Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
Sijui hii kitu ina ukweli kiasi gani..... amueni wenyewe!
Unajua kwamba mbowe pia anadaiwa ? tukimuita nae another chenge kutakalika kweli humu ?? well, for that matter, mbowe is/was another chenge as well !
Mbowe alikopa na kesha lipa data ziko wazo dispute sijui why zipo ila tungoje mahakama iamue .Mahakama ni za CCM so nashangaa uoga unakuwawepo wa nini .Mbowe kakopa na kawekeza ndani ya tanzania ajira kawapa walioweza kupata na deni kalipa na madai mengine yako Mahakamani.Chenge kahamisha pesa na kapeleka nje ya Nchi naomba kada uone utofauti wa Mbowe na Chenge .
Dawa ya jino kung'oa na dawa ya deni ni kulipa...
na deni lisilolipika una renegotiate au una settle au ... unalirefinance.. .n.k n.k ... ama?
Una komaa kama Mh Mbowe mpaka kieleweke!
Sijui hii kitu ina ukweli kiasi gani..... amueni wenyewe!
Mimi hii habari haijanikalia vizuri, maana naona imejaa innuendos! Kama hawa wakuu documentary proof wanayo, watuambie basi jina la benki, kiasi cha pesa kamili (sio hizo round figures na abts),lini Mheshimiwa alikopa, alitumia jina gani (yeye binafsi, kampuni yake n.k) na alikopa kwa makusudi gani. Hapo ndio ahukumiwe.
Au ndiyo uandishi wetu? Kila taarifa kama vile tunang'olewa meno!
Unajua kuna wengine wamekaa mkao wa kula tu hapa. Kwa hiyo watatetea hata ambavyo haviwezi kutetewa. Mwizi ni mwizi tu; awe kaiba kuku, chungwa au ng'ombe. Hawa waliokwishaonyesha makucha yao mapema kabisa, wakae pembeni. Na wale walioko madarakani na wamethibitika kuliibia taifa na kufifisha mashirika ya umma wapigwe chini tu.
Siyo rahisi kupata watu wasio na doa, lakini lazima watu wawajibike kwa matendo yao. Siasa ya Tanzania imekuwa ya kila fisadi kukimbilia ili kushibisha zaidi matumbo yao. Ukishajulikana wewe ni fisadi, kaa pembeni kabisa. Kamalizeni na wadeni wako huku ukijua umeshapoteza sifa ya uongozi, labda uhamie sayari nyingine.
Sasa itakuwa kila siku ni kupambana na mafisadi tu. Akiondoka fisadi huyu, anaingia fisadi mwingine and the saga continues. No way!! Kwa wale mlioahidiwa vyeo kwa kuwakingia kifua mafisadi (whether wako serikalini, NGO au kwenye vyama mbadala) kawaambieni kwamba kazi ya utetezi ni ngumu kwa maana huu ni wakati mbaya sana kwao.
Hii inaonyesha jinsi JK na serikali yake ya CCM jinsi walivyo bega kwa bega kutafuna pesa ya walipa kodi kiroho mbaya, na jinsi wasivyo na nia ya kupiga vita UFISADI.