inaendelea
Ilipoishia......
Ngurumo alinipa maelekezo ya namna ya kuwatoa wale ng'ombe na jinsi wale viumbe watakavyo sababisha ajali na baada ya hapo watakuwa ni mali yangu,watanifata kila mahali na nitakuwa na uwezo wa kuwatuma popote unapotaka.............
Je hao viumbe ni akina nani? na je nitafanikiwa kuwatoa hao ng'ombe.......
Sasa tuendelee
Baada ya ngurumo kunipa maelekezo ya namna ya kuwatoa wale ng'ombe,ilinifikirisha sana,akili yangu ilienda mbali kidogo,ikabidi nimuulize,
"Hiyo ajali ikitokea huyo dereva atanusurika?
Ngurumo:Kama ana kinga anaweza kupona lkn kama hana kinga ni lazima atakufa
"Hii iliniogopesha sana"
Mm:kwani hakuna njia nyingine?maana naona Kama tunaenda kuua mtu asiye na hatia!
Ngurumo:kijana mbona una huruma sana,utajiri utauweza?....hao ng'ombe hawatolewi kwa kuchinjwa,wanatolewa kwa ajali hakuna njia nyingine(alisisitiza mzee ngurumo)
Baadaye kidogo akaniambia wewe hofu yako ni dereva kufa,basi usijali,nitaangalia namna ya kumkinga lkn hiyo ni gharama nyingine,itabidi ulipie...
Ajali nyingi ni za mchongo
Mara nyingi ajali ikitokea tunaishia kumlaumu dereva lkn nyuma ya pazia,ajali nyingi ni platform ya kutolea kafara,ukipanda chombo chochote cha moto,iwe ni basi,meli,treni,ndege hata iwe bodaboda usidharau,fanya sala na ukishuka ushukuru....
Ile siku ikafika
Mzee ngurumo alinipeleka kwa mtu wake ambaye alikuwa ni mfugaji,kwa kuwa alikuwa tayari ameshampanga,tulimkuta anatusubiri
Ngurumo:unaona jinsi ng'ombe wake walivyo wakubwa,ndio maana nikakuleta huku.
Nililipa 1.6M,kila ng'ombe alinicost laki nane,dereva akaja,tukawapakia.
Safari ikaanza
Mimi na mzee ngurumo tulipanda pikipiki,tukatangulia mbele,jamaa anatufata kwa nyuma,moyoni niliwaza kile kinachokwenda kutokea......tulitembea Kama dk 15 hv, ngurumo akatoa kifuko mfukoni kilichokua na unga,tulipofika njia panda akamwaga ule unga na Kuna maneno akayasema...,ilitokea Lori hz tipper za mchanga iko moto vibaya ikaigonga ile canter ubavuni kwa nyuma,kwasababu ya speed ile canter ilienda chini,lile lori likaingia kwny mtaro.
Wakati huo sisi tumepark pikipiki tunaangalia ile ajali,nikawa nawaza kwa mzinga ule sidhani Kama Kuna mtu atatoka salama,nilianza kujiskia vibaya.......
Ngurumo:twende tukacheki Kama wale ng'ombe wamekufa au la!
Watu walikuwa wameshajaa eneo la tukio,mzee ngurumo alienda moja kwa moja kutazama ng'ombe,Mimi nilienda kucheki wale madereva,yule wa Lori alikuwa mzima amekaa chini,yule aliyebeba ng'ombe walimtoa kwny gari wamemlaza chini,dah!nikasema kimoyo moyo"huyu atakuwa ameshavuta.....
Ghafla mzee ngurumo akanishika begani,akaniambia kijana" deal done"(huku akitabasamu)
Mm:mbona sasa yule dereva amekufa?(nilimuuliza kwa huzuni)
Ngurumo:yule hajafa amezimia tu.
Tulifanya mchakato wa kuwapeleka hospitali na kweli yule bwn alikuwa hajafa.
Baadaye kidogo tulikodi gari nyingine,tukabeba wale ng'ombe,tukaenda kuwazika.
Ngurumo:Sasa kila kitu kipo sawa..naomba urudi nyumbani ikajiandae maana usiku wa leo(ilikuwa alhamisi)wale viumbe watakuja,ila naomba uzingatie haya masharti matatu 1),usimwambie mtu yoyote mambo haya 2)usimguse mwanamke kwa miezi sita na baada ya hapo itakubidi uoe maana zinaa na utajiri havipatani na 3)kila siku ya alhamisi usiku,utakuwa unachoma udi,dukani na nyumbani kwako(mzee ngurumo alimaliza kutoa maelekezo)
Haya masharti sikuyaona Kama yana ugumu wowote ila lile sharti la pili kwa sehemu niliona ni kipengele 😀
Nikarudi home
Nimefika home nimechoka,nikaweka mazingira vizuri kwa ajili ya ugeni wa vile viumbe,nikaingia gheto(bed room)nikachoma udi za kutosha,kwasababu harufu ilikuwa kali ikabidi nitoke nikalale sitting room,nilipitiwa na usingizi mzito,niliamshwa na mlio wa simu,kucheki nani ananipigia,kumbe ni mtu wangu wa dukani,nilimpa maelekezo wakati wa kufunga achome udi za kutosha,baada ya Kama nusu saa aka nitext"boss nimeshachoma na duka tumeshafunga"
Nikacheki saa,ni saa mbili na nusu usiku,ghafla nikaskia mlango unagongwa..........mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio,nikajisemea ndio wale viumbe wamekuja...nikawa najiuliza hivi viumbe zipoje,sura zao zipoje?nilijiuliza bila majibu....mlango ulizidi kugongwa....nilisogea pale mlangoni huku natetemeka..........................
******************************
Nilitamani nimpigie mzee ngurumo walau anipe neno moja la kunitia moyo maana nilihisi kuishiwa nguvu......nini kitajiri baada ya kufungua mlango?...........stay there!