Hiyo sababu ya saba, Watanzania, ndio kiini cha tatizo. Si CCM, si Kikwete, si serikali.
ECONOMIST wametutandika fimbo wote, kwamba Watanzania ni watu slow, tusio na mwendo wa kwenda mbele, hatuna "dynamism." Hatuna ujuzi, tumezidiwa na Wakenya na Waganda, tunawaogopa. Tuko slow wanasema mpaka tumeshindwa hata kutumia hela tulizoomba, $ 2.4bil. Ukweli si kejeli, ashakum si matusi.
Kikwete sio dawa, sio ugonjwa. Miundombinu yetu ya reli na bandari imechoka mbaya, "rickety," wanasema. Reli, bandari, ndege, barabara, magari ya usafirishaji yalianza kuchoka toka enzi Nuhu anaibuka kutoka kwenye Gharika ya Kwanza ya Dunia. Kikwete kakikuta hiki kifafa cha miundombinu, na hana dawa.
Wananchi wa Tanzania, sio Kikwete, wote tumejaa uvivu, uchovu, ukilaza, uzembe wa mawazo na kazi. Jumatatu unaingia saa sita, jana ulilala msibani ukihani marehemu Mzee Dau, baba wa shangazi yake mke mdogo wa jirani yako. Jummanne inabidi uombe udhuru kumpeleka Pili hospitali. Jumatano unaenda kwenye mazishi, haupo kazini nusu siku. Alhamisi unaondoka mapema kuwahi lifti ya Mama Tarimo maana ukiikosa hii basi usafiri jioni udhia mtupu, isitoshe yabidi uwahi kwenye send off. Ijumaa unatakiwa harusini, ulitoa mchango. Wiki ijayo huna udhuru, utajitahidi kutulia kazini unasoma "Acha Umbea" na "Alasiri," ukichoka unachomoka kidogo kutafuta supu ya utumbo, ukirudi ni kusogoa na kunywa chai na maandazi. Nusu ya maisha yako ya kazi ni livu, na mshahara utapata wote. Sio wewe tu utapata mshahara mzima, na marehemu Mzee Dau nae atalipwa.
Sasa kama hapo tatizo ni Kikwete basi waandishi wa makala hiyo wametutusi wote maana wamesema Mrisho atachaguliwa tena, wameongea kwa ukomo wa uhakika, atachaguliwa tena, na itakuwa ni kwa kishindo cha mmomonyoko wa ardhi ya uchaguzi, landslide. Kwa nini, kwa sababu Chama cha Mapinduzi kimewachota watu akili, wanasema kimetukuka katika longolongo dufu, "ponderous propaganda."
Na wametuasa kusikiliza wenyenchi ndani ya chama kutaka kuwapeleka tena wananchi kwenye Ujamaa kwa kigezo cha mporomoko wa ubepari duniani. Wachambuzi wa The Econonimist wanasema genda ulole.
Asante Dillunga kwa maelezo ambayo ni ukweli mtupu.
Bishanga nashukuru pia kwa maelezo positive....Ila hizi siasa ni mambo ya mijini na ndio maana politics za JK kushinda zitaendelea tuu.
Nimeamua nigusie posting zote mbili yani hii hapo juu pamoja na ya Bishanga...Ni postings mbili zenye jumbe ambazo zinaufanya mjadala huu kuwa wa maana sana kwa Watanzania especially hao wenye kutuongoza na wenye nafasi za kuchangia kwenye jamii kwa vitendo.
Dillunga uliyosema ni kweli lakini umezungumzia wananchi wenye kufanya kazi maofisini,na ni wazi umezungumzia tatizo hilo kama ni utamaduni wa mtanzania,na hivyo basi mtanzania kama mtanzania bila ya kujali kama ni wa ofisini huko mijini ama wakulima huko vijijini,wote tayari wako kundi moja.
Kwa upande mwingine Bishanga ametolea mifano mizuri sana tu based on points zilizoko kwenye makala hii....Kwamba tunaweza tukawekeza kwenye kilimo cha irrigation,na akatolea mfano wa bonde la mto Rufiji,tulishasema sana na wengi waliotutangulia walishasema sana,bila Kilimo hatwendi mahali.
Kilimo pekee ndio kinachoweza kumwondoa hata asiye na elimu kutoka kwenye umasikini na baada ya hapo akaweza kusomesha watoto na hence maendeleo
Maendeleo na elimu vinategemeana lakini utajiri unaweza kuleta vyote kama ukitumiwa vizuri.
Angalia ukweli mtupu kuhusu sisi kuwa na "Tiny middle class" kwenye East African population...Huku tukiwa na tatizo kama hilo bado tunatembeza bakuli,halafu kwasababu ya ukweli kwamba tuna viongozi ambao wanatoa maamuzi kwa niaba yetu wananchi,huwa ninashangazwa pale tunapotumia dhana ile ile ya kuwalaumu wananchi kwa kujifananisha na viongozi kwamba hatuna cha kufanya simply kwasababu wote sisi mpaka Kikwete ni wavivu,na umetoa mifano ya maofisini ya wananchi sambamba na Kikwete ambaye kiukweli naye hakai ofisini...Yani ukweli mtupu,ila nini cha kufanya?
