THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya............57
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA...
Sandra,Fungo na Inspekta Aron wako njiani kwenda kumsaidia Jajusi Shadow ambaye ametekwa na Madam Sultana.
Wakati huo huo upande wa pili Mwanadada Sharma Khumar anaonekana kuvutiwa na binti Annah, anamuagiza mlizi wake amfuate
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEA...
Haukupita muda aliingia mwanaume mmoja ndani ya mgahawa huo akiwa amevaa kofia kubwa ya duara pamoja na miwani ya jua. Alijipenyeza ndani ya mgahawa huo akatembea hadi upande wa pili kule alipokaa mwanadada Sharma Khumar. Huyu ndiye alikuwa mtu aliyepanga kukutana naye eneo hilo aliitwa Bwana Andiwelo katabi mkemia mkuu wa serikali. Andiwelo katabi ni mshirika kati ya watu wanaoifahamu siri ya kuwepo kwa vimelea vya V-COBOS nchini ukiacha marehemu Dokta Gondwe na Mheshimiwa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa, Andiwelo alikuwa mmoja wao pia. Hata kile kikao cha mwisho kilichofanyika katika nyumba ya Mheshimiwa Cosmas Kulolwa wote wawili yaani mwanadada Sharma Khumar na Andiwelo katabi walikuwepo lakini leo wanaamua kukutana pembeni ya mji wakiwa wawili tu kwa ajili ya mazungumzo yao ya siri.
"Nambie Miss Sharma simu yako imenitisha sana, vipi kwema?" Andiwelo alianzisha mazungumzo.
"Kwema, kwa nini utishike mbona nilishakweleza kila kitu Andiwelo"
"Ni sawa lakini muda mrefu umepita nikajua ulishahairisha huu mpango wako hatari"
"Hapana siwezi, unajua kabla Profesa Fernando Arturo hajatuzunguuka ni vema tukawahi kuchukua kilicho chetu mapema"
"Lakini wewe umejuaje kama atatuzunguuka?"
"Andiwelo mimi nimefanya kazi na hawa wamexico kwa muda mrefu sana naelewa mipango yao yote, wakishapata wanachokitaka watatuua sisi wote kisha watarudi kwao kufufua upya maabara yao ya ZMLST huku wakiendelea kupiga pesa za ugonjwa wa V-COBOS, sisi tunatumika tu rafiki yangu"
Alieleza Miss Sharma Khumar
Mkemia mkuu wa serikali Andiwelo katabi alitulia kwa muda huku akijaribu kuyatafakari maelezo ya Miss Sharma kisha akaongea.
"Hili jambo tunalotaka kulifanya ni hatari sana Miss Sharma, ona marehemu Dokta Gondwe alijaribu kwenda kinyume na Profesa Fernando kama hivyo unavyotaka tufanye haikuchukua muda akawa ameuawa mchana kweupe, huyu jamaa ana watu kila kona mbaya zaidi yupo pamoja na Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa naye anawatu kila kona huoni kama ni hatari, atatuchinja kama kuku"
"Kuhusu hilo usijali ndio maana nilitangulia kuja hapa nchini kabla ya wao kufika nimeshaweka mipango yangu sawa hakuna kitakacho haribika"
"Mipango ipi Sharma?" Aliuliza Andiwelo lakini kabla hajajibiwa yule mlinzi wa Miss Sharma alifika.
"Mkuu yule binti nimemleta yule pale" alisema mlinzi huku akinyoosha kidole pale alipokaa Annah.
"Umeshaongea naye?" Aliuliza Miss Sharma
"Hapana"
"Ongea naye mwambie nataka kufanya kazi na yeye"
"Sawa bosi" alijibu mlinzi kisha akapiga hatua kumfuata Annah huku akiacha mazungumzo ya bosi wake na Andiwelo yakiendelea.
[emoji294][emoji294][emoji294]
"Sikia binti bosi wangu amekupenda anataka kufanya kazi na wewe kama uko tayari akuajili niambie, ni hilo tu" alieleza kwa kifupi yule mlinzi mara baada ya kurudi pale alipomuacha Annah.
Annah ambaye muonekano wake ulikuwa tofauti kabisa na tulivyomzoea kipindi kile akiwa karibu na Inspekta Aron, aliinua uso wake uliofubaa na kumtazama yule mlinzi.
"Yaani umeniita kwa sababu ya hilo au kuna lingine?" Annah aliuliza kibabe
"Ni hilo tu, tunataka kuyatengeneza maisha yako. Nakuona kabisa wewe ni mrembo ila maisha unayoishi yanakufanya uonekane kama kichaa fulani hivi" Alisema yule mlinzi kauli iliyomfanya Annah amkate jicho kali sana. Mlinzi akawa makini akijipanga kwa lolote kwani alikumbuka vizuri dakika chache zilizopita Annah alitoka kumkung'uta muhudumu mmoja wa mgahawa huo.
