The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

hivi hawa wananchi wanafikiri Rais ni nani? Kama wao wamemchagua mbunge bomu hayo ni matatizo yao. Kama mbunge wao ameshindwa kuwatetea Bungeni na kumuunga mkono huyo Zitto wenu, sasa wanataka Rais afanye nini. Tusipoangalia watu watasubiri hadi Rais aje awasongee ugali! Huu ni upuuzi, kama kweli wamehamasika na kuamka, waende kuandamana kwa mbunge wao, wasimsumbue Rais wetu kwa mambo ya kipuuzi. Washindwe na kuregea kabisaaa! wanakera.

Asanteni.
 
hivi hawa wananchi wanafikiri Rais ni nani? Kama wao wamemchagua mbunge bomu hayo ni matatizo yao. Kama mbunge wao ameshindwa kuwatetea Bungeni na kumuunga mkono huyo Zitto wenu, sasa wanataka Rais afanye nini. Tusipoangalia watu watasubiri hadi Rais aje awasongee ugali! Huu ni upuuzi, kama kweli wamehamasika na kuamka, waende kuandamana kwa mbunge wao, wasimsumbue Rais wetu kwa mambo ya kipuuzi. Washindwe na kuregea kabisaaa! wanakera.

Asanteni.

Bi Senti:
Nadhani inafaa umpe pole mbunge. Kama umesoma aliyokuwa akiyasema bungeni utamuonea huruma. Kumbuka, mbunge anachangia mawazo yake chini ya darubini ya chama kilichoshika hatamu.
Sanasana, labda umshawishi huyo mbunge ajiunge na vyama vya ushindani; jambo ambalo kwa sasa hivi wengi waliomo ndani ya CCM haiwezekani kwa sababu ya matumbo yao. Labda tuvute subira kidogo, who knows, may be Kabwe has opened the door. Let's vuta subira a little longer and see who enters through that door first. Fingers crossed.
 
hivi hawa wananchi wanafikiri Rais ni nani? Kama wao wamemchagua mbunge bomu hayo ni matatizo yao. Kama mbunge wao ameshindwa kuwatetea Bungeni na kumuunga mkono huyo Zitto wenu, sasa wanataka Rais afanye nini. Tusipoangalia watu watasubiri hadi Rais aje awasongee ugali! Huu ni upuuzi, kama kweli wamehamasika na kuamka, waende kuandamana kwa mbunge wao, wasimsumbue Rais wetu kwa mambo ya kipuuzi. Washindwe na kuregea kabisaaa! wanakera.

Asanteni.


Wananchi WASIMSUMBUE RAIS...!!!!

Kusaini mgodi wa Madini kwa niaba ya nchi ni UPUUZI...!!! Kweli, kuelimisha watanzania sio kazi ndogo.
 
Mimi nafikiri wanaotakiwa kupewa pole ni wananchi wa maeneo yanayozunguka machimbo ya dhahabu na vito vingine. Ni wao ambao wameshindwa kubana serikali zao za mitaa na miji yao na kuonesha msimamo wao. Serikali isipoangalia sehemu hizi za madini zitaanza kuwa kama kule Delta Nigeria ambako watu walifikia mahali wamesema inatosha. Ni wananchi wenyewe ambao wamekaa kimya na kuwachagua watu wa chama kile kile. Well, u get what you paid for. Ila Rais wamwache ana mambo mengi na muhimu zaidi kulikuwa kuwababy sit watanzania.

asante.
 
"Tunataka huduma za maji na umeme, tunataka barabara ya lami, asilimia 70 ya dhahabu inakwenda sisi tunaachiwa 30, tunakwenda wapi?


HONGERA WANANCHI BUZWAGI KWA KUENDELEZA YALE YA KIGOMA WALIPOMPOKEA KWA JENEZA NA MADEBE MATUPU YA MAJI NA MABANGO PALE RUSSIA MASIKANI




. "Ni kweli kabisa mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini nchini Uingereza baada ya kuambiwa kufanya hivyo na Wizara ya Nishati na Madini," alisema Mwanyika.


Alisema ulipowadia wakati wa kusaini mkataba wa mgodi huo, alimpigia simu Waziri Karamagi, lakini yeye alimwambia aende wizarani kwa ajili ya kupata maelekezo. Mwanyika alipokwenda wizarani, aliambiwa waziri alikuwa Uingereza na Rais Kikwete hivyo, wampekekee huko akausaini.


