The dark side of business

The dark side of business

Dark side ipo...kwa waaminio hayo...kwa jamii na mataifa yote, kama ilivyo kwa light side. Wengine humu ni waumini sana wa dark side...ila wanaipinga haipo ili tu kuficha siri (uchafu). Duniani njia ni mbili tu either kwa Mungu (Muumba wa vyote) au shetani (baba wa uovu)
 
Ilipoishia...
ghafla yakaanza mapicha picha,mara nikute damu kwny kiti ninachokalia pale ofisini,Mara hirizi,pesa zikawa zinapotea kimazingara,hua siamini uchawi lkn hiki kilichokuwa kinatokea ni uchawi bila chenga,nilifukuza wafanyakazi lkn haikusaidia(nilihisi wananipiga)nilipiga moyo konde lkn changamoto zilizidi to the extent nikaanza kuogopa biashara,kwa kweli nilibaki njia panda,ila Kuna wazo likanijia,juu ya nini cha kufanya....................

Sasa tuendelee
Mawazo ya kuhisi nalogwa yalitawala kichwani mwangu na ni kawaida ya mbongo kuwaza hivyo,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi,nimwelezee hii changamoto ya pesa kupotea kimazingara,nasema kimazingara kwasababu nilifukuza wafanyakazi nikabaki mwenyewe lkn kila nikipiga hesabu mtaji unakata tu,hata ungekuwa wewe ungehisi kuna namna Kuna mchezo unachezewa,ikabidi nimtafute mzee fabi,yeye ni mzoefu kwny biashara na mambo kama hayo itakuwa amepitia.
Mm:habari mzee wangu za siku.
Mzee fabi:salama,nani mwenzangu
Mm:ni Mimi,rafiki yake na fabi(nikajieleza mzee akanikumbuka,nikamweleza changamoto ninayopitia)
Mzee fabi:kijana mambo hayo Ni kawaida sana kwenye biashara,kwani fedha zako hapo dukani hua unaziweka kwenye nini?
Mm:naziweka kwenye draw
Mzee fabi:usiweke fedha kwenye draw ya mbao,nenda mjini kanunue safe.
Mm:mzee ninapitia changamoto za fedha kupotea kimazingara,hiyo safe itanisaidia kweli?(niliuliza kwa mshangao)
Mzee fabi(huku akicheka):kijana nimefanya biashara zaidi ya miaka 30,ninajua mengi,fanya nilichokuambia..
Kwa kweli sikutaka kuuliza sana nikaonekana ni much know,nikashindwa kusaidika.

Nilienda town,nikanunua safe ya kilo 50 nikaanza kuweka fedha zangu humo na u can't believe,sikupoteza tena fedha baada ya kufanyahivyo.

Nilijaribu kutafuta uhusiano wa kupoteza fedha na kuziweka kwny safe then hazipotei,sikupata jibu,kumuuliza mzee nilishindwa,niliogopa kumkera kwa maswali,hii kitu mpk leo bado inanifikirisha,nilijaribu ku Google walau nitaambulia chochote,sikupata kitu,nikajua Kuna elimu nyingine zimefichwa ni wachache wanajua,wadau tupo hapa kujifunza sijui kila kitu so kama kuna mdau hapa jf anajua atumegee kuhusu hiyo elimu,inakuaje uchawi ushindwe kupenya kwny safe?hii ni sayansi ya namna gani?
In short hii changamoto iliisha kiihivyo,nikaendelae na business zangu Kama kawaida,lakini baadaye kidogo ikaibuka changamoto nyingine iliyonitikisa kibiashara..................
******************************
Nilichojifunza kwa mzee fabi ni kwamba kupata changamoto kwny biashara ni kawaida ila tatizo ni namna unavyozitatua,hebu tuone changamoto ya safari hii nitatoka vp..........let's keep diving
 
Ilipoishia..........
Ile changamoto ya kupoteza fedha iliisha kiivyo nikaendelea na business zangu Kama kawaida,lkn baadaye kidogo iliibuka changamoto nyingine Tena,iliyonitikisa kibiashara........