"Siwezi naondoka"alisema Annah huku akiinuka tayari kuondoka.
"Aah.. subiri... Subiri kwanza kwani wewe unatakaje eeh!?" Aliuliza yule mlinzi.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati huo mazungumzo ya Miss Sharma na Mkemia mkuu Bwana Andiwelo yaliendelea. Mara akaja tena mlinzi.
"Boss yule dada amekataa anataka kuondoka"
"Umempa pesa?"aliuliza Sharma
"Hapana nimemwambia tu tutampa pesa nyingi"
"Muonyeshe pesa, maneno matupu huwezi kumshawishi mtu wa aina ile au unataka na wewe akupige?" Alisema Sharma, bila kupoteza muda yule mlinzi aliondoka hadi pale alipomuacha Annah.
"Dada usiondoke kaa kwanza nakuja dakika 1 tu" alisema Mlinzi huku akipiga hatua ndefu ndefu akatoka nje ya mgahawa akawa anaelekea waliposimamisha gari yao.
Annah alitulia huku akimtazama mwanamke aliyetaka kumuajili kwa macho ya kuibia ibia, akatega sikio akitamani kusikia kile walichokuwa wakizungumza watu hao wawili, kwa bahati nzuri safari hii waliongea kwa sauti kubwa kiasi, walijisajau.
[emoji294][emoji294][emoji294]
"Miss Sharma sijakuelewa vizuri hebu nifafanulie mpango wako nikuelewe" Alisema Andiwelo.
"Tatizo lako ni uoga, unafikiri watakuua kama walivyomuua Dokta Gondwe hapana niamini mimi nitakulinda"
"Hamna sio kwamba naogopa ila nachukua tahadhari"
"Sawa, nimekwambia tutaendelea kuwa karibu nao na kufanya kazi kwa pamoja kama kawaida lakini tutakuwa tukiwazunguuka kwa siri sana" alieleza Miss Sharma
"Kivipi?"
"Tutamtumia kijana mmoja ambaye naye malengo yake ni kama yetu"
"Nani huyo?"
"Anaitwa Tino, mtoto wa marehemu jenerali Phillipo Kasebele na ni kaka wa marehemu Inspekta Aron pia"
"Mnh wewe umewajuaje wote hao?"
"Nilikwambia nilitangulia kuja hapa nchini sio kushangaa magari, nilikuja kufanya kazi"
"Sawa sasa nimeanza kukuelewa ila huyo Tino utamtumia vipi wakati na yeye anataka kitu tunachokitaka sisi"
"Baada ya kifo cha Dokta Gondwe Tino amepoteza muelekeo hana kwa kuanzia, anahangaika anataka kumteka Osward lakini pia anawaza kukuteka hata wewe ili tu apate pa kuanzia sasa kama tutamuweka karibu na kumpa mwanga atatuamini na kuanza kufanya kazi na sisi"
"Kivipi?"
"Sisi tuna taarifa ya wapi vilipo vimelea vya V-COBOS na jinsi ya kuvipata lakini hatuwezi kwa sababu hatuna nguvu kazi, Tino anayo nguvu kazi vikosi imara sana avilivyoachwa na Dokta Gondwe lakini hana taarifa muhimu kama tulizonazo sisi"
Alieleza Miss Sharma akijaribu kuufungua ubongo wa Andiwelo.
"Anha! Nimeanza kukuelewa kwamba sisi tutaendelea kubaki huku tuliko upande wa Profesa Fernando lakini tutakuwa tukivujisha siri kwa Tino"
"Yes! Hiyo ndio maana yangu kubwa"
[emoji294][emoji294][emoji294]
Annah akiwa amejikausha huku masikio yake yakiwa yamesimama kama sungura alishtushwa na burungutu la pesa zilizomwagwa juu ya meza. Zilikuwa ni pesa nyingi sana kutoka kwa yule mlinzi wa Miss Sharma Khumar.
Annah alibaki ameduwaa huku akizitazama zile pesa lakini amini usiamini mawazo ya Annah hayakuwa kwenye zile pesa bali yalikuwa mbali akijaribu kuyatafakari maneno kadhaa aliyoyasikia kutoka kwa Sharma Khumar na mgeni wake Andiwelo.
"Kumtumia Tino....kifo cha Dokta Gondwe...kifo cha Aron...Rais mstaafu..kumteka Osward...." Haya ndio maneno yaliyokuwa yakipitapita kwenye kichwa cha Annah wakati huo. Kwa kuwa lengo la Annah siku zote ilikuwa ni kulipa kisasi kwa Tino na wenzake waliohusika na mauaji ya baba yake, kisasi kwa wote waliohusika kumuweka mwanaume ampendae hatiani yaani Inspekta Aron hadi kusababisha kifo chake, kisasi kwa wote waliohusika kupindisha ukweli hadi Osward akaachiwa huru, Annah aliona kabisa ni kama miujiza imemfuata pale alipo. Pesa zilizokuwa mezani si kitu bali kufanya kazi na Miss Sharma Khumar ndilo lilikuwa jambo la msingi zaidi kwani aliamini moja kwa moja kuwa atamsogeza karibu na wabaya wake.
