The Emperor Jean-Bedel Bokassa

The Emperor Jean-Bedel Bokassa

Umekosea jukwaa. Ungeweka kule sub forum ya siasa. Yaani jukwaa la historia. Waombe mods wauhamishe.
 
Huliogopi hili jitu?
115107-004-42ACAD17.jpg
 
aiseeee hatari sana ..hii kweli africa
 
Tuwekee na Jean Bedel Bokassa wa Tanzania 😡

Kiongozi wa Central Africa aliye badilisha katiba na kujiapisha mfalme ili atawale maisha

Siku ya kuapishwa kwake alikalia kiti cha cataract 24 ya thahabu yenye uzito wa tani mbili.

Taji lake ka dhahabu na almasi liligharimu $20 million. Gharama za sherehe nzima ilikuwa $80 million

Alifilisi nchi, alikwenda Libya kuomba mkopo kwa Ghadafi, alipewa mkopo kwa masharti ya kuslim na kueneza dini ya ki-Islam Central Africa
Jina lake la kuslim aliitwa Salah Dinne Ahmed Bokassa

Alirudia dini yake ya u-Katoliki kabla mauti hayajamfika.

Bokassa aliua takriban watu 100 wakati wa utawala wake, wapinzani wake walipotea

Bokassa alifuga mamba, wahalifu wote na wezi walikuwa chakula cha mamba wake

Akiwa weak ndani ma mia ya wanafunzi baada ya kukataa kununu uniforms zilizo shonwa na kampuni ya mmoja wa wake zake
 
Hii ni cha Mtoto ukilinganisha na maharamia wa Europe
naam nikweli mkuu nikweli ..niliwahi kuskia unyama amabo aliufnya Christopher Columbus nikachoka kabisa..halafu mbaya zaidi wao wakifnya hawaitwi magaidi
 
naam nikweli mkuu nikweli ..niliwahi kuskia unyama amabo aliufnya Christopher Columbus nikachoka kabisa..halafu mbaya zaidi wao wakifnya hawaitwi magaidi
Walitu brainwash sana hawa watu katika maisha yetu!
Sasa tumeamka!
 
Kiongozi wa Central Africa aliye badilisha katiba na kujiapisha mfalme ili atawale maisha

Siku ya kuapishwa kwake alikalia kiti cha cataract 24 ya thahabu yenye uzito wa tani mbili.

Taji lake ka dhahabu na almasi liligharimu $20 million. Gharama za sherehe nzima ilikuwa $80 million

Alifilisi nchi, alikwenda Libya kuomba mkopo kwa Ghadafi, alipewa mkopo kwa masharti ya kuslim na kueneza dini ya ki-Islam Central Africa
Jina lake la kuslim aliitwa Salah Dinne Ahmed Bokassa

Alirudia dini yake ya u-Katoliki kabla mauti hayajamfika.

Bokassa aliua takriban watu 100 wakati wa utawala wake, wapinzani wake walipotea

Bokassa alifuga mamba, wahalifu wote na wezi walikuwa chakula cha mamba wake

Akiwa weka ndani ma mia ya wanafunzi baada ya kukataa kununu uniforms zilizo shonwa na kampuni ya mmoja wa wake zake
This is africa!
 
Alikuwa mjinga sana. Alipokufa rais wa ufaransa De Gaulle alilia kuliko mjane wa Rais huku akilia baba baba. Haoahao wafaransa waliosaidia kumuweka kwa sababu walijua ni mjinga ndiyo waliomtoa baada ya kuona ujinga wake umepita mipaka.
 
Alijifananisha na Napoleon hata uniform zake za jeshi aliiga mavazi ya Napoleon
 
Miongoni mwa watawala waliokuwa na visa na vituko vingi katika bara hili la Afrika ni mfalme wa kujipachika wa Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa.

Jean Bedel Bokassa akiwa anaongoza nchi masikini kabisa duniani, alifanya sherehe ya kujisimika kama mfalme mwaka 1977 kwa kutumia kiasi cha sawa na shilingi bilioni 32 za Kitanzania za wakati huu. Lile taji lake la Ufalme peke yake liligharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu!.

Jean Bedel Bokassa alikuwa dikteta wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Alikuwa na wake kumi na saba (17) na watoto hamsini (50).

Alifanywa yatima wafaransa walipomuua baba yake akiwa na miaka sita (6) baada ya baba yake kufa mama yake naye alijiua.

Alipata kupigana vita ya pili ya dunia chini ya Wafaransa. Baadaye alikuja kumpindua rais aliyekuwa ndugu yake mwaka 1965. Alijipa cheo cha field marshall na kutengeneza uniform maalumu sababu ya wingi wa medals alizojipa. Akienda kutembelea nchi alikuwa anagawa almasi.

Alikuwa ana majumba zaidi ya sita Ufaransa. Pia alikuwa na majumba mengine nchi mwake, katika majumba yake mengine yaliyokuwa nchini mwake, Jumba lake mojawapo lilikuwa na bwawa la mamba na simba wa kufugwa, alitumia mamba hao na simba kuulia wapinzani wake.

Wake zake walikuwa Mchina, Mjerumani, Msweden, Mtunisia na Mromania. Aliwaweka nyumba tofauti na alikuwa akiwatembelea kila siku na kusababisha foleni kubwa barabarani kutoka na wingi wa safari hizo huku akiambatana na misafara.

Alipinduliwa na wafaransa baada ya kuua wanafunzi waliokua wanaandamana. Alifungia wanafunzi 30 kwenye jela ya mtu mmoja.

Walipompindua kwenye friji yake walikuta nyama za watu.

Mwishoni mwa maisha yake alitumia kusoma bible na huku akiwa anajiita mtume wa yesu. Hatimae alifariki mnamo mwaka 1996 kutokana na ugonjwa wa moyo.
 
Back
Top Bottom