Hiyo article ya Economist haijasema chochote kipya.
Funny thing, kwenye hii hii nchi ambayo tunaona inadhiki sana, minorities (wahindi, waarabu, wasomali, wazungu) wanaonekana mambo yao yanawanyookea na si rahisi kusikia wanalalamika ovyo kila saa. Hata wageni wanatoka nchi fukara na kuja kuneemeka hapa. Kuna kitu gani hawa watu wanaona/wanafanya sisi waafrika weusi hatuwezi? Kwanini ni sisi tu waafrika weusi tunalalamika Kikwete, CCM, serikali, viongozi, Mungu,..nk? Mpaka hata wasomi. Aibu.
Jibu, hatutengenezi vitu vya thamani. Hao minorities hapo juu wanajishugulisha na uzalishaji mali, biashara na utoaji huduma kwa ufanisi. Wengi wetu sisi waafrika weusi kazi ni utegemezi: kutegemea ajira, Rais, CCM, serikali, miujiza, ushirikina, neema za Mungu na misaada.
Sasa tuanze kuzalisha mali, kufanya biashara na kutoa huduma kwa ufanisi. Tuuze kwenye soko ndani na nje ndo "tutatoka". Mapharmasia wetu kweli hawawezi kutengeneza dawa yoyote ya kisasa? Ma-engineer wetu kweli hawawezi kutengeneza mashine yoyote? Au kifaa chochote cha umeme. Nini kinawatoa wahindi na wachina?
Haya mambo ya kulalamika uongozi mbovu hayana msingi. Nchi kama Italy inaendeshwa kimafia na kifisadi kama sisi lakini kwasababu watu wa kawaida wanatengeneza vitu na kuuza, mambo yao ni mazuri.
Miafrika mieusi mienzangu, tujishugulishe na tuzalishe. Tukiweza hayo mengine yatafuata.