The Guardian (UK)- UAE owns 8% of Tanzania’s forest

Uzunguni huwa hawakai kimya huwa wanaongea ukweli tena bungeni au kwa waandishi
Rejea Braverman alipotimuliwa, ila umasikini unafanya watu wawe dhalili
 
Huko Quora (Mtandao wa watu wenye Akili ) kuliwahi kuwa na mjadala jamaa huu ,jaribu kuingia humo muone watu wanavyoshusha NONDO
Kuna watu waliandika pia issues hata mimi nimeandika humu
 
Halafu wanakataa kuwapa uraia pacha diaspora wenye vinasaba vya Tanzania ili kuwazuia kuwa na uhalali wa umiliki wa ardhi.
Acha watuonee, ila tupigieni kelele tuje kuwekeza jamani
Wao wanaleta unafiki ooh hati maalum
Yaani vitu vya ajabu tu ili mradi raia wa nje apewe anachotaka si mzungu wala mwarabu wote
Na unajua kwanini?
Wao wanahonga hela ndefu
Mimi wanajua siwezi kuwapa mamilioni ya dollars
 
Carbon credits si strength yako! Kununua carbon credits through CDM si Kununua ardhi! So wacha kupotosha! Hamna tatizo UAE Kununua cc zinazotengenezwa na 8% equivalent of our forest!

sasa nani unayemwambia anapotosha? mimi au the Guardian?
 
Upotoshaji upo hapa! Carbon credits ni kulipia emissions rights! Kijakazi
 

Wanakuja kuwatimua masikini kwenye ardhi tuliyobarikiwa na wanafaidi wao
Hapo unafikiri waliowapa wamepewa kiasi gani cha fedha na tamaa zao
Hawa ndio wanapeleka wafanyakazi wa ndani uarabuni badala ya wauguzi
Wanajali matumbo yao tu
 
Tatizo ni hongo mkuu, viongozi wanapewa hela ndefu sana
Yaani madili mwisho wameanza kutuuza kuwafanyia kazi za nyumbani huko uarabuni
 
Sasa nenda Google ujue what's carbon credits and what's clean development mechanism!

siyo mimi niliyoandika hiyo article, the Guardian ni renowned newspaper Dunia nzima linasomwa na kila mtu kama wewe unajua kuliko wao unaweza wasahihisha, mimi nimeleta article kama ilivyo sijaiandika …
 
Mkuu 'Kimbukiko', heri ya wewe unaweza hadi kujua mipangilio ya biashara hiyo; huko vijijini wanajua lolote kuhusu haya mambo?

Badala ya kuanza kuuza maeneo yetu, kwa nini huu usiwe mjadala mzuri wa kuwa elimisha wananchi, ili na wao waweze kushiriki?
Hawa wananchi huko vijijini hawajui lolote. Kitakachotokea ni hapo watakapo anza kuambiwa hawana ruhusa kuingia na kufanya shughuli yoyote katika baadhi ya maeneo ya nchi yao, ambayo yamegawiwa kwa wageni kinyemela.

Hivi watu wa nchi hii hawana haki ya kushiriki na kunufaika na mali za taifa lao? Tunaambiwa tutanufaika kwa kupata kazi za upagazi, siyo!
 
Upotoshaji upo hapa! Carbon credits ni kulipia emissions rights! Kijakazi
Upo kwenye dili nini? Umelipwa kiasi gani?

Nini kimepotoshwa na BBC na The Guardian?
Haya masoko yapo tayari EU, China ila sio kwa mfumo huu mnaouweka.

DP world mlisema hivihivi kabla TEC haijaingilia kati na wadau wengine kupiga kelele kama Primof Shivji, Sauti ya Watanzania nk.

Ngorongoro na Loliondo mlisema ni upotoshaji pia.

Mikataba mingine ni ipi mliyosaini huko na mtayosaini sasa mpo huko Dubai kisirisiri?
 
Tatizo kubwa bado hapa nchini ni ujinga. Watu hawajua kuchambua habari na kuzifahamu.
Carbon credit haina maana unauza msitu au nchi nyingine inaumiliki, ni kutumia misitu yako kujipatia pesa bila hiyo misitu kukatwa au huyo anaenunua kuja kuishi hapo au kumiliki chochote. Serikali ikiamua kubadili matumizi ya hiyo misitu na kufanya miradi mingine basi hapo mapatano yanaishia hapo.
 
Je kwa private individual anaweza kuingia makubaliano hayo?
 
Kwa private individual anaweza kufuata utaratibu upi wa kuweza kufanya hii biashara ya Carbon Credit ?
 
Je inahitaji msitu wenye ukubwa gani minimum kuingia hiyo contract?
 
Wewe unaelewa hivyo ulivyo eleza; ambavyo siyo lazima iwe sahihi.

Hujaeleza huyo anayewekeza yeye anafaidika vipi na uwekezaji huo; na wala huelezi atakuwa akifanya shughuli zipi kwenye hiyo misitu.
Hujaeleza chochote, kama sisi wenyewe kama taifa hatuwezi kuifanya hiyo kazi na kwa nini iwe lazima kumpa huyo mwekezaji.
Hujatueleza hata kidogo, makubaliano na huyo mwekezaji yapo vipi, bila shaka utasema ni siri- kwa nini iwe siri kutumiwa mali zetu na watu wengine? Husemi chochote kuhusu huyo mwekezaji alipatikana kwa njia zipi, au nayo ni siri? Palikuwepo na ushindani wowote, au yeye mwekezaji kawatafuta tu Samia na ndugu zake wakakubaliana juu ya mali asili zetu?

Wewe husemi chochote kabisa kuhusu uwajibikaji wa hii serikali kwetu sisi wananchi wake. Unachojuwa wewe ni kuwa serikali na viongozi wake hawana wajibu wowote kwetu, wanaweza tu kujiamria lolote wanalotaka kufanya wao, liwe na faida au hasara kwa taifa letu hayo sisi hayatuhusu!

Watu wa aina yako ndio sasa mnao tamba sana katika nchi hii, lakini mwisho wenu utawadia tu.
 
Aisee
Nyinyi Waha ni wabishi sana, japo wanasema bisha ueleshwe nyinyi huwa mnapenda ligi...
Hivi unaelewa maana ya Carbon Credits jinsi inavyofanya kazi?
Kwa hiyo unataka tuifanye wenyewe na nani? na nchi gani?
Hakuna hiyo kitu tufanye wenyewe, kwenye soko la Carbon Credits
Ni hizo nchi zinazotoa mafuta ndio zinatakiwa zikusanye carbon credits, au kwa vile tuna mawese ya Kigoma basi na sisi tukusanye wenyewe kwa mpango upi?
Hamuwezi kuachwa mkusanye wenyewe carbon credits, mtachakachua vifaa vya upimaji, wabongo wezi kila kona,

Kama hutaki ni basi unakaa na misitu yako, na siku ukitaka kununua mafuta huko wanakucheki kama uko kwenye soko la carbon credits kama haupo, unakula bei ya kuruka, na matokeo mnapiga kelele kiwese kikipanda bei....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…