Mpaka sasa nashindwa kupredict lineup ya City kwa msimu ujao...
So far wachezaji wenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza ni wanne tu,wachezaji wenye uhakika wa namba ni Ederson, Laporte, Walker na Bernardo...
Beki ya kushoto kuna ushindani mkubwa,sijui ni nani ataanza kati ya Angelino, Mendy na Zinchenko...
Beki wa kati atakayesaidiana na Laporte kuna ushindani mkubwa kati ya Eric Garcia,Otamendi na Stones...
Kiungo mkabaji kuna ushindani mkubwa kati ya Fernandinho na Rodri...
Nafasi ya kiungo mshambuliaji,nani akae benchi,De Bruyne, Foden au David Silva..?
Vipi kuhusu Gundogan..!?
Kudadadeki, hii timu ina kikosi kipana ajabu..!
Bernardo atacheza kama winga au kiungo wa kati,akicheza kama winga nafasi ya winga iliyobaki anacheza nani, Mahrez, Sane au Sterling..?
Vipi kuhusu nafasi ya mshambuliaji,Jesus ataendelea kukaa benchi au ni muda wa Aguero kuanza kupumzika..!?
Weka kikosi chako cha kwanza kwa msimu ujao,mimi binafsi nimechemka ila ninaamini msimu ujao idadi ya wanaoichukia hii klabu inaenda kuongezeka,maana vipigo viko palepale,tunaenda kubeba tena "takataka" zote za Uingereza..!
Ila HATERS wanakaribishwa kuja na excuse yao ya kombe la UEFA.