The Emperor Jean-Bedel Bokassa

The Emperor Jean-Bedel Bokassa

Kaka Mtambuzi naona watu wamekutafsiri vibaya (kwa mawazo yangu sijui ya kwako),, unaweza ukaja ukafuta utata huu lakini??
 
jamaa alikuwa dikteta wa CAR. aliikuwa na wake 17 na watoto hamsini. alifanywa yatima wafaransa walipomuua baba yake akkiwa na miaka 6. baada ya babaake kufa mamayake nae alijiua.alipigana WW2 chini ya wafaransa.alimpindua rais aliyekuwa ndugu yake mwaka 1965.alijipa cheo cha field marshall na kutengeneza uniform maalumu sababu ya wingi wa medals alizojipa. akienda kutembelea nchi alikuwa anagawa almasi.

alikuwa anamajumba zaidi ya sita ufaransa. jumba yake la CAR lilikuwa na bwawa la mamba na simba wa kufugwa. alitumia mamba hao na simba kuulia wapinzani wake. wake zake walikuwepo mchina, mjerumani, msweden, mtunisia na mromania waliekutana club. aliwaweka nyumba tofauti na alikuwa akiwatembelea daily na kusababisha jams.alijjitawadha kuwa mfalme kwa sherehe ya 22m USD. huku akipanda farasi kama wafalme wa ulaya. alipinduliwwa na wafaransa baada ya kuua wanafunzi waliokua wanaandamana. alifungia wanafunzi 30 kwenye jela ya mtu mmoja.walipompindua kwenye friji yake walikuta nyama za watu.

mwishoni mwa maisha yake alitumia kusoma bible na alikuwa anajiita mtume wa yesu. alifariki 1996.
pak009_346_007.JPG
 
Nishawahi kumsikia kwenye baadhi ya mashairi ya wanamuziki wetu.

"Niite GK aka Bokassa wenye chuki wamekwisha nasa"
 
Huyu mutu alikuwa ni balaaa, mutu ya simba na mamba, iko kuwa na vyeo hakunaga mutu yingine imepata kuwa nayo.
 
Bokasa alikuwa na viatu vilivyotengenezwa kwa dhahabu tupu.
 
aliwahi kuwalaza wanafunzi wa shule moja barabarani kwny msafara wake kisa hawakutokea kumpokea, aliagiza lori la jeshi liwapitie hao wanafunzi waliojipanga kwny njia...hamna hata mmoja aliyesalia baada ya lori kuwakanyaga, dereva alijiua kwa kukamata kumbukumbu mbaya maishani mwake!!!
 
Bahati mbaya, kifo hakiogopi vyeo wala dhahabu ulizonazo.
 
nyerere alimwongeleaje huyu jamaa,watunza kumbukumbu za mwalimu funguken bas
 
Kuna wakati mwandishi mmoja alihoji inashangaza baadhi ya mtendo ya Viongozi wa Kiafrika, mpaka unajiuliza wamefikaje hapo walipo huku watu au viongozi wenzao wanawatizama na wasijue kwamba huyu Mtu anayepanda ngazi ana matatizo ya akili au mwendawazimu?!!
 
Afrika kuna viongozi wa ajabu sana! Kwanini hatupati madikteta wa kuleta maendeleo kama Hittler hivi? Tunapataga vilaza wa kujivika madini, kuua na kuoa wake wengi hahahaaaa!!
 
Afrika kuna viongozi wa ajabu sana! Kwanini hatupati madikteta wa kuleta maendeleo kama Hittler hivi? Tunapataga vilaza wa kujivika madini, kuua na kuoa wake wengi hahahaaaa!!

mobutu seseko nyumba yake nzima ilikuwa dhahabu mpaka vitasa na mtoto wake alikuwa anasoma day school UK
 
makeke yake yote kaishiaaaa kufa kama mbwaaa tu ...vp walimzika na dhahabu zake na mali zake ameenda nazo huko mbona kila kitu kaacha duniani, tatizo viongozi wa afrika hawajifunzi kwa wenzao...wakina mabotu
 
makeke yake yote kaishiaaaa kufa kama mbwaaa tu ...vp walimzika na dhahabu zake na mali zake ameenda nazo huko mbona kila kitu kaacha duniani, tatizo viongozi wa afrika hawajifunzi kwa wenzao...wakina mabotu

kufa ni kufa tu, usiogope kutafuta pesa eti kwa sababu utakufa kama mbwa, kwaniukiwa maskini utaishi milele?!!!...cha muhimu ni kutafuta pesa kihalali!
 
Back
Top Bottom