UWONGO!!!

Vilevile, aliwahakikishia wananchi hao wa Kahama kuwa ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni zitatimizwa kama vile kuleta maji kutoka Ziwa Victoria ambapo vijiji kumi vitarajia kufaidika.


MRADI WA MAJI WA ZIWA VICTORIA ULIBUNIWA NA KUTEKELEZWA NA AWAMU YA TATU ..TUNAKUMBUKA MZEE..HUU MRADI WAKATI WA KUBUNIWA ILIBIDI MKAPA AMTUME WAZIRI WA MAJI LOWASSA CAIRO KUWAELEZA NIA YETU YA KUUJENGA KINYUME CHA MATAKWA YA CAIRO ..huu mradi umeleta mapinduzi makubwa kwenye HAKI za matumizi ya NILE...kikwete kwa mimi amataka kujipa sifa..KWA KUWA HUU MRADI YEYE AMEUKUTA UNAMALIZIKA HAHITAJI KUUCHUKULIA KAMA MFANO WA AHADI ALIZOTEKELEZA....YEYE AZINDUE TU!!! ALIYEUBUNI NA KUULIPIA NI AWAMU YA TATU..




Alisema majaribio ya maji yanatarajiwa kufanyaika Septemba na baadaye mradi kukamika Desemba mwaka huu.


mh hili la mradi wa MAJI NA LA UWANJA WA TAIFA MPYA USITEGEMEE SIFA KUTOKA KWA WATU MAKINI..WEWE SUBIRI HESHIMA YA UFUNGUZI TU..SANASANA NA WEWE FIKIRIA KUMALIZIA VIWANJA VYA ALI HASSAN MWINYI ,TABORA..CCM KIRUMBA NA AMRI ABEID ARUSHA ILI ANGALAU VIIFIKIE LEVEL YA INTERNATIONAL ILI NA SISI TUANDAE ALL AFRICAN GAMES AU AFRICAN CUP OF NATIONS KABLA HUJASTAAFU....RUDISHA VIWANJA VYOTE KUOKA MIKONONI MWA CCM ZIPEWE HALMASHAURI HUSIKA KWA SABABU VILIJENGWA NA MICHANGO NA KODI ZETU..

HAPA HONGERA..

Ahadi ambayo Rais alitoa ni ujenzi wa shule ambapo awamu yake ilikuta shule 78 na sasa ziko shule 265 yaani shule mpya 187.

SUALA LA UJENZI WA MAJENGO YA SHULE MPYA ZA SEKONDARI ..TUNAMPONGEZA MH RAIS KAMA MOJA YA HATUA MUHIMU ZA UTEKELEZAJI WA ILANI YAKE YA UCHAGUZI..HAPA AWAMU YA NNE WAMEJITAHIDI..SASA TUNATAKA UBORA WA HIZI SHULE..VITABU,MAABARA ,MADAWATI,WALIMU .MAKTABA ets
 
Let us hope they're beginning to see. There is a lot of work to be done though; they should always recognize that.

Hii lugha ya "wenyewe"..."they"....haisaidii. Mtu unaongea as if wewe haikuhusu bwana...aagghhhh....
 
MOJA ya wabunge makini nimrod MKONO Alipata kugoma kwenye sherehe ya kukabidhi dola laki mbili kwa halmashauri yake ya musoma zilizotolewa na barrick akisema hicho kiwango ni kama tusi ..kwa jamii inayozunguka migodi..ni kidogo mno..nashangaa rais anasifia nini? mkono hakuchangia bungeni hoja ya zitto..na amesema hatakaa ahudhurie sherehe alizoziita za kipuuzi....kumbukeni huyu kwa access yake anajua kiwango wanachoingiza hawa mabwana...
 
hivi hawa wananchi wanafikiri Rais ni nani? Kama wao wamemchagua mbunge bomu hayo ni matatizo yao. Kama mbunge wao ameshindwa kuwatetea Bungeni na kumuunga mkono huyo Zitto wenu, sasa wanataka Rais afanye nini. Tusipoangalia watu watasubiri hadi Rais aje awasongee ugali! Huu ni upuuzi, kama kweli wamehamasika na kuamka, waende kuandamana kwa mbunge wao, wasimsumbue Rais wetu kwa mambo ya kipuuzi. Washindwe na kuregea kabisaaa! wanakera.

