The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Tetesi
MAN CITY WANAMTAKA VAN DIJK


Manchester City wapo tayari kupambana kwa nguvu zote kumpata beki wa Southampton Virgil van Dijk uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Mirror .
 
Tetesi
MAN CITY HUENDA WAKAMPOTEZA KINDA WAO KWA LIVERPOOL


Liverpool wana tumaini la kumsajili kinda mahiri wa Manchester City Javairo Dilrosun, kwa mujibu wa ESPN .
City walikuwa na tumaini kubwa kubaki na kinda huyo wa miaka 19 baada ya kumpoteza Jadon Sancho aliyetimkia Dortmund majira ya joto, lakini Juventus, RB Leipzig na Valencia pia zinatamani huduma yake,
 
Numbisa

Punguza kidogo hizo news unazoweka hapa maana nyingi zipo online mda wote, ukiziweka hapa kwa kila jambo basi thread inakuwa kubwa na tunakosa kupata mawaitha ya wana jf wenzetu. hapa tupeane mawaidha yetu, how you feel for the team? hizo news ambazo hata kwenye simu tunapata zipunguze kidogo.

sorry kama utakuwa umenielewa vibaya
 
tujadili je ni faida gani man city kumaliza wa kwanza kwenye Group lao ? na kama anaemaliza wa kwanza anakutana na anaemaliza wa pili kwenye group lingine kuna faida gani kama hao waliomaliza wa pili ni --- Real Madrid , Juventus , Bayern Munich , .........
 
Kumbe kuna watu nawakera kwa news, poa mkuu. Sitaleta news yoyote hapa.byeee
Numbisa

Punguza kidogo hizo news unazoweka hapa maana nyingi zipo online mda wote, ukiziweka hapa kwa kila jambo basi thread inakuwa kubwa na tunakosa kupata mawaitha ya wana jf wenzetu. hapa tupeane mawaidha yetu, how you feel for the team? hizo news ambazo hata kwenye simu tunapata zipunguze kidogo.

sorry kama utakuwa umenielewa vibaya
 
Kumbe kuna watu nawakera kwa news, poa mkuu. Sitaleta news yoyote hapa.byeee
sorry mkuu
ungetumia tu neno linguine tofauti na hili la kusema kuna watu unawakera, mm sijakereka bali nilikuwa natoa ushauri tu. au hupendi kushauriwa? ungetumia lugha nyingine tu. News lete ila zichuje chuje.
 
Shukran wakuu
Ulivyosema kuw hutaleta news yoyote hapa imekuw kweli!! Mtu 1 hawezi kukutoa hapa. Tunaehitaji taarifa zako tupo wengi sana tunaomba urudi mkuu.
Numbisa kwenye haya majukwaa huwezi kumfurahisha kila mtu. Nasio kila mtu anatembelea majukwaa mbalimbali ya mpira.Kwahiyo mie binafsi naomba uendelee kutuletea news mbalimbali.
 
Tetesi

SANE KULAMBA DILI MPYA CITY


Manchester City watampa Leroy Sane mkataba mpya ambao utamwezesha kulipwa £80,000 kwa wiki, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha Pep Guardiola tangu ajiunge na City akitokea Schalke na mshahara kwae utapandishwa sasa, lakini atalazimika kuwasubiri Kevin De Bruyne, David Silva na Fernandinho kusaini mataba mpya kwanza.
 
Tetesi

PEP KUIMARISHA SAFU YA ULINZI


Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amegeuza macho yake kwa beki wa Real Sociedad Inigo Martinez akijipanga kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa Januari, kwa mujibu wa The Sun .
 
Pep Guardiola ameomba radhi kwa ushangiliaji wake mbaya Manchester City iliposhinda dhidi ya Southampton.
Raheem Sterling aliweka kamba safi sana mnamo dakika ya 96, akiiwezesha Man City kuongeza pengo la pointi Ligi ya Uingereza.
Klabu hiyo sasa imewezidi mahasimu wao Manchester United kwa pointi nane, baada ya kushinda mechi 13 kati ya 14 msimu huu na kupata sare moja.
Guardiola alishangilia goli hilo kwa kukimbilia dimbani, na sasa amehakikisha anaomba radhi baada ya mihemko yake kumwondoka.

