni TVT hawataweza kuonyesha ukweli wa wananchi na kuuliza who is Karamagi .Maana wanazidi kuchanganyikiwa kwa tamko la Ikulu leo . Hawajui kama kweli Rais anaunga mkono mambo ya Karamagi ama hapana . Niko hapa najionea nikisha kuwa na habari kamili kama kawaida nitawapa .
 
Mheshimiwa Mwanakijiji kuna Ndugu zetu kwenye Vijiji vya Chapulwa,Mwendakulima na Mweme wamehamishwa kutoka kwenye Vijiji vyao ili kuwapisha Wawekezaji,na mpaka leo hii bado hawajalipwa kama walivyoahidiwa!.Kwa Mtazamo wako watakuwaje na Furaha kumuona Mkuu wa Kaya ambaye hawajali?.Tunayoyaona kwenye vyombo vya habari sio ukweli halisi huko field!,Waungwana Tafuteni muda muende huko Kahama na sehemu nyingine zinazochimbwa madini ili muone Utofauti wa maisha ya watu.Lengo sio kuimarisha na kuinua maisha ya mlalahoi,bali ni kuchukua madini kwa uharaka na nguvu zote!,kwani kesho mambo yaweza kubadilika.
 
nasikia msafara wake umekwamishwa kuingia Buzwagi wananchi wanataka wapewe maelezo... mbona mbunge wao hakuambiwa kuwa mkataba umesainiwa?
 
Kuna kitu kibaya sana ambacho watanzania tunacho; NIDHAMU YA WOGA...wakati wa ziara hii ya mkuu wa Kaya; kauli hii itathibitika.
 
Wananchi waanze sasa kuishitaki serikali na haya makampuni kwa kutowalipa fidia na rasilimali zao ambazo ni haki yao. Huwezi ati kulipa $200 000 kwa mwaka ati iwasaidie wananchi wakati hicho kiwango ni asilimia ndogo tu ya mshahara wa manager wa mgodi. Hii serikali ya JK ina kiburi sana.
 
nasikia msafara wake umekwamishwa kuingia Buzwagi wananchi wanataka wapewe maelezo... mbona mbunge wao hakuambiwa kuwa mkataba umesainiwa?

Mkjj

Napenda kujua tafadhali.

- Mbunge wao ni nani?

- Aliongea lolote bungeni kumshukuru Zitto kwa kuleta hoja?
 
kwa kuwa jk ameshindwa kupambana na haya mambo kama mwnamme na njia pekee aliyoona ni kuongopea wananchi kwa maana ya kuwafumba mamcho.
 
Yaani kesi ya ndedere uipeleke kwa nyani,jamani hapo hakuna jipya.Kwa ujumla mkoa wa shinyanga unamadini mengi sana tena kupita kiasi.kwa upande wa kahama ni wilaya tajiri sana lakini wananchi wake ni masikini kwa sasa. kabla ya uwekezaji mji wa kahama ulikuwa unapanuka kwa kasi ya ajabu kwa watu kujenga majumba lakini baada ya hawa wawekezaji mji umedumaa.ni wilaya ambayo inalisha mkoa wa shinyanga na mikoa jirani.kwa kilimo cha mazao ya biashara ni tumbaku,pamba,karanga,na mpunga ndio usiseme.hapo mwenakulima na mwime si mbali na mji ulipo kwa sababu wakazi wengi wa mjini wanachota maji ya kunywa mwime. na mimi nikiwa mmojawapo.msije shangaa mkasikia mji unahamishwa yangu macho.
 
mbunge wa kahama mjini alilalamika bungeni lakini ndio siku amina alipo kufa .kuna post humu Halisi aliweka,ngoja niitafute niiunganishe hapa
 
Kaka Yebo Yebo Mbunge huyo ni James.D Lembeli.Hapo awali alishawahi kuzungumza Bungeni kuhusu machimbo hayo ya Buzwagi.Sina kumbukumbu nzuri lakini nafikiri ktk Hotuba ya Waziri Mkuu,lakini cha ajabu ni kwamba wakati zitto anatoa Hoja Binafsi kuhusu watu wa jimbo lake(Kahama)Mbunge huyu kwa uoga alikaa kimya!.Mbunge huyo ni Journalist na kuna wakati aliwahi kuwa Presenter kwenye Radio ya Dutchwelle.
 
Wananchi waanze sasa kuishitaki serikali na haya makampuni kwa kutowalipa fidia na rasilimali zao ambazo ni haki yao. Huwezi ati kulipa $200 000 kwa mwaka ati iwasaidie wananchi wakati hicho kiwango ni asilimia ndongo tu ya mshahara wa manager wa mgodi. Hii serikali ya JK ina kiburi sana.


Hili ni moja kati ya mambo yaliyonishangaza kusikia Mheshimiwa Karamagi anatamba kuwa makampuni yanatoa dola laki mbili kwa mwaka kusaidia maendeleo. Ile kamisheni ya rada tu ilikuwa milioni 12, sasa jamani hii laki mbili si ni kuwatukana wananchi kabisa, tena matusi ya nguoni.
 
Mkjj

Napenda kujua tafadhali.

- Mbunge wao ni nani?

- Aliongea lolote bungeni kumshukuru Zitto kwa kuleta hoja?

Yebo Yebo; nenda kwenye mjadala wa CHADEMA na Karamagi - utaona aliyosema mbuge, James (somebody)
 
Back
Top Bottom