Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uliza lolote tu mkuu wala usihofu tupo hapa kujifunza.
Hiyo hofu unayoisikia ndani mwako kuna mawili..
✓Ni self-defense nafsi yako inatengeza ili usijepata maumivu tena kama uliyoyapata nyuma. Hivyo inafanya hivo kukulinda yasikukute mabaya. So inawezekana ni hofu tu iliyotengenezwa ila hakuna ukweli.. since we create our own demons in the mind wakati kiuhalisia hakuna demons.
✓Inawezekana kabisa nafsi yako ishatambua kuna hatari huko mbele na inajaribu kukuonya..
[emoji117][emoji1371]Nini kifanyike..?
Usidharau onyo lolote unalopewa na sauti ya ndani yako, cha kufanya anza kuchunguza taratibu na kuweka mipango ya kuthibitisha kama kuna penzi kweli hapo au unachezewa
Mtu anahudumu kwenye Yoga. Au mcheza yoga anaitwa Yogi. Wakiwa wengi ni Yogis.Yogis ni nini?
Yes a life of purpose but what purpose.Purposes ziko mbili tu,for God or Satan na hizi purposes zote mbili zina a silent voice!For Gods' purpose is the Holy Spirit and for Satan is the voice of Satan or his Demons.Ni nani ambaye ana Roho Mtakatifu?Ni Mwana wa Mungu tuu,yaani yule ambaye amempokea Bwana Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yake.The rest itakuwa whispers of satanic entities.View attachment 1485284
Salute.
August 17 mwaka 2018 niliweka mada humu ambayo inakichwa cha habari kisemacho “ https://www.jamiiforums.com/threads/watu-wanasema-mimi-ni-nani-swali-alilouliza-yesu-linalofungua-ubongo-wa-mwanadamu-kujitambua.1469399/post-27991776“. Lengo kuu la mada hiyo ilikua kumfanya mtu ajiulize maswali ambayo yatamletea majibu ya kujitambua kwamba yeye ni nani, Bahati mbaya mada hiyo haijibu moja kwa moja kwamba “wewe ni nani?” Ili ujitambue wewe ni nani lazima uanze kujua kusudi lako (purpose) ni lipi ndio utapata jibu kua wewe ni nani hasa. Hivyo basi mada hii ni Sequel ya mada hiyo ya mwaka 2018, Kwa mpangilio uliosahihi ili uelewe vizuri concept hii ya kujitambua mimi ni nani na kusudi langu ni lipi.
Kila mwanadamu ana kitu Fulani kilchopo ndani ya kichwa chake kitaalamu wanaita Internal Monologue au self-talk au inner voice. Hii ni sauti Fulani ipo ndani ya vichwa vyetu hua ni sauti ndogo tena ya upole sana, Sauti hii imeundwa na kitu kinachoitwa Self –Concept au sense of self. Self-Concept ni ile hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future selves (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo).
Self-schemas: katika saikolojia na sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Kama tulivyoona hapo juu kwamaba inavoice imeundwa na self-concept, self-concept ndio hupelekea mtu kuweza kujitambua kwamba yeye ni nani, hivyo basi vyote hivi humuweka mwanadamu aweze kujitambua na kujielewa.
Kusudi (Purpose)
Kila mwanadamu ameumbwa kwa “Kusudi/Purpose” Fulani, Hili ni lengo kuu lililofanya tuumbwe na kuwekwa hapa duniani, ukifungua kitabu cha Katekismu katoliki swali la kwanza kukutana nalo linauliza kwanini Mungu kaniumba? Mungu katumba ili tumwabudu na kumtumikia. Hilo ndio kusudi au lengo kuu lililofanya sisi tuumbwe na kuwekwa hapa duniani, si vinginevyo! Lakini mbali na hilo kusudi kuu pia kuna kusudi ndogo ambayo kila mtu kapewa tofauti na mwingine, Lakini pia unaweza kuta kusudi lako linafanana na mwingine.
Wakati mungu anamuumba mwanadamu mwili wa mwanadamu ulikua ni kasha tu au kama mdoli au kipande cha mgomba tu ambao haujui chochote, Mungu alimuwekea mwanadamu pumzi yake ya uhai (Roho) akapata uhia na utambuzi, kama pumzi hiyo ilitoka kwa Mungu basi nayo ina uungu ndani yake. Roho imeundwa na Mind,intellect na Impression..subconcious mind iliyopo ndani ya Mind ndio sehemu kuu ya Roho, Subconcius Mind ndio data bank yako yaani inahifadhi taarifa zako zote,imani yako,Ujuzi na utambuzi wako,kumbu kumbu zako lakini kubwa zaidi ndio sehemu inayohusika na mfumo wa kukuongoza wewe. Huko juu tumeona kwamba kila mtu ana sauti Fulani iliyopo ndani yake, yaani ndani ya Mind yake…Sauti hiyo imeundwa na self-Concept ambayo inakuwezesha kutambua wewe ni nani lakini pia tumeona kwamba Subconcious Mind ndio inahifadhi kila kitu kwa mantiki hiyo Tunaweza kusema kwamba Sauti ile ndogo ambayo tunaisikia ndani yetu inatoka ndani ya Subconscious mind ambayo ipo ndani ya Roho. Roho imewekwa na Mungu hivyo ile sauti ndogo ndio wewe (Who you are) maana muda wote kama umeisikiliza kwa makini hua inakuambia mambo mema tu, muda mwingi hukushauri na kukumbusha ulipotoka, ulipo na unakoelekea. Muda mwingine hukuonya kwa kukukumbusha adhabu ambazo unaweza kuzipata kama utaacha kuishi ndani ya kusudi kuu kwa kuhitimisha sasa tunaweza kusema kwamba ile sauti ndogo inatoka ndani ya Roho mtakatifu-Mungu aliye ndani yako.
Sauti ndogo ile ndio hutuelezea kusudi la maisha yetu hapa duniani, bahati mbaya kwa ukiburi na kujifanya tuko wabize sana maishani hua hatuna muda wa Kusikiliza sauti ndogo iliyo nadani yetu ili tujue kusudi letu…. Kua makini Yule mwovu hua anatuma Virus kushambulia server zako rohoni ili kuinterupt request zote zinazotakiwa kua processed mwisho unajikuta unamsikiliza yeye. Mwovu kautawala mwili anatumia mwili wako kuivamila roho yako. Ndio maana unakuta sauti ndogo ile inataka ufanye kitu Fulani chema, kumbuka yeneyewe haiwezi tenda inategemea mwili, bahati mbaya roho inakuta Shetani kashafunga Firewall na Virus kibao kwenye mwili, mwili unakataa request za kutekeleza yale mema roho inayotaka unakua unaprocess request za kwenda kufanya yale mwili upendayo kama starehe. Cha kufanya ni kuinstall Antivirus za maombi na matumaini kwa muumba wako
Unaishi ndani ya kusudi/mpango wa Mungu?
Mfumo wa maisha yetu ya dunia ya sasa ukiangalia unaweza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu jinsi tunavyoishi. Ukichunguza kwa makini utaona tunaishi katika mfumo Fulani ambao watu walikaa wakaunda. Kwamba mtoto akizaliwa akue aende shule, akimaliza shule atafute kazi au kuoa kisha aanzishe familia yake na kuihudumia kwa kujitafutia kipato. Lakini je hivyo ndivyo muumba aliumba tuishi? Unaweza kuona mtu maisha yake yote anayatumia kwenye mahangaiko ya kutafuta maisha, je tulikuja duniani kutafuta maisha? Jibu ni NO. hatukuja kutafuta pesa wala utajiri duniani, hatukuja kutembea hapa duniani kuna kitu Fulani tumeletwa kuja kukifanya na si kutafuta maisha wala utajiri.
Inawezekana sisi waafrika ndio tunaongoza kutokuishi ndani ya kusudi letu tuliloumbiwa kutokana na mfumo mgumu wa maisha yetu, lakini kwa kiasi Fulani tunaishi ndani ya mpango wa Mungu alivyotaka. Tunaishi kijamii baina ya mtu na mtu, shida na raha tunachangia majirani. Lakini kusudi la kila mmoja mmoja mmoja hatuliishi. Mtu anaamka saa 10 usiku kila siku kwenda kujitafutia kipato, anayatumia maisha yake yote kutafuta pesa za kujikimu. Mwisho anafika uzeeni hajapata alichosumbukia maisha yake yote, anakufa hajui kama maisha yana maana kubwa zaidi ya kutafuta pesa.
Ukipata muda kaa jichunguze mfumo mzima wa maisha yako kuanzia asubuhi mpaka usiku, toka ulipozaliwa hadi leo ulipo. Je unavyoishi ndivyo ilitakiwa iwe? Je ni kweli ulikuja
Je nitalifahamu vipi kusudi langu..?
Kwanza kabisa ili ujue kusudi lako inabidi uelewe kwamba wewe ni nani? Ulitoka wapi? Upo wapi na kwa sababu ipi? Na nitaelekea wapi? Majibu ya maswali haya yote yanajibiwa kwamba “kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vionekanovyo na visivyonekana na vyote viliumbwa kwa kusudi yake na kwa ajili yake” Wakolosai 1:16
Kama unataka kujua kwanini upo duniani hapa inabidi uanze kumkiri Mungu muumba wako kua ndie aliyekuumba,ulizaliwa kwa kusidi lake wazazi wako hawakupanga wewe uzaliwe ni yeye ndio aliyepanga uzaliwe. Hukutokea duniani hapa bahati mbaya, huwezi kulifahamu au kutambua kusudi la maisha yako kama hutoanza Kumtanguliza muunmba wako kukuonyesha kusudi alilokuumbia. Kila mtu kaumbwa na kusudi lake hapa duniani bahati mbaya wengi hatuishi ndani ya kusudi letu maana hatumuweki mbele Muumba wetu atujulishe kusudi letu, Lakini pia kwa hali ya ajabu kabisa usishangae kusudi lako likawa lipo tofauti na wengine kwa kiasi Fulani..Kuna watu wameletwa hapa duniani wao kusudi lao kuu ni kusaidia watu wengine wanatimiza makusudi yao. Kwa mfano Yohana mbatizaji alikuja duniani kwa ajili ya kukahakikisha kusudi la Yesu Kristo linatimia kwa kumuandalia njia. Pia mitume wa Kristo kusudi lao ilikua kusambaza kusudi la Kristo kwa walimwengu wote. Mungu ndie aliyekuumb naye ndio anayejua kusudi lako ni lipi, mwambie akuonyeshe kusudi lako.
Maana ya maisha yako hapa duniani utaijua kama utalijua kusudi la maisha yako, kusudi la maisha yako linatoka kwa Mungu. Muombe Mungu akujulishe kusudi lako atakueleza kwa kupitia ile sauti ndogo iliyopo ndani ya roho yako. Chukua muda wako sikiliza sauti ndogo iliyo ndani yako inakueleza nini, siku zote kusudi lako hua ni jema machoni pa watu wanaokuzunguka na mbele za Mungu muumba wako. Sikiliza ile sauti inakuambia ufanye nini, kitu chema..anza kukiishi.Binafsi nilikua nikiona watu wanaoomba barabarani naogopa kukutana nao pengine nawakwepa, nikiona watu wanashida roho inaniuma sana ndio nikajua roho yangu inataka nifanye nini kuhusu watu wenye shida.I pledged and dedicated my life to those who need help, hatakama itakost uhai. Bahati mbaya bado sijafika hatua nayotaka hasa.moja ya kitu nifanyacho ni kushare na wenzangu chochote kile kilichopo ndani ya akili yangu-for free.
Nyie hamuwaonei wivu baadhi ya watu waliosihi ndani ya kusudi lao, wameacha alama duniani mpaka leo tunawakumbuka. Namuonea wivu sana Nyerere,yesu,newton,Da’Vinci,Mother Teresa,Paulo,St.stephano nk nk. Natamani siku moja niishi ndani ya kusudi langu kwa asilima japo 60% hata nikifa niwe nimekufa kihalali. Maana dunia na wakazi wake watakua wamefaidika uwepo wangu hapa duniani.
“Mungu anasema Nilikuumba katika fikra zangu kwanza kabla ya kukuweka tumboni mwa mama yako, nilikujali toka siku unazaliwa. Nitakujali ukiwa kijana mpaka ukiwa mzee na siku zote za maisha yako. Maana mimi ndio nilikuumba na nitakujali”
Ahadi za Mungu ni timilifu, akisema anatenda. Japo tunamkosea pakubwaaa ila anatujalia mengi sana tuliyomuomba na mabayo hatujamuomba. Usiokope kumuuomba muumba wako akujuze kusudi lako, yeye ni muumba wako na baba yako, Onyesha utii japo kidogo juu yake uytaaona neema nyingi maishani mwako. Hukuumbwa uje kubeti,kuibia watu, kua karaha na kikwazo kwa wenzako, kuja kuua watu, kuja kuonyesha umahiri wako wa kua na wanawake/wanaume wengi kwa wakati mmoja.
Miasha ni mafupi mno, ukiyaangalia unaweza kuona hayana maana tumekuja kupoteza muda tu hapa duniani bora tusingezaliwa. Huwezi kuona maana ya maisha yako kama hujajitambua. Ukijitambua utajua kusudi la maisha yako na maisha yako utayaona yana maana kubwa. Hivyo basi tusikilize sauti ndongo iliyo rohoni mwetu inayotoka kwa Mungu inatuambia kusudi jema la maisha yetu, tukishajua kusudi letu tutajitambua na maisha yetu yatakua yenye maana kubwa hapa duniani.
Be Humble,Be kind. Life is too short and full of surprises.
-The End...
{comment,like n share}
View attachment 1485282
~Da'Vinci
Hiyo isikusumbue sana mkuu,kwa kuwa katika matamanio yako hayo unaweza kumkosea Mungu.Remember God does not concern Himself with what you do to the World in pride,but rather what you do to him and others in Agape love.Ishi maisha matakatifu,kama unaweza kuwafanyia cho chote wanadamu wenzio do it,but in Agape love,kama huwezi jizatiti kumpendeza Mungu.Los angelitos: Je, siku ukiondoka dunia na watu watakukumbuka kwa lipi...?
Mates,Moja kati ya maswali ambayo hua najiuliza kila siku ni je ikitokea leo nikaondoka je jamii iliyonizungukai tanikumbuka kwa yapi? Je dunia itanikumbuka kwa lipi/jambo lipi nililoitendea? au ndio nikiondoka watanifukia tu na kunisahau au watabaki wananikumbuka kama mtu niliyefanya kitu...www.jamiiforums.com
Purpose ya Maisha ni Nini?Kwa yogis wenzangi hii inaitwa Divine Sound na mshirika wake ni Mwanga wa Milele yaani Divine Light.
Purpose ya Maisha ni Moja tuu. Zingine ni makoseo ya True Purpose.
The purpose of life ni kumtumikia Mungu in any way which pleases him mkuu.This includes to make others know God and his Son Jesus Christ,to be of service to others,to live a righteous life etc.etc.Purpose ya Maisha ni Nini?
vipi kuhusu mohammadThe purpose of life ni kumtumikia Mungu in any way which pleases him mkuu.This includes to make others know God and his Son Jesus Christ,to be of service to others,to live a righteous life etc.etc.
Usinipeleke huko,mwenye macho haambiwi tazama.vipi kuhusu mohammad
Huku ni kupunguza utukufu wa Mungu. Hakunaga vitu viwili au nguvu mbili. Hapa kuna Mungu tuu. You and everythings sorrounds you, are part of One, the almight God. Na upo hapa kuushuhudia ukweli huu na kuukubali. That is the purpose of life. Mapungufu yote uyapatayo ni darasa iliujifunze mpaka pale utakapobarikiwa kugundua ukweli. Only that you are looking for answer of life in wrong directions, the outside, to the space, science, books bad enough using your limited mind. The answer is just there with you, in you.Yes a life of purpose but what purpose.Purposes ziko mbili tu,for God or Satan na hizi purposes zote mbili zina a silent voice!For Gods' purpose is the Holy Spirit and for Satan is the voice of Satan or his Demons.Ni nani ambaye ana Roho Mtakatifu?Ni Mwama wa Mungu tuu,yaani yule waambaye amempokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.The rest itakuwa whispers of satanic entities.
To know YourTrue Self, to know the TRUTH, to join the holy Oneness.Purpose ya Maisha ni Nini?
Hizo sauti japo ni tofauti lakini kwa usikivu wenye concetration utagundua zime originate from one source, hiyo source inabadilika frequency kuwa fine and deeper zaidi ya namna saba. Hii sauti ina faida sana kwa nafsi yako hasa kupata self realization.Sahihi.. Shetani na Mungu zote sauti zao ni silently. Ila utazitofautisha kwa sababu Devil's voice ina Command utende kitu ila God's voice ina please utende kitu fulani.
Lakini hata ambao hawajampokea still bado roho wa Mungu huja kuwakumbusha mkuu
Wewe mkuu unamuamini Mungu kweli?Mbona Biblia iko wazi sana kuhusu the two opposing forces.Go back and read the Bible.Huku ni kupunguza utukufu wa Mungu. Hakunaga vitu viwili au nguvu mbili. Hapa kuna Mungu tuu. You and everythings sorrounds you, are part of One, the almight God. Na upo hapa kuushuhudia ukweli huu na kuukubali. That is the purpose of life. Mapungufu yote uyapatayo ni darasa iliujifunze mpaka pale utakapobarikiwa kugundua ukweli. Only that you are looking for answer of life in wrong directions, the outside, to the space, science, books bad enough using your limited mind. The answer is just there with you, in you.
Swali jepesi kwani shetani kaumbwa na nani? Au kajiumba?Wewe mkuu unamuamini Mungu kweli?Mbona Biblia iko wazi sana kuhusu the two opposing forces.Go back and read the Bible.