'The Economist' Takes Gloves off on Kikwete...

i completely agree with the "economist", Tanzania has become worse in all sectors during this JK era,he has not improved anything...but i think the history prooves itself...najua hapa katika ukumbi huu kuna watu wanahistoria nzuri sana ya nchi yetu..mimi natoa challenge mtu alete historia ya uongozi wa JK kabla ya uraisi wake....especially kwenye perfomance za utendaji...inapofika hatua raisi hana uwezo wa kuamua vitu kwa ajiri ya chi yake then ameshindwa kazi...lakini pia kitu kingine kikubwa anachomuumiza pia ni historia ya namna alivyoingia madarakani....makundi yalikuwa mengi and njia chafu zilitumika sana kiasi cha kwamba hana kauli kwa wazamini wake....
yes he will win by the majority na kama kawaida atahemewa....hivi ni nani ambaye anaweza akamkemea raisi?? yeye ndio raisi wa nchi, mwenyekiti wa CCM chama tawala..no one can go agaist him...he is atop...

report kama hiyo ya the economist zimekuwepo hapa nchini kwa muda kujaribu kuassess kazi za JK na nyingi zimeonyesha uozo mkubwa katika utendaji wake...liko wazi sana..hata ile hotuba ya spika kumshukuru raisi kwa speech pale bungeni alipokwenda kuzungumzia EPA, ilikuwa ni kijembe cha utendaji..kkwamba serikali(JK) inaongea sana kuliko kutenda...
 
JK has been ineffective leader indeed...support this...hata watanzania nazani sasa wamemjua who he is...? ila tutamchagua tena tu...we are not prepared for changes...hata wengi hapa wanaochangia pamoja na kuonyesha hisia zao katika masuala haya bado tunaunafiki wa kisiasa kama viongozi wetu...mbona wakenya kila kukicha wanajitoa kwenye vyama vyao na kuazisha vingine kwa ujasiri na watu wanawasupport...kwanini hawa waliomo ccm na kutokubaliana na chama wasijitoe tukawapa support...je wanaogopa maslahi au wanahofia unafiki wa watanzania...
 
mtazamowangu,
Mkuu yawezekana kabisa kuwa Kikwete ana mapungufu yake kama kiongozi lakini hatuwezi kupotosha ukweli kwamba sisi wenyewe ndio wenye Mapungufu kwa kuyaona hayo mapungufu yake kuwa sio sababu ya kutomchagua..
Kutazama historia yake hakuwezi kutuambia jibu zaidi kwa nini sisi huwa tunawachagua viongozi ambao tuna claim ni wabovu..Na haitakuwa kumtendea haki Kikwete peke yake wakati hata Mwinyi na Mkapa wote hawa wamechaguliwa bila kuwa na historia yoyote yenye maana kuweza kushika wadhifa huo..
Sidhani kama kuna mtu hapa anaweza kutuambia kwa nini tuliwapigia kura viongozi hao kama sio imani kubwa tuliyoijenga kwa chama CCM..ndivyo economist walivyosema, maelezo yao yana ukweli mwingi lakini nachofahamu mimi ni baada ya matokeo.. Wao pia ni kama sisi hapa JF tunazungmzia mambo yaliyokwisha tokea, maamuzi yaliyokwisha tokea bila kutoa mwanga zaidi wa maradhi yetu..

Dilunga,
Mkuu hili swala la misaada kusema kweli linachanganya.. Ukisoma mwanzo wa sentesi hiyo imesema:- "Tanzania is not even spending all the aid it is given.
Hapa inaonyesha huwa hatutumii fedha yote tuliyopewa, kisha ukisoma kinachofuata kinapingana na utangulizi huu...kupotosha kile utakachowalaumu waandishi lakini message imefika kwa wasomaji kuwa sisi ni omba omba lakini hatufahamu kupanga vipaumbele wakati nchi kama Kenya imetuacha..
 
