The dark side of business

The dark side of business

Kitu kimoja nilichojifunza adi muda huu ni kwamba,Haina budi kujifunza jinsi ulimwengu wa kiroho unavyofanya kazi.
Naona kama mojawapo ya viumbe tunaoishi katika huu ulimwengu hatuwezi kujitenga na nature,Everthing matter na kila kitu kinachotokea kwenye maisha yetu sio kwa bahat mbaya,we are concern.
Tuwe makini na ishara ambazo ulimwengu(nature)inajaribu kutuambia,hatuwezi kujitenga na nature.
You're very right
 
Kuna mtu anaitwa INFROPRENUER amekuwa akikosoa sana huu Uzi Hadi akafungua Uzi wake kupinga utajiri wa kishirikina, nimemwandikia kisa halisi cha kijana alimaliza form four 2022, akafeli MTIHANI wa Taifa kwa kupata div. Four ya 32,... LAKINI Leo anamiliki bajaj MBILI za abiria MPYAAA, kwamba ana MAONI Gani katika kisa hiki, naona kapotea
 
EPISODE 11
Ilipoishia...

nilikuwa njia panda,sijui niwatoe hao ng'ombe au niache? Nikiacha lazima mambo yangu yataharibika na nitapatwa na majanga lakini pia nikiwatoa harafu ndio iwe kweli ni wadogo zangu,nitapata laana ya mzee kwa kumwaga damu isiyo na hatia......

Sasa tuendelee
Baada ya kuwaza sana,mwisho wa siku nilifanya maamuzi magumu,niliamua nisiwatoe wale ng'ombe lakini sikutaka kumwambia ngurumo wala bijan,nilifanya maamuzi kimya kimya.

Nilijua haya maamuzi mwisho wa siku yatanigharimu,lazima yataibua vita kubwa sana, ukizingatia ngurumo na bijan ni wakongwe kwenye mambo ya kiroho,nilijiona Kama nacheza na moto.

Mara nyingi nikiwa kwenye situation Kama hizi namkumbuka mzee fabi,huyu mzee nilipenda kumwita"wisest person in the world" nilijua tu huyu mzee hatashindwa kunisaidia,hivyo nikapata wazo la kusafiri na kwenda A town,nilitaka nisafiri kimya kimya bila hata kumwambia mzee fabi.

Safari kuelekea chuga
Nilifanya maamuzi ya kukimbilia chuga ili ile siku ya kutoa ng'ombe ikifika,mimi nisiwepo,niwe chuga mafichoni,nilichukua baadhi ya nguo na vitu muhimu,nikaondoka.....

Nilifika A town,moja kwa moja nikamcheki fabi,nikamwambia niko town kwa dharula(fabi alinielekeza anapoishi,safari hii alikuwa anaishi kwake,ametoka pale kwa mzee wake)

Nilifika kwa fabi,tukapiga story za hapa na pale,lakini sikumwambia nimekuja chuga kufanyanini..(baada ya maongezi,nilimwomba fabi aniruhusu nikapumzike,maana nilikuwa nimechoka kimwili na kiakili)

Baada ya kuingia chuga na kuonana na fabi,niliamua kuzima simu ili ngurumo akinitafuta asinipate.

Kesho yake
asubuhi wakati fab anajiandaa kwenda job na mimi nilijiandaa ili tuondoke mwote(kumbuka saa hiyo fabi anafanya kazi palepale kwa mzee wake).

Tulifika dukani kwa mzee fabi,tukapanda juu mpaka kwenye ofisi ya fabi(ofisi yake ni kama hatua kumi kutoka ilipo ofisi ya mzee wake)
Nilikaa pale ofisini kwa fabi ili nimsubiri mzee.....

Baada ya muda kidogo mzee fabi aliingia,nikamfuata ofisini kwake.
Mm: nimekuja tena mzee wangu, changamoto haziishi!

Mzee fabi(alicheka,kisha aliendelea kusema)..isee wewe ni kiboko, changamoto gani hizo zisizo kwisha?