Asanteni.

Wananchi WASIMSUMBUE RAIS...!!!!

Kusaini mgodi wa Madini kwa niaba ya nchi ni UPUUZI...!!! Kweli, kuelimisha watanzania sio kazi ndogo.


Nyie ndio mnaopaswa kuelimishwa badala ya hao wananchi wanaofungua ukurasa mpya wa historia dhidi ya utapeli,dhuluma,ujambazi,ubabaishaji na usanii.Kwani mmeambiwa kuwa suala pekee walilokuwa wanalalamikia ni hilo la mkataba wa madini?Kama mlikurupuka ku-comment kabla ya kuisoma vizuri habari husika basi kipande hiki kinaweza kuwasaidia kutafakari upya maandihsi yenu

Wananchi hao waliokuwa wamejipanga barabarani, walikuwa na mabango mbalimbali yakionyesha shida wanazokumbana nazo kila siku na kumtaka Rais Kikwete kutoa tamko kuhusiana na kero zao. Katika mabango hayo kulikuwa na ujumbe kama "Tunataka huduma za maji na umeme, tunataka barabara ya lami, asilimia 70 ya dhahabu inakwenda sisi tunaachiwa 30, tunakwenda wapi?

Hivi kwa busara zenu mnadhani kuna mbunge mwenye jeuri ya kupambana na hawa majambazi wanaokingiwa vifua na aliyewachagua (JK)?Na hata kama wananchi hao wangekuwa wanalalamikia suala la mgodi,bado walikuwa na haki ya kufanya hivyo kwani alosaini mkataba huo sio Mbunge wao bali Karamagi,ambaye hakuteuliwa na mbunge wa Buzwagi,bali JAKAYA MRISHO KIKWETE.Na ofisi yake leo inamtetea Karamagi kwamba hakufanya kosa kusaini mkataba huo bila kumjulisha Rais.Sasa kama Rais hakujulishwa naye anaona poa tu,hivi mnapomlaumu huyo mbunge si mnamwonea tu.Kutomuunga mkono Zitto sio sahihi lakini sote tunajua kwanini hakufanya hivyo,na hilo halihitaji mjadala.

Angalau hao wazalendo wa Buzwagi wamemudu kufanya kitu flani ambacho kinaweza kuleta domino effect hata kwenye maeneo mengine.Nyie mnawaolaumu mna lolote mlilofanya,hata kama ni la kipuuzi,ambao linaweza kuingizwa kwenye vitabu vya historia?Kuelimisha Watanzania kunakuwa kugumu zaidi kwa vile baadhi ya wenye uwezo wa kutafakari wanazembea kufanya tafakuri jadidu,na badala yake wanachukua short cut ya kulaumu.
 
Nimeyasikiliza hayo matangazo ya VOA na nimeshindwa kung'amua wananchi walikuwa wako kwenye hali (mood) gani. Ndio maana niliulizia kama kuna video ya tukio hilo lakini baadhi yenu mkaniona kama naazima ukurasa kutoka kwenye kitabu cha Mwafrika wa Kike...Lol.
 
Sijui wananchi wataendelea kukumbuka adha hizi hadi siku ya uchaguzi?
Moja ya matatizo yetu wananchi ni kusahau masahibu yanayo tufika yaliyosababishwa na tulio wachagua.Kusahau kwetu siku zote huja ghafla hasa pale mwanasiasa mwenye jina asimamapo na kutoa hadithi ya kubuni kuwarubuni wananchi ili apate kura.
" Mambo hayakua hivyo ndugu wananchi pateni hoja nzima kutoka kwangu mimi Mbunge wenu"
**********************************************
Utawala mzima wa CCM umeoza tukipata walau 55% ya wabunge kutoka upinzani hata kama rais anatoka CCM bungeni moto utawaka.
Pia sheria nyingi zitapata wasaa wa kutazamwa upya.
*****************************************************

Kelele zetu za kwenye mtatandao zinafanya kazi ipasavyo hili linanipa moyo sana.
Kwa mfano nimeona mabadiriko katika lugha ya kila siku mitaani Neno FISADI linazidi kujikitika na kutumika ipasavyo.