mkandara,

suala la sisi kushindwa kuona mapungufu ya wanaotuongoza ni kile mimi ninachokiita unafiki wa kisiasa..sio kwamba hatuoni na kujua ila ni mfumo ambao umetugubika na kuubadilisha huu lazima zifanyike juhudi za ziada...leo hii hata CCM ikiamua kumsimamisha Lowasa au Chenge kugombea uraisi..atashinda tu.....
 
mkandara,

leo hii hata CCM ikiamua kumsimamisha Lowasa au Chenge kugombea uraisi..atashinda tu.....
Hapo sasa ndipo naposhindwa kuelewa kwa nini tunadai kwamba tunataka maendeleo...
Na hii ndio tofauti kubwa ya Tanzania na nchi nyinginezo.
 

umenena sawa sawa kabisa. inabidi mkija likizo muanze kuulizia hatua za kufuata ili uweze kujiandikisha katika daftari la kura.
 


Me too! I hate watu wanaopenda overgeneralization wakidhani italeta chachu au effect kwa wengine positively.

Ni mategemeo yangu kwamba akina Rev. Kishoka, Dilunga,... watawaomba radhi WATANZANIA!
 
Hapo sasa ndipo naposhindwa kuelewa kwa nini tunadai kwamba tunataka maendeleo...
Na hii ndio tofauti kubwa ya Tanzania na nchi nyinginezo.

Mkandara,

Kama tukikupa nafasi uwe Rais wa Tanzania, unafirikiri unaweza ukafanya kipi cha ajabu sana ambacho kitatofautiana na CCM..........

Ninakuuliza hili swala la msingi kutokana na ukweli kwamba U cant destabilize a country while you don’t who how to stabilize it . Usemi huu uko proved na wamarekani katika vita yao na Iraq ,walienda Iraq Bila kujua baada ya Kumtoa Saadam Hussein WATAWEZAJE ku stablize Iraq ,kutojua ukweli huu it ended to cost them Billions of USD mpaka leo, Vita ya mienzi ikawa ya miaka.

Ninakuuliza swali hili kwasababu Tanzania tuna tatizo, Watu wanafikiri ikitoka CCM ndio itakuwa suluhisho la matitizo yetu yote....

Mwisho ninadhani ni mhumi tuanze kujua sera, especially z watu amabo mko au mnaelekea kwenye siasa.

Kila siku watu tunapiga zogo but I would like to see the alternative action plan ya kuipeleka nchi yetu mbeleh ?
 

Me too! I hate watu wanaopenda overgeneralization wakidhani italeta chachu au effect kwa wengine positively.
Ni mategemeo yangu kwamba akina Rev. Kishoka, Dilunga,... watawaomba radhi WATANZANIA!

LazyDog, inawezekana ikawa kweli kuwa wakati mwingine tunafanya generalization, lakini hebu tuangalie data zifuatazo kwa kulinganisha na jirani zetu.

1. Tulikuwa wa kwanza kupata uhuru hapa Afrika Mashariki.
2. Tuna watu wengi (population wise) kuliko jirani zetu.
3. Sehemu kubwa ya ardhi yetu ina rutuba na inafaa kwa kilimo.
4. Tuna hali ya hewa ambayo kwa kiwango kikubwa ni nzuri.
5. Tuna mito na mabonde makubwa yanayoweza kustawisha kila aina ya mazao.
6. Tuna misitu ambayo ni hazina kubwa katika kutunza mazingira.
7. Tuna mali asili inayojumuisha Tanzanite isiyopatikana popote kwingineko.
8. Tuna mbuga za wanyama zisizo na mfano dunia nzima.
10. Tuna vivutio vya watalii vinavyojulikana hata kwa watoto wadogo anzia Asia, Ulaya hadi Marekani.
11. Tumekuwa na utulivu mkubwa na hatujawahi kushuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe kama jirani zetu.
12. Tumekuwa wapokeaji wazuri tu wa misaada kwa mamilioni toka tupate uhuru kuliko wenzetu.