Sasa tuendelee

Baaba ya mzee fabi kunipa ujanja wa kuweka hela kwenye safe,nilijiona mshindi,Kuna siku ambayo sitakuja kuisahau,siku hiyo nafika dukani simkuti mlinzi,mimi hua nawahi sana kufika ili nionane kwanza na mlinzi ndio mambo mengine yaendelee,sasa siku hiyo sijamkuta,piga simu hapatikani,nikaenda dukani nakuta geti imerudishiwa tu,kuingia ndani naona paa imevunjwa,nikajua jamaa wameingia,isee mapigo ya moyo yalienda mbio,akili ikanijia nicheki ile safe, nayo haipo😭jamaa wameibeba kabisa,dah!hapo ndio nikajua sijui,kwenye ile safe kulikuwa na zaidi ya 10M,hiyo ilikuwa my saddest day tangu nianze biashara,nilitetemeka all the day,nilitafuta yule mlinzi bila mafanikio,hiyo kazi nikawaachia polisi,mpaka leo hajaonekana,sitamsahau yule mzee alinifanyia umafia wa kiwango cha kasusura!wadau sijui nisemeje ila kuna wakati unaweza kujiona the luckiest guy in the world and within a minute ukajiona the most cursed person in the world,ile daladala nayo ilipata ajali(nilikuja kuiuza kwa hasara kama screpa)it was sad time,nilitafuta ushauri kwa watu sikupata msaada wa maana na wengi walinishauri niende kwa wataalamu nikasafishe nyota,niondoe mikosi,nikawapuuza,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi lkn nilijishtukia ikabidi nimtafute kwanza fabi(fabi baada ya kumaliza six,mzee wake alimpeleka kwenda kusoma nje,lkn kipindi hicho alikuwa ameshamaliza yupo chuga kusimamia buss za mzee wake)
Mm:habari fab,za kitambo hiyo,mishe vp?
Fabi:isee mambo safi chalii yangu,niko chuga,nasimamia biashara za mzee,vp ww,upo kwny ajira au umejiajiri?
Mm:nimejiajiri,ajira zinachelewesha kaka(tukacheka then mazungumzo yakaendelea)
Nilimweleza fabi changamoto ninazopitia,so akaniambia usijali,we njoo chuga tutayajenga.

Chuga town
niliingia chuga,mida ya saa mbili usiku,fabi akaniambia nimemweleza mzee wangu changamoto unazopitia,amehaidi atakusaidia,nilifurahi sana,siku hiyo mzee fabi hakuwepo(kila siku ya ijumaa halali nyumbani,analala ofisini) akaingia asubuhi

Mzee fabi:vp kijana mbona umepungua sana?
Mm:kawaida tu mzee wangu si unajua vijana ni kupambana
Nikaendelea kusema
Mm😛ole na kazi maana niliambiwa umelala ofisini.
Mzee fabi:yah,wakati mwingine kazi zinakuwa nyingi huna budi kulala ofisini,anyway kuhusu suala lako,tutakwenda baadaye kuzungumzia ofisini.

Huyu mzee kwny duka lake moja la hardware ni jengo la ghorofa moja kwa juu ndio ameweka ofisi yake.
Nikafika ofisini kwake,yeye akaelekea dukani,mm akanipa funguo nitangulie ofisini,nikaingia ndani,nikaona kuna shelfu kubwa imejaa vitabu,kwa ukutani Kuna picha kubwa ya triangle ndani ya kioo,nikiwa nashangaa shangaa pale,mzee akaingia akaniambia hivyo vitabu vyote nimevisoma,najua vitu vingi kuliko ww ijapokuwa sikusoma kama ninyi akimaanisha(mm n fabi)akaendelea kusema"elimu ya maisha haifundishwi shuleni,ipo katika kusoma vitabu"narudia tena kusema,huyu mzee alikuwa na nondo sio za nchi hii,ameniachia hazina kubwa sana kwny akili yangu,mzee aliongea mengi lkn alinisisitiza niielewe biashara kiroho la sivyo nitakuwa napiga double march time,sikuwa nimemwelewa hasa alimaanisha nn kuhusu kusoma vitabu na hasa alimaanisha vitabu gani,maana Mimi pia ni msomaji mzuri wa vitabu,nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza sema sikutaka kumchimba sana,mzee akainuka kwenye kiti akaenda kwenye shelfu akachomoa kitabu kimoja,akasema nenda kasome hicho,akanipa nauli na 2M ya kuboost mtaji,kwaana niliyumba vibaya,nikamshukuru sana mzee,then nikarudi zangu,kuendelea na haso.
******************************
Hiko kitabu kimebeba Siri gani....tunaelekea patamu,hii si ya kukosa...............
 
Tanzanian Dream nakuomba sana tena sana hicho kitabu iwe siri ya wachache tu,
Tanzanian Dream wewe shusha nondo, Iko hivi kama kitu ni siri ya wachache kitabaki kuwa siri ya wachache hata kama kitawekwa hadharani, Namaanisha utakisoma na hauta elewa.
kama mtu ni muda wake wa kuelewa ataelewa tu na kama mtu sio muda wake wa kuelewa hawezi elewa ata umuwekee vitabu 100.
Ndio maana unaona kuna watu wanampinga mleta mada na kuna wengine wanam - support anachosema.
Kwahiyo bwana Shy land usiwe na wasiwasi wacha mleta mada afunguke, Kwani hujawahi sikia msemo unasema wanamasikio lakini hawasikii na wana macho lakini hawaoni?
 
Back
Top Bottom