Ufisadi ni zaidi ya Rushwa.
Ni uwezo wa kiongozi wa kitaifa kutumia cheo chake na uwezo wake wote wa kisiasa na kiserikali kujinufaisha yeye na familia yake pengine na rafiki zake. Kisha kutumia uwezo huohuo kuvuruga nanmna yeyote ya tukuma zenye nia ya kufukua na kuweka wazi uoza alio nao.
Fisadi siku zote ananunua ndimi na midomo ya watu ili kuifunga isiseme au inene ayatakayo,
anatishia kufungia chombo au vyombo vya habari,
anazuia upatikanaji wa habari,
anachelewesha utoaji wa haki katika kila jambo,
ananunua vyombo vya habari na kutia maneno yake kwenye vyombo hivyo kuuficha ukweli.
Mafisadi siku zote wako tayari kuvuruga elimu ambayo ni msingi wa maendeleo,

Hatahivyo, mafisadi wote Duniani wana udahifu mwingi unao karibia kufanana.

Ni makatiri sana.
Hawana huruma.
Hawajari kitu.
Wanajua vizuri sana kuwatumia watu wanaowazunguka kwa faida yao.
Ni rahisi kumnawia mikono mtu mwadirifu kama adhabu ya uadirifu wake.
MAfisadi wote Mioyoni mwao ni waoga kweli kweli(Phobia)
Mara zote asili ya uoga wao ni mambo yaliyowatukia Utotoni, wakiwa shule za msingi shule za sekondari na mitaani wakati wa kicheza cha ndimu na wenzao.

Ukichunguza maisha ya Fisadi yeyote tangu utoto wake utaona maisha yake yana tobwe kubwa,Pengo, Social gap ambalo yeye anadhani ataliziba kwa kujikweza juu ya kila mtu Kiuchumi Kiutamaduni na Kisiasa.

Kwa lugha nyingine ni kwamba mafisadi wote ni wagonjwa wa akili.

Wana ukichaa wa aina fulani unao wanyima aibu ya kuwa na utu walau kidogo.
Tanzania yetu inaongozwa na wagonjwa ambao Under same Temperature and Pressure walitakiwa kuwa wagonjwa wa nje wa Hospitali ya Mirembe au Isanga kule Dodoma.

Mafisadi wengi walidharirishwa kijinsia wakiwa watoto wadogo wakapata moyo wa jiwe.

Kama mnabisha subirini tutakavyoanza kuwahukumu na kuwapa vifungo vya nguvu (miaka 40 jela) katika siku chache zijazo watakavyoweka wazi maisha yao ya utotoni na jinsi walivyofanywa kiasi cha kuwafanya wawe hayawani.

Aina nyingine ya woga walio nao unatafsiriwa katika namna wanavyo handle masuala ya ngono leo hii.

Wengi wa Mafisadi hawakuwa active kingono hadi walipofika miaka 20.Au walilazimishwa kufanya ngono kinyume na matakwa yao.
Wakiwa makinda kuongea na wasichana ni jambo llilo wadharirisha sana kiasi cha kuwachukia wasichana.
(Hii vile vile inawahusu wanawake kadhaa walioko madarakani)
Leo hii Tabia yao kimahusiano na wanawake ni kulipiza kisasi tu.
Wanaacha mburungutu makubwa ya noti kwa wake zao lakini hawshiriki mkesha wa jungu kuu na wake zao wengine kwa miezi kadhaa.
Hii ndiyo asili ya kutembea na wanawake wengi ovyo ovyo na kutapanya fedha za umma kujaribu kuwakomoa wanawake. Tabia hii inafanyika ndani ya mioyo yao huku nje wakijitahidi kuonekana ni waungwana kweli kweli.
Wengine hufikia hata kutembea na visichana vidogo chini ya miaka 14 ili kutoa adhabu kufidia udhaifu wao wakiwa na umri huo.