Tuatauzungumzia vipi uchumi wa Tanzania bila kuhusisha kilimo? Kama mawazo yetu yamebakia kwenye kazi za maofisini na uongozi na siasa,vitu ambavyo hata hivyo hupatikana kimatabaka,je siyo sababu kubwa kuwa Taifa limekwama? Hakuna nidhamu ya kazi kwasababu hata taratibu za uajiri ni za kujuana nk.
Nchi nyingi sana ziliwapatia wananchi wao maendeleo na elimu kwa kuzitumia rasilimali zake,kwa mfano hapa USA ni miji mingi sana ilijengwa mara baada ya ugunduzi wa either madini ya shaba,gold,mafuta na hata makaa ya mawe,chumvi nk,wananchi ambao hata hawakusoma walipata maendeleo na kuwasomesha wanao na kutengeneza jamii ya na kuboresha miundo yao ya kijamii,nimetembelea miji ambayo ilijengwa na kilimo na bado Kilimo ndio kinaiendesha,pia miji ambayo rasilimali walizonazo zimeijenga na baada ya hapo kujijengea misingi ambayo ndiyo baadaye unaona kuna wasomi na wafanyabiashara wakubwa wanaoibuka na kuuendeleza utajiri ule ama kuinvest smartly...Mambo hayaanzii juu,huanzia chini,huu ni ukweli usioipingika.
Na hivyo basi kama alivyosema Bishanga na pia kama walivyosema watanzania wengine,we can kama tukibadilisha mentality yetu....Alipotupitisha mwalimu ni tofauti na walikopita wananchi wa mataifa yetu ya jirani,lakini mimi naamini kama tungepata viongozi wa maana,basi tungekuwa matawi ya juu,hatuwezi kabisa kuwa na utajiri wote tulio nao halafu bado turidhike na kiongozi mwenye kusafiri kila kukicha kuomba eti kwasababu watanzania ni wavivu wanakunywa supu tu,huo ni utamaduni wa watanzani walio wengi wenye kukaa mijini ambako hawakuzoe kuwa na kazi na hata kazi zenyewe pia hazitolewi kimaadili ya kazi nk. Na hao ni asilimia ndogo sana ya watanzani na ndio hao tunaoendelea kuwachambua kuanzia kwenye the ecomomist hadi hapa JF
Mkuu Dillunga sijui umetokea maeneno gani,lakini nakuhakikishia hao watanzania unaowaona huko maofisini wanakokunywa supu ya utumbo,maandazi na chai,huko vijijini kwenye asilimia kubwa ya watanzania si hivyo dugu yangu....Kama kweli kilimo kikipewa kipaumbele basi ungekuja na stori ya jinsi mkulima huyu ama yule alivyofanya bidii na kupata mazo bora nk.
Product karibia zote zinazotumika kwa wingi zimetokea mashambani,hata hapa USA, na miji mingi tu,hao wanaowaita blue color workers,hawajasoma,ila wako well trained kwenye shughuli flani flani za maendeleo ya kiuchumi...Something minor as packaging kinatukwamisha watanzania. Unakuta tuna uwezo wa ku export product flani lets say food product,packaging tu ambayo hata mtoto aliyemaliza lasaba anaweza kuwa trained na kurun machine,lakini hakuna mipango wala taratibu za kuelekea huko,badala yake eti tuendelee kuomba hadi hapo tutakapotengemaa,sasa sijui kutengemaa kwa namna gani maana si wanasema hata misaada mingine hatutumii? Sasa kama ni hivyo si ina maana mafisadi wanatufundisha kuitumia? Watanzania wenye kuombewa misaada ni wachache na ndio wanaopiga kura na kunywa chai na maandazi,lakini si wa vijijini....Politics hovyo sanaa!
Kuna watu wanashika jembe na wana uchungu vibaya mnoo! Hawana nafasi kwenye siasa zetu maana maisha yao hayaandikwi wala hayagusiwi kwenye mijadala ya macritic kama sisi.
Cha msingi ni sisi kuanza kufikiria kama watanzania wenye kuelewa tulikotoka na kujuwa kuwa hatuwezi kuendelea kama tutataka kujipatia maendeleo kwa kujaribu kujenga middle class bila ya kuzingatia kuwa majority ya watanzania wako rural areas...Na huku siasa zikiwa mijini huko kwenye supu na nyama choma na bia tukisubiri next campaign.
Mkuu kwa kumalizia,ni kweli uliyoyasema hapo juu lakini hukuwataja wakulima na watu wa vijijini ambapo kama kweli tunataka tujishindanishe na majirani zetu,basi ni lazima wawe included kwenye jedwali.
Bishanga pia nashukuru kwa maneno mazuri yenye kutia moyo ambayo yanaweka mtizamo mwingine chanya wakati mjadala huu ukiendelea.
Tumekikimbia kilimo kila mtu ni mjini na siasa,kweli hapo tulitegemea nini?