"Vipi mbona umeduwaa unazitaka hizi pesa, basi kubali kufanya kazi na bosi wangu"
"Sawa nimekubali" Annah alijibu upesi huku akizichukua zile pesa kuzirudisha kwenye mfuko. Yule mlinzi akawa anatabasamu akiamini kuwa pesa ndio kitu kilichomnasa Annah, la asha.
Dakika 10 baadae Annah alionekana akiwa ameongozana na Sharma Khumar wakitoka nje ya ule mgahawa yule mlinzi akiwa nyuma yao, wakaingia ndani ya gari na kuondoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili Inspekta Aron, Sandra na Fungo tayari walishafika msituni ilipo ngome ya Madam Sultana na sasa walikuwa wamejificha msituni pembeni kidogo ya ngome hiyo wakawa wanapiga hesabu za kikomandoo namna ya kuingia kumsaidia mwenzao Jajusi Shadow.
Kwa mbali waliweza kuona watu waliokuwa kwenye ngome hiyo wakiwa bize kupakia mizigo ndani ya gari tatu zilizokuwa zimewekwa tayari kuondoka.
"Ni kama wanataka kwenda sehemu" alisema Fungo huku akitazama kupitia darubini.
"Ndio, zile ni siraha sijui wanakwenda wapi!" Alijibu Sandra kisha akageuka kumtazama Inspekta Aron pembeni yake.
"Vipi Aron mbona uko kimya, au bado unamuwaza mama yako?"
"Hapana, Dunia ina siri nzito sana unaweza ukawa unaishi ilimdradi ukiamini watu wote wako hivyo kumbe wenzako unaoishi nao wamebeba vitu vizito mno na hujui"
"Una maana gani Aron?"
"Unamuona huyo dada anayewaongoza watu kupakia mizigo kwenye gari"
"Ndiyo namuona"
"Huyo ni shemeji yangu anaitwa Jesca ni mke wa kaka yangu Tino nilikuwa namuona wa kawaida sana na siku zote alikuwa ananitaka kimapenzi, nilimuona malaya malaya tu mwanamke asiyejitambua kumbe na yeye ni hatari kama alivyo kaka yangu Tino"
"Mmh! Kweli kifo chako kimekufanyaa uyajue mengi, kwa hiyo huyu dada anafanya kazi na mama mkwe wake huku akimzunguuka mume wake Tino si ndio hivyo"
"Hata sina majibu inafikirisha sana hadi kichwa kinaniuma, hebu tuachane na hayo tuingie kazini tumchomoe ndugu yetu"
"Subiri..subiri wanaondoka"alisema Fungo
"Haya gari zote tatu zimeondoka vipi Jajusi Shadow anaonekana wapi yupo ndani au wameondoka naye?"
"Yupo ndani"
"Haya twende kazi wanaume" alisema Sandra huku akisimama, akatoa kibanio cha nywele zake kisha akaziachia na kuzilaza kwa nyuma, akachomoa bastola mbili moja akaishika mkono wa kulia na nyingine mkono wa kushoto, akaanza kupiga hatua kuelekea mbele ilipo ngome ya Ambross.
Inspekta Arone yeye akavaa barakoa yake vizuri kama ilivyo kwa Sandra naye akachomoa bastola mbili alizokishwa zisindilia risasi za kutosha kisha akaanza kumfuata nyuma. Fungo yeye alikuwa na bunduki aina ya AK47, akachomeka magazine iliyojaa siraha kisha akaanza kumfuata Inspekta Aron nyuma.
Hazikupita dakika Tano milindimo ya risasi ilianza kushika kasi na kusikika karibu kila kona ya msitu huo. Walinzi wachache waliokuwa wamesalia kwenye ngome ya Ambross inayomilikiwa na Madam Sultana walikuwa kwenye shughuli nzito kuwakabiri Sandra,Fungo na Inspekta Aron.
Je, nini kitafuata?
Annah kwenye himaya ya Sharma Khumar...
Najma bado anatamani kuuchimba ukweli wa kifo cha baba yake....
Jesca anakwenda kuchukua chupa ya kijivu yenye kinga na tiba dhidi ya vimelea vya V-COBOS....
Inspekta Aron ndani ya kundi la kikomandoo na leo anaifanya kazi yake kwa mara ya kwanza kumuokoa Jasusi Shadow....
Mambo ni mengi, muda ni mchache USIKUBALI KUPITWA...!!
ITAENDELEA...