Liverpool na Tottenham zimepangwa katika makundi ya kifo katika upangaji wa makundi huku Manchester United ikitupwa kwa Ronaldo.
Katika upangaji huo wa ratiba ya hatua ya makundi uliofanyika Monaco, Spurs imepangwa kundi B ikiwa pamoja na Barcelona, PSV na Inter Milan.
Liverpool iliyocheza fainali msimu uliopita ipengwa kundi C pamoja na mataji wa PSG, Napoli na Red Stars
Manchester United watakutana na nyota wao wa zamani Cristiano Ronaldo baada ya kupangwa na mabingwa wa Serie A, Juventus.
Ronaldo, ambaye alichezea Man United kati ya 2003 na 2009, amejiunga na Juve kwa gharama ya pauni 99.2milioni Julai baada ya kucheza kwa miaka tisa Real Madrid.
Wapinzani wao wengine ni Valencia na Young Boys katika Kundi Group H.
Mabingwa wa England, Manchester City wametupwa Kundi F, pamoja na Shakhtar Donetsk, Lyon na Hoffenheim.
Mabingwa watetezi Real Madrid, wamepewa kundi rahisi wakiwa Kundi G pamoja na Roma, CSKA Moscow na Viktoria Plzen.
Makundi
Kundi A: Atletico Madrid, Dortmund, Monaco, Club Brugge
Kundi B: Barcelona, TOTTENHAM, PSV, Inter Milan
Kundi C: PSG, Napoli, LIVERPOOL, Red Star Belgrade
Kundi D: Lokomotiv Moscow, Porto, Schalke, Galatasararay
Kundi E: Bayern Munich, Benfica, Ajax, AEK Athens
Kundi F: MAN CITY, Shakhtar, Lyon, Hoffenheim
Kundi G: Real Madrid, Roma, CSKA Moscow, Viktoria Plzen
Kundi H: Juventus, MAN UTD, Valencia, Young Boys