BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Kikwete apokewa kwa mabango Buzwagi
*Yeye awaambia matatizo yao yatashughulikiwa na mkoa
*Barrick wasema Karamagi aliwaita kusaini mkataba London
Na Mwandishi Wetu, Kahama
WANANCHI wa vijiji vya Kakola na Tegete wilayani hapa, jana walizuia kwa muda msafara wa Rais Jakaya Kikwete kwa mabango wakati akielekea katika mgodi mpya wa madini wa Buzwagi jana. Rais Kikwete yupo katika ziara ya siku nane kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani Shinyanga.
Wananchi wenye mambango na wasio na mabango, walijipanga katikati ya barabara na hivyo kuzuia msafara wa Rais ambao ulikuwa ukielekea katika mgodi mpya wa Buzwagi ambao ulizua mjadala mkubwa baada ya Mbunge wa Kigoma Kasikazini, Zitto Kabwe, kuwasilisha hoja binafsi akitaka kuundwe Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza mazingira ya utiwaji saini wa mkataba wa mgodi huo uliofanyika jijini London Februari mwaka huu na waziri wa nishati na madini, Nazir Karamagi.
Wananchi hao waliokuwa wamejipanga barabarani, walikuwa na mabango mbalimbali yakionyesha shida wanazokumbana nazo kila siku na kumtaka Rais Kikwete kutoa tamko kuhusiana na kero zao. Katika mabango hayo kulikuwa na ujumbe kama "Tunataka huduma za maji na umeme, tunataka barabara ya lami, asilimia 70 ya dhahabu inakwenda sisi tunaachiwa 30, tunakwenda wapi?
Baada ya kusimama, Rais Kikwete aliwaambia kwamba matatizo ambayo wanakumbana nayo kila siku yatashugulikiwa na serikali ya mkoa na kwamba huduma za maji zitakamilika baada ya mradi wa maji kutoka katika Ziwa Victoria kuhitimishwa.
Hata hivyo, Rais Kikwete, wakati akihutubia wananchi katika mgodi wa Buzwagi, hakuongelea mjadala unaondelea sasa dhidi ya mazingira ya utiwaji saini wa mkataba wa mgodi huo huko London, Uingereza. Badala yake, Rais alishukuru kampuni ya Barrick kwa kukubali kutoa fungu katika mapato yake na kuzipa halmashauri za wilaya zinazozunguka migodi hiyo. Pia alishukuru kampuni hiyo kwa kujenga nyumba za wanakijiji ambao walikuwa katika maeneo ya machimbo ya migodi ya dhahabu.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Barrick, Deo Mwanyika, alisema ni kweli mkataba wa mgodi wa Buzwagi ulisainiwa nchini Uingereza. "Ni kweli kabisa mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini nchini Uingereza baada ya kuambiwa kufanya hivyo na Wizara ya Nishati na Madini," alisema Mwanyika.
Alisema ulipowadia wakati wa kusaini mkataba wa mgodi huo, alimpigia simu Waziri Karamagi, lakini yeye alimwambia aende wizarani kwa ajili ya kupata maelekezo. Mwanyika alipokwenda wizarani, aliambiwa waziri alikuwa Uingereza na Rais Kikwete hivyo, wampekekee huko akausaini.
Pia Mwanyika alisema ni kweli walisaini mkataba huo hotelini kwa kuwa Barrick hawana ofisi London bali ofisi yao ipo Canada. Hata hivyo, hakueleza kwa nini hawakusaini mkataba huo katika Ubalozi wa Tanzania ulioko London Uingereza. Mwanyika alisema walilazimika kumfuata Waziri kwa kuwa muda wa kusaini mkataba ulikuwa unaelekea ukingoni.
Mapema Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi wa Kakola kuwa hawatahamishwa kutoka katika kijiji hicho ili kutoa nafasi ya kupanua mradi wa machimbo ya dhahabu ya Bulyanhulu. Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi hao akiwa njiani kuelekea Kahama ambako alifungua shule ya sekondari na nyumba za wananchi wa Buzwagi zilizojengwa na kampuni ya Barrick kama fidia ili kupisha mgodi mpya wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni hiyo.
"Hamtahama na matatizo yenu mengine mtaendelea kuyazungumza ili mpatiwe ufumbuzi," alisema Rais Kikwete. Vilevile, aliwahakikishia wananchi hao wa Kahama kuwa ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni zitatimizwa kama vile kuleta maji kutoka Ziwa Victoria ambapo vijiji kumi vitarajia kufaidika.
Alisema majaribio ya maji yanatarajiwa kufanyaika Septemba na baadaye mradi kukamika Desemba mwaka huu. Ahadi ambayo Rais alitoa ni ujenzi wa shule ambapo awamu yake ilikuta shule 78 na sasa ziko shule 265 yaani shule mpya 187.
Kuhusu ahadi ya barabara Rais Kikwete alisema tayari tathimini imeanza na ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni za mwaka 2005 ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.