Jean-Bedel Bokassa alizaliwa 22 February 1921 na alifariki 03 November 1996. Alijulikana pia kama Bokassa wa Afrika ya Kati na Salah Eddine Ahamed Bokassa, alikua ofisa wa jeshi na mkuu wa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati alijichukulia madaraka kwa kuuondoa utawala wa rais ambae alikua binamu yake 01 January 1966 mpaka alipotolewa madarakani kwa mapinduzi ya yaliyosaidiwa na Wafaransa 20 September 1979. Katika kipindi hicho akiwa ametawala kwa miaka 11 kama raisi kutoka 01 January 1966 - 04 December 1976, kutoka hapo mpaka 20 September 1979 alijiapisha kama raisi wa maisha wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa miaka mitatu ya mwisho alitawala kama mfalme wa Afrika ya Kati na alikua dikteta. Utawala wa kifalme ulikua kuanzia 04 December 1976 mpaka 21 September 1979. Kufuatia kutolewa kwake madarakani Jamhuri ya Afrika ya Kati ilirudi chini ya David Dacko. Utawala wa kifalme wa Bokassa haukutambulika kisheria na nchi nyingine duniani.
Alizaliwa kwenye Ikweta ya Afrika ya Wafaransa, mtotot wa chifu wa kijiji, Bokassa alikua yatima katika umri wa miaka 12. Alipata elimu katika shule ya wamishionary na lijiunga na jeshi la kikoloni la Wafaransa akiwa askari wa cheo cha chini kabisa. Alijipatia sifa kubwa wakati wa vita na Indochina, na alishinda medali na kupanda cheo kufikia kapteni. Wakati Ikweta ya Wafaransa ya Afrika ilipopata uhuru na kuwa Jamhuri ya Afrika ya kati mnamo mwaka 1960, raisi mpya David Dacko ambae alikua binamu wa mbali, alimkaribisha Bokassa aje kuwa Mkuu wa Majeshi. Mwaka 1966 Bokasa alitumia nafasi yake kumtoa madarakani Dacko na kujitangaza kuwa raisi. Akaanza kujichukulia madaraka yote makubwa ya serikali kuwa kwake binafsi, yeye mwenyewe alisimamia hukumu za mateso.
Mwaka 1939 wakati Bokassa anajiunga na jeshi la mkoloni la Kifaransa.
Katika utawala wa Bokassa alianzisha sheria kuwa wezi wawe wanakatwa sikio kwa makosa mawili ya mwanzo na mkono kwa kosa la tatu. Decemba 1976 akijifananaisha na shujaa wake Napoleon, alijivika madaraka ya ufalme wa Ufalme wa Afrika ya Kati, shughuli hiyo iliambatana na sherehe ya kusimikwa na iligharimu US$ million 20 ( sawa na $ million 80 za leo), kwakifupi sherehe hiyo ilifisi nchi. Shada lake la kifalme ambalo liliwekwa urembo wa almasi tu liligharimu US$ million 5 sawa na US$ million 20 za leo. Mwaka 1979 aliweka ndani wanafunzi waliokataa kununua sare za shule kutoka kampuni iliyoendeshwa na mmoja wa wake zake. Bokassa mwenyewe alishuhudia vifo vya wanafunzi 100 kati ya hao yalioongozwa na Kikosi cha Mfalme.
Mnamo 20 Septemba, 1970, Jeshi la Wafaransa lilimtoa madarakani na kumrudisha Dacko kuwa raisi. Bokassa alikimbilia nchini Ufaransa ambako alikua na na nyumba kwenye shamba pamoja na majengo mengine aliyonunua kwa hela alizoiibia serikali. Baada ya kutolewa kwake madarakani, nchi ya hiyo ilirudisha jina lake la Jamhuri ya Afrika ya Kati. Akiwa hayupo nchini humo, mashtaka ya Bokassa yaliendelea mahakamani na hukumu iliyotelewa ilikuwa ni kuuwawa. Makosa yake ya kula nyama za binadamu yalifutwa lakini alikabiliwa na kosa la kuuwa wanafunzi na makosa mengine. Hukumu ya kifo baadae iliondolewa na baadae alihukumiwa kufungwa kwenye chumba peke yake bila mawasilianao na binadamu wenzakae, adhabu hii ilidumu kwa miaka sita na baadae alirudi na kuishi maisha ya kawaida katika mji mkuu wa nchi yake Bangui, alifariki Novemba 1996.
Maisha ya Mwanzo ya Bokassa.
Bokassa alizaliwa 22 February 1921 akiwa mmoja wa watoto 12 wa Mgboundoulou Bokassa, chifu wa kijiji na mke wake Mari Yokowo Bobangui, katika kijiji cha M'Baka eneo la Lobaye kando ya eneo la msitu wa ikweta, wakati huo likiwa chini ya utawala wa kikoloni wa Wafaransa. Mgboundoulou alilazimishwa kupanga ratiba ya kazi kwa wanakijij kufanyia kazi kampuni ya Forestiere ambayo ilikuwa ya Kifaransa. Mgboundoulou aliamua kuwa hawezi kuendelea kufuata amri za Wafaransa na aliwaachia huru wanakijiji waliowekwa kizuizini na kampuni ya Foestier. Wafaransa waliona kitendo kile ni kiburi, Mgboundoulou alichukuliwa akiwa amefungwa minyororo mpaka Maiki. Hiyo ilikuwa November 1927, alipigwa mpaka akauwawa katika mji nje ya nyumba ya District Commisioner. Wiki iliyofuatia, mama yake Bokassa hakuweza kuvumilia machungu ya kufiwa na mumewe na kuachiwa watoto, aliamua kujiua.
Ndugu na jamaa ilibidi wamlee Bokassa na nduguzake, waliamua itakuwa vizuri Bokassa ajifunze kusoma na kuandiaka Kifaransa, alipelekwa kwenye shule ya missionary mjini Mbaiki, akiwa mtoto wenzake walimtania sana kuhusu yeye kuwa yatima. Bokassa alikua mfupi na mwenye umbo lililojaa na alikua mwenye nguvu. Katika masomo alipenda kitabu cha Kifaransa kilichoandikwa na Jean Bedel. Mwalimu wake aligundua hilo na kuanza kumuita Jean-Bedel. Akiwa kijana Bokassa alisoma Ecole Saint Louis mjini Bangui, chini ya Paroko Gruner. Gruner alimsomesha Bokassa akitegemea atakua padre lakini aligundua uwezo wake wa darasani haukumudu vigezo vilivyohitajika kwa masomo hayo . Matokeo yake alipelekwa kwenye shule ya Paroko Compte's mjini Brazzaville, kule alijifunza upishi. Baada ya kumaliza shule, babu yake alishauriwa na Paroko Gruner kumpeleka Bokassa kwenye jeshi la Kifaransa.
Maisha ya jeshini.
Akiwa mwanajeshi Bokassa alipewa cheo cha koplo July 1940 na sagent meja Novemba 1941. Wakati huo majeshi ya Mjerumani yalijaribu kuingilia eneo la Mfaransa na Mjerumani alipigwa vibaya sana. Baada ya hapo Bukassa alijiunga na Kikosi cha Mfaransa cha Afrika na walifanikiwa kuteka mji wa Brazzaville. Mnamo tarehe 15 August 1944, alikua katika mapigano Operation Dragoon Mapigano hayo yalitoa kabisa majeshi ya Wajerumani katika pwani ya Frejus. Baada ya hapo alipelekwa Senegal kwa mafunzo zaidi ya kijeshi. Baada ya mafunzo hayo Bokassa alipelekwa Indochina kama mtaalamu katika shambulio la Saigon-Cholon. Kabla ya kumalizika kwa kazi ya kikosi Bokassa aliona majeshi ya adui na hii ilisaidia kupanga mashambulizi yaliyowaletea ushindi. Kwa tukio hili Bokassa alitunukiwa Legion d'honner ambayo ni nishani ya heshima kwa ofisa wa jeshi la Kifaransa na ilikuwa na alama ya Coix de guerre (Grand Cross).
Akiwa Indochina, Bokassa alifunga ndoa na binti wa Kivietnam wa umri wa miaka 17 aliyeitwa Nguyen Thi Hue. Walijaliwa kupata mtoto wa kike alieandikishwa kama raia wa Ufaransa. Bokassa alipoondoka Indochina aliiacha familia yake hiyo changa akitegemea atarudi muda si mrefu. Aliporudi Ufaransa Bokassa aliachwa katika kituo cha Frejus, ambako alifundisha mawasiliano ya redio kwa wanajeshi wapya. Mwaka 1956, alipandishwa cheo kuwa Second Lieutenant na miaka miwili baadae kuwa Lieutenant. Baada ya hapo Bokassa alikua msaidizi wa mafunzo ya kiufundi jeshini katika mji wa Brazzaville na 1959 baada ya miaka 20 nje, alirudishwa kwenye mji wake wa Bangui. Huko alipandishwa cheo kuwa Kaptain mnamo 01 July 1961.
Koloni la Kifaransa la Ubangi-Chari (Oubangui-Chari Kifaransa), lilikua sehemu ya Ikweta ya Mfaransa Afrika na ilikua na madaraka kuanzia 1958 na baadae uhuru kamili 13 August 1960 na kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mwaka 1962 Bokassa aliacha jeshi la Kifaransa na kujiunga na jeshi la jamhuri, akiwa na cheo cha kamanda. Akiwa binamu wa rais David Dacko na mpwa wa babu yake Dacko Barthlelemy Boganda, Bokassa alipewa jukumu la kuunda jeshi jipya la Jamhuri. Mwaka mmoja baadae Bokassa alikuwa mkuu wa wanajeshi 500 katika Jeshi la Afrika ya Kati. Uhusiano wake na raisi pia na uzoefu wake katika nchi za nje, Bokassa aliweza kupanda vyeo haraka na kufikia Kanali wa kwanza katika Afrika ya Kati.
Bokassa alipenda kuonekana kwa watu kuwa yeye ni kiongozi, mara nyingi alivaa medali zake za jeshini na katika sherehe alipenda kukaa karibu na rais David Dacko kuonyesha umuhimu wake serikalini. Bokassa maranyingi alibishana na Paul Douate, ambae alikua katibu mkuu wa rais ambae alimshutumu Bokassa kwa kutofuata utaratibu wa kukaa mezani kwa rais, na yeye kujiweka kartibu na raisDacko. Pamoja na majaribio mengi ya kupindua serikali, Dacko kwa nguvu kubwa alipinga wazo la Bokassa kutaka kumpindua hadharani, alisema "Kanali Bokassa yeye anapenda kukusanya medali na ni mjinga sana kutaka kuendesha jaribio la kutaka kupindua nchi". Mawaziri wengine kwenye serikali ya Dacko waliona kuwa Bokassa ni tishio kubwa katika uongozi. Jean-Arthure Bandio, waziri wa mambo ya ndani alipendekeza jina la Bokassa kwenye kikao cha mawaziri akitegemea atavunja uhusiano wa karibu katika jeshi na tabia ya kanali ya kupenda kujulikana.
Hali ya kutoelewana kati ya Dacko na Bokassa.
Serikali ya Dacko ilikalibiliwa na matatizo mengi kati ya mwaka 1964-1965: uchumi ulikubwa na mfadhaiko, uongozi ulianza kuyumba na mipaka ya nchi ilishambuliwa kutoka Sudan ya Kusini na Congo. Nchi zilizokuwa makoloni ya Kifaransa yalitaka kuwa na serikali zisizoitegemea Ufaransa. Dacko alianzisha mahusiano ya kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China chini ya uongozi wa rais Mao mnamo September 1964, Serikali ya Mao ilileta ujumbe ulioongozwa na Meny Yieng na wajumbe wengine, ujumbe huu ulizunguka nchi nzima ukionyesha films zenye sera ya ujamaa, hii ilitokea mara tu baada ya Ufaransa kuipatia nchi hiyo mkopo wa francs million 20 bila riba. Mkopo huo ulishindwa kuikwamua serikali ki uchumi, rushwa kati ya viongozi na uongozi mbovu vilichangia.Bokassa aliona kuwa anahitaji kuchukua madaraka ili asuluhishamatatizo hayo, kikubwa zaidi ni kuitoa serikali katika mawazo ya siasa za ujamaa. Uchu wa madaraka ndio lilikuwa shinikizo kubwa la Bokassa kuanzisha mipango ya kijeshi ya kutwaa uongozi.
Misaada ya Mataifa ya nje.
Muammar al Gaddafi alimsaidia Bokassa. Ufaransa pia ilitoa msaada. 1975, rais wa Ufaransa Valery giscard d'Estaing alisema binafsi ni "rafiki wa familia" ya Bokassa. Wakati huo Ufaransa ilipekeleka misaada ya pesa na misaada ya kijeshi kwenye koloni lake hilo la zamani. Wakati huo huo Bokassa alimchukua rais d'Estaing kwenye safari za kuwinda pia aliwapelekea Ufaransa uranium.
Urafiki huo wa kindugu kati ya serikali ya Bokassa na Ufaransa ulifika kileleni mnamo mwaka 1977 wakati ya sherehe za kusimikwa ufalme Bokassa. Waziri wa ulinzi wa ufaransa alituma majeshi ili kuzuia sherehe hizo na pia alitoa ndege 17 za kijeshi pia na wataalam wa kijeshi kuhakikisha mafanikio.
Sherehe za kusimikwa kwa Bokassa kama mfalme ziliendelea kwa siku mbili na kugharimu £ za Uingereza million 10, hii ni zaidi ya bajeti ya serikali ya mwaka. Sherehe zilipangwa na mwanamziki wa Kifaransa Jean-Pierre Dupont. Mhunzi kutoka Paris Claude Bertrand alitengeneza taji na Bokassa alikaa juu ya kiti cha kifalme kilichotengenezwa kwa tani mbili za dhahabu chenye umbo la ndege eagle.
10 October, 1979, gazeti la Kifaransa la Canard Enchaine liliandika kuwa rais Bokassa amempa aliekuwa fedha wa Ufaransa Valery Giscard dEstaing vipande viwili vya almasi mwaka1973 hii ilikuwa kashfa kubwa sana ya kisiasa iliyoitwa Uhusiano wa Almasi na hii ilipelekea Giscard d'Estaing kushindwa kwenye uchaguzi wa 1981. Uhusiano na Ufaransa uliyumba sana kutokea hapo na hii ilipelekea Bokassa kuwa na mahusiona mazuri zaidi na Muammar al Gaddafi wa Libya.
Baada ya kukutana na Gaddafi mnamo September 1976, Bokassa alipadili dini na kuwa Mwislam na kubadili jina kuwa Salah Eddine Ahamed Bokassa, lakini Decemba 1976 alirudia imani yake ya Kikatoliki. Inaaminika kubadili kwake dini kulitokana na hali mbaya ya uchumi nchi yake iliyokuwa inaikabili na hii ilipelekea uhakika wa misaada ya pesa kutoka Libya. Pesa aliyoahidiwa ilipofika, Bokassa alirudia imani yake ya dini pia alishapanga kusimikwa kama mfalme kwenye kanisa lake la Kikatoliki la Bangui.