The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

Rejea zipo nyingi nyingi ila kama unataka genuine waweza tafuta Biblia ukajisomea
Kwahiyo haya uliyo yaandika naweza kuyapata kwenye Biblia sio?

Kwenye vitabu gani vilivyomo kwenye Biblia ili nikajisomee ?
 
Heee Yesu alikua sio familia ya kifalme ila ni koo ya Ufalme..
Hawakuwa matajiri hata kidogo mkuu. Hata biblia inaelezea. Yesu alitakiwa azaliwe kwenye famili duni. Waisrael walikuwa wanategemea atatoka familia kubwa na maarufu ndio maana walimkataa kua sio yeye. Maana yesu waliyemuwaza sio aliyekuja
Hali ya kiuchumi ya familiya ya mzee Yusuph bila shaka ilikuwa ni ya kawaida tu, hakuwa tajiri kama wakina Zakayo watoza ushuru. Ndiyo maana kuna rekodi katika kitabu cha Yohana anamwambia yule mwanafunzi aliyempenda kwamba amtunzie mama yake. Ukisoma vizuri vitabu vile vinne yaani Mathayo, Marko, Luka na Yohana unaweza kupata picha halisi ya hali ya kiuchumi ya familiya ya Mzee Yusuph

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ngumu.
Nataka tumzungumzie Jesus mwanadamu
ebu nipe historia ya yesu nifahamu mkuu maria alibeba mimba yani!?na hapa unasema yesu baba yake ni joseph isije ikawa walianza kutoana bikra alafu wakaja kuoana kama tufanyavyo sisi wanadamu wa kizazi cha dot com. tunaita kutest mitambo mwisho mnazaa.nijibuni tu kwa nini akimbie kwao kama ajazini mpaka arudi na mtoto na huko alikokimbilia ni kwa nani mbona amumtaji aliekua amemuhifazi ktk kipindi chote cha ujauzito.nijibu kibinadamu mkuu kama unavyotaka
 
Duh! Hebu anza kutudadavulia; personality ni nini,na iweje Yesu alikuwa nazo 2,wengine wanazo zaidi ya 24!! Pia usisahau kututajia angalau wawili wenye nazo zaidi ya mbili,wasopungua 3
Sina muda wa kukaa nikaandika mambo marefu kwa sasa.. ila kama una muda pitia pitia usome huu ugonjwa Dissociative identity disorder (DID)
 
Sina muda wa kukaa nikaandika mambo marefu kwa sasa.. ila kama una muda pitia pitia usome huu ugonjwa Dissociative identity disorder (DID)
inakuaje mada uanzishe wewe maswali usiweze jibu mkuu mie naona wewe ni mbabaishaji tu!mie sijui kitu kitu ila tunaweza pata kitu kupitia wewe.ungemjibu huyo mdau na kujibu wengine sie tusio na jua tungepata mwanga Ebu jibu kama ngumu kumesa futa uzi wako
 
Naona wanikazimisha kujibu...
Kufuta sitafuta, maana mada haihusiani na maswali unayouliza...
 
Mleta mada mimi naweza kusema umechambua vyema sana mada yako ila umezukunguka mzunguko mrefu sana ambao ungeleta mkanganyiko mkubwa kwa wenye kuamni.

Maana huyo uliemtolea mfano pamoja na kuwa yupo kwenye safu ya Umungu lakini kila kilichotokea juu yake kilikuwa kimeratibiwa.

Kuanzia tokeo lake, kazi yake,huduma zake kwa jamii na mwisho wake yote yalikuwa ndani ya uratibu na mwenye kuratibu yupo juu ya yote juu ya vyote na juu ya wote kwa hio hakuna chochote kingechoweza kupangua mipango yake.
Na ndio maana huyo Yesu aliwahi kusema yote aliyonituma Baba nimetekeleza.
Kwa maana ya kwamba hakufanya kile alichofanya kwa niaba yake bali kwa niaba ya alie juu yake. Kwa namna hio huo ushindi ni wa yule alieratibu hayo na kwa vile hashindwi na chochote ndio maana ikawa vile ulivyosema.

Kuhusu muda huo ndio umekua mtihani kwetu sisi tuliojengwa nje ya matumizi sahihi ya muda.
Na muda pia umeratibiwa hivyo hauendi kinyuke na alie uweka. Kama wewe ama mimi tutaenda kunyume na muda tutakuwa tumevunja kanuni ya ulimwengu ambayo haijalishi unaijua ama laa bali ulimwengu utakuadhibu kwa vile ulivyo kwe na unavyotaka.
Mimi na yeyote chochote pamoja na muda tupo ndani ya ulimwengu. Na ulimwengu humpa ukinzani yule anaekwenda tofauti ili urejee kwe uhalisia laa ulimwengu utapingana nawe na kukupa maumivu.
Kwa hio muda unazingatia kusudi la alieuweka.
Muda umewekwa kwa ajili yetu na kila kilichopo.
Kama sisi hatuta utumia ipasavyo huyo alieuweka muda na kutuweka sisi atatoa adhabu.

Ukweli saa 24 zinatumika kwa tajiri na maskini.
Lakini maskini hubakiwa na maumivu zaidi ya tajiri.
Sababu yaweza kuwa kuna makosa hapo awali yalifanywa na hayajalipwa na itakuwa hivyo mpaka malipo yafanyike.

Namna gani ya kulipa upotevu wa muda, hio ni mada nyingine, lakini hongera mkuu kwa mada ilio nzuri saaana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada unasema umri wako ni miaka 20 kama ni kweli basi Mungu atakuwa amekujalia kipawa fulani. Ninachojua vijana wengi wa umri Kama wako wamejikita kwenye mambo ya kipuuzi tu . Mambo yasiyowasadia hata kidogo. Wengi wao wako kwenye vibanda wakibenti mechi za ligi za Ulaya.

Wengi wao hawana uwezo wa kusoma hata makala fupi yenye aya 10 kumi tu.

Wengi wao wake kwa waume wanashinda wakitazama thamthlia za Korea na India bila hata kuelewa maudhui ya senema hizo.

Katika umri huu mdogo ulio nao nani kakufundisha maarifa haya yote?

Nani kakupa hii hekima?

Ni Muumba wa ulimwengu ndio kanipatia kipawa hiki
 
Back
Top Bottom