Hiyo sababu ya saba, Watanzania, ndio kiini cha tatizo. Si CCM, si Kikwete, si serikali.
ECONOMIST wametutandika fimbo wote, kwamba Watanzania ni watu slow, tusio na mwendo wa kwenda mbele, hatuna "dynamism." Hatuna ujuzi, tumezidiwa na Wakenya na Waganda, tunawaogopa. Tuko slow wanasema mpaka tumeshindwa hata kutumia hela tulizoomba, $ 2.4bil. Ukweli si kejeli, ashakum si matusi.
Labda ilikuwa muhimu kwao kutambua kuwa haiwezekani watu zaidi ya milioni 40 kuwa viongozi,hence the need for a government.Failure ya government si lazima itafisiriwe kuwa failure ya wananchi.Tunapozungumiza serikali,kwa maana ya government tunamaanisha bunge,mahakama na executive ( ambayo kwa kiswahili ni serikali pia).Failure ya vyombo hivyo vinavyopaswa kuwatumikia wananchi (kwa vile haiwezekani kila Mtanzania kuwa ndani ya serikali) haiwezi kutafsiriwa directly kuwa ni failure ya kila Mtanzania,unless tunazungumzia makosa katika kuiweka madarakani serikali iliyopo sasa.
Kikwete sio dawa, sio ugonjwa.
Aliahidi kuwa dawa,wapigakura wakamwamini na kumkabidhi urais 2005.Ni ugonjwa kwa vile hawezi kujiepusha na kushindwa kwa Tanzania kufika inapostahili kuwa.Kwani dawa ni nini?Si ni kitu chochote kinachoweza kutibu?Lakini dawa pia inaweza kuwa feki,and for that matter,nadhani JK ni dawa ila ni dawa feki.Au pengine ni dawa iliyoisha muda wa matumizi.
Miundombinu yetu ya reli na bandari imechoka mbaya, "rickety," wanasema. Reli, bandari, ndege, barabara, magari ya usafirishaji yalianza kuchoka toka enzi Nuhu anaibuka kutoka kwenye Gharika ya Kwanza ya Dunia.
Hivyo vyote havikuzaliwa namna hiyo,vimefikishwa katika hali hiyo na watu flani.JK alipokuwa anataka tumpe urais hakuwa blind,na aliona hiyo miundombinu "rickety",lakini bado aliwaaminisha Watanzania kuwa atarekebisha mambo.
Kikwete kakikuta hiki kifafa cha miundombinu, na hana dawa.
Unaposema alikikuta,it sound as if JK alikuwa mjamzito kisha akazaa mtoto mwenye kifafa na asijue kama amtelekeze au amvumilie.Huyu ni Mtanzania mwenzetu anayefahamu vema mazingira ya nchi yetu.Si kwamba aliamka akawa rais,NO.Alizunguka takriban kila kona ya TZ na kuona namna gani hali ilivyo.Alikuwa akifahamu fika jukumu zito lilo mbele yake.Kama alikuwa anajua hana dawa,je aliomba urais ili iweje?I hope sio kupata fursa ya kuingia kwenye kumbukumbu za maisha yake kuwa "you see,na mie nilishawahi kuwa rais"...au kuendeleza ligi dhidi ya Vasco Da Gama
Wananchi wa Tanzania, sio Kikwete, wote tumejaa uvivu, uchovu, ukilaza, uzembe wa mawazo na kazi. Jumatatu unaingia saa sita, jana ulilala msibani ukihani marehemu Mzee Dau, baba wa shangazi yake mke mdogo wa jirani yako. Jummanne inabidi uombe udhuru kumpeleka Pili hospitali. Jumatano unaenda kwenye mazishi, haupo kazini nusu siku. Alhamisi unaondoka mapema kuwahi lifti ya Mama Tarimo maana ukiikosa hii basi usafiri jioni udhia mtupu, isitoshe yabidi uwahi kwenye send off. Ijumaa unatakiwa harusini, ulitoa mchango. Wiki ijayo huna udhuru, utajitahidi kutulia kazini unasoma "Acha Umbea" na "Alasiri," ukichoka unachomoka kidogo kutafuta supu ya utumbo, ukirudi ni kusogoa na kunywa chai na maandazi. Nusu ya maisha yako ya kazi ni livu, na mshahara utapata wote. Sio wewe tu utapata mshahara mzima, na marehemu Mzee Dau nae atalipwa.
Hayo ni matusi ya nguoni kwa wazee wetu kule vijijini wanaoshinda juani kutwa nzima wakipinda mgongo kujipatia chakula,na ziada ya kupeleka vyama vya ushirika only for vyama hivyo kuwageuza wazee hao kuwa mtaji wao.I really hate (sorry I have to use this strong word) watu wanaopenda overgeneralization.Hivi Watanzania wangekuwa wavivu katika namna unayotaka kutuaminisha tungepata uhuru?Umeshawahi kuongea na wazee wetu kuhusu namna uhuru ulivyopiganiwa (forget about the sketches you read in history books).Uhuru ulivyotafutwa huko Maneromango,Kilwa Kipatimu,Mahenge,Ujiji,nk unaweza kuwa tofauti sana na hadithi unazosoma kwenye vitabu vya historia.Huko ndiko mapambano kati ya Mtanganyika namkoloni took place.
By the way,hata kama hiyo verdict yako kuhusu uzembe,etc ingekuwa sahihi,iweje tena useme JK sio miongoni mwa wenye tabia hiyo?Au Wakwere sio Watanzania?I hope you meant "Wananchi wa Tanzania,NA SIO JK PEKEE,tumejaa...."
Na mfano wako wa uvivu kwa vile mtu anaingia kazini saa tatu hauwatendei haki mamilioni ya Watanzania wanaopenda kuwa waajiriwa lakini wamekuwa jobless kutokana na SAPs na mipangilio ingine ya ajabuajabu.Nenda vijijini ukafanye huo utafiti wako kuthibitisha iwapo kuna wakulima wanaongia shambani saa sita.Na hiyo jumanne,mkulima hana wa kumwomba udhuru zaidi ya shamba na jembe lake.Ana anajua akifanya hivyo,hana pa kukimbilia.Ni jembe na shamba masaa 12 ya siku,wiki 52 za mwaka.Again mfano wako wa mazishi ya jumatano ni wa mfanyakazi as if Watanzani wote ni waajiriwa.
Kaka,sie tuliotoka familia za wakulima tunajua kuwa huendi shamba kwa lifti,unless kuwe na punda au something like that au ubahatike kupata lifti ya baiskeli.Na hizo send off unazozungumzia ni kwa watu wa mijini wanaojiweza.Hayo magazeti unayozungumzia ni kwa ajili ya wachache wenye kumudu "kupoteza fedha kwenye makaratasi" (utaulizwa kijijini,hivi hilo gazeti ukishasoma utashiba?hizo shs 400 za gazeti zinaweza kununua japo kipakti cha chumvi au fungu la bamia.)
Nusu ya maisha ya Mtanzania unayepaswa kumzungumzia sio kazi,bali ulalahoi huko mashambani.Hao wenye kazi ni asilimia ngapia ya Watanzania?
Sasa kama hapo tatizo ni Kikwete basi waandishi wa makala hiyo wametutusi wote maana wamesema Mrisho atachaguliwa tena, wameongea kwa ukomo wa uhakika, atachaguliwa tena, na itakuwa ni kwa kishindo cha mmomonyoko wa ardhi ya uchaguzi, landslide. Kwa nini, kwa sababu Chama cha Mapinduzi kimewachota watu akili, wanasema kimetukuka katika longolongo dufu, "ponderous propaganda."
Hapa sina la kuongeza.Nakuunga mkono asilimia 100.Kikwete sio tu sehemu ya tatizo bali pia ni tatizo.Kwa Watanzania,tatizo ni uoga (some claim usio na sababu za msingi) kuwa angalau they know something about CCM (mabaya ni mengi kuliko mazuri,but that's not a point I'm trying to make: put it this way:angalau hao CCM tunawajua...hawa CUF hata hawaeleweki maana mara leo Hamad Rashid ana-sound as if angependa Rostam asiitwe fisadi,kesho Lipumba anaropoka lile....mara Zitto tulomdhani shujaa wetu nae anataka tununue "cheni bandia tuliyoporwa na majambazi kisha wanatuletea tuninunue tena" (isomeke MITAMBO YA DOWANS)....and lots of uncertainties.Ni rahisi kulaumu lakini tukumbuke kuwa hapa hatuzungumzii kuchora katuni kwa penseli ambapo ukikosea unafuta.Kuongoza nchi sio suala la trial and error.It's sort of a catch-22 situation we are in:CCM has not only proved a failure but it' also a useless political party for the time being.Hatuwezi kupata mabadiliko chini ya utawala wa chama hiki kilichoishiwa na mbinu za uongozi.HOWEVER,what's the alternative?Tuna vyama vya upinzani lakini havijawa tested enough kuaminiwa kulipeleka taifa hili kule kunakostahili.Ok,let's assume kuwa ni bora hao "serengeti boys wa kisiasa" kuliko "taifa stars ya enzi za kichwa cha mwendawazimu".Lakini,what if we are wrong?What if,kwa kuwaweka hao "mbadala" tukaishia kungo'ana macho wenyewe kwa wenyewe?
Na wametuasa kusikiliza wenye nchi ndani ya chama kutaka kuwapeleka tena wananchi kwenye Ujamaa kwa kigezo cha mporomoko wa ubepari duniani. Wachambuzi wa The Econonimist wanasema genda ulole.[/
Kwa hili,binafsi namlaumu Nyerere.Why?Because when he realized that Ujamaa wouldnt work and had proved a failure,hakuwa na ujasiri wa kuwaomba radhi Watanzania.Anyway,kuomba radhi isn't a big deal,tungeweza kumsamehe kama angalau angetuchagualia mtu anayedhani angekuja na mawazo mapya yenye kuangaliwa what went wrong kwenye ujamaa na what needs to be done.He brought in MWINYI!Do I need to say more?
Pengine lawama pekee anayostahili Mwinyi ni kukubali kupokea nchi wakati hana ufumbuzi wa matatizo yaliyokuwa yanaikabili wakati huo.Same thing with fisadi Mkapa (angalau huyu alikuwa na mkakati wa kijitajirisha).Same thing with JK,ambaye nae pengine si wa kumlaumu sana kwa vile alishakuwa na mission yake ya kumpiku Vasco Da Gama sambamba na kuleta maisha bora kwa kila fisadi.
Bottom line is,tuwe makini katika kulaumu WATANZANIA,a group of peoples made of 40+ million of them,ambao takriban 3/4 yao wanaishi vijijini ambako hali ni tofauti sana na hiyo analysis ya urban Tanzania (which is basically Dar,a city attracting every 'specie' of human being,including hao wazembe,wavivu,wasengenyaji,nk......you could find such species in every metropolitan......lakini you could go further na kujiuliza:kwanini watu wanakimbia vijijini na kuja Dar (generic name for MIJINI)?