LazyDog ni wazi tunachokosa ni mpangilio na uongozi bora - je ni kwa nini :-

1. Tumeweza kuendela kuchagua chama kile kile kutuongoza kwa miaka zaidi ya arobaini (40).
2. Tumeweza kuchagua viongozi wasio na vision yoyote ya kututoa kwenye umasikini.
3. Tumepiga kambi kwenye huu umasikini na kuukumbatia kama jadi na halali yetu.
4. Tumekubali nchi yetu kugeuzwa kichwa cha mwendawazimu - kila kinyozi anajifunzia.
5. Tumeruhusu hazina yetu kuporwa na kuhujumiwa bila kuwawajibisha tuliowakabidhi ulinzi wa hizo mali.
6. Kila uchaguzi tunawasindikiza hao hao kwa nderemo na vifijo hadi meza iliyojaa vinono nasi twarudi kwenye njaa na umasikini wetu.
7. Tunaruhusu makubaliano yetu na watawala (katiba) ibakwe na kunajisiwa tukishuhudia bila kuuliza kulikoni.

LazyDog, nitakwambia ni kwa nini - ni kwa sababu hizo hizo unazozikataa. Ukipika chakula chako na kukiweka mezani, hutamruhusu mbwa akikaribie - ukifanya hivyo utalala njaa. Ukilima shamba lako ukapanda mpunga hutakubali ndege wakaribie hilo shamba - ukifanya hivyo hutavuna mchele. WaTz kwa kushindwa kulinda kilicho chetu, tumebaki masikini - we definitely lack something and that's the naked but bitter truth, sigh.
Mtaji mkubwa wa CCM ni ujinga wetu wa Tz​
 
Mag3, I agree, tusipokuwa tayari kukoselewa tutaendelea hivihivi na mwisho wake ni mbaya! Lazydog huu si wakati wa unafiki au false indignation! Instead of being incensed by what Mag3, Rev Kishoka have said and you claim have generalized, you should take it as constructive criticism.
Mi nakubali kwamba hata mimi binfasi najikuta niko katika kundi la wanafiki na pia ni mwogo, most of us are unable even to use our real names, ndo maana unaitwa LazyDog na mimi Susuviri, maana tungetumia majina yetu ya kweli ya John na Juma tungebaki tunasifia CCM na JK. But annonymity ndo inatupa nguvu ya kuwa wazi. Sasa inabidi tufike mahali tukubali kusema ukweli bila kuogopa.
Rev Kishoka, nimewahi kuongea na wewe na bado naendelea kuamini kuwa muda mwafaka umefika kwani watanzania wako tayari kwa ajili ya mabadiliko wamechoka, lakini wanahitaji viongozi majasiri, what are we going to do about it? Mimi nadhani nasubiri hiyo private candidate nichukue fomu, 😀 (unaona sasa? Tunakuja na excuse tu, what is your excuse?)
 
Ni kweli kabisa kwamba aliyeandika article ya The Economist ana lake jambo ikiwa ni pamoja na kukasirishwa na hatua ya Tanzania ya kukataa kuiingiza ardhi katika moja ya "mali" za EAC. Lakini pia ni kweli kwamba uchumi wetu na mambo yetu kwa ujumla yamekuwa na hitilafu kubwa ya kuendeshwa kisiasa badala ya kitaaluma.

Maamuzi ya kiuchumi yanafanyika kisiasa na matokeo yake ni kwamba maamuzi ya wanasiasa ndio yanabebwa na kutekelezwa na matokeo yake ni kuanguka pua chini. Mifano ni mingi. Unaanzia katika umeme. Ni kwa nini hadi leo hatujafikisha hata asilimia 10 ya watu wote kupata umeme miaka takriban hamsini baada ya uhuru? Ni kwa nini leo hii baada ya kuwa tumegundua gesi asilia nyingi kiasi hicho bado tunathubutu kujenga kituo cha umeme cha megawati 45?!!! Kitu gani kinatuzuia sisi kujenga mitambo mikubwa ya umeme kwa ajili basi walau ya kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme kufikia walau asilimia 20 miaka hamsini baada ya uhuru? Yote ukiangalia kwa makini ni kwa sababu maamuzi ya kitaaluma wamenyang'anywa wanataaluma na yanafanywa na wanasiasa ambao kwa hakika uwezo wao ama ni mdogo sana ama haupo kabisa na hili halihitaji mjadala mrefu sana. Mungu Ibariki Tanzania!!!!
 

