Duh...!, Mkuu
Kiranga, kwanza kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko hili kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
Hawa jamaa ni media ya mabeberu, jarida la the Economist, walimsakama sana Magufuli, Baba wa watu alipotwaliwa wakashangilia na kuanza vizuri na Samia kwa kumsifu sana
Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri
Sasa wamemgeuka!
Maadam na sisi Tanzania tuna waandishi, na wana uwezo na Kiingereza kilichonyooka kuweza kuandikia the Economist, kama hiki walichoandika kumhusu Rais Samia ni ukweli, tunyamaze, tuchutame, lakini kama ni uongo, tukanushe!
Enzi za Magufuli, walianza hivi hivi na mauongo yao, nikawashauri serikali yetu tuukanushe uongo huo, uongo unapo rudiwa rudiwa bila kukanushwa unageuka ukweli!
Mfano mzuri wa mauongo ya The Economist
The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja
Nikawashauri serikali yetu, tuyakanushe mauongo haya!, nikapuuzwa!, wakapuuza hawakukanusha!
Uchaguzi wa 2020, Watanzania wakawataa wapinzani, wakaichagua CCM, ni wapinzani wawili tuu ndio waliingia bungeni, hivyo ikatikea kweli Bunge likawa ni bunge la chama kimoja na upinzani ukafutika kiukweli!.
P