Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Karim
Jee toyota ndiyo huyu ambae alikuwa waziri enzi za mwalimu? Sasa watoto wake ndiyo wanaendeleza biasharaHizo ni imani na matambiko tu hayana uhusiano wowote na mafanikio yao
Na wewe kachinje mbuzi ma utoe kafara uone kama utatoboa?
Hao jamaa wana mitaji na management nzuri na experience ya biashara
Familia na koo za Kihindi hapa Afrika Mashariki ni za muda mrefu, wanafanyabiashara tangu Tanganyika koloni la Uingereza
Ndio maana mikoa kadhaa Tanzania kuna mitaa inaitwa Uhindini jiulize kwa nini.
Kuna hii point aliwahi kuizungumza Mzee wa kupambania kwenye uzi mmoja ina ukweli sana:
Koo nyingi za Kihindi zilohama kutoka India miaka ya zamani na kwenda maeneo mmbalimbali kama East Africa, S.A, Canada, Uingereza n.k zilikuwa za wafanyabiashara
Mfano ni familia ya Karimjee hii ndiyo familia ya kwanza kuingiza na kuuza magari ya brand ya Toyota hapa Tanzania mwaka 1965. Mpaka leo kampuni ya Toyota wameweka hilo kwenye kumbukumbu zao. Karimjee waliingia East Africa mwaka 1825
Familia ya akina Gulam Dewji baba yake na Mo ni hivyohivyo ni wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi waliokuja East Africa kama wafanyabiashara mwanzoni mwa miaka ya 1800s
Ndivyo na Wahindi waliohamia mataifa mengine. Kwa hiyo ni familia ambazo zina historia ya pesa na vibunda tangu miaka hiyo. Hebu imagine tangu 1800s watu wanapiga business!
Kwa hiyo ni mwendo wa kurithishana vibunda. Na koo zinakua kuoa na kuolewa na kupeana mitaji.
Ndio maana unaona hawa Wahindi wachache waliopo hapa wanaonekana wako vizuri financially