The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

Mleta mada mimi naweza kusema umechambua vyema sana mada yako ila umezukunguka mzunguko mrefu sana ambao ungeleta mkanganyiko mkubwa kwa wenye kuamni.

Maana huyo uliemtolea mfano pamoja na kuwa yupo kwenye safu ya Umungu lakini kila kilichotokea juu yake kilikuwa kimeratibiwa.

Kuanzia tokeo lake, kazi yake,huduma zake kwa jamii na mwisho wake yote yalikuwa ndani ya uratibu na mwenye kuratibu yupo juu ya yote juu ya vyote na juu ya wote kwa hio hakuna chochote kingechoweza kupangua mipango yake.
Na ndio maana huyo Yesu aliwahi kusema yote aliyonituma Baba nimetekeleza.
Kwa maana ya kwamba hakufanya kile alichofanya kwa niaba yake bali kwa niaba ya alie juu yake. Kwa namna hio huo ushindi ni wa yule alieratibu hayo na kwa vile hashindwi na chochote ndio maana ikawa vile ulivyosema.

Kuhusu muda huo ndio umekua mtihani kwetu sisi tuliojengwa nje ya matumizi sahihi ya muda.
Na muda pia umeratibiwa hivyo hauendi kinyuke na alie uweka. Kama wewe ama mimi tutaenda kunyume na muda tutakuwa tumevunja kanuni ya ulimwengu ambayo haijalishi unaijua ama laa bali ulimwengu utakuadhibu kwa vile ulivyo kwe na unavyotaka.
Mimi na yeyote chochote pamoja na muda tupo ndani ya ulimwengu. Na ulimwengu humpa ukinzani yule anaekwenda tofauti ili urejee kwe uhalisia laa ulimwengu utapingana nawe na kukupa maumivu.
Kwa hio muda unazingatia kusudi la alieuweka.
Muda umewekwa kwa ajili yetu na kila kilichopo.
Kama sisi hatuta utumia ipasavyo huyo alieuweka muda na kutuweka sisi atatoa adhabu.

Ukweli saa 24 zinatumika kwa tajiri na maskini.
Lakini maskini hubakiwa na maumivu zaidi ya tajiri.
Sababu yaweza kuwa kuna makosa hapo awali yalifanywa na hayajalipwa na itakuwa hivyo mpaka malipo yafanyike.

Namna gani ya kulipa upotevu wa muda, hio ni mada nyingine, lakini hongera mkuu kwa mada ilio nzuri saaana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana mkuu kwa mchango wako maridhawa..
Kwanini Watu weusi hatujali muda hadi tunasemwa kua no hurry in Africa.? Malezi au silka yetu?
Japan watu wanapiga kazi, wanajali muda mno kuliko chochote unaweza kuta mtu anakaa kazini masaa 14
 
Mtu anabishana na Wikipedia sio mtu wa kubishana nae unamuacha tu.

Hata utumie efforts zako zote kumuelewesha hatakuelewa hata kidogo na ndio mana sikumjibu chochote aisee.

Hatari sana...!
Nduki, Wikipedia haijawahi kuwa reliable source of information for 100%. Kwa sababu mtu yoyote anaweza ku edit na kuingiza data zake.

Hata wewe ukitaka unaweza kuedit ukaweka jina lako pale juu. Hivyo mtu kubishana na Wikipedia ni sahihi kabisa kama hajaona reliable source added to it.

P.S sijui usahihi wa mnachobishana ila nimetaka kukujuza tuu hata wewe usiamini 100% taarifa za Wikipedia. Tumia Wikipedia ili kupata more reputable sources, ila kamwe usiitumie kama source.
 
Asiyejua maana usimwambie maana.
Ignorance is bless .
 
Nduki, Wikipedia haijawahi kuwa reliable source of information for 100%. Kwa sababu mtu yoyote anaweza ku edit na kuingiza data zake.

Hata wewe ukitaka unaweza kuedit ukaweka jina lako pale juu. Hivyo mtu kubishana na Wikipedia ni sahihi kabisa kama hajaona reliable source added to it.

P.S sijui usahihi wa mnachobishana ila nimetaka kukujuza tuu hata wewe usiamini 100% taarifa za Wikipedia. Tumia Wikipedia ili kupata more reputable sources, ila kamwe usiitumie kama source.

