Ningefurahi sana kama Zinchenko angeendelea kucheza kama beki wa kushoto,dogo anaelekea kuwa LB mzuri sana kama atapata mechi za kutosha na kama atakuwa "injury free"...
Kuhusu namba tisa,kwakweli siku hizi soko la namba tisa halisi limekua gumu sana...
Ila tuna dogo tulimuuza kwa mkopo,anaitwa Lucas Nmecha,kama tukimtengeneza vizuri atakuja kuwa mshambuliaji mzuri sana,Ila hili linategemea na mipango ya Guardiola..!
Kuhusu Joao Felix,mimi naona dogo yupo "overrated" sana,sioni kama ana cha kuongeza katika timu yetu,tutapigwa pesa tu..!
Kuhusu Bruno Fernandes,huyu siamini kama kweli tulikuwa na uhitaji wa huduma yake,as long as KDB yupo fit hatumuhitaji Bruno Fernandes, ila nafikiri ni uoga wa benchi la ufundi kuhusu majeruhi ya KDB ndio inatusukuma kutaka kumnunua huyu Mreno,lakini nikubali tu kuwa jamaa ni BONGE la mchezaji..!
Chief,mimi nafikiri dirisha lijalo la usajili tungewekeza nguvu zetu katika kupata wachezaji wawili muhimu katika nafasi zifuatazo:
1) Kiungo mkabaji, tutafute kiungo mkabaji wa kueleweka, tusipopata mchezaji wa kueleweka kucheza hii nafasi,hakika itatugharimu sana msimu ujao..!
Kwa soko la usajili lilivyo nashindwa hata kusuggest ni mchezaji gani wa kumsajili katika hii nafasi..!
2) Beki ya kulia, hivi karibuni nimekuwa na mashaka sana na kiwango cha Kyle Walker, isajiliwe beki namba mbili ya kueleweka kwaajili ya kumsaidia huyu muhuni wa Kiingereza,tungempata Wan Bissaka kutoka Crystal Palace hakika tungekuwa tumeramba dume..!