Ukiiangalia Tanzania in isolation,unaweza kuwa na kila haki ya kumhukumu kila Mtanzania.Lakini laiti ukijaribu kuiangalia Tanzania kama sehemu ya mfumo,naamini utagundua kuwa pengine huwatendei HAKI Watanzania kwa ujumla wao kwa kudhani kinachokwaza mabadiliko ni,say UZEMBE,UVIVU,etc.

Hebu angalia North Korea,kwa mfano.Huku tatizo kubwa si umasikini (japo ni tatizo pia) bali ni haki za binadamu.Je nao ni wazembe kama Watanzania kwamba wasiunganishe nguvu zao kuung'oa mfumo unaowakandamiza wengi na kunufaisha wachache?

Angalia ukweli mchungu kuhusu iRAQ.Pamoja na madhara makubwa yaliyojitokeza baada ya uvamizi wa Marekani,kuna ukweli usiopingika kuwa udikteta wa Saddam umekomeshwa (lakini sio kwa chuki waliokuwa nayo the oppressed majority under the Saddam regime bali the Americans and their allies).Hapa simaanishi kuwa uvamizi huo ulikuwa wa haki au umemaliza matatizo ya Iraq,bali nachojaribu kupigia mstari ni namna isivyo rahisi (kama unavyofikiri) kubadili mfumo (japo it is not impossible).

Ni rahisi kushangaa kwanini CCM inaendelea kuwa madarakani iwapo mtu hajishughulishi kujiuliza kwanini Silvio Berlusconi anaweza kuzichezea siasa za Italy as if ni sehemu ya empire yake ya biashara.Na Italy ina resources nyingi zaidi za kuleta mabadiliko kuliko akina sie tulopata uhuru less than half a centruy ago.

Binafsi huwa napenda kuwashauri wanaopenda ku-generalize lawama dhidi ya Watanzania kujaribu kuangalia mifano kutoka tawala dhalimu za kikomunisti (kwa mfano USSR),kwanini ilichukua miaka mingi kung'oka na kwanini kung'oka kwake bado hakujaweza kuwa ufumbuzi kabisa wa matatizo ya nchi zilizokuwa ndani ya himaya hiyo.

Kinachoweza kukusaidia kidogo ni kuangalia role ya state apparatus katika kuhakikisha mfumo dhalimu unaendelea kuwa madarakani.Reforms za miaka ya 90 kwa Tanzania zilijumuisha viinimacho kadhaa.Kwa mfano,wakati katiba ilibadilishwa na kuruhusu mfumo wa vyama vingi,mentality ya the ruling class haikubadilika (na kwa vile tangu uhuru,maamuzi na influence ya matendo na mtazamo katika jamii ni sort of top-down model,jamii imejikuta nayo ikiafiki-mostly unwillingly-kuwa hilo ni sahihi).Katika line hiyhiyo,japo sheria ziliwekwa wazi kuwa taasisi za ulinzi na usalama zisijihusishe na siasa wala kufungamana au kushabikia chama flani,sote tunajua kuwa hilo bado ni tatizo kwani ulinzi na usalama wa Tanzania umegeuzwa kuwa synonymous na existence ya CCM.Ukidhani nachoandika hapa ni hadithi,waulize CUF walivyopewa lesson kuhusu unholy alliance kati ya the ruling power and state apparatus.

