Ilipoishia..........
Ile changamoto ya kupoteza fedha iliisha kiivyo nikaendelea na business zangu Kama kawaida,lkn baadaye kidogo iliibuka changamoto nyingine Tena,iliyonitikisa kibiashara........
Sasa tuendelee
Baaba ya mzee fabi kunipa ujanja wa kuweka hela kwenye safe,nilijiona mshindi,Kuna siku ambayo sitakuja kuisahau,siku hiyo nafika dukani simkuti mlinzi,mimi hua nawahi sana kufika ili nionane kwanza na mlinzi ndio mambo mengine yaendelee,sasa siku hiyo sijamkuta,piga simu hapatikani,nikaenda dukani nakuta geti imerudishiwa tu,kuingia ndani naona paa imevunjwa,nikajua jamaa wameingia,isee mapigo ya moyo yalienda mbio,akili ikanijia nicheki ile safe, nayo haipo😭jamaa wameibeba kabisa,dah!hapo ndio nikajua sijui,kwenye ile safe kulikuwa na zaidi ya 10M,hiyo ilikuwa my saddest day tangu nianze biashara,nilitetemeka all the day,nilitafuta yule mlinzi bila mafanikio,hiyo kazi nikawaachia polisi,mpaka leo hajaonekana,sitamsahau yule mzee alinifanyia umafia wa kiwango cha kasusura!wadau sijui nisemeje ila kuna wakati unaweza kujiona the luckiest guy in the world and within a minute ukajiona the most cursed person in the world,ile daladala nayo ilipata ajali(nilikuja kuiuza kwa hasara kama screpa)it was sad time,nilitafuta ushauri kwa watu sikupata msaada wa maana na wengi walinishauri niende kwa wataalamu nikasafishe nyota,niondoe mikosi,nikawapuuza,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi lkn nilijishtukia ikabidi nimtafute kwanza fabi(fabi baada ya kumaliza six,mzee wake alimpeleka kwenda kusoma nje,lkn kipindi hicho alikuwa ameshamaliza yupo chuga kusimamia buss za mzee wake)
Mm:habari fab,za kitambo hiyo,mishe vp?
Fabi:isee mambo safi chalii yangu,niko chuga,nasimamia biashara za mzee,vp ww,upo kwny ajira au umejiajiri?
Mm:nimejiajiri,ajira zinachelewesha kaka(tukacheka then mazungumzo yakaendelea)
Nilimweleza fabi changamoto ninazopitia,so akaniambia usijali,we njoo chuga tutayajenga.
Chuga town
niliingia chuga,mida ya saa mbili usiku,fabi akaniambia nimemweleza mzee wangu changamoto unazopitia,amehaidi atakusaidia,nilifurahi sana,siku hiyo mzee fabi hakuwepo(kila siku ya ijumaa halali nyumbani,analala ofisini) akaingia asubuhi
Mzee fabi:vp kijana mbona umepungua sana?
Mm:kawaida tu mzee wangu si unajua vijana ni kupambana
Nikaendelea kusema
Mm😛ole na kazi maana niliambiwa umelala ofisini.
Mzee fabi:yah,wakati mwingine kazi zinakuwa nyingi huna budi kulala ofisini,anyway kuhusu suala lako,tutakwenda baadaye kuzungumzia ofisini.
Huyu mzee kwny duka lake moja la hardware ni jengo la ghorofa moja kwa juu ndio ameweka ofisi yake.
Nikafika ofisini kwake,yeye akaelekea dukani,mm akanipa funguo nitangulie ofisini,nikaingia ndani,nikaona kuna shelfu kubwa imejaa vitabu,kwa ukutani Kuna picha kubwa ya triangle ndani ya kioo,nikiwa nashangaa shangaa pale,mzee akaingia akaniambia hivyo vitabu vyote nimevisoma,najua vitu vingi kuliko ww ijapokuwa sikusoma kama ninyi akimaanisha(mm n fabi)akaendelea kusema"elimu ya maisha haifundishwi shuleni,ipo katika kusoma vitabu"narudia tena kusema,huyu mzee alikuwa na nondo sio za nchi hii,ameniachia hazina kubwa sana kwny akili yangu,mzee aliongea mengi lkn alinisisitiza niielewe biashara kiroho la sivyo nitakuwa napiga double march time,sikuwa nimemwelewa hasa alimaanisha nn kuhusu kusoma vitabu na hasa alimaanisha vitabu gani,maana Mimi pia ni msomaji mzuri wa vitabu,nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza sema sikutaka kumchimba sana,mzee akainuka kwenye kiti akaenda kwenye shelfu akachomoa kitabu kimoja,akasema nenda kasome hicho,akanipa nauli na 2M ya kuboost mtaji,kwaana niliyumba vibaya,nikamshukuru sana mzee,then nikarudi zangu,kuendelea na haso.
******************************
Hiko kitabu kimebeba Siri gani....tunaelekea patamu,hii si ya kukosa...............