Mm:mzee umenisaidia mambo mengi ila kwa sasa napita kwenye wakati mgumu,hata sijui nifanyaje?(ilibidi nimweleze mzee fabi kila kitu sikumficha,mambo ya giza yote niliyofanya nilimwambia....hapa kwa Mara ya kwanza navunja lile sharti la kwanza la kutunza siri)

Mzee fabi:kijana unapita mahali pagumu(aliongea huku akinyanyuka na kwenda kwenye shelfu ya vitabu)

Mzee fabi:nilikuambia elimu ya maisha ipo kwenye vitabu,tangu nimekupa kile kitabu cha "dark path" je kuna kitabu kingine ulisoma?

Mm:baada ya kusoma kile kitabu sikuwahi kugusa kitabu tena..

Mzee fabi akiwa pale kwenye shelfu,akachomoa tena kitabu kimoja akanipa,akaniambia nenda kasome na hicho.

Mm:mzee wangu nahitaji kinga ya kiroho ili mzee ngurumo na wale viumbe wasiweze kunidhuru,kitabu hakiwezi kunisaidia.

Mzee fabi:akaniuliza,kwenye mchezo wa mbio za farasi ni farasi gani mara zote anashinda?

Mm:kwa kweli sijui

Mzee fabi:farasi anayeshinda mara zote sio mwenye mbio kuliko wote,sio mwenye nguvu kuliko wote,sio mwenye umri mkubwa,sio mwenye umbo kubwa bali ni yule ambaye ni mwepesi kufuata maelekezo ya jockey (rider)

Mzee fabi alimalizia kwa kusema"winning is in following instructions"

Baada ya mzee fabi kunipa huo msemo ilibidi niwe mpole,nifate kile anachoniambia...

Hii ilikuwa ndio ile siku ya kuwatoa wale ng'ombe,ilibidi nitafute chaka moja la bata pale town walau nipoteze mawazo,niliingia milestone bar,pale panasifika sana kwa nyama choma,nilivuta muda pale mpk saa nne usiku,nikarudi kwa fabi.

Niliamka asubuhi na hangover,nikasema ngoja nifungue simu nione kama ngurumo alinitafuta...ile kuwasha simu,meseji zilianza kuingia... kucheki ni meseji za ngurumo.

Sms 1
Kijana nakupigia hupatikani,muda ndio huu,fanya haraka tukutane pale kwa siku ile.

Baada ya lisaa,akatuma tena meseji nyingine.

Sms 2
"kijana umeingia mitini sio,umegoma kuwatoa hao ng'ombe?

Sms 3
Umevunja masharti,nilikuambia mambo haya usimwambie mtu,wewe umemwambia huyo mzee wako,umeikasirisha mizimu.

Sms 4
Umeenda kujificha huko Arusha,unadhani sitajua,kwa usalama wako njoo utoe hao ng'ombe,nakupa siku saba la sivyo kitakacho kupata tusilaumiane.......

hizi meseji za ngurumo zilinitetemesha,nilifikiria nirudi nikaombe msamaha au niendelee kukomaa na msimamo wangu...

Baada ya kusoma zile sms ilibidi nizime tena simu,maana nilihofia anaweza kunipigia na nikakosa cha kusema..baada ya kuwaza sana nilifanya maamuzi ya kurudi kabla hizo siku saba hazijaisha....maana ule mkwara wa ngurumo haukuwa wa kitoto.

Niliingia home usiku mnene
Nimefika home,nikafungua mlango,nikazama ndani...nakuta meza,makochi zimepinduliwa,tv imepigwa chini,vyombo vimesambaa kila mahali,yaani ndani kulikuwa hakutamaniki..nilijiuliza kitu gani kimetokea mle ndani,sikupata jibu....niliingia chumbani nakuta vioo vimepasuliwa,godoro limechanwa chanwa,nguo zimetapakaa kila mahali......