Nilichoweka hapo juu ni kitabu ambapo hiko kitabu kinazungumzia hao watu 100 then hiko kitabu ndio kikawekwa kwenye Wikipedia, sasa kwenye editing unayosema inaweza kufanyika labda mtu a-edit hiko kitabu ambapo sidhani kama kuna mtu mjinga yoyote ambaye anaweza kufanya ujinga huo.

Lakini pia, nasimamia nnachokiamini katika msimamo wangu kwa vile nnavyoamini, sasa hawezi kutokea mjinga mwengine eti aniaminishe kitu ambacho hakiniingii akilini halafu nikamuamini, kwa hilo siwezi ntamuangalia na kumuacha abaki na ujinga wake.
 
Ni Muumba wa ulimwengu ndio kanipatia kipawa hiki
Kipawa kipi ulichopewa!??Cha kuchambua vitu !??ama ufundi wa kuwasilisha mawazo ya wataalam na wanafalsafa wengine!???

Ukiwa mwanazuoni lazima ukubali na kujifunza kuwapa credit walioandika hivyo ambavyo wewe umetohoa na kuleta hapa

Plagiarism ni jambo baya sana hebu tupe vyanzo vya andiko lako hili nasi tupate kujifunza na kuchuja wenyewe!!

Niwe muwazi naheshimu jitihada zako za kujua na kuchimba vitu kwa undani ili kupata elimu mpya ila jifunze kuweka reference bila kujali ni nyingi kiasi gani

Siwezi kuweka reference maana yote hayo nayatoa kichwani. Sana nitaweka biblia ndio nilikojulia habari za Yesu.
Ila mada kama nimeitafsiri hua naweka reference.
 
Kipawa kipi ulichopewa!??Cha kuchambua vitu !??ama ufundi wa kuwasilisha mawazo ya wataalam na wanafalsafa wengine!???

Ukiwa mwanazuoni lazima ukubali na kujifunza kuwapa credit walioandika hivyo ambavyo wewe umetohoa na kuleta hapa

Plagiarism ni jambo baya sana hebu tupe vyanzo vya andiko lako hili nasi tupate kujifunza na kuchuja wenyewe!!

Sent using Jamii Forums mobile app

😀😀😀😀
 
Salute
Mnamo mwaka wa 4BC jijini Galilaya katika kitongoji kiitwacho Nazareth kulikuwa na familia ya Bw. Joseph na mkewe Maria; walipata mtoto wa kiume wakamwita Jina Yeheshua au Yesu.

Ilikua ni moja ya kaya ya kimaskini, Bw. Joseph alikua anajishughulisha na shughuli za uchakataji wa mbao yaani useremala pia mkewe Bi. Maria alikuwa anajihusisha na shughuli ndogo ndogo za mikono. Yesu alifundishwa kusoma na kuandika tu maana wazazi wake hawakuweza kumudu gharama za kumpeleka shule zaidi, lakini alisoma pia masomo ya dini kwa walimu wa kiebrania waitwao “Rabi”. Kijana huyu alikuwa akisaidiana na baba yake kufanya shughuli za uchakataji mbao.

Alipotimiza miaka 30 kijana huyu ndio nyota yake ya mafanikio ilipoanza kung’aa, alianza kazi zake za kufundisha watu kama “Rabi” mambo mbalimbali yahusiyo falsafa ya maisha. Alifundisha kwa muda wa miaka mitatu tu, so alipokua na miaka 33 alifariki dunia kwa kuwambwa msalabani na dola ya Rumi iliyokua inatawala nchi nyingi kipindi hicho.

Kosa lake lilikua ni uhaini kwa kujiita mfalme wakati nchi hiyo ilikuwa ina mtawala ambaye ni Herode na Gavana Pilato wakiwa chini ya mtawala Kaisari Tiberius, pia kuweka maandamano yasiyo na kibali.

Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe. Japo kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hapo zamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini kijana mdogo sana ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watuwote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.

Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.

Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.