Ni rahisi kukaa mbele ya computer yako na kuwabebesha lawama nzito Watanzania wote kwa ujumla wao kana kwamba WAMEJITAKIA HAYA YOTE YANAYOENDELEA japo yanawaumiza!Ni rahisi pia kulaumu kuhusu mchango wao (Watanzania) katika umasikini wa nchi yetu as if umasikini ni anasa flani wanayoipenda.Ni muhimu kuangalia mahusiano kati ya umasikini na inequality,na faida yake kwa any oppressive ruling class/domonant class.

Changanuzi za ki-Maksisti zinaweza pia kuwa na manufaa katika kuelewa kinachoendelea ndani ya Tanzania (kama u-muumini wa Umaksisti) japo pengine mapendekezo yao kuhusu namna gani tabaka tawala linavyoweza kuondolewa yanaweza yasiwe viable katika mazingira ya kisasa.

Finally,kuna wanaoamini kwamba katika bara la Afrika,na pengine sehemu kubwa ya "dunia ya tatu",vyama tawala huwa haviondolewi madarakani bali vinaondoka vyenyewe,aidha kutokana na internal conflicts ndani ya chama (like matokeo ya poor nomination of candidates in the case of KANU),kujisahau kupita kiasi (tuite kuvimbiwa madaraka-kama ilivyokuwa kwa Kaunda huko Zambia),au factors zinazoshabihiana na hizo....Wenye mawazo hayo wanaweza kuwa realistic kwa vile kama chama tawala ndio jaji,mwendesha mashtaka na mzee wa baraza (as influence ya CCM ilivyo kwenye election process na mechanism kama tume ya uchaguzi,namna vyombo vya usalama vinavyoendelea kuwa waangalizi wa usalama wa ccm na wafuasi wake badala ya watanzania wote regardless ya political affiliations zao,nk,nk,nk) ni dhahiri basi kushindwa kwa CCM is more of matokeo ya uzembe wake au kujisahau than consolidation ya chuki,hasira,nguvu (kama zipo),and the likes dhidi ya chama hicho dhalimu.

SAFARI BADO NI NDEFU.ILI TUFIKE,HII BLAME GAMES ZINABIDI ZIWE MORE REALISTIC THAN SIMPLY EMOTIONAL!
 
Last edited:

Nkamagi,

What did Bob Geldof tell Mwanasesere?
 
Viongozi tulionao hawako kwa ajili ya masilahi ya Taifa ila kwa ajili ya manufaa binafsi. .

Taffu,

Wengi wa hawa viongozi, ukiwauliza kwa nini waliamua kuwa watumishi wa umma au wawakilishi, hawawezi kukuba jibu la maana au kwa ufasaha!

Sikatai kuwa wengi ni kwa ajili ya ubinafsi, lakini ukiwauliza kwa nini hawakwenda katika Sekta binafsi au mashirika na kuwa waajiriwa na si wapigiwa kura, utakuta hawana jibu la msingi na hivyo kuimarisha ubatili wa Uongozi wao!
 

Ukweli,

Kabla ya mfumo wa Dunia kuanguka miezi 8 iliyopita, Rais Kikwete alitumia muda wake mwingi tangu achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania kutembeza bakuli kuomba misaada badala ya kufanyia kazi Ilani ya uchaguzi wa 2005 ya CCM, kutoa msukumo wa maendeleo ya kujitegemea kupitia MKUKUTA na MKURUBITA na hata kufanyia kazi malemgo ya Millenia.

Hivyo si kweli kuwa kuanguka kwa uchumi wa Dunia ni kihalalisho cha Kikwete kuendelea kubembeleza misaada na kutembeza bakuli.

Kiufanisi, Rais Kikwete kafanikiwa sana kutembelea dunia, lakini kuwa nguzo na msukumo wa uzalishaji mali wa ndani ya nchi na kuwa na matumizi mazuri ya hazina, hajafanya lolote zaidi ya kuwa mlalamikaji na mfujaji.