*****************************
Nini kimetokea pale nyumbani kwangu,nani kafanya ule uharibifu...............usikose episode ya mwisho(episode 12)
Mzee Fabi kweli ni wise
 
Utafutaji halali unapokumbana na mizengwe inayotishia mafanikio halali, Akili za watu Huwa zinapinduka.... Na ndivyo Maana kama ni fitina za kimwili, watu hutafutana Hadi kieleweke, na kama ni fitina za kiroho, watu pia hupambana mpaka kieleweke, ni katika kupambana huko baadhi ya watu hujikuta wamejisokota na kuwa watumwa wa MATATIZO mengine mazito zaidi kama mtoa Uzi anavyotufahamisha.
Any way, imagine wewe ndiyo Tanzania, umenunua midege mikubwa, miboeing na miairbus, unataka ufanye biashara halali, unapata WAZO ulaya nitapata soko, halafu KABLA HATA HUJAZINDUA SAFARI YAKO HATA MOJA TU, unasikia umepigwa Pini juu kwa juu hakuna KUPELEKEA ndege yako huko, kwa sababu ndege zako hazina viwango🤔🤔🤔 unajiuliza waliotengeneza miboeing na miairbus ya Ethiopia, Kenya na Emirate waliweka viwango TOFAUTI na KWAKO?? Je ukipata WAZO kwamba washindani wako ndiyo wanaokupiga Pini, utakuwa unakosea?
Ingekuwa ni gemu huria hujaenda kwa Mzee Ngurumo kweli?😂😂😂
 
Maisha yankuwaga magumu pale unakuta kile unachotegemea ghafla kinaenda mlama

Alafu unategemewa.

Unaanza kujiuliza umekosea wapi? Utalalamika wee na kuliiaa wee lakini mambo hayabadiliki, kumbe kuna mzizi umeshawekwa.

Ndicho hicho kinalpelekea watu kufanya maamuzi magumu

Maisha yamekuwaa magumu ila pia watu wamezidi kuwa waovu

Sasa usiombe ukutane na maisha magumu yaliyoletwa kwako na mtu muovu.

Utaliaaaa snaaa hadii kukufuru
 
Kuna mtu anaitwa INFROPRENUER amekuwa akikosoa sana huu Uzi Hadi akafungua Uzi wake kupinga utajiri wa kishirikina, nimemwandikia kisa halisi cha kijana alimaliza form four 2022, akafeli MTIHANI wa Taifa kwa kupata div. Four ya 32,... LAKINI Leo anamiliki bajaj MBILI za abiria MPYAAA, kwamba ana MAONI Gani katika kisa hiki, naona kapotea
Huyu ni mtoto wa early 20s hajui maisha
 
Maisha yankuwaga magumu pale unakuta kile unachotegemea ghafla kinaenda mlama

Alafu unategemewa.

Unaanza kujiuliza umekosea wapi? Utalalamika wee na kuliiaa wee lakini mambo hayabadiliki, kumbe kuna mzizi umeshawekwa.

Ndicho hicho kinalpelekea watu kufanya maamuzi magumu

Maisha yamekuwaa magumu ila pia watu wamezidi kuwa waovu

Sasa usiombe ukutane na maisha magumu yaliyoletwa kwako na mtu muovu.

Utaliaaaa snaaa hadii kukufuru
Umeona eeh? Hapo ndipo utakapoelewa Maana ya msemo wa "Mwanangu kua uyaone"
 
Cha kwanza achana na mke wa mtu

Kama ni mtu muombe Mungu aondoe hio laana maana ulifanya makusudi

Pia mtu yoyote anawza kukutamkia chochote na kikawa kwa hio shetani anajakikisha uone mke wa mtu yule ndie kiunganishi cha mafanikio yako ili uendeelee kuwa nae kitakachofatia ni ufirwe, uulie au ukamatwe ugoni na kama hutakamatwa , gundu litakukaa.
Gundu lipi
 
Back
Top Bottom