Kaacha miongozo ambayo ilikuja kutengeneza taasisi kubwa yenye nguvu na washirika wengi ambayo ni Catholics. Inaonyesha watu wengi mashuhuri duniani wamepita kwenye taasisi hii au ni wafuasi wa mafundisho ya huyu kijana mdogo. Yeye ndiyo binaadamu zaidi maarufu ulimwenguni. Kaacha historia ambayo haiwezi vunjwa maisha yote maana jina lake limeshindwa kufutika. Hebu fikiria kama alifanya mambo yake kwa muda wa miaka 33 tu ila umaarufu wake unazidi kukua na wafuasi wanazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Wakuu mimi kiukweli namuonea sana wivu huyu kijana, haiwezekani kwa muda wa miaka 20+ niliyoishi hapa duniani sijawahi kufanyiwa Happy birthday, sidhani kama kuna mtu mwingine tofauti na mama anayekumbuka siku yangu ya kuzaliwa. Lakini kijana mdogo aliyekufa miaka mingi sana iliyopita karibia dunia nzima wanajua siku ya kuzaliwa kwake na hua wanasherhekea nyumbani huwa wanapika wali kabisa na kuchinja yule mbuzi mnene tuliemchunga muda mrefu halafu mimi first born kwenye kumbukumbu yangu ya kuzaliwa sijawahi pewa hata andazi.

Kinachoniumiza zaidi najua siku nikifa tu watu watanisahau mara tu baada ya kutandua msiba wangu, sitakumbukwa na yoyote kama yesu tunavyomkumbuka labda nyie wa huku JF mtanikumbuka kwa posts zangu.

Kiukweli mimi sikubali, kwanini Yesu atushinde watu wote wakati alikuwa binadamu sawa kama sisi? Tunakosea wapi? Kweli tumeshindwa kuvunja rekodi zake nasi basi tukumbukwe hata kwa muda wa miaka 10? Lakini je, huyu kijana mdogo alifanyaje hadi akaweza kufanya mambo makubwa yote haya ndani ya muda mdogo?

Maneno yote huko juu ni kuonyesha jinsi huyu kijana alivyoweza fanaya mambo mengi ndani ya muda mchache lakini kubwa la msingi ni kujua je aliwezaje? Alitumia nini?

Yesu aliwezaje?

Ukichunguza utajua kabisa huyu mtu alikuwa ana vitu anafanya ili kutimiza mipango yake hiyo yenye matokeo makubwa. Yesu alitumia vitu vitatu ili kufanya yote hayo. Kwanza kabisa alikua anajtambua (nilishaliongelea hili), pili alikuwa anafahamu kusudi lake (nitaliongelea hili panapo majaliwa) tatu alijali muda kuliko kitu chochote. Yes! Hapa ndiyo kwenye kiini cha mada yetu; Time Management. Jinsi nidhamu nzuri ya matumizi ya muda inaweza kukuletea mafanikio makubwa.

Japo Yesu hakuwa na elimu kubwa lakini alijitambua na alitambua kusudi lake mapema mno ndiyo maana alitumia muda wake vizuri sana akaweza kufanya mambo mengi makubwa. Alithamini muda wake alifanya kazi yake kwa nidhamu ya hali ya juu muda ukiwa ndio silaha yake kuu.

Kuna mtu aliwahi muuliza The Godfather Mwl. Julius Nyerere kwamba anawezaje kufanya mambo mengi kama vile kuhudhuria vikao, kuwa na familia yake, kuandika vitabu na makala kwenye magazeti, kuongoza nchi, kufanya ziara n.k kwa wakati mmoja? Nyerere alisema yeye anaheshimu muda. Muda wa kula anakula tu, muda wa kikako anakua kikaoni, kutembea anatembea tu, muda wa kulala analala tu n.k n.k

Najua humu wengi wetu hili ni ngumu sana. Unakuta mtu yupo anatembea kwenda mahali fulani lakini muda huohuo anasimama kuchat, muda wa kulala yeye anasoma kitabu, muda wa kusoma yeye anakula, muda wa kula ndiyo kwanza anaanza kuongea na simu, muda wa kazi yeye anaingia JF, muda wa kutafuta watoto yeye anapiga stori na mwenzi wake.

In short, muda hatuuthamini hasa huku kwetu Afrika, ndiyo maana Wachina wanatuendesha sana na tunaona kuwa wanatunyayasa huko makazini maana wao wamekulia kwenye malezi ya kufanya kitu kutokana na muda unaruhusu kufanya nini, sasa ile silka yao wakiileta huku twaona hawa watu wapo kama mashetani.

Kijana amka jali muda wako ulionao. Kwani nyie wenzangu hamumuonei wivu huyo jamaa huko juu aliyefanya mambo mengi ndani ya muda mfupi? Moja kati ya utajiri mkubwa binaadamu alionao ni muda.

