The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Zitto alipua bomu jingine

2007-08-22 18:52:13
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Siku chache tu baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mhe. Zitto Kabwe kukataliwa hoja yake ya kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge ili ichunguze utata uliopo katika mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, sasa mbunge huyo kijana zaidi amelipua bomu jingine zito kama lilivyo jina lake.

Mhe. Kabwe amelipua bomu hilo jana na kuwaacha watu kibao waliokuwa wakifuatilia maelezo yake kupitia kituo kimoja cha luninga kubaki midomo wazi.

Akizungumza katika kipindi cha `Je Tutafika` ambacho hurushwa na kituo cha Channel Ten na kuongozwa na Bw. Makwaia wa Kuhenga, Mhe. Zitto akasema kwa mara nyingine tena, Serikali imeingia mkataba wa gesi ya Mkuranga anaodai hauna maslahi ya kutosha kwa taifa na wawekezaji wa kampuni moja ya Ireland.

Mhe. Zitto akasema mkataba huo ambao umengiwa na Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Waziri Nazir Karamagi, unaiacha nchi ikiwa na uwezekano wa kunufaika kidogo na raslimali hiyo kulinganisha na wawekezaji hao.

Kwa mujibu wa Mhe. Zitto, Serikali katika mkataba huo itaweza kuambulia asilimia 30 ya faida wakati katika nchi jirani kama pale Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo, mkataba kama huo huiwezesha Serikali ya Rais Kabila kupata asilimia 45.

``Tayari mkataba huo umeshasainiwa hivyo bado taifa litaendelea kukosa maslahi yanayostahili,`` akasema Mhe. Kabwe.

``Kama kampuni hiyo imekubali kule Congo kuchukua asilimia 55 na kuliachia taifa hilo asilimia 45, inakuwaje kwa Tanzania wakatae?,``akahoji Bw. Kabwe.

Katika kipindi hicho, pia alikuwepo Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Adam Malima (CCM), ambaye amesema kuwa lengo la Serikali kuingia mikataba mbalimbali na wawekezaji ni kutaka kuinua uchumi wa nchi na hivyo kunufaisha watu wake, hasa kwa kupitia kodi zitakazolipwa na wawekezaji hao pamoja na mirahaba.

Kipindi hicho pia kilimuhusisha Prof. Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hivi karibuni, Mhe. Zitto aliibua hoja ya kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza sababu za Waziri Karamagi kusaini mkataba wa Mgodi wa Buzwagi Jijini London, Uingereza na mambo mengine kadhaa aliyodai kuwa yana utata.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipigwa kumbo na yeye akaishia kusimamishwa bungeni hadi Januari mwakani kwa la kumsingizia Waziri Karamagi kuwa amedanganya.

SOURCE: Alasiri


Kweli ukistaajabu ya Musa ............................
 
Zitto alipua bomu jingine

2007-08-22 18:52:13


SOURCE: Alasiri


Kweli ukistaajabu ya Musa ............................

What Mb. Malima alijua kuhusu huu mkataba, ndio maana alikuwa anashikia kidedea kuhusu Zitto kuadhibiwa kumbe ana siri yake as well.
 
Jana JK alikwenda kwenye dinner ya usiku hapa kahama kwenye ukumbi wa lake house na alishindwa kuongea na pia hakusalimia .anaonekana kuchanganywa sana na labda ni kuwa ni juu ya yale majibu ya mkurugenzi wa barrick kuwa Karamagi na Kikwete ndio waliwaita wande london kusaini mkataba husika na hili nafikiri liwekewe tread yake kwani hili linaibvua hoja mpya kuwa kumbe waziri ndio alidanganya zaidi kuwa alikuwa anawahgi kumbve yeye ndio aliwaita kwenda bar kusaini mkataba husika.


jk naye kama waliitwa wote na best yake au akifahamu[offcorse alijua]..ni aibu..ndio maana bungeni ccm walikuja juu sana..na kwa kweli kwa migodi jk hana la kutuambia ana conflict of interest na pesa za kampeni walimpa..kupitia kwa rostam ambaye ndie mwenye tenda ya exploration ya almost migodi ..sioni kama alikuwsa serious kusema ana review mikataba...