Wengine jamii iliwa let down kwa sababu moja au nyingine. Kwa mfano watoto wengine kwa sababu fulani ilionekana kila kundi la watoto wanalojiunga nalo inafanyika mbaya na mtaa mzima unamnyooshea kidole cha lawama new member ambaye leo hii nifisadi na kusema ndiye mwalimu mpya wa vitendo viovu.
Mafisadi wengi walipatwa na visa kama hivi vya kulaumiwa kwa ukali na ubinafsi binafsi na jamii nzima wakati walikuwa wakifanya jambo ambalo mtoto yeyote angeweza fanya.
Matokeo yake leo wakiwa na nyadhifa kubwa za kitaifa ambazo jamii inawategemea kutoa maamuzi yenye kuijari jamii.
Watu hawa hawana huruma hata chembe kwa jamii kwani kwao muda uliopo ni mwafaka kwa kutoa adhabu kali kwa kila mwanajamii ndiyo

Ufisadi hauanzii hewani una misingi yake.

Wako Viongozi ambao wako kwenye ufisadi kwa sababu wametekwa nyara. Hawako huru kutoa maamuzi yao binafsi kwa kuogopa kutolewa kafara na kupoteza kipato. Mafisadi wa namna hii ni Kondoo wanao lazimika kutabasamu na kucheka cheka na Mbwa Mwitu.
Mafisadi wa kundi hili siku zote ndio watumwao kwenda kutoa vitisho mbalimbali katika jamii ili wakikamatwa jamii nzima ishindwe kuamini macho na masikio yao. Watu kama Anna.

Sisi wengine ambao petu ni pakavu tia mchuzi tumekata tamaa kiasi cha kudhani uongozi na wizi wa mali ya umma ni vitu viendavyo sambamba kwa hiyo kiongozi yeyote asilaumiwe wala kuulizwa kwa kuiba mali ya umma.
Mh!
Hapa tunaongea kulaumiwa na kuulizwa baada ya mwaka 2010 madai yetu makubwa yatakuwa ni kuwafungulia mashtaka viongozi wote wezi na pindi wapatikanapo na hatia kuwalazimisha kurudisha hadi shillingi ya mwisho serikalini.
Kwetu sisi tulio na moyo wa kuku wa kusubiri kuchinjwa jambo la kuwashitaki viongozi litatutia hofu kiasi cha kutufanya tufe kabla ya siku zetu.

***************************************************************
Kila system hata zile system imara na madhubuti kabisa zinajengwa na watu wenye akili kama yako na yangu na ambao katika ujenzi wa system hizo wamefanya makosa mengi ambayo hulazimika kuyalinda kwa gharama kubwa mambo yakienda mrama.

Kama system ya kusambaza maji dar imepata hitilafu kila mtu anajitahidi kujua kulikoni na watu wengi hujaribu kutoa mapendekezo yao ya namna ya kutatua kasoro huku wakilaumu watu.
Walio itengeneza system ile ili iendelee kuharibika mara kwa mara ili wao waendelee kula nao huja na hoja za hapa na pale huku wakilaumu vitu badala ya watu

kama system ni ya kuwawezesha WAKOLONI kuiba mali zetu zote za asili kadiri wawezavyo kama
Dhahabu
Almasi
Tanzanite
Wanyama
Samaki
Kodi
Ardhi
Visiwa
Mito na Fukwe
Zaidi akili na utu wa watu
System hii inapoleta kasoro na kushindwa kufanya kazi wananchi wengi huuliza maswali mengi. Kazi kubwa ya wajenzi wa system hii ya kihabithi ni kutumia misuri yao ya kiserikali kuziba masikio ya wananchi wasisikilize ukweli wa mambo.
Watakuwa tayari kutumia mabilioni ya shilingi kuhakikisha kwamba wanawapendezesha mabwana zao huko ughaibuni na kidogo wanachama wao(WanaCCM) ili kulinda Tabaka la wakoloni Tabaka la Viongozi wa CCM Tabaka la Wanachama wa kawaida wa CCM na Watanzania wengine.

Kama ingekuwa inawezekana viongozi wetu wa CCM wangebadiri rangi zao na kuwa Wazungu au Waarabu na Wahindi.

Leo hii mwaka 2008 karne ya 21 Utashangaa sana kusikia CCM bado wanatamani kutawaliwa na Wazungu na waarabu wakati hata nusu karne tangu tuwatimue haijafika.

Leo hii Mwaka 2008 karne ya 21 inashangaza kuona wanachama wa CCM wengi kama si wote wanaunga mkono maamuzi ya kuenzi Mwizi wetu wa madini na Mwongo mkubwa chini ya kiapo nazir karamagi
na wako tayari hapo tarehe 25 Augusti kuandamama kuunga mkono uendelezaji wa UKOLONI MAMBOLEO kupitia agent wao CCM.