Kama umefanikiwa kuwa na leo basi wewe ni tajiri mkubwa, leo hii ndio muda wako amka ukafanye yale unayotamani kufanya. Usisubiri kesho, kesho haipo siku zote ipo leo tu! Achana na kupoteza muda wako kwa kwenda location kupiga picha za kupost Facebook upate like 300, unadhani siku ukifa kuna mtu atakukumbuka kwa kuacha picha zenye like nyingi na quality nzuri huko FB? Sahau hili.

Yesu alijitambua mapema ndiyo maana aliweza fanya mambo makubwa, jitambue kijana mwenzangu hautakumbukwa kwa kuweza kutaja kikosi kizima kinachocheza ligi daraja la tatu huko Italy au England. Tumia muda wako huu ulionao leo kwa kufanya mambo yatakayoacha alama isiyofutika hapa duniani.

Huyo ndio Yesu the Greatest man, hakuna mtu mwingine kama yeye, hakuna atakayeweza kuvunja rekodi zake alizoacha sana tunaweza fuata matendo yake ili kufanya mambo makubwa kwenye maisha ila kumpita tuache legacy kubwa kuliko yeye haitawezekana kamwe.

Tujali muda jamani, ipo siku tutajutia huu muda tuanaopoteza kufuatilia mwanamke mmoja miezi sita halafu kila siku unatumia zaidi ya masaa 4 kuwasiliana nae wakati muda huo ungefanya mambo mengi ya msingi ndani ya miezi hiyo 6 yakamfanya huyo mwanamke akajileta mwenyewe.

Utajiri wetu mkubwa sisi watoto wa maskini ambao tunaweza kuutumia kupunguza kiwango cha umaskini kwenye familia zetu kama Yesu alivyofanya kwenye familia yetu ni MUDA. Jali muda utakutunza uzeeni.

JE WEWE BINAFSI NI NANI UNAONA NI GREATEST MAN ALIYEFANYA VITU VIKUBWA AMBAE TWAWEZA KUJIFUNZA KUPITIA YEYE?
Ahsanteni.
Like & Share

Da’Vinci
El maestro.
You are so genius, be blessed, so touching with some morals

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuwahi kujua kama kazi ninazoziona alizofanya Yesu, zilifanyika ndani ya miaka mitatu tuu. Mitatu tuu? Hili nimelijua leo.

Kwa hiyo huyu Yesu ni mtoto wa Joseph?. Joseph ndio alikuwa biological father wa Yesu?.
That's interesting!!!.

Asante sana umetushauri vizuri kwenye jambo zima ya time mgt , kuutumia muda tulionao kwenye matumizi mazuri. Kufanya jambo kwa wakati wake.

Good Job!
I unfeigned appreciate you madam Paula, I always get in touch with the way you are organized, It sounds so amazing when I see this name Paula Paul, speaking not in a clandstine you're so amazing!
Bravo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sipati picha mtu unasubiria kufanya mambo uzeeni halafu yaende tofauti na hapo tayari ni mzee. Stress zake ni kama za huyu jamaa 'dr shika'.
Dr shika ni mtu mwenye iq ya pekee, very smart person lakini kuna ins zinamsumbua

Nilichojifunza kupitia scenario ya mzee Shika na ushika wake ni just a curse toka kwa wazazi wako au ukoo, amini kuna makabila wako very sensitive sana ukijifanya wajua, that man anasumbuliwa na laana,nduguze wamekwisha lakini hakuwahi kukanyaga home kwao hata alipopata pesa aliishia kutanua karibu na kwao nauli kama ten afike lakini hakuona maana, tusalini lakini kitu mizimu ni ya kuacha kama ilivyo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hee mkuu nakuaminiaga unajua vitu vingi ila leo umeni dissapoint. Kumbe inawezekana na wengine hawakuona jina la muhamad kwenye hii post..
Hebu angalia mtu namba 2 yupo yeye.
Inawezakana wengi hawalijui jina halisi la muhamad
Hahaha aise Yeah nimeona now .....but Muhammad Jina la baba Yake sio hilo uliloandika .... anaitwa Muhammad ibin abdillah ...ukisema ibin Allah kwa waumini wa kiislam watadhania kuwa una maanisha kwamba ni mtoto wa Mungu wao ...... Any way asante ngoja niifute ile comment Yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom