Political is everything, bila political integration hatuwezi kuungana kwenye economic na social fronts.
Tanzania tuna mengi mazuri....na jirani zetu pia wana yao mabaya na mema vilevile.
My view ni kuwa na EA ambayo ni melting pot ya all these cultures. That is the only way forward. Unahisi tutajifungia mpaka lini? Bila kuungana hatuwezi na wala hatutawai kuwa na sauti on the global stage........Nyerere said "Unity may not make us rich, but it can make it difficult for Africa and the African peoples to be disregarded and humiliated."
At least tukiungana we have a shot of facing the world...together....that is the real battle we should be fighting!
Kuna mambo ambayo yalikuwa na faida kwa kipindi kilichopita. Na Nyerere kweli aliyasema hayo na yalikuwa na mwafaka kwa kipindi hicho.
Hapa hatujifungii hapa kila mmoja anakuwa na nchi yake na ustarabu wake. Huu umoja unaoutaka ulishindikana mikononi mwa Nyerere mwenyewe, maana ndani ya huo umoja wengine walikuwa wanafiki na mpaka sasa hivi bado wengine ni wanafiki. Kitu kikubwa ambacho tunaweza kujifunza ni kutokana na CoW, hiyo ndioy case study ya kutuonesha ni namna gani sasa jinsi nchi za EA walivyo wanafiki.
Tukiongelea Political Federation kwamba ni kila kitu. Kweli kwa namna moja ninaweza kusema hivyo. Lakini Political Federation itakuwa na mwelekeo mzuri kama Social Federation imekaa vizuri. Mwalimu Nyerere alifanya vizuri sana kuhakikisha Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) tunaishi kwa pamoja bila kubaguana. Kitu kikubwa alicho kifanya ni kuunganisha wananchi wote na kuwa kitu kimoja. Taifa likawa na sauti moja.
Lakini tukiangalia EA Federal Republic, hakuna dalili yoyote inayofanyika kuunganisha hawa watu. Zaidi sana unafiki unafanyika chini chini ili kuvuna mali kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. Na mwelekeo huo kama nchi yenye rasmali nyiki haitakuwa makini jambo litakalotokea ni kuvuna mali na mwisho wa siku kuuvunja muungana na wachache wameneemeka na mali.
Jambo jingine ambalo tunaweza kusema ni Case study kuhusu huu muungano ni kuhusu Mradi wa bomba la mafuta toka Hoima mpaka Tanga. Hapo ndipo utakapoelewa je, hii federation imekaa vipi. Uhuni mkubwa ulitumika na kutumia ulaghai wa hali ya juu. Sasa kama kweli kuna nia ya dhati ya kuwa na federal nation kwanini kuwe na ugomvi na kununiana kwa mradi huo?
Msimamo wangu ni kwamba kwa sasa tubaki katika ujarani mwema na wale wanaoona kwamba wanaweza kuungana waungane wao. Siyo kulazimisha tuwepo wote kwa pamoja wakati socially tunatofautiana sana.
Halafu je, Ideology ya hii federal republic itakuwa socialism au Capitalism? Lazima tuelewe na kwanini tuwe katika mfumo ule? Je, kenya ipo tayari kuuacha mfumo ilionao wa kwamba msingi wa maendeleo kuwa ni mtaji(Capitalism) na kwenda kwenye mfumo wa msingi wa maendeleo kuwa ni watu(Socialism).
Hapa si jambo dogo tumeenda mbali mno. Katika muungano tutasababisha civil conflicts ambazo haina haja ya kuwepo.
Kwa mfano mdogo tu kule Loliondo conflicts kila wakati na sababu ni kwamba wahamiaji kutoka kenya kuja kuvamia protected areas na kuharibu vyanzo vya mali asili.
Mwisho naweza kusema kwamba kwa sasa tuendelee kuwa na ujirani mwema tu.