THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

THE MODERN WAR: Simulizi ya kijasusi mapenzi na upelelezi

THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya.................50
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Anyway la kuwa na liwe" Aliwaza Inspekta Aron kisha akafungua ile nailoni akachukua vile vidonge na kuvibugia mdomoni akavimeza.
Haraka akaichukua ile karatasi na lailoni iliyokuwa na vidonge akaingia chooni akavitupa katika tundu la choo na kuviflash na maji. Akiwa anatoka chooni Inspekta Aron alianza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wake haukupita muda akajikuta anakakosa nguvu, akaanguka chini na kutulia kimya.

SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]
Ilikuwa ni asubuhi ya huzuni kuu, asubuhi yenye msiba wa kitaifa siku ambayo mwili wa aliyekuwa waziri wa afya Dokta Isaack Gondwe ulikuwa ukiagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Nachoma ambako ndiko mazishi yangefanyika.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa walihudhuria msiba huo nyumbani kwa Dkt Gondwe.
Katika meza kuu alionekana Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zumo Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa pamojaa na viongozi wengine wakubwa wakubwa kutoka nje na ndani ya nchi.
Mkemia mkuu wa serikali Andiwelo katabi, Kigogo Mzee matula baba yake Osward pamoja na Osward mwenyewe walikuwa ni moja kati ya watu waliohudhuria kuomboleza msiba huo. Siri iliendelea kubaki sirini hakuna aliyejua kuwa wahusika wakuu wa mauaji ya Dokta Gondwe walikuwa ni moja ya waombolezaji katika msiba huo. Amri ilitoka kwa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa huku Osward akiwa ndiye mtekelezaji wa mwisho wa mauaji hayo ya kikatili na baada ya hapo kesi yote wakamuangushia kijana mchapakazi anayewaandama kila kukicha yaani Inspekta Aron.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Katika kambi kuu ya marehemu Dokta Isaack Gondwe vijana wake wakiongozwa na Tino walikuwa wamevalia suti nyeusi na kusimama uwani ndani ya ngome hiyo. Walionekana wamepanga mistari miwili huku mbele yao picha ya Marehemu Dokta Gondwe iliyopambwa vizuri na kuzunguushiwa maua ikiwa imewekwa sehemu maalumu kama heshima ya kumuaga aliyekuwa mkuu wao. Hawataka kwenda nyumbani kwa Mheshimiwa kuuaga mwili wake kama wengine walivyofanya la hasha, bali waliazimia kumaliza kila kitu ndani ya ngome hiyo. Simazi ilikuwa imetawala kwa vijana hao, kila mmoja akiitazama picha hiyo na kukumbuka yale mema yote aliyowafanyia enzi za uhai wake.
Tino akiwa amesimama mbele ya wenzake karibu kabisa na ile picha yeye hakuwa akiumia kama ilivyokuwa kwa vijana wengine bali alikuwa akilaumu na kutoa laana kali kwa Dokta Gondwe mtu aliyekuwa akimchukia kupita maelezo.

"Umekufa kifo kirahisi sana Gondwe sikutaka ufe kwa raha kama hivyo. Mtu kama wewe ilibidi upitie mateso makali kabla ya kifo chako. Umetembea na mke wangu Jesca mwanamke ninaempenda kuliko ninavyojipenda mimi. Ukalala naye bila hata kujali ni mke wangu, kijana ninayekutumikia kama punda. Ulaaniwe Dokta Gondwe...." Aliwaza Tino mawazo hayo yakikatishwa na simu yake iliyokuwa ikiita mfukoni mwake. Akaichukua na kutazama jina la mpigaji kisha akapokea.

"Ndiyo.....nini?.....Aron kafanyaje?.....imekuwaje?.....wapi?...." Tino alimaliza mazungumzo kisha simu ikakatwa kwa haraka haraka ilionekana taarifa alizozipata kumuhusu mdogo wake Inspekta Aron hazikuwa nzuri.
"Nilijua tu mwisho wako utakuwa mbaya mdogo wangu, Rest in peace Aron" Tino alizungumza kwa sauti ya chini.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Nyumbani wa marehemu Dokta Gondwe msiba ulikuwa ukiendelea. Osward na baba yake mzee matula walikuwa wamekaa sehemu moja huku wakionekana kufanya mazungumzo ya hapa na pale.
"Unajua bado sijakuelewa, unasema hujui chochote kuhusu kifo cha Dokta Gondwe bosi wako!?" Aliuliza Mzee matula
"Nilishasema sijui baba"
"Sasa umewezaje wezaje kushinda kesi mahakamani? Yani namaanisha ni yeye ndiye nilimuomba ashughulikie kila kitu lakini amekufa kabla ya hukumu ya kesi yako na wewe umeshinda kesi kivipi yani?"
"Baba majibu ya hayo maswali mimi sina, haki tu imetendeka mimi nikashinda kesi" Alijibu Osward
"Mpuuzi mmoja wewe, haki haki gani? Kama ungekuwa na haki ungeburuzwa mahakamani kwa miezi yote hiyo" Alisema Mzee matula akimuangalia mwanae usoni huku akiwa hayaamini maelezo yake hata kidogo, alijua wazi mwanae kunakitu anaficha na huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe.
"Anyway mpango wetu uko pale pale hakikisha baada ya hapa unamuoa Najma mapema iwezekanavyo sawa kijana wangu"
"Sawa baba, nampenda sana sitochelewa" Alisema Osward kauli iliyoonekana kumutoa kwenye mudi Mzee matula kwani alikuwa akimtaka Najma kimapenzi na hii ilikuwa ni ndoto yake tangu kitambo, aliamini kama mwanae atamuoa basi itakuwa ni moja ya njia ya kumsogeza karibu binti huyo mrembo mwenye msimamo.
Wakati wakizungumza hayo mara Osward akashikwa begani kutokea nyuma, akageuka kuangalia aliyemgusa.
"Asia!?" Osward aliita kwa mshangao,
Alikuwa ni Asia mmoja kati ya wanawake wa kikosi hatari wanaojiita Malaika weusi alimuonyesha ishara Osward kuwa amfuate akafanya hivyo huku mzee matula akiwa hajaona chochote macho yake yakiwa yanamtazama binti Najma ambaye alikuwa kwa mbali akiomboleza msiba wa baba yake pamoja na ndugu wengine.
"Ooh! Mashallah mtoto mzuri mtoto mtamu, hata akiwa analia bado anavutia" Aliwaza Mzee matula huku akitabasamu baadae akajishtukia kuwa yupo msibani, akatulia.

