Wewe unaelewa hivyo ulivyo eleza; ambavyo siyo lazima iwe sahihi.
Hujaeleza huyo anayewekeza yeye anafaidika vipi na uwekezaji huo; na wala huelezi atakuwa akifanya shughuli zipi kwenye hiyo misitu.
Hujaeleza chochote, kama sisi wenyewe kama taifa hatuwezi kuifanya hiyo kazi na kwa nini iwe lazima kumpa huyo mwekezaji.
Hujatueleza hata kidogo, makubaliano na huyo mwekezaji yapo vipi, bila shaka utasema ni siri- kwa nini iwe siri kutumiwa mali zetu na watu wengine? Husemi chochote kuhusu huyo mwekezaji alipatikana kwa njia zipi, au nayo ni siri? Palikuwepo na ushindani wowote, au yeye mwekezaji kawatafuta tu Samia na ndugu zake wakakubaliana juu ya mali asili zetu?
Wewe husemi chochote kabisa kuhusu uwajibikaji wa hii serikali kwetu sisi wananchi wake. Unachojuwa wewe ni kuwa serikali na viongozi wake hawana wajibu wowote kwetu, wanaweza tu kujiamria lolote wanalotaka kufanya wao, liwe na faida au hasara kwa taifa letu hayo sisi hayatuhusu!
Watu wa aina yako ndio sasa mnao tamba sana katika nchi hii, lakini mwisho wenu utawadia tu.