The financial times: Iran inapata faida kubwa kwenye vita, Urusi yaondolewa vikwazo

The financial times: Iran inapata faida kubwa kwenye vita, Urusi yaondolewa vikwazo

AKILI NI NYWELE, KILA MTU ANA ZAKE!

Mbali na kushambuliwa kijeshi, Iran inaingiaza zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 140 kwa siku kutokana na kuuza mafuta yalipanda bei. Hii ni zaidi ya Bilioni 300 za kitanzania kwa siku. Hii inamaanisha kwamba Iran ataendelea kupata mabilioni ya pesa kuendeleza vita na hata akiba endapo vita itakuwa imekwisha.

Upande wa pili, Marekani na Ulaya wameiondolea Urusi baadhi ya vikwazo ili kuruhusu mafuta na gesi kutoka Urusi viuzwe kwenye soko la dunia ili kuzuia uhaba na mfumuko mkubwa wa bei ambao utayumbisha uchumi wa dunia. Kuondolewa vikwazo kwa Urusi inamaanisha kwamba vita vya Ukraine vitakuwa vikali zaidi kwasababu atapata fedha nyingi kuwashinda hata Ulaya.
View attachment 3560363
​
View attachment 3560364
View attachment 3560365

Taifa ambalo linashindwa vita linaendeleaje kupata $ 140 Milion kwa siku ???

For those who thought this was only KINETIC and not also ECONOMIC I feel sorry for them....
​
Vita ni biashara ya watu sisi tuendelee kuwa mashabiki
 
1. $140m ni estimates, ngumu kuendelea kuwa hivyo muda mrefu vilevile Iran anauza oil for discount. Vinginevyo Iran apate usaidizi hapo Strait of Hormuz Iran ikisimama yenyewe itazidiwa.

2. US wamepunguza sanctions for 30 days only hiyo itakuwa hadi April 11. Bad siku 22 hivi. Hii ni faida kubwa kwa Russia/Putin. Hapa US hana leverage tofauti na hapa bei ya crude itaenda zaidi ya $150.

3. Bibi Netanyahu anapendekeza IMEC corridor kama long lasting solution, hapa cargo/oil itakuwa inasafirishwa nchi kavu, inaanzia India halafu by sea hadi UAE halafu railway kupitia Saudi Arabia na Jordan halafu wanaingia bandari ya Haifa Israel. Lengo hapa ni kuhamisha business kabisa kupitia Straight of Hormuz. India wametoa lease for life kufanikisha hii mambo.

4. Iran ikitanikiwa kufunga strait of Hormuz for at least 6 months italeta shida kubwa. Fikiria bei ya oil? Sulfur itakuwa haipiti, kumbuka sulfur ni byproduct ya oil refining. Na sulfur inatumika kwenye extraction of copper. Sasa hapa hii inaathiri kila kitu drone manufacturing, semiconductors/AI.

5. Baada ya muda US atafanikiwa ku-control strait of Hormuz. Beberu lazima atahamishia jeshi pale. Allies wake watamuunga mkono ni swala la muda tu. Kwa maoni yangu US anaenda polepole kuepuka kuharidi order iliyopo na kuumiza zaidi uchumi wa dunia. US is a $29-30 trillion dollar economy. Kifupi yupo na pumzi kubwa yakudumu muda mrefu.
 
Marekani na Israeli wamekosea mahesabu.

Malengo yao yafanana ila malengo ya kistratejia ndo shida kuelewana.

They have the same objectives but different strategic objectives.
Israel anamponda Marekani kama ambavyo Austro-Hungary aliiponza Imperial Germany.

Malengo yao yalifanana, ila malengo ya Kistratejia yalitofautiana.

Huu uzi niliandika mwaka 2024, vijana wakanipinga sana:
​
 
Lakini hii imekaaje kwani hiyo Strait of Hormuz si inamilikiwa na mataifa mawili Iran kwa upande wa kaskazini na Oman kwa upande wa kusini.

Sasa inakuwaje Iran inakuwa na the lion share..!!!??? I don't understand.
 
Hii dunia ina reserve kubwa sana ya mafuta ni swala la kuongoza uzalishaji sehemu zingine.
 
Lakini hii imekaaje kwani hiyo Strait of Hormuz si inamilikiwa na mataifa mawili Iran kwa upande wa kaskazini na Oman kwa upande wa kusini.

Sasa inakuwaje Iran inakuwa na the lion share..!!!??? I don't understand.
Hakuna anayemiliki strait of Hormuz, hii inajulikana ni international waterway. Iran anatumia leverage tu kwasababu inapita kwenye shore yake na pale ana military. In fact meli nyingi zinapita karibu na costal ya Oman 🇴🇲
 
Sawasawa na pia hiyo yafanana ni ile vita ya Gallipoli ambayo iliua watu wengi sana na hima ya Ottoman ikawa mshindi.

Lakini "behind the scene" kwa jicho la kijasusi Marekani yajiandaa kufanya "ground invasion" na itakuwa battle ambayo haijawahi kutokea na zaidi ya battle ya Gallipoli. Nimesema hapo juu Pentagon wameomba bilioni 200 ziidhinishwe na seneti.

Huenda hii vita ikawa endelevu hadi Marekani ipate inokitaka pale Iran na si kingine bali ni gramu zipatazo 450 za Uranium. Na hii watasaidiana na vikosi maalum vya NATO, IDF na Marine ambao wapo njiani kuelekea uwanja wa vita.

Kwa sasa hivi chukua yale usomayo na kuangalia kwenye runinga kisha changanya na knowledge yako ya kiuchambuzi na uelewa wa siasa za kijiografa.
 
Mahaba yakizidi akili zinapotea,huna tofauti na CCM sasa.
The Economist.jpeg


Blind Fury.png

Epic Fury 3.png
Epic Fury 4.png

Epic Fury 5.png
Epic Fury 6.png
Epic Fury 7.png

Epic Fury 8.png
Epic Fury 9.png
 
Hakuna anayemiliki strait of Hormuz, hii inajulikana ni international waterway. Iran anatumia leverage tu kwasababu inapita kwenye shore yake na pale ana military. In fact meli nyingi zinapita karibu na costal ya Oman 🇴🇲
Sehemu ya Oman inayopakana na Hormuz inaitwa Musandam Peninsula, haipakani na Oman ni sehemu ya Ardhi kama Alaska Marekani ipo independent na wakaazi wa Hilo eneo culture wise ni Wairan zaidi kuliko waarabu, Hata management yake wanashirikiana na Iran, Hilo eneo Lina milima mikali so limejitenga kabisa na Nchi za kiarabu, hata Leo hii kukitokea vita usishangae wakawa upande wa Iran.

images (1) (10).jpeg

Kutoka Musandam kwenda Oman ama UAE inabidi upande boti Jinsi milima ilivyo mikali.
 
Naona wasomi viladha wanakushukia kama mwewe!!!

Oyaaaah, hii JF wameifanyaje tena jamani!?
Msomi kiladha gani ametuletea haya mapichapicha?
Yaani siwezi kwenda next page au previous page mpaka niende tena juu kabisa mwanzo wa uzi!!?

Maxence Melo mnyang'anye kompyuta huyo msomi kiladha, anatuvurugia JF yetu.
 
Sehemu ya Oman inayopakana na Hormuz inaitwa Musandam Peninsula, haipakani na Oman ni sehemu ya Ardhi kama Alaska Marekani ipo independent na wakaazi wa Hilo eneo culture wise ni Wairan zaidi kuliko waarabu, Hata management yake wanashirikiana na Iran, Hilo eneo Lina milima mikali so limejitenga kabisa na Nchi za kiarabu, hata Leo hii kukitokea vita usishangae wakawa upande wa Iran.

View attachment 3560495
Kutoka Musandam kwenda Oman ama UAE inabidi upande boti Jinsi milima ilivyo mikali.

Upo sahihi, Musandam kama inavyoonekana hapo kwenye ramani haipakani na Oman kwa maana ya sehemu moja ya ardhi lakini bado eneo hili lipo chini ya mamlaka ya Oman. Kifupi ni mkoa wa Oman. Polisi, kodi, sheria zote zinasimamiwa na Oman kama nchi. Pia upo sahii kuhusu kuingiliana kwa tamanuni kati ya Musandam na maeneo ya coastal ya Iran.
 
Back
Top Bottom