Osward na Asia walisogea pembeni kabisa mahali pasipo na watu wakawa wanazungumza.
"Enhe vipi tena?"
"Unajua siwaelewi"
"Kivipi tena?"
"Tangu jana nimewambia wenzangu Erica na Elina wamekamatwa wako polisi lakini hata hamjali mko kimya"
"Lakini Asia Mheshimiwa alisema tumuachie yeye atafanya mchakato watoke"
"Mchakato gani mi nilikuwa na imani atawatoa mapema ili wasijekuwa ushahidi katika kesi ya Inspekta Aron lakini huyo Aron mwenyewe amekufa Mheshimiwa atawatoa ndugu zangu kweli?"
"Unasemaje wewe Aron kafanyaje?"
"Ooh! Hivi hujasikia bado Inspekta Aron amekutwa amekufa akiwa rumande wanadai sababu ni shambulio la moyo sijui ma nini huko hata siwaelewi"
"Lini saa ngapi?"
"Sasa hivi imetangazwa fungua data ingia mtandaoni uone"
Alisema Asia na hapo Osward alitoa simu yake akawasha data na kuingia kwenye mtandao wa Instagram. Ni kweli habari zilizokuwa zikisambaa kwa kasi mda huo ni kuhusu kifo cha Inspekta Aron muuaji wa Dokta Gondwe.

"Aa! Haiwezekani sio rahisi" alisema Osward huku akikuna kichwa chake
"Unataka kumaanisha nini!"
"Asia sio bure kuna kitu hapa"
"Kivipi? Au Mheshimiwa ndio kamuua eti!!"
"Sijui na sina maana hiyo. Maana yangu ni kwamba tunachezewa akili hapa Asia"
"Aah! We nawe jamani sasa nani atuchezee akili Osward tatizo lako huwa unapenda kufanya kila kitu kionekane kigumu"
"Niamini mimi Asia unajua nini? Jana Inspekta Aron alikuwa ametoroka kabisa pale hospitali, kwa uwezo wake alionao na kwa namna kesi yake ilivyo ngumu, alikuwa na uwezo wa kukimbia na kwenda mbali asikamatwe lakini unajua nini alifanya?"
"Enhee sijui.."
"Alirudi kujikamatisha mwenyewe kwa polisi akawaomba wamfunge pingu"
"Kwa hiyo!?"
"Kwa hiyo nini wewe unaona ni hali ya kawaida hiyo, hebu achana na mimi" Osward aliongea huku akionekana kukasirika akawa anaondoka
"Sasa unakwenda wapi?"
"Hospitali mochwari"
"Kufanyaje?"
"Mpaka nishuhudie mwenyewe kwa macho yangu kuwa Inspekta Aron amekufa ndio nitaamini, halafu kijana mdogo kama yule anakufaje kwa magonjwa ya moyo, magonjwa ya wazee hayo" Alisema Osward kisha akaondoka na kutokomea kwenye msongamano wa watu.
Taarifa za kifo cha Inspekta Aron zilianza kusambaa kwa kasi sana, hatimae zikawafikia hadi watu waliokuwa msibani. Minong'ono ya hapa na pale ikawa inasikika watu wakijadili.
"Malipo ni hapa hapa Dunia"
"Bora amekufa muuaji mkubwa yule"
"Au serikali imemnyonga moja kwa moja imeona isipoteze muda"

Haya yalikuwa ni baadhi ya maneno ya watu mbalimbali kwenye msiba huo. Taarifa hii ilimfikia hadi Mheshimiwa Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa akinong'onezwa na mmoja kati ya viongozi pale mbele. Profesa Cosmas alitoa macho kwa mshangao.
"Hii inawezekanaje, nani kamuua?" Aliwaza Profesa Cosmas, alijua wazi hajahusika kabisa kwenye habari ya kifo hicho kipya. Wakati hayo yakiendelea Rais Alfredo Zumo yeye alikuwa anawatazama tu kwa jicho la pembeni, alielewa ni nini kinaendelea wakati huo.Huu ulikuwa ni mpango wake yeye na vijana wake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Dakika kumi na saba zilimtosha Osward kufika hadi ilipo hospitali ya taifa Kirunguru ambapo kwa mujibu wa maelezo hapo ndipo Inspekta Aron alipopelekwa mara baada ya kukutwa amaenguka sakafuni katika chumba alichokuwa amefungiwa.
Polisi walikuwa wamatapakaa nje na ndani ya hospitali hiyo. Osward hakujali alianza kupiga hatua kuelekea lango kuu la kuingilia ndani ya hospitali hiyo, wakati akipiga hatua alisikia baadhi ya mazungumzo ya Polisi wakiongea.

"Imekuwaje taarifa ya kifo cha Aron isambae kabla ya sisi kutangaza?"
"Hata mimi ndio nashangaa mkuu yaani wanaeleza kila kitu utafikiri walikuwepo sijui ni nani labda daktari au wafanyakazi wa hospitali walioshuhudia"
"Hapana sio rahisi, utaratibu wanaujua mbona."

Polisi walikuwa wakiulizana na kujibizana wenyewe. Mazungumzo haya yalimfanya Osward kuendelea kuamini kile anachokiamini tangu awali kuwa kuna mchezo unaendelea.
"Samahani dada naomba nikuulize" Osward alizungumza na nesi mmoja mara baada ya kuingia hospitali
"Bila sahamani"
"Mochwari iko wapi, nimekuja kuuchukua mwili wa ndugu yangu mmoja amefariki usiku wa kuamkia leo"Osward alidanganya.
"Toka nje kata kulia tembea hadi mwisho wa hili jengo mbele utaona jengo la mochwari limejengwa peke yake, lakini kwanza anzia pale dirishani upate utaratibu wa kuuchukua mwili wa ndugu yako"
"Asante sana dada"
"Usijali, pole kwa msiba"
"Asante sana" Baadae yule nesi aliondoka, Osward alitembea na kutoka nje akakata kona kulia kama alivyoelekezwa.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati huo huo nyuma ya jengo la hospitali hiyo kulikuwa na gari dogo jeusi aina ya Noah likiwa imeegeshwa pembeni ya barabara. Ndani ya gari hiyo kulikuwa wanaume wawili wa kwanza ni Jasusi Shadow, mwingine aliitwa Fungo na wa tatu ambaye ni mwanamke aliitwa Sandra. Kama ilivyo ada wote walikuwa wamefunika sura zao kwa vitambaa vyeusi.