Mwenye kuandika hata kama ana mabwana, ni wa nchi alikotoka na ni wao ndio wanatoa misaada kwetu kwa kuwa tunaendelea kudai sisi ni masikini wa kutupa na hivyo waone aibu watunusuru.

Ikiwa tuna fedha nyingi za misaada takriban Dola Bilioni 2.5 zimekaa hazijafanyiwa kazi, ni kwa ni ni basi Kikwete na timu yake kila siku wako safarini wakiomba misaada?

Mwamba ngoma huvutia kwake, na hivyo hata kama mwandishi wa Economist yuko biased, ana haki kufanya hivyo maana kodi yake badala ya kumfundisha mtoto wake au kumpa yeye matibabu ya daraja la juu, inawawanywa kwa fungu fulani kwenda saidia Watanzania ambao wana uwezo wa kujitegemea lakini hawataki kusimama kidete na kujitegemea na wanaongozwa na Serikali isiyo na shukrani na iliyo kosa utashi wa kufanya kazi.
 

MchunguZI,

In comparison to what China is investing in Congo and Kenya, the $20 million Dollars trade agreement is not enough!
 


Me too! I hate watu wanaopenda overgeneralization... Ni mategemeo yangu kwamba akina ... Dilunga,... watawaomba radhi WATANZANIA!



Wa vijijini ndio worse off!

Nime generalize? Afadhali wa mjini wanashinda wanakunywa chai chapati kazini na kusoma "Sani," wa vijijini hata kazini hawaji, hawagusi kitu, kazi wao ni kunywa pombe, kukalia vigoda. Wanachojua ni kusimamia tohara za vi teenager vya kike na kushinda kwenye ngoma, hususan wanaume. Unasema walipigania uhuru? Angalia hawa waliopigania uhuru wanavyo walaani wazee wa vijijini walivyolegalega toka enzi za uhuru the '60s:

``Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi. Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine ye yote katika Tanzania.

Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina mama wa mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni ya kina baba vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi sasa hazifanyi kazi yo yote ila kupiga soga, kucheza ngoma na kunywa pombe, ni hazina kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo ya nchi yetu kuliko hazina za mataifa matajiri`` TANU, ARUSHA, Januari 29, 1967


Kwa hiyo, si mjini si vijijini, wavivu, tusisafishane. Tena wa vijijini nusu yao nzima ni wafanyakazi wafu. Shughuli za mjini ni send off, shughuli za vijijini ni ngoma. Mdundiko na Sindimba na Rythm and Blues na Mayenu. Difference without distinction.

Mtanzania akikwambia "naenda kwenye shughuli" usidhani anaenda kupima kiwanja au shamba. Tafrija. "Kikao" ni get-together ya mikakati ya tafrija ya kipaimara cha mtoto. Akisema anaenda kwenye rehearsal usidhani ni practice ya kitu cha maana zaidi ya upambe wa tafrija. Kama sio ndoa ya mke wa pili basi ni Iddi pili. Maulidi haziishi. Kuna Pasaka mpaka Jumatatu. Na Jumatano za Majivu, na Ijumaa za Mateso. Na Ubarikio wa vinjiti.

Hizo ndizo "shughuli," ukisikia Mtanzania anakwambia anaenda kwenye "shughuli." Sote na Kikwete wetu ni slow.
 

Hata kama anayelalamika na kutukana ni Mkenya, kwani kasema uongo?
 
Me too! I hate watu wanaopenda overgeneralization wakidhani italeta chachu au effect kwa wengine positively.

Ni mategemeo yangu kwamba akina Rev. Kishoka, Dilunga,... watawaomba radhi WATANZANIA!

Lazydog,
Niwaombe radhi Watanzania kwa kosa gani nililolifanya?
 
Nimepata hiyo ya Bob Geldof. naambatanisha, lakini Bob anamzunguzmai Kikwete na tabia yake ya kucheka cheka anapozungumzia snigger....!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…