sishangai wanavijiji majirani wanashangaa kuwa hata mwaka wa pili haujaisha ameshajenga KIJIJI CHA MAHEKALU pale LUGODA..kati kati ya vibanda vya udongo na nyasi vya wenyeji....kweli uchumi unapaaaaaaaaa!!!...eti walikuwa wakisema ooh huyu anafaa hana tamaa ya mali wengine mkamfananisha na mwalimu..nani kasema..???

tujifunze ..inawezekana muheshimiwa anayo nia njema moyoni..lakini kwa kuwa wapo waliotoa pesa zao na kutumia kila njia ashinde ...atakuwa hana kauli..NANI KASEMA HANA UBIA???..Kwa hili mwalimu alituonya tujiepushe na wagombea kubebwa na wafanyabiashara .,..ambao mara zote hutaka faida..wakati ccm imejengwa kweye MISINGI YA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI..ni lini kimeacha kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi????
 
The buck stops with JK. Huyu jamaa ni kilaza na limbukeni huwezi kuongoza nchi kwa mishen town. Inflation inapanda kwa kasi wakati yeye na EL wanagawa pesa kama njugu ambazo hawajui zilitoka wapi. Wako busy kuchuma utajiri kwa sababu ya matumbo yao. Hii ndio sababu mnaweza kuelewa tangu ashike madaraka angalie safari alizopiga za huko Mwanza kwenye share zake halafu trip za Uarabuni.

Hivi sasa ana kiwewe maana wabongo wamekwisha mjulia janja yake .............................na bado tutaona mengi subirini.

Maneno yako dua ni ya kweli tu if and only if nchi inajengwa na raisi!

Inflation inaletwa na raisi, uchumi imara mkuu [macro-economics] uliojengwa na BWM unaweza tu kudondoka kiasi hicho!

We don't expect a genius president of course, neither we do not expect present wa kufanya micro-management... if that is what we expect then... we are all wrong...
 
Maneno yako dua ni ya kweli tu if and only if nchi inajengwa na raisi!

Inflation inaletwa na raisi, uchumi imara mkuu [macro-economics] uliojengwa na BWM unaweza tu kudondoka kiasi hicho!

We don't expect a genius president of course, neither we do not expect present wa kufanya micro-management... if that is what we expect then... we are all wrong...

..yeye ndo msimamizi mkuu!

..sasa these things are happening under his guard!
 
Kilitime,
Maneno yako dua ni ya kweli tu if and only if nchi inajengwa na raisi!

Inflation inaletwa na raisi, uchumi imara mkuu [macro-economics] uliojengwa na BWM unaweza tu kudondoka kiasi hicho!
We don't expect a genius president of course, neither we do not expect present wa kufanya micro-management... if that is what we expect then... we are all wrong...

Mjomba vipi tena ktk hilo! maanake nakuona unasifia Mkapa na Macro - economics kuwa ndio ujenzi wa rais lakini hapo hapo unakataa mengineyo!..
Hili neno macroeconomics limetuharibu kabisa kwani tunashindwa hata kuona mapana ya somo hili ktk mazingira yetu.
Inflation na hata high Unemployment rate vinatokana na mipango mibaya ya Uongozi!..
Nitakwambia kwamba Mkapa alichojenga ni mikakati inayolinda maslahi ya wageni kwa sababu Tanzania leo hii haina inachozalisha na kuuza nje zaidi ya kununua toka nje na kulimbikiza madeni tukitegemea huruma na msamaha wao.
Tunachokiuza tanzania ni Utamaduni wetu ikiwa ni pamoja na vinyago, Khanga na ile mali Mungu alotujalia toka kuumbwa kwa dunia hii ( madini na mbuga za Wanyama). Kwa hiyo Mkapa alijenga macroeconomics inayozunguka vitu hivi kutokana na ushauri wa hao wezi wakubwa INF na ndio maana unamuona JK akizunguka dunia nzima kujaribu kuuza kisichouzika ila mirathi yetu - he had nothing to sale.
Katika lugha ya biashara tunasema Tanzania tunazalisha kisha tunatafuta soko (demand)utadhani mama ntilie anayeandaa chakula usiku akitegemea rehma za mwenyezi Mungu auze chakula chote kesho yake! hapo mjomba hata micro haiwezi kutusaidia kitu isipokuwa labda tuweke imani za wachawi kama hao kina Ntilie wanapopewa pawa za kupakulia chakula wakiambiwa ni mkono wa mtoto.
Matayarisho yetu yalitakiwa kutuwezesha sisi kuzalisha na ku supply kile kinachohitajiwa huko nje na sio kinyume kama maandalizi tuliyoachiwa. Utalii bado tunategemea Mbuga za wanyama na historia ya visiwa vyetu na ndipo tulipoweka sera zetu. Zaidi ya hapo, hata JK alipokuwa Nasdaq alishindwa kuelezea vitu tulivyokuwa navyo ambavyo zinaweza kuingia sokoni ila kuiuza nchi kwa wenye kutamani mke!.
Kifupi, mjomba nasikia kichefuchefu mnaposimama hapa na kumsifia Mkapa ambaye kahujumu uchumi wa wa nchi yetu viabaya sana kiasi kwamba zuga lao, JK husingiziakushikwa na shock!.
 
Zitto aanza na Malima

na Asha Bani

ADAM Malima, amekuwa mbunge wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanza kurushiwa makombora ya hoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini aliyesimamishwa, Kabwe Zitto.
Malima alifikwa na kishindo hicho cha Zitto usiku wa kuamkia jana, wakati wa kipindi cha televisheni cha ‘Je, Tutafika?’ Kinachoendeshwa na mwanahabari mkongwe na wa siku nyingi, Makwaia wa Kuhenga.

Akizungumza katika kipindi hicho cha mahojiano, Zitto alieleza kushangazwa kwake na kauli aliyoitoa Malima bungeni wiki iliyopita wakati akichangia hoja binafsi ambayo ilihitimishwa kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kusimamishwa ubunge kwa miezi mitano.

Malima katika mchango wake huo wa Jumanne ya wiki iliyopita, alimsifu Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kwa uamuzi wake kuweka mbele masilahi ya taifa kwa kusaini mkataba wa uchimbaji madini wa Buzwagi na Kampuni ya Barrick Tanzania.

Mbali ya hilo, Malima alimtaka Karamagi kutumia kasi yake hiyo hiyo kusaini mkataba wa uchimbaji wa gesi katika Jimbo lake la Mkuranga iwapo atapatikana mwekezaji mwingine wa aina ya Barrick.

Akizungumza katika kipindi hicho cha televisheni, Zitto alianza kwa kuhoji hoja hiyo ya Malima iwapo aliitoa kwa niaba ya wananchi wa Mkuranga au kwa niaba yake mwenyewe.

Mbunge huyo ambaye sasa amejijengea umaarufu mkubwa tangu asimamishwe na Bunge, alimtaka Malima na Watanzania kutambua kuwa mikataba ya aina hiyo imekuwa na atthari kubwa kwa uchumi wa taifa.

Akitoa mfano, Zitto alieleza kushangazwa kwake na makubaliano yaliyomo katika mkataba mmoja wa kutafuta mafuta katika maeneo mawili ya Tanzania, kule Mkuranga anakotoka Malima na Kigoma, kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Alisema chini ya mikataba hiyo miwili, serikali na wawekezaji hao wanaotafuta mafuta kutoka Ireland wamekubaliana kugawana mapato yatakayotokana na mafuta yatakayopatikana kwa uwiano wa asilimia 30 (zitakazokwenda serikalini) na 70 zitakazochukuliwa na mwekezaji huyo.

Zitto alisema jambo la ajabu ni kwamba kampuni hiyo hiyo ya uwekezaji, imeingia mkataba kama huo wa kutafuta mafuta nchini Kongo, ambako mgawanyo wa mapato yakakayopatikana ni asilimia 45 (kwa serikali) na 55 kwa mwekezaji.

Mbunge huyo kijana alieleza kushangazwa na Malima aliye tayari kuona mikataba mibovu ya namna hii inayoliibia taifa hata kwa kulinganishwa na mataifa mengine jirani ikisainiwa kwa kasi.

Mashambulizi hayo ya Zitto yanakuja siku chache tu baada yeye mwenyewe kuorodhesha majina ya wabunge 10 ambao atahakikisha anawashitaki kwa wapiga kura wao, akiwamo Malima, ambao walikuwa mstari wa mbele kumshambulia bungeni hata kufikia hatua ya Bunge kumsimamisha.

Aidha, Zitto aliwaeleza watazamaji wa televisheni hiyo kuwa, kamati ya kupitia mikataba ya Wizara ya Nishati na Madini ilikataa pendekezo la Karamagi la kusainiwa kwa mkataba wa Buzwagi, kabla waziri huyo hajafikia hatua ya kulazimisha kukubaliwa kwa matakwa yake.

Akijibu hoja hizo za Zitto ambazo zilikuwa na mwelekeo mmoja na zile zilizotolewa na Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Malima alisema mara nyingi wataalamu hulazimika kusaini mikataba katika mazingira magumu.

Pasipo kufafanua kuhusu hoja ya Zitto ya mgawanyo wa mapato katika mikataba hiyo, Malima alisema historia ya nchi za Ulaya kuzikandamiza nchi maskini ndiyo msingi wa kuwapo kwa uonevu wa namna hiyo.

Zitto kwa upande wake alipinga mtazamo huo wa Malima akisema viongozi wetu wamekuwa wakiingia mikataba, wakiweka mbele masilahi yao binafsi na kusahau yale ya wananchi, na akatoa mfano wa mkataba wa Buzwagi.

Alisema kuwa, mbali ya ufisadi kukithiri katika mikataba ya madini, Watanzania tumekuwa na tatizo la kutokuwa na uzalendo katika kuzilinda rasilimali zetu.

Zitto alisema ni jambo la kushangaza kwa serikali na wananchi kukaa kimya wakati mchanga wa madini ukisafirishwa nje ya nchi, kwa madai kuwa hapa nchini hakuna teknolojia ya kutosha ya kupata dhahabu kutoka katika mchanga huo.

Alisema wakati tukiambiwa hivyo, ni ajabu kwamba, vijana wanaoishi maeneo ya migodini hudandia katika malori yanayosafirisha mchanga huo kwenda nje na kuchota vifusi hivyo na kwenda navyo mitoni wanakosafisha na kupata dhahabu wanayoiuza.

“Kwa hilo nashangaa kuona vijana wa Kahama huamua kupanda juu ya makontena hayo wakiwa na vikalai na kuanza kuuchota na kuumwaga chini baada ya hapo wanaenda kuchuja na kutenganisha na kupata dhahabu, sasa hiyo teknolojia ambayo Serikali inadai hatuna ni ipi?” alihoji Zitto.

Naye Mbunge wa Karatu, Dk.Willibrod Slaa (Chadema), ametoa mwezi mmoja kwa serikali kuanza kufuatilia kile alichokiita ubadhirifu ndani ya Benki Kuu (BoT), kabla hajafikia hatua ya kulazimika kuwataja kwa majina wahusika wote katika kashfa hiyo.

Alisema anatarajia kutangaza majina hayo ya vigogo wanaomiliki makampuni ambayo yamekuwa yakifuja fedha za walipa kodi kupitia BoT, Septemba 15 mwaka huu, katika viwanja vya Jangwani.

Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari, Dar es Salaam, aliouitisha ili kutoa maelezo ya ziada kuhusu ubadhirifu ndani ya BoT.

Alisema tuhuma za msingi za ubadhirifu ndani ya BoT, ambazo wananchi wanatakiwa kuzijua ni tuhuma ya benki hiyo kulipa deni la Meremeta Co. Ltd sh bilioni 155 kinyume cha utaratibu.

Dk. Slaa, alisema kwa muda wa miaka minne sasa wabunge wa kambi ya upinzani wamekuwa wakiihoji serikali iwaeleze Meremeta ni mali ya nani na imeandikishwa wapi, mahesabu ya kampuni hiyo yanatolewa kwa nani na taifa linafaidika nini kutokana na kampuni hiyo ambayo imekabidhiwa mgodi wa dhahabu wa Buhemba, mkoani Mara.

Alisema pamoja na kuihoji serikali miaka yote hiyo, imeshindwa kutoa majibu ya kuridhisha, licha ya kusema kampuni hiyo ni kampuni ya Serikali na inaendeshwa na JWTZ kwa lengo la kukisaidia kikosi cha Nyumbu.

Alisema utafiti wake umebaini kwamba Meremeta Co. Ltd, ni kampuni ya serikali, iliandikishwa Uingereza kwa hati ya usajili namba 3424504, kama ilivyotolewa London na Ofisi ya Msajili wa Makampuni, Agosti 19 mwaka 1997.

Oktoba 3 mwaka 1997, kampuni hiyo ilipata ‘hati ya kutimiza masharti namba 32755. Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa Tanzania ina hisa 50 katika kampuni hiyo na hisa nyingine ni za kampuni ya Afrika Kusini iitwayo Triennex Co. Ltd yenye hisa 50 pia.

Alisema uchunguzi wa ziada unaonyesha kampuni mbili zaidi zina hisa moja moja, nazo ni London Law Society Ltd (hisa 1) na London Law Secretarial Service Ltd yenye hisa moja.

“Wananchi hapa kuna utata mkubwa, Meremeta ni ya nani? Meremeta ina hisa ngapi? Kama Meremeta imeandikishwa kama kampuni ya kigeni Tanzania ni kwanini imepewa fedha za walipa kodi wa nchi hii?

Alisema Watanzania lazima wafahamishwe, kampuni hiyo ilipata faida au hasara kiasi gani, na kwamba taarifa ya Waziri wa Nishati na Madini inaeleza kuwa mwaka 2006/7 imepata tani 2.7 za dhahabu.

“Mapato haya yameenda wapi? Utata huu unaelezwa vipi iwapo serikali inaeleza kuwa Kampuni ya Meremeta imefilisiwa na shughuli zake kuchukuliwa na TANGOLD Ltd?” alisema.

Tuhuma ya pili ya ubadhirifu ndani ya BoT kwa mujibu wa utafiti wake ni kuhusu Kampuni ya TANGOLD na kwamba Bunge mara kadhaa limeelezwa kuwa kampuni hiyo ni mali ya serikali kwa asilimia 100.

Hata hivyo alisema utafiti wake umeonyesha ni kampuni ya kigeni iliyoandikishwa kwa mara ya kwanza nchini Mauritius Aprili 8 mwaka 2005, na kupata hati ya kutimiza masharti namba 55661 ya Februari 2000 hapa nchini.

Mbunge huyo alisema Memorandum and Article of Association ya kampuni hiyo haionyeshi popote kuwa ni mali ya serikali wala kuwa na uhusiano na serikali.

Tuhuma ya tatu ni BoT kulipa fedha kwa Kampuni binafsi ya Mwananchi Gold Co. Ltd, alisema kampuni hiyo imeandikishwa nchini kama kampuni binafsi katika mwaka wa fedha wa 2004/2005 na 2006/2007, kampuni hiyo imelipwa na BoT jumla ya dola za Marekani zipatazo 5,512,398.55.

Taarifa za ukaguzi zinaonyesha kuwa hadi Desemba 21, kampuni hiyo ilikuwa imelimbikiza riba ya dola za Marekani 62,847.91, sawa na sh 78,753,459. Hii ni kwa sababu kampuni hiyo ilitakiwa kulipa deni lake ndani ya miezi sita na hadi tarehe hiyo ya ukaguzi, yaani miezi 18 baadaye, ilikuwa haijalipa hata senti moja.

“Isitoshe deni la dola za Marekani 2,807,920, ilionekana kwa taarifa ya ukaguzi kudhaminiwa kwa dhahabu ghafi iliyonunuliwa kwa fedha hizo za mkopo. Yaani Watanzania tumekaangwa kwa mafuta yetu,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kwa mujibu wa taarifa za BRELA, Benki Kuu ina hisa 500 katika kampuni hiyo na NDC ina hisa 375, Kampuni ya Mwananchi Trust Company Ltd ina hisa 1,123 na Chimera Co. Ltd ina hisa 500.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BRELA, kampuni hiyo ilisajiliwa kwa hati namba 44962 ya Desemba 12, 2002 kama kampuni binafsi na kwa maana hiyo hairuhusiwi kuchukua fedha kutoka kwa umma.

Dk. Slaa alisema uchunguzi wake huo ana imani nao, kwa kuwa umejengwa kwa msingi wa nyaraka za BRELA na Idara ya Usalama wa Taifa.

Aliwatahadharisha watu wanaosema nyaraka mbalimbali zinazoibuliwa ni feki, kwani kuna chombo kimoja ndani ya Jeshi la Polisi chenye mamlaka ya kuthibitisha nyaraka hizo ni feki au la.
 
Jamani, mbona magazeti madogo madogo ya Bongo yameripoti kuwa Kikwete alizomewa kule Kahama, yeye na yule Mbunge wao? Mbona magazeti makubwa hayakuliweka hilo hadharani, au hawakuona kuzomewa huko.. au hakukuwepo?
 
Jamani, mbona magazeti madogo madogo ya Bongo yameripoti kuwa Kikwete alizomewa kule Kahama, yeye na yule Mbunge wao? Mbona magazeti makubwa hayakuliweka hilo hadharani, au hawakuona kuzomewa huko.. au hakukuwepo?

Kuna video ya hilo tukio.....?
 
Mahali popote Rais anaposafiri wanarekodi kwenye mikanda ya video n.k tatizo ni je tunaweza kuwa na access nayo? hilo ni swali jingine kabisa.
 
kweli lakini....lakini, hao wanaorekodi ni watu wa chama (ccm) na serikali tu au vyombo binafsi kama chanel 10, itv, star tv nao wanarekodi but they all kiss up to the ccm govt.? dunno
 
Jamani, mbona magazeti madogo madogo ya Bongo yameripoti kuwa Kikwete alizomewa kule Kahama, yeye na yule Mbunge wao? Mbona magazeti makubwa hayakuliweka hilo hadharani, au hawakuona kuzomewa huko.. au hakukuwepo?

Ukishakuwa kizwezwe lazima utazomewa tu, haiwezekani msafara uzuiwe na wewe usionje joto ya jiwe.
 
Habari za kazi,

nawaletea nyaraka hizi. zitasaidia sana katika mjadala.


Zitto,

Ebu nipe muunganisho wa haya na yaliyojadiliwa humu "16netjuly07.doc":

Mheshimiwa Spika, kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi wa Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini.

Katika majibu ya waziri ni wapi alidanganya? Na ni vitu gani alivyoeleza na havimo kwenye mkataba ambao ameusaini?
 
Jamani, mbona magazeti madogo madogo ya Bongo yameripoti kuwa Kikwete alizomewa kule Kahama, yeye na yule Mbunge wao? Mbona magazeti makubwa hayakuliweka hilo hadharani, au hawakuona kuzomewa huko.. au hakukuwepo?

Kuna ripota mmoja yuko Kahama, kanijulisha sasa hivi kwamba mzee alizomewa, lakini wana USALAM wa taifa, wakawaweka sawa waandishi hiyo isitoke. Waliwatarget zaidi wa magazeti yanayofahamika na kuheshimika...vijana wakalamba mshiko wakaandika kilichochujwa.

Anasema mojawapo ya mabango liliandikwa "SURA NZURI HAITUSAIDII..." Mzee akashtuka, na ndiyo maana katika hotuba zake zote amejiepusha kulizungumzia hilo.

Wanaendelea ku-corrupt vyombo vyetu vya habari na kutawala kwa uwongo, gizani.
 
Kuna ripota mmoja yuko Kahama, kanijulisha sasa hivi kwamba mzee alizomewa,
Anasema mojawapo ya mabango liliandikwa "SURA NZURI HAITUSAIDII..." Mzee akashtuka,

..kama yashakuwa haya basi tena!

..togwa linaanza kuchacha sasa!
 
Unajua mimi nawashangaa hawa watu waliomshabikia Kikwete tokea mwanzoni na sasa wanaanza kum-second guess. Swali langu kwao ni nini kilichowafanya wamshabikie namna hiyo? Kwenye nchi za wenzetu watu huangalia rekodi yako, yale uliyokwishayafanya katika nafasi za uongozi ulizowahi kushika na kuamua wakushabikie au la. Sasa sijui rekodi ya Kikwete kabla ya kuukwaa uraisi ilikuwaje....kuna mtu anayeijua?
 
Hii ni choo kabisa. Haijawahi kutokea katika Tanzania kiongozi wa nchi kuzomewa na wananchi tena ambao anafikiri anawatawala. Hebu angalia ni wapi huko yalikotokea – Buzwagi ..... what? bu ... Buzwagi? Anyway wataficha lakini picha zitatoka tu we wape muda wakishamaliza pesa za peremende walizopewa.

Halafu kama umesikia leo ati atajenga barabara zote nchini? Uongo mwingine bwana? Tanzania inasifika kwa kuwa na barabara ambazo hazina lami yaani nchi yetu ina barabara za lami kilometre 6,808 tu ukilinganisha na idadi ya kilometre 72, 083 ambazo hazina lami. Sasa kama ahadi ni ya kuweka lami au vifusi sielewi, au ni barabara mpya zisizokuwa na lami. (Hizo ni figure ambazo zinajulikana)
 
Unajua mimi nawashangaa hawa watu waliomshabikia Kikwete tokea mwanzoni na sasa wanaanza kum-second guess. Swali langu kwao ni nini kilichowafanya wamshabikie namna hiyo? Kwenye nchi za wenzetu watu huangalia rekodi yako, yale uliyokwishayafanya katika nafasi za uongozi ulizowahi kushika na kuamua wakushabikie au la. Sasa sijui rekodi ya Kikwete kabla ya kuukwaa uraisi ilikuwaje....kuna mtu anayeijua?


Hii rekodi ya miaka kama miwili haikutoshi?
 
Nyani Ngabu,
Kusema kweli mimi ni mmoja kati ya wale waliomshabikia JK ktk Uchaguzi uliopita. Lakini kitu kimoja nakuomba uzingatie ni kwamba tulivutiwa na uzuri wa sura, Kijana na mwana harakati kutoka chuo Kikuu. Kisha muhimu zaidi kwangu ni kwamba tuliambiwa huyu JK alikuwa kipenzi kikubwa cha mwalimu isipokuwa Umri wake tu ndio ulikuwa shaka kubwa la mwalimu kama alivyomtolea nje Salim A Salim wakati wa Mwinyi..... Mkombozi amekuja, hata makanisa na misikiti ilitupa salaam.
Kwa hiyo nilitegemea mengi dhidi ya Mkapa yangetokea na hasa hii mikataba ya Uongo!.. Zuga kubwa alokuja nalo JK lilikuwa kuhusu Mali zetu na hasa madini..
Hakuna Mdanganyika hata mmoja ambaye hakuvutiwa na salaam hizo na kama kuna mtu anayeweza kuleta mabadiliko basi mwanajeshi huyu ndio pekee niliona kuwa choice yangu kati ya wagombea...kumbuka pia Mwaikambo na Kombe walikuwa watu wake wa karibu, kwa hiyo nilikiona kisasi against the Mafia!
Well, I was wrong!, mke ndio kisha ingia ndani kinachofuata ni kutafuta mbinu za Kumtalakia. Moja ya mbinu zangu nimeanza uhusiano wa karibu na familia nyingine - Chadema!
 
Back
Top Bottom