The Inner voice: Sauti ndogo iliyo ndani mwetu ikitueleza kusudi la maisha yetu

The Inner voice: Sauti ndogo iliyo ndani mwetu ikitueleza kusudi la maisha yetu

Mwanzoni nilijua Yaga it's just Exercise kumbe ni dini mkuu...??
Dini ni Imani, ambayo inafanana na ukweli, lakini bado kuna chembechembe za doubt , ile iwekweli basi inabidi uelimike na kujua kweli. Kwa lugha nyingine kuna tofauti kati ya kuamini na kujua. Dini zina dili na kuaminisha (kukujenga kiimani), Yoga inadili na kukufunza namna ya kujielimisha. (Exercise to learn Spiritual knowledge). Ni sawa na kusema pale dini inapoishia ndio yoga inapoanzia.
 
Naomba uniambie dini inaishia wapi na Yoga inaanzia wapi
Labda mfano wa walimu hawa utajibu swali lako:

Mwalimu A: Amini kwamba Mungu yuko mbinguni na anataka umwabudu kwa nguvu zako zote (anaonyesha na njia za kumuabudu mungu) ili ukifa na ukizikwa siku ya mwisho atamtuma mwanae waki pekee aje akufufue upae na mbinguni utaishi milele.

Mwalimu B: Mungu yupo, mimi ni mwanae, ukiniamini nitakukuonyesha njia ambayo ukiifuata na kutembea mpaka mwisho, utagundua siri kuwa wewe sio hivyo ulivyo bali feki sio nafsi yako ya kweli, kwa nafsi ya kweli wewe ni mzima milele.

Mwisho wa mwanafinzi wa Ml. A sawa na dini mwisho wake ni kuamini. Hajui hata kama sio kweli.Jibu ni baada ya kifo. Hakuna namna kumkabili Mwalimu hata kama kakudanganya.

Yoga ni Mwanzo wa mwanafunzi wa Ml. B anawajibika ketekeleza kwa vitendo na kujituma kupita njia aliyo onyweshwa. Ili athibitishe without doubt kuwa ni kweli. Guarantee yeye na ml. ni kufika mwisho wa njia na unaweza kumkabili mwalimu na kuachana nae kama analeta longolongo.

Ml. A anajenga Imani = Dini.
Ml. B anatoa elimu = Yoga.

Wanafinzi wa Ml. B alianza Ml. A ila alimalizana kuamini akaamua kutafuta ukweli.

I hope umeelewa.
 
Relax mate.. Think about your mother how she loves you and she don't want to lose you.
Alikupenda huyo mwanamke?? Uliona pendo lake ni la kweli kwako??
Nliliona ni la kweli maana alinitaka mwenyewe ila siamini kilichotokea mbaya zaidi matukio yamefuatana ata sielewi kaka niko kwenye giza nene
 
Thanks nimejifunza but bado nastruggle kujua kusudi langu apa duniani I think Natakiwa niwe karibu na Mungu zaidi ili Mungu anifunulie
Huu uzi waliupeleka jukwaa la dini......unaweza kukupa mwanga kiongozi
Salute comrades
NB: bandiko hili nimetumia maandiko ya biblia hata kama unaona haikuhusu nakusihi endelea kusoma unaweza pata kitu.

Katika dunia yetu hii tumeona ni sentensi ya maneno kadhaa tu ndio imeubadirisha huu ulimwengu wetu na kuufanya uendelee. Unaweza kuona sentensi kama vile Newton’s laws of motion zilivyochangia maandeleo ya dunia yetu karibia asilimmia 50 ya maendeleo ya ulimwengu yanaweza kuwa yameletwa na hizo sentesi (laws) tatu za mwanasayansi Issac Neawton kiteknolojia, kiuchumi, pia katika mafunzo ya kiroho hizo laws tatu zinafanya kazi. Au unaweza kuona formula ya E= mc2 ya mwanasayansi Albert Einstein ilivyopelekea mauaji ya mamilioni ya watu huko Hiroshima na Nagasaki Japan, aidha mwanasayansi toka ugiriki Archimedes sentsnsi yake kuhusu kuzama na kuelea kwa kitu ilivyoleta maendeleo makubwa kwenye usafiri wa maji nk. Hivyo unaweza kuona kua hua ni sentensi au maneno ya mtu ndio yameleta makubwa hapa duniani baada ya kuchambuliwa na kufanyiwa kazi.

Swali alilouzaYesu wanafunzi wake linavyowasha taa ya kujitambua kichwani mwa binaadamu.

Luka 9:18-21 "Yesu aliwauliza wanafunzi wake kua je makutano hao wanasema ya kua mimi ni nani? Wanafunzi wake wakajibu yohana mbatizaji wengine wanasema wewe ni Eliya lakini petro akamjibu kua Ndiwe Kristo wa Mungu".

lengo la mada yangu ni kufundisha juu ya mtu kujitambua yeye ni nani (to know your identity), katika swali hilo alilouuliza yesu unaweza kuona ni swali rahisi tu lakini likichambuliwa limebeba ufunguo wa kufungua akili ya mtu kujitambua.
Maneno ya muhimu kwenye swali hiyo ni watu wanasema mimi kua ni nani? Yesu alipouliza swali hilo sio kwamba alikua anataka wamwambie jina lake hasha alitaka afahamu je watu wanamjua yeye ni nani, ndipo petro anamjibu kua ni Kristo wa Mungu. Je nawe ushajiuliza wewe ni nani na watu wanasema wewe ni nani? Twende nikupatie majibu.

Mimi ni nani?
Hapo ulipo anza kujiuliza maswali haya na ujijibu mwenyewe,
Je hivi nilivyo ndivyo natakiwa niwe? Yaani ukijiangalia tabia zako, matendo yako ndivyo unatakiwa uwe? Jibu unalo.

Watu wanasema mimi ni nani?
Ulishwahi kuona mtu Fulani akitaka kumchumbia binti Fulani anaanza kwanza kuulizia kwa watu wanaomfahamu kama vile majirani, mrafiki ni kwasababu watu wa pembeni wanakufahamu zaidi, je leo hii wewe memba mwenzangu wa jf mtu akiuyliza jirani zako kua wewe ni nani atajibu vipi? Je unatabia nzuri, unatabia mbaya, mpole, una hekima, mwizi n.k. jibu unalo mwenyewe.

Rafiki na ndugu/ wazazi wangu wanasema mimi ni nani?
Je mtu akija leo hii kwenu akauliza wazaizi wako nao wakasema ukweli kuhusu wewe bila kuficha kitu watasema wewe uko vipi, kuna watu wakiwa mbele za watu wanaficha tabia zao mbaya wakiwa mbali na kwao lakini wakiwa kwao wanatabia chafu. Mfano unaweza kuona msichana akiwa mbele za watu anakula chakula kidogo mno lakini akiwa kwao hadi anagombania chakula na wadogo zake.

Mungu anasema mimi ni nani?
Hivi ulishawahi jiuliza unahisi Mungu wako anafahamu wewe ni nani, je wewe ni mpole, mwenye dhambi, mchaji, mwenye hekima n.k. kumbuka kabla ya kutungwa kwenye mamba ya mama yako ulianza kutungwa kwenye fikra za Mungu kwahiyo anakufahamu zaidi unavyojifahamu. jibu unalo mwenyewe.

Kwanini nipo hapa duniani?
Ushajiuliza kwanini upo duniani nab ado upo hai na mzima wa afya wakati kila siku watu wanafariki na wengine ni wagonjwa hawajiwezi. Upo hapa duniani tumtumikie mungu na kumuabudu. Utafahamu kusudi lako (purpose) mungu kukuumba na kukuweka hapa duniani kwa kumcha na kumuomba Mungu. Zaburi 13.9, muhubiri 7:13

Nilitoka wapi?
Jiullize mimi nilitoka wapi? binnadam origin yake imegawanyika sehemu mbili. Kwanza mwanadamu anatoka kwa Mungu yaani kuumbwa toka kwenye fikra za Mungu hadi kuwekwa kwenye tumbo la mama yake. Pili familia anayotokea ndio chimbuko lake la pili hata akijitambulisha atasema anatoka familia Fulani lakini kiuhalisia anatoka kwa MUNGU. Mwanzo 1-1, Yohana 1:1-5

Je nifanye nini?
Baada ya kujiuliza maswali hayo hapo juu na kuona udhaifu wako ulipo juu ya kujitambua basi fanya haya ili kuwasha taa ya ufahamu ndani ya ubongo wako. Mwalimu wangu alikua ananiambia batani ya kuwasha taa ya kujitambua ndani ya ubongo unayo mikononi mwako uamuzi ni wako kuwasha upate mwanga au uendelee kukaa giza.
Fanya haya :-
Mche na kumuomba mungu
Jiongezee maarifa kwa kusoma vitu mbalimbali kila siku
Kusudia mwenyewe kutaka kujitambua
Tengeneza utofauti wako na watu wengine
Ongeza thamani ya kile unachokifanya
REFERENCE
Katika kuandika bandiko hili nimetumia rejea mbalimbali kama vuile.
Biblia ya Gideon Version
Katekisimu katoliki jimbo la iringa toleo la kumi na mbili 2013
Kitabu cha The purpose driven to life by Rick waren
Google

Written by
Da’Vinci
Jf expert member
 
Back
Top Bottom