Nimesema 'naomba radhi' kwa sababu sikuweza kujizuia," alisema Guardiola. "Nilikuwa na furaha sana. Nilimkimbilia Raheem lakini sikuwa na kasi ya kutosha, lakini kwa pamoja tulifurahi."
Guardiola alibambwa kwenye video akimkemea nyota wa Southampton Nathan Redmond baada ya mechi wakiwa kwenye mzozo, lakini Guardiola anasema alikuwa akimsifia tu mchezaji huyo mwenye miaka 23.
"Nilimwambia Redmond jinsi alivyo bora," alidai.
"Msimu uliopita alituvuruga hapa, lakini leo hakuweza kushambulia kwa sababu muda wote alikuwa akikaba."

Mkatalunya huyo alishangilia kama chizi baada ya winga wake kuipatia goli la ushindi Manchester City katika mechi dhidi ya Southampton
 
David Silva ametia saini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kukaa Manchester City hadi mwaka 2020.
Kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Man City kutoka Valencia kwa kitita cha £24m mwaka wa 2010.
Kiungo huyo ameshinda taji la ligi ya Premia mara mbili, kombe la FA na vikombe viwili vya ligi akiwa na City.
Klabu hiyo ya Pep Guardiola imo alama nane mbele kileleni mwa ligi ya Premia baada ya ushindi wa mechi 12, ushindi wao wa hivi karibuni ukiwa siku ya Jumatano dhidi ya Southamton.
Silva, ambaye amesaidia ufungaji wa magoli manane, usaidizi ambao hakuna mchezaji yeyote wa kiwango chake ametimiza, amesema anatarajia kuongeza tuzo zaidi Etihad.
''Najivunia kwa kile nilichojivunia na City kwa misimu saba na nusu hapa pamoja na Pep akiwa meneja. Najihisi tuko katika nafasi nzuri kushinda vikombe msimu huu na kuendelea,'' alisema Silva.

''Mbinu tunayoitumia kucheza soka ni nzuri na ni furaha yangu kuwa miongoni mwao na natarajia kushinda mataji mengi miaka ijayo.
 
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema anajutia sana mazungumzo ambayo alifanya na mchezaji wa Southampton Nathan Redmond punde baada ya mechi yao kumalizika Jumatano.
City walishinda 2-1.
Guardiola, ambaye aliingia uwanjani na kuzungumza na winga huyo, ametakiwa kufafanua kuhusu kitendo hicho chake na Chama cha Soka cha England.
Redmond amesema Mhispania huyo alikuwa tu anamsifia.
Ijumaa, Guardiola alisema: "Siwezi kujidhibiti. Natumai nitaweza kufanya hivyo, natumai naweza kuimarika."

Meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amepewa hadi Jumatatu kutoa ufafanuzi.
"Kile Redmond alichosema ndicho hicho, navutiwa naye kama mchezaji na namshukuru kwa aliyoyasema," amesema.
"Iwapo FA wanataka taarifa yangu tena, ninaweza kufafanua chochote wanachotaka nifafanue. Ikiwa hawaniamini, sijui nafanya nini hapa."
Guardiola alimwendea Redmond muda baada ya Raheem Sterling kufunga bao la ushindi la City dakika ya 96 uwanjani Etihad.
Alianza kusema kwa sauti na kuashiria kwa mikono yake, huku Redmond akionekana kufunika mdomo wake na kumjibu.

Redmond baadaye amesema: "Nilimwambia kwamba nilikuwa ninafanya kile nilichoambiwa na meneja wangu kufanya kwenye mechi hiyo. Hivyo tu."
City watakuwa wenyeji wa West Ham saa 16:00 GMT Jumapili nao Southampton watakuwa ugenini dhidi ya Bournemouth saa 13:30 siku hiyo.
 
Tetesi
ARSENAL NA MAN CITY ZAMWANIA EVANS


Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans amezivutia Manchester City na Arsenal kwa ajili ya uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa The Telegraph .
Ilitipotiwa kuwa ofa ya Arsenal ya £25 milioni ilikataliwa Agosti 31 kwa ajili ya mchezaji huyo, kwani WBA wanataka kiasi kisichopungua £30m.
 
Asante wagonga nyundo piga hawa wachovu wanajikuta sana
Waliishachoka hata wasiwatishe
Piga kbs matobo hilo li cheusi mangara
Piga mashuti hapo golini kuna pazia tu mtafunga
Yatoeni kbs ulimi machovu haya
 
Back
Top Bottom