"Mwili wa Inspekta Aron tayari uko mochwari kabati namba 471, tuna nusu saa tu kuhakikisha tunamchoma Aron hii sindano kifuani kwake upande wa kushoto katikati ya mbavu ya tano na ya sita ulipo moyo kisha afanyiwe CPR (cardiopulmonary resuscitation) makosa kidogo tu yanaweza kutufanya tukampoteza Inspekta Aron moja kwa moja, kuweni makini nawakumbusha tena tuna nusu saa tu kila kitu kiwe kimekwisha tofuauti na hapo Aron atakufa" alieleza yule mwanamke Sandra, mmoja kati ya watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
ITAENDELEA...

Simulizi hii ni Tsh 1000 tu lipia kwa mpesa namba 0756862047 jina Saul au Airtel money namba 0788967317 jina Saul
Kisha njoo WhatsApp namba hzo hzo[emoji120]
 
dakika hizo zimegeuka masaa 48 Sasa kijana wetu alone Bado mzima kweli?
 
THE MODERN WAR
(vita ya kisasa)
Sehemu ya .......51
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Mwili wa Inspekta Aron tayari uko mochwari kabati namba 471, tuna nusu saa tu kuhakikisha tunamchoma Aron hii sindano kifuani kwake upande wa kushoto katikati ya mbavu ya tano na ya sita ulipo moyo kisha afanyiewe CPR (cardiopulmonary resuscitation) makosa kidogo tu yanaweza kutufanya tukampoteza Inspekta Aron moja kwa moja, kuweni makini nawakumbusha tena tuna nusu saa tu kila kitu kiwe kimekwisha tofuauti na hapo Aron atakufa" alieleza yule mwanamke Sandra, mmoja kati ya watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
Osward alijipenyeza mpaka upande wa pili ambako ndipo kulikuwa na jengo la kuhifadhia maiti yaani mochwari. Kwa mbali Osward aliona gari mbili zikiondoka kutoka usawa wa jengo la hilo, walikuwa ni watu waliokuja kuchukua maiti ya ndugu yao. Osward alianza kupiga hesabu ni jinsi gani ataweza kufika na kuingia ndani pasipo kuonekana.
Alikuwa amedhamiria kabisa kuona na kuhakikisha mwili wa Inspekta Aron kama upo hapo ndipo ataamini kuwa ni kweli Aron amekufa. Osward alimjua vizuri Aron kuwa ni mtu makini sana kwa jinsi alivyo pambana naye kipindi kile akiwa gerezani haikuwa rahisi hata kidogo kuamini Aron anaweza kufa kirahisi namna ile. Hakika Osward alikuwa na kila sababu ya kufanya hiki alichokuwa akikifanya mda huu.

"Najua huwezi kufa kirahisi hivi Aron bila shaka unataka kutoka kwenye 18 zangu, lazima ufungwe mbwa wewe halafu bado hata hujaniambia ni wapi ulimzika kijana wangu Big" Osward aliwaza.
Baada ya hali kutulia Osward aliangaza macho huku na kule hakuona mtu, taratibu na kwa tahadhari kubwa alianza kupiga hatua kuelekea jengo la mochwari. Kabla hajafika mbali mara alisikia vishindo vya watu wakija kutokea nyuma yake. Ilibidi Osward achukue simu na kuzuga kama anafanya mawasiliano.

"Eeh! Nimeshafika hapa ndio tunafanya taratibu za kuuchukua mwili... Sawa mama...poleni sana...." Osward aliigiza hadi wale watu wawili waliovalia makoti meupe na barakoa walipopita, nao pia walikuwa wakielekea mochwari mmoja alikuwa wa kike mwingine wa kiume.

"Unamkumbuka huyu jamaa anajifanya kuongea na simu?" Yule wa kiume alimuuliza mwenzake swali, alikuwa ni jasusi Shadow, walikuwa kwenye harakati za kumsaidia Inspekta Aron kama walivyojadili.
"Simjui ni nani?" Alijibu yule mwanamke aliitwa Sandra mwanadada anaefanya kazi nyeti ofisi ya usalama wa taifa akiwa karibu sana na Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zumo
"Ni Osward yule ambaye Inspekta Aron alikuwa akipambania kesi yake, na ndio sababu hasa ya Inspekta Aron kusingiziwa kesi ya mauaji" Alieleza jasusi Shadow wakati huo walikuwa wakiikaribia fensi ya kuingia mochwari.
"Aah! Osward... ndio huyu kumbe, sasa inakuwaje yuko hapa?" Aliuliza Sandra
"Bila shaka atakuwa ametumwa kuja kufuatilia taarifa za kifo cha Aron"
"Mmh! Itabidi tumdhibiti mapema bila hivyo ataleta shida na pengine akatuchelewesha si unajua tuna nusu saa tu" Sandra alitoa wazo
"Ndio ngoja aingie 18 zetu" alisema jasusi Shadow.

Baada ya Sandra na Jasusi shadow kupita Osward akiamini ni wafanyakazi wa hospitali hiyo alitulia kwa muda huku akiwaza afanye nini maana ilikuwa ni ngumu kwenda mochwari pasipo sababu za msingi.

" Nifanyaje sasa!?" Aliwaza Osward, mwisho akapata wazo kuwa asogee karibu pengine angeweza kupata mwanya wa kuingia pasipo kuonekana. Akaanza kupiga hatua kusogea.
Alipanda kwenye ngazi kisha kaanza kufuata uelekeo wa korido moja fupi ambako mbele yake ndipo ulikuwepo mlango wa kuingia ndani ya mochwari. Osward alikuwa makini akiangaza macho yake huku na kule, kabla hajafika mbali mara alisikia sauti ya mtu akikohoa kutokea nyuma yake wala hakujua ni wapi ametokea. Osward alishtuka sana na kugeuka alikuwa ni yule mwanadada Sandra.


"Tukusaidie nini kaka?" Aliuliza Sandra
"Aa..ni..nimekuja kumuona ndu.ndugu yangu" Osward aliongea kwa kujiumauma huku akitafuta sababu ya kujitetea.
"Ndugu yako yupi? Huku ni mochwari inakuwaje ukaja kumtafuta maeneo haya"
"Aah! Ni mochwari?" Osward alijifanya kushangaa.
"Ndio naomba urudi kule uliza pale mapokezi watakusaidia kukuelekeza ni wapi umpate ndugu yako" Sandra alitoa maelekezo.
"Sawa nashukuru sana dadangu samahani kwa usumbufu"
"Bila samahani"
Osward alianza kuondoka akapishana na Sandra lakini wakati wanapishana macho ya Osward yalipita kwa haraka sana kwenye kutambulisho alichokuwa amekivaa Sandra hapo Osward aliweza kugundua kitu cha tofauti. Kitambulisho kilikuwa na sura tofuauti kabisa na Sandra tena kilikuwa kitambulisho cha mwanaume.

"Ni wao, hawa ni wamoja" Osward aliwaza wakati huo akiendelea kupiga hatua kuondoka.
Baada ya kutembea kwa umbali mrefu Osward aligeuka kuangalia lakini hakumuona yule dada tayari alikuwa ameingia ndani ya jengo la mochwari.

"Hapana sio bure kuna kitu kinaendelea hapa" aliwaza Osward akaangaza macho huku na hule hakuona mtu taratibu akaanza kurudi tena kule mochwari safari hii akiwa makini kuliko mwanzo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Osward aliweza kujipenyeza tena kwa mara nyingine mwisho alipata upenyo akawa anachungulia ndani ya mochwari akashuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Aliwaona Shadow na Sandra wakiutoa mwili wa mtu aliyefungwa sanda kutoka kabatini kisha wakamvua ile sanda wakachukua sindano moja na kumchoma kifuani. Baada ya kuangalia kwa makini Osward aligundua kuwa ulikuwa ni mwili wa Inspekta Aron.

Baada ya kumchoma sindano Sandow alianza kukikandamiza kifua cha Inspekta Aron mara kadhaa huku Sandra akiufungua mdomo wa Inspekta Aron na kumpulizi pumzie mdomoni (CPR). Walifanya hivyo kwa zaidi ya dakika tano. Mara ghafula Inspekta Aron alikohoa na kufungua macho yake.

"Ooh! Thanks God he is alive" (Ooh! Asante Mungu ni mzima) Alisema Sandra na kutabasamu.
Aron aliinuka akaangaza macho yake kushoto na kulia kisha macho yake yakatua kwenye sura za watu waliokuwa mbele yake Sandra na Jasusi Shadow.
"Niko wapi hapa" Aron aliuliza sauti yake ikiwa kama mtu aliyetoka usingizini.

"Relax Aron umefanya kitu sahahi sana kama tulivyokuelekeza kwenye ile barua sasa ni wakati wetu wa kukutoa hapa" alisema Sandra.
Inspekta Aron alijaribu kuvuta kumbukumbu na mwisho akakumbuka kila kitu.

"Hapa ni wapi?" Aliuliza
"Hii ni mochwari ya hospitali ya taifa Kirunguru, uko hapa kwa sababu umekufa, kila mtu anaamini umekufa" alieleza Jasusi Shadow
"Wewe ni yule jamaa wa siku zote?" Inspekta Aron aliuliza baada ya kusikia sauti ya Shadow haikuwa ngeni tena, tayari alishaizoea.
"Ndiyo ni mimi" Jasusi shadow alijibu huku yeye na Sandra wakitabasamu.
"Aron umefanya kile ulichotakiwa kufanya sasa ni zamu yetu utatusikiliza sisi na kufuata maelekezo yetu ili tukusaidie" Alisema Sandra
"Okay nawasikiliza"
"Kwa sasa taarifa za kifo chako zimeshaanza kusambaa na tayari daktari ameshathibitisha kifo chako hivyo muda si mrefu ndugu zako watakuja kuuchukua mwili wako hivyo hatuwezi kuondoka na wewe sasa hivi kwa sababu itaibua maswali mengi kwa nini maiti yako ipotee" alieleza Jasusi Shadow.
"Kwa hiyo nitatoka muda gani mnataka mpaka wakanizike?"
"Hapana tunao mpango"
Majadiliano yaliendelea wakati huo Osward alikuwa mahali amejificha akisikia kila kitu.
"Nilisema huu ni mchezo, sasa hawa ni akina nani? Kwa nini wanamsaidia Aron" Osward alijiuliza maswali huku akiingiza mkono wake mfukoni kuchukua simu akageuka nyuma na kusogea pembeni kidogo. Haraka akabonyeza simu yake na kuitafuta namba ya Rais mstaafu Profesa Cosmas Kulolwa kisha akapiga. Simu ikawa inaita upande wa pili ikaita mara ya kwanza bila kupokelewa, akapiga tena kwa mara ya pili.

"Pokea basi Mheshimiwa nikupe habari za moto moto" alisema Osward lakini mara ghafula alihisi kitu cha baridi kimemgusa shingoni haraka akageuka. Uso kwa uso Osward alijikuta anatazamana na mdomo wa bastola ya Sandra.
Osward alitoa macho kwa hofu huku mapigo yake ya moyo yakianza kumuenda mbio, kifo kilikuwa usoni kwake. Sandra alimuonyesha ishara kwa kunyoosha mkono akimtaka Osward ampe ile simu ambayo tayari ikuwa imepokelewa na Profesa Cosmas Kulolwa.

Osward alinyoosha mkono wake akampa ile simu, Sandra akaipokea na kuikata.
"Weka mikono yako kichwani alafu ongoza njia ingia humo ndani" Alisema Sandra.
Hali akitetemeka Osward alifanya kama alivyoambiwa akaweka mikono kichwani kisha akaanza kupiga hatua kuingia mochwari Sandra akawa anamfuata nyuma huku akiwa ameweka bastola yake kwenye mgongo wa Osward.

Alipoingia ndani akakutana na Inspekta Aron pamoja na Jasusi Shadow wakimtazama kwa macho makali kiasi cha kumfanya Osward azidi kuogopa.
Jasusi Shadow na Sandra walitazamana kisha wakapeana ishara fulani wanazozijua wao mara Sandra aliinua mkono wake wa kushoto juu akaushusha kwa nguvu kwenye shingo ya Osward ambaye hakupata maumivu bali aliona nyota nyingi hewani kisha giza nene akaanguka chini kama gunia akiwa amepoteza fahamu. Sandra aliichomeka bastola yake kiunoni mwake akatembea hadi pale walipo Inspekta Aron na Jasusi Shadow wala hakujali tena kuhusu Osward.

Tayari Jasusi Shadow na Sandra walikuwa wamemuelekeza mpango mzima Inspekta Aron jinsi watavyo hakikisha wanamtoa huku habari za kifo chake zikiendelea kubaki palepale na watu wote kuamini Aron amekufa.

"Mh!" aliguna Inspekta Aron
"Usijali ni mchezo mgumu lakini salama, hatua ya kwanza ndio ilikuwa ngumu ila hii ya mwisho ni rahisi sana, kuwa mtulivu na mwenye subira pia" Alisema Sandra
"Vipi kuhusu huyu Osward?" Aliuliza Aron
"Hadi aje kuzinduka tayari kila kitu kitakuwa kimekwisha"
"Lakini ameshaona kila kitu na anajua mimi niko hai"
"Ni kweli ila unafikiri kwa huu mapango wetu nani atamuamini, ataonekana kichaa tu kwanza hawezi kusema chochote" alijibu Jasusi Shadow.

Baada ya hapo Sandra na Jasusi Shadow walisaidiana kumfunga Inspekta Aron sanda kwa mara nyingine kisha wakafungua kabati wakavuta droo moja kubwa yenye namba 471 wakamuweka Aron kama alivyokuwa awali kisha wakaisukuma na kuifunga vizuri.

" Vipi mwanangu unapumua vizuri humo?" Aliuliza Jasusi Shadow
"Mmmmmm" Aron aliitika baada ya hapo wakamalizia kwa kufunga milango ya kabati hilo.
" Na huyu je tumuweke wapi?" Aliuliza Shadow
"Tumuweke ndani ya lile kabati kule nafikiri halitumiki kwa sasa ni la zamani" Sandra alitoa wazo.
Mwisho wakasaidia kumuinua Osward wakambeba na kumuingiza ndani ya lile kabati chakavu kisha wakalifunga vizuri.

"Kila kitu tayari"
"Yes tayari, weka kora ya koti lako vizuri"
"Okie twende"
"Sawa"
Jasusi Shadow na Sandra walizungumza kisha taratibu na kwa kujiamini wakaanza kutembea kutoka nje ya jengo la mochwari.

Je nini kitafuata?
Mpango huu utafanikiwa kwa asilimia mia moja?
Ni mpango gani?
Vipi kuhusu Najma, Osward na Annah?
Maabara ya ZMLST wanafanya nini hivi sana?
Vipi kuhusu Sultana?
ITAENDELEA...


Simulizi hii ni Tsh 1000 tu lipia kwa mpesa namba 0756862047 jina Saul au Airtel money namba 0788967317 jina Saul
Kisha njoo WhatsApp namba hzo hzo[emoji120]
 
simulizi nzuri ina ubunifu mkubwa tatizo inatoka kiubahili sana, ingekua unatoa vipande hata vitatu, ila mzee unatoa kimoja na ni kifupi sana, that's why engagement unapata ndogo, nenda kaangalie novel la singanojr uone lilivyojaa raia na namna anavyopost episode za kutosha
 
simulizi nzuri ina ubunifu mkubwa tatizo inatoka kiubahili sana, ingekua unatoa vipande hata vitatu, ila mzee unatoa kimoja na ni kifupi sana, that's why engagement unapata ndogo, nenda kaangalie novel la singanojr uone lilivyojaa raia na namna anavyopost episode za kutosha
Simulizi imeanza march 21, leo ni may 23 tuko episode ya 50 ...
Unataka nipost kwa mlolongo upi, kumbuka hii ni kazi na kila mtu anazo taratibu zake. Toa lawama kwa wale ambao hawamalizi simulizi zao humu JF. Issue ya engagement inaonekana kwa wale wanao-support kaz zetu hata kwa hzo buk buk sio kwa comment nyng za wanaosoma bure...
KARIBU ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII kwa taratibu zilizopangwa na mwandishi
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya............52
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
"Kila kitu tayari"
"Yes tayari, weka kora ya koti lako vizuri"
"Okie twende"
"Sawa"
Jasusi Shadow na Sandra walizungumza kisha taratibu na kwa kujiamini wakaanza kutembea kutoka nje ya jengo la mochwari.

Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
[emoji294][emoji294][emoji294]
Taratibu za kuandaa msiba nyumbani kwa marehemu jenerali Phillipo Kasebele zilikuwa zikiendelea huku watu wakianza kukusanyika kimakundi makundi kuungana na wengine wakiwa tayari kuomboleza msiba wa Inspekta Aron mdogo wake Tino na mtoto wa kamanda ambaye aliwahi kuwa maarufu marehemu jenerali Phillipo Kasebele.
Maneno ya hapa na pale yalikuwa ni mengi mno kila mmoja aliongea lake kueleza hisia zake juu ya mfuatano wa matukio hayo ya kustaajabisha na kuuzunisha pia. Kwanza yalianza na kusambaa kwa picha chafu za ngono za marehemu Dokta Gondwe ikafuata kifo chake huku Aron akiwa ndio muhusika mkuu wa mauaji hayo alafu ikafuatiwa na kifo cha ghafula cha Inspekta Aron mwenyewe.
"Atakuwa amejiua"
"Labda serikali imempa sumu"
"Hapana sio serikali labda ni ndugu au jamaa wa Dokta Gondwe wamelipa kisasi"
"Maskini alikuwa kijana mdogo"
"Nasikia amekufa kwa ugonjwa wa mshituko wa moyo hii inawezekanaje kwa kijana mdogo kama yule, magonjwa ya moyo wapi na wapi?"
"Pengine ni kweli alikuwa na hofu baada ya kukamatwa"
"Kweli malipo ni hapa hapa Duniani kaua naye kafa"
"Hamna mi naamini hakuua"
Haya yalikuwa ni mazungumzo ya hapa na pale kati ya watu waliokuwa wamehudhulia msibani.
Mara Tino na mkewe Jesca walionekana wakitoka ndani wakiwa wameongozana.

"Kwani lazima twende wote?" Aliuliza Tino
"Sasa mumewangu utaendaje kuchukua maiti peke yako si twende wote"
"Hii ni kazi ya wanaume"
"Basi tafuta watu ongozane nao"
"Usijali wewe baki hapa na wageni, alafu kwa nini ulichelewa kunipa taarifa"
"Swali gani hilo mme wangu tuko msibani jamani" Jesca alijitetea
"Kwani sipaswi kukuuliza, nakuona tu siku hizi uko bize, nikitoka na wewe unatoka si ndiyo!!" Tino alifoka.
Tangu siku alipoitazama ile picha ya ngono ya mkewe na marehemu Dokta Gondwe alibadilika kitabia na kuwa mkali sana kwa mke wake, hata mapenzi yake yalipungua licha ya kwamba aliendelea kuifanya hii kubaki kuwa siri yake.

"Basi nenda nitabaki na wageni, naona ndugu zetu wengine hao wanafika" alieleza Jesca.
Tino hakujibu chochote akapiga hatua hadi lilipo gari lake wakati akifungua malango mara akawaona Inspekta Jada akiwa na Wakili Andrea getini wakiingia. Tino alisita akawasubiri hadi walipofika karibu yake.

"Pole Tino" Inspekta Jada aliongea kwa masikitiko makubwa sana lakini Tino hakumjibu kitu akamtazama kuanzia juu mpaka chini kisha akasonya.

"Naona umefurahi sasa, hiki ndio mlikuwa mkikitafuta wewe na Aron sio?" Aliuliza Tino huku akimtazama Inspekta Jada kwa macho makali, Inspekta Jada akawa kimya.
"Nakuliza wewe afande usie na haya, umesababisha mdogo wangu amekufa kizembe kwa kumuingiza kwenye misheni hatari hatari, hivi mlikuwa mnajiona akina nani kwanza, mfupa ulimshinda fisi wewe kuku poli utauweza? Haya ona sasa matokeo yake, ameondoka wa kwanza unafuata wewe" Tino alifoka kiasi cha kuwafanya watu waliokuwa karibu kubaini kuwa mazungumzo kati ya Inspekta jada na Tino hayakuwa ya kheri. Jada naye hakutaka kuonyesha unyonge akasogeza uso wake karibu na uso wa Tino sasa wakawa wanatazamana jicho kwa jicho pua kwa pua.

"Sikiliza wewe baba bure, kwani yule uliyekuwa unamtegemea sana yuko wapi sasa hivi, huyu Dokta Gondwe uliyemuona Mungu mtu kwako nakuuliza yuko wapi? Sasa sikia ameanza yeye na wewe utafuata, hiyo michezo yenu michafu mliyokuwa mkiifanya itawageukia na kuwatafuna mmoja baada ya mwingine hadi muishe wote. Aron alisimama kwenye haki na amekufa katika haki, hata kama na mimi nikifa wataibuka kina Aron wengine na HAKI ITAENDELEA KUPIGANIWA daima, fahamu hilo Tino" Inspekta Jada aliongea kwa kujiamini

"Ooh! Bado kichwa ngumu, basi sawa tutaona. Naenda kuchukua mzoga wa rafiki yako badae" Alisema Tino kisha akaondoka.

"Aisee huyu jamaa anaroho ngumu kama sio mdogo wake aliyefariki" Alisema wakili Andrea
"Mpuuzi tu hana lolote"
"Sawa twende tukakae lakini vipi wale wadada uliowakamata wamesema chochote?"
"Wale mapacha Erica na Elina?"
"Ndiyo"
"Hamna hawajaongea, nasikia amri imetolewa kutoka juu kuwa waachiwe hakuna ushahidi wowote kwamba ni waharifu"
"Dah! Hivi ni nani anaipeleka serikali kihunihuni hivi"
"Alaa! Kwani hujui"
"Sijui nini Jada?"
"Hii nchi bado ipo mikononi mwa uongozi uliopita wao ndio kila kitu"
"Alafu kweli, hapo umeongea Jada"
"Kama Aron angekuwa hai nisingekubali hili agizo la hawa wanawake kuachiwa, najua wao wanafahamu kila kitu kuhusu kifo cha Dokta Gondwe na kusingiziwa kwa Aron sema basi tu" Inspekta Jada aliongea kwa uchungu sana Andrea akawa anamtazama kwa macho yaliyojaa huruma. Mambo yalikuwa ni magumu sana kwa upande wao, kila hatua waliyopiga walikuwa wanakutana na kizuizi na sasa hali inakuwa mbaya zaidi baada ya kushindwa kesi mahakamani, Aron kukamatwa na mwisho anafariki pia Annah anapotea ghafula hajulikani alipo mpaka sasa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Dakika 20 baadae Tino akiwa na baadhi ya Vijana wake walifika hospitali ya taifa Kirunguru kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu mdogo wake Inspekta Aron. Walifika wakiwa wamejikamilisha kwa kila kitu, tayari Tino alishanunua jeneza la bei ghali kwa ajili ya kuuhifadhi mwili wa mdogo wake Inspekta Aron.
Walianza taratibu muhimu za kuuchukua mwili wa Inspekta Aron lakini wakati wakiwa kwenye harakati hizo wasijue hili wala lile mara kuna mtu aliyevaa mavazi ya wauguzi wa hospitali hiyo alionekana akitembea kuelekea lilipo gari la Tino. Alipofika alifungua mlango wa gari upande wa dereva akaingia ndani. Baada ya dakika kama tatu hivi alitoka na kuondoka zake, huyu hakuwa mwingine bali Jasusi Shadow.
Hakuna aliyemuona wala kuhisi chochote Tino na watu wake walikuwa mochwari wakisaidiana kuuweka mwili wa Inspekta Aron kwenye jeneza.
Inspekta Aron aliweza sana kujituliza na kuigiza kama mtu aliyekufa hadi wanautoa mwili wake kwenye kabati na kuuweka ndani ya jeneza hakuna hata mmoja aliyemshtukia wote waliamini Aron amekufa. Walitoka na jeneza hilo na mwisho milango ya mochwari ikafungwa hakuna aliyejua uwepo wa Osward mle ndani akiwa katika moja kati ya makabati ya zamani ya kuhifadhia maiti, bado alikuwa hajarejewa na fahamu zake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Safari ya kuurudisha mwili wa Inspekta Aron nyumbani ilianza huku Tino mwenyewe akiwa ndiye dereva. Ndani ya gari yake walipanda vijana wake watatu huku wengine wanne wakiwa ndani ya gari la pili wakifuata nyuma taratibu.
Wakati huo Jajusi Shadow, Sandra pamoja na Fungo walikuwa kazini wakifuatilia kwa kila hatua huku mpango wao ukiwa unaenda vizuri hadi dakika hii.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Tino akiwa anaendasha gari yake kwa mwendo wa wastani alifika mahali penye mteremko akawa anajaribu kufunga breki taratibu lakini ni kama kuna kitu alihisi hakipo sawa katika gari yake, breki ilikuwa haishiki vile ipasavyo. akakanyaga tena na tena lakini bado breki haikufanya kazi, akajaribu tena kufunga breki ya mkono(hand break) lakini bado hali akawa ni ile ile.
Kabla hajajua nini afanye mara ghafula gari ilijibadili gia na kujiongeza mwendo yenyewe.

"Nini hiki?" Aliongea Tino
"Vipi mkuu kunashida" Aliuliza kijana mmoja baada ya kumuona bosi wake ni kama anahangaika sana na usukani wa gari. Tino hakujibu chochote badala yake akazidi kupambana kuimiliki gari yake ambayo ilionekana wazi inamshinda.
Baada ya dakika kama moja na sekunde chache hatimae gari ilianza kupunguza mwendo yenyewe ikiwa imefika katikati ya daraja moja refu sana huku chini yake kukiwa na mto mkubwa wa maji.

"Sielewi nahisi kunakitu hakipo sawa kwenye hii..." Hatimae Tino alifunguka kwa vijana wake lakini alishindwa kumalizia sentesi yake mara baada ya gari lake kukunja kona lenyewe na kuanza kuelekea pembeni kwenye kingo za daraja hilo.
Tino na vijana wake ambao tayari walishaelewa kuwa kuna Tatizo waliogopa huku wale waliokuwa wakifuata nyuma wasijue ni nini hasa kilichokuwa kikiendelea wakati ule. Walishangaa inakuwaje mkuu wao anaacha njia na kuelekea pembeni ya daraja jambo ambalo lilikuwa ni hatari.

Bila hata kuongea chochote kingine Tino alikuwa ni wa kwanza kufungua mlango wa gari na kuruka nje wakifuatia vijana wake nao wakaruka wote.
Haukupita muda gari liliacha ardhi na kuanza kwenda chini huku likijibamiza mara kadhaa kwenye kuta za daraja hilo refu kabla ya kufika chini na kitumbukia ndani ya maji.
Tino na vijana wake wote pamoja na wale waliokuwa wakiwafuata nyuma walishuka na kuja kuungana na wenzao wakawa wanachungulia chini lilipozama gari la bosi wao likiwa na jeneza la maiti ya mdogo wake.

"Kwani imekuwaje?"
Aliuliza kijana mmoja ambaye ndiye aliyekuwa dereva wa gari lile la pili.
"Sisi pia hatuelewi ni kama gari lilianza kuleta shida si ndio hivyo mkuu?" Alijibu kijana mwingine huku akimtupia swali bosi wake, wote wakamgeukia wakitaka kusikia atajibu nini.
"Wazee hapa tumepigwa" Alisema Tino.

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Mtunzi: Saul David
Sehemu ya.................53
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Kwani imekuwaje?"
Aliuliza kijana mmoja ambaye ndiye aliyekuwa dereva wa gari lile la pili.
"Sisi pia hatuelewi ni kama gari lilianza kuleta shida si ndio hivyo mkuu?" Alijibu kijana mwingine na kumtupia swali bosi wake, wote wakamgeukia wakitaka kusikia atajibu nini.
"Wazee hapa tumepigwa" Alisema Tino

SASA ENDELEA....
[emoji294][emoji294][emoji294]
Mara tu baada ya gari la Tino kitumbukia na kuzama ndani ya maji Inspekta Aron alifungua jeneza akatoka wakati huo tayari maji yalishaingia na kujaa garini, akapambana na kufungua mlango wa gari huku akijitahidi kubana pumzi yake. Hatimae alifanikiawa kutoka kwenye gari lakini tayari alikuwa ameanza kuchoka na kuishiwa pumzi akiwa ndani ya maji.
Akiwa katika hali hiyo mara ghafula akatijokeza mtu mmoja akiogelea kwa kasi kama samaki kumfuata, mtu huyo hakuwa mwingine bali Sandra yule dada afisa usalama wa taifa ambaye alikuwa akifanya kazi na Jasusi Shadow chini ya Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zumo.
Sandra alikuwa amevaa mtungi wa gesi mgongoni mwake uliounganishwa moja kwa moja na maski iliyofunika pua na mdomo wake ikimsaidia kupumua. Sandra alikuwa amevaa pia vifaa maalumu vilivyomsaidia kuogelea kwa kasi, aliogelea haraka hadi karibu na Aron akachukua maski nyingine na kumvisha puani na mdomoni hapo Inspekta Aron alipata ahueni.
Kabla ya kuogelea na kuondoka Sandra alimpa ishara fulani Inspekta Aron, wakaogelea kwenda chini zaidi hadi walipolifikia gari la Tino likiwa limegusa ardhi chini ya kina kirefu cha maji.
Sandra atupia kifaa fulani chenye rangi ya udhurungi ndani ya lile jeneza baadae wakawa wanaogelea kuondoka, hawakufika mbali mara gari na lile sanduku vikalipuka na kusambaratika vipande vipande. Inspekta Aron na Sandra waliendelea kuogelea chini kwa chini huku wakisaidiwa kupumua na ule mtungi wa gesi alioubeba Sandra.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Ilikuwa ni majira ya saa saba usiku ndipo Osward aliporejewa na fahamu zake. Alifumbua macho taratibu na kujikuta amelala sehemu asiyo ielewa, alikurupuka kwa kasi bila kutegemea akajikuta anadondoka chini sakafuni kutoka ndani ya lile kabati. Osward aliumia kiasi lakini alijikaza na kukaa chini.
Kulikuwa giza totoro ndani ya chumba kile cha mochwari taa zilikuwa zimezimwa zote. Osward alijaribu kuvuta kumbukumbu mwisho akakumbuka kila kitu namna alivyowaona wale watu waliokuwa wakimsaidia Aron kutoka kwenye kabati la maiti na kisha kumzindua alafu mwisho wakamkamata. Hakujua ni nini kilitokea baada ya hapo.
"Kwa hiyo hawakuniua? Kwamba bado niko mochwari?" Osward alijiuliza maswali mwenyewe huku akijaribu kusimama. Hakuwa na simu wala kifaa chochote ambacho kingemsaidia kumpatia mwanga angalau hata aweze kuuona mlango wa kutokea. Osward alianza kuhangaika akitembea kwa namna ya kupapasa akijaribu kwenda kwa hisia akawa anautafuta mlango. Wakati akizidi kuhangaika mara ghafula alisikia mlio wa mlango ukifunguliwa taratibu. Osward aliganda pale alipo hakurudi nyuma wala kwenda mbele akawa anasikilizia huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio.
Mara alisikia sauti za watu wakinong'ona, walikuwa watu wawili mmoja mhudumu wa mochwari na mwingine ni mmoja kati ya walinzi wa hospitali hiyo. Walikuja usiku huo kufanya kazi za magendo kinyume na utaratibu wa hospitali ndio sababu hawakuwasha taa. Sikuzote walikuwa wakifanya hivyo hasa kuchukua maji yaliyooshewa maiti, wakati mwingine kukata kucha au vidole vya maiti pamoja na mambo mengine mengi yasiyofaa. Hizi ni dili zilizokuwa zikiwaingizia kipato kikubwa, walikuwa wakiagizwa na watu wenye imani za kishirikina.

Osward alianza kirudi nyuma taratibu akihofia kuonekana bahati mbaya alikanyaka kipande kidogo cha mbao kilichotoa mlio na kuwashtua wale watu mlangoni.
"Nini?"
"Sijui hebu washa tochi mulika pale ni kama kunakitu"
"Mmh!!"
"Washa tochi haraka mulika palee"
Walinong'ona wale watu na mwisho wakawasha tochi ya simu na kumulika pale alipo Osward. Uso kwa uso wakagonganisha macho yao
Aaaaaaaaa!!
Aaaaaaaaa!!
Wote walipiga kelele kwa pamoja, hakukuwa na muda wa kujiuliza mara mbilimbili wale watu walitupa kila walichonacho na kutimua mbio wakiamini wameona mauzauza ndani ya jengo la maiti. Osward naye hakuwa na muda wa kupoteza tayari alishauona mlango akatoka mbio bila kusimama akafika hadi geti la kuingilia hospitali hiyo akaondoka zake.
Hadi dakika hiyo ni yeye pekee ndiye aliyekuwa anafahamu kuwa Inspekta Aron hajafa yuko hai lakini taarifa zilizokuwa zikisambaa mtaani mpaka sasa ni kuwa Tino aliyekuwa amebeba maiti ya mdogo wake Inspekta Aron ambaye ni muuaji wa Dokta Gondwe amepata ajali daraja la Kilolo gari pamoja na maiti ya Aron vimezama ndani ya maji na mpaka sasa hakuna kilichopatikana.
[emoji294][emoji294][emoji294]

ASUBUHI SIKU INAYOFUATA...
Inspekta Aron, Sandra pamoja na Jasusi Shadow walikuwa ndani ya ile nyumba ya siri msituni nyumba ya marehemu jenerali Phillipo Kasebele. Mambo yote yalikuwa yameenda vizuri na sasa walifanikiwa kumuokoa Inspekta Aron dhidi ya mkono wa sheria huku wakitengeneza mazingira ya kuwaaminisha watu kuwa Inspekta Aron amekufa.
Hadi dakika hiyo Inspekta Aron hakuwa ameelezwa chochote si Shadow wala si Sandra waliotakiwa kuongea naye wakati huo hilo liliachwa kuwa jukumu la Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zumo ambaye baada ya dakika chache alifika na msafara wake wa magari mawili tu.
Baada ya salama Sandra na Shadow walitoka nje ya kile chumba wakamuacha Inspekta Aron pamoja na Mheshimiwa Rais.
Ilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwa Inspekta Aron kumuona Rais wa nchi maeneo hayo, shauku ya kutaka kujua ni nini kinaendelea iliongezeka mara dufu. Rais alilitambua hilo, bila kupoteza muda wakakaa na kuanza mazungumzo.

"Pole na hongera kwa kila kitu Aron, tumekuleta hapa kwa kusudi maalumu kusudi ambalo ni ndoto za marehemu baba yako ambaye siku zote alikuwa anatamani nchi yetu iendelee kuwa na utulivu na amani ya kutosha. Kwanza kabisa nataka uelewe kwamba umekufa, Dunia nzima inaamini kuwa wewe umekufa kuwepo hapa na sisi maana yake umezaliwa upya na rasmi utaanza kufanya kàzi pamoja nasi"
Rais Dkt Alfredo Zumo alizungumza maneno ambayo bado yalimuweka fumboni Aron. Baadae Rais aliendelea kueleza

"Aron, kama unavyojua baