Dua
JF-Expert Member
- Nov 14, 2006
- 3,236
- 669
Zitto alipua bomu jingine
2007-08-22 18:52:13
SOURCE: Alasiri
Kweli ukistaajabu ya Musa ............................
2007-08-22 18:52:13
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Siku chache tu baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mhe. Zitto Kabwe kukataliwa hoja yake ya kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge ili ichunguze utata uliopo katika mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, sasa mbunge huyo kijana zaidi amelipua bomu jingine zito kama lilivyo jina lake.
Mhe. Kabwe amelipua bomu hilo jana na kuwaacha watu kibao waliokuwa wakifuatilia maelezo yake kupitia kituo kimoja cha luninga kubaki midomo wazi.
Akizungumza katika kipindi cha `Je Tutafika` ambacho hurushwa na kituo cha Channel Ten na kuongozwa na Bw. Makwaia wa Kuhenga, Mhe. Zitto akasema kwa mara nyingine tena, Serikali imeingia mkataba wa gesi ya Mkuranga anaodai hauna maslahi ya kutosha kwa taifa na wawekezaji wa kampuni moja ya Ireland.
Mhe. Zitto akasema mkataba huo ambao umengiwa na Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Waziri Nazir Karamagi, unaiacha nchi ikiwa na uwezekano wa kunufaika kidogo na raslimali hiyo kulinganisha na wawekezaji hao.
Kwa mujibu wa Mhe. Zitto, Serikali katika mkataba huo itaweza kuambulia asilimia 30 ya faida wakati katika nchi jirani kama pale Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo, mkataba kama huo huiwezesha Serikali ya Rais Kabila kupata asilimia 45.
``Tayari mkataba huo umeshasainiwa hivyo bado taifa litaendelea kukosa maslahi yanayostahili,`` akasema Mhe. Kabwe.
``Kama kampuni hiyo imekubali kule Congo kuchukua asilimia 55 na kuliachia taifa hilo asilimia 45, inakuwaje kwa Tanzania wakatae?,``akahoji Bw. Kabwe.
Katika kipindi hicho, pia alikuwepo Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Adam Malima (CCM), ambaye amesema kuwa lengo la Serikali kuingia mikataba mbalimbali na wawekezaji ni kutaka kuinua uchumi wa nchi na hivyo kunufaisha watu wake, hasa kwa kupitia kodi zitakazolipwa na wawekezaji hao pamoja na mirahaba.
Kipindi hicho pia kilimuhusisha Prof. Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Mhe. Zitto aliibua hoja ya kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza sababu za Waziri Karamagi kusaini mkataba wa Mgodi wa Buzwagi Jijini London, Uingereza na mambo mengine kadhaa aliyodai kuwa yana utata.
Hata hivyo, hoja hiyo ilipigwa kumbo na yeye akaishia kusimamishwa bungeni hadi Januari mwakani kwa la kumsingizia Waziri Karamagi kuwa amedanganya.
SOURCE: Alasiri
Kweli ukistaajabu ya Musa ............................