************************************************

Viongozi wa CCM wanatafuta furaha ya kweli kwa kujirimbikizia Fedha haramu.

Kwako kiongozi wa CCM Furaha ya kweli katika maisha yako hailetwi na uwingi wa fedha katika mfuko au account yeyote ya benki.
Furaha ya kweli inaletwa kwa kujenga uwezo wa kiuchumi wa jamii nzima ya Kitanzania.
 
labda niseme kidogo,mradi wa bomba la maji ulijengwa miaka ya 92-95,hapa kikati sina kumbukumbu vizuri ulikamilika lini,lakini ulitoka victoria mpaka bulyankulu kwenye machimbo.lakini vijiji ambavyo vimepitiwa na mradi huu havikunufaika na mradi huu kwa maana ya kupata maji.kwa hiyo sasa wanaweka bombo kutoka bulyankulu kwenda buzigwa.(nitawapa ramani kidogo,yaani ujenge bomba kutoka ubungo kwenda post mpya.sasa hawa watu wa manzese,magomeni,ndio wanao lalamika)na ilibomba linapita kahama mjini ambapo pia hakuna maji.
 
Ndiyo
Tutapa akina Ken Sorowiwa wengi sana kutoka Kahama.
Mchimba madini ni lazima atoe kodi kubwa ya kutosha pia umiriki wa migodi ni lazime uwe wa ubia.

Jakaya Kikwete na serikali yake ni Maharamia
 
Hii lugha ya "wenyewe"..."they"....haisaidii. Mtu unaongea as if wewe haikuhusu bwana...aagghhhh....

Kura ndio niliyo nayo na uchungu wa maonevu yanayotendeka. Uongozi wa kisiasa, I don't think so. That's why ......'they,' who aspire to lead katika ushindani.
Timu ya kabumbu ni wachezaji 11, usitake mashabiki nao tuingie uwanjani. Kazi ni kuwapigia mayowe wachezaji sisi tukiwa nje ya uwanja.
 
Kura ndio niliyo nayo na uchungu wa maonevu yanayotendeka. Uongozi wa kisiasa, I don't think so. That's why ......'they,' who aspire to lead katika ushindani.
Timu ya kabumbu ni wachezaji 11, usitake mashabiki nao tuingie uwanjani. Kazi ni kuwapigia mayowe wachezaji sisi tukiwa nje ya uwanja.

Kama una uwezo wa kucheza ni bora uingie uwanjani kuliko kupiga mayowe ukiwa pembeni. Kwa kuingia unaweza ukaleta tofauti na kuanza kufunga magoli. Key words..."Kama una uwezo wa kucheza"...lakini kama uwezo huna endelea kukaa pembeni na kupiga mayowe
 
Big up wana JF for updates. No doubt kuwa wana JF kwa kiasi fulani mnasaidia kuwafumbua watu wacho. Wananchi kumdindia JK ni haki yao ya kidemokrasia, na wana haki kama waziri wao anawageuka na kuwakamua, na kama mbuge wao akiulizwa anaambiwa shut up, na kama Zitto anasimamishwa, kwanini wao wasisimame??? It is a historic event in Tanzania, Nadhani kwa upande mmoja hata JK mwenyewe moyoni mwake atawasupport watu hao, lakini kutokana na fadhila za Karamagi hataweza kumtupa.
 
Kama una uwezo wa kucheza ni bora uingie uwanjani kuliko kupiga mayowe ukiwa pembeni. Kwa kuingia unaweza ukaleta tofauti na kuanza kufunga magoli. Key words..."Kama una uwezo wa kucheza"...lakini kama uwezo huna endelea kukaa pembeni na kupiga mayowe

Lakini huo sio uamzi wako. Ni uamzi wangu. Niachie mwenyewe.
 
Okay, back to the issue.
Gazeti la Mwananchi ni la nani? Nauliza hivi kwasababu, video anayoulizia Nyani Ngabu inaleta maana. Kwasababu nikisoma stori ya Mwananchi na nikilinganisha na VOA, naona kama Mwananchi wanapoza stori. Au nyie mnaona vipi? Maana mimi naona kwama Mwananchi wanasema wanakijiji walipewa stori ya Mtukula, Jinja....unakatiza kisumu.....you get the gist.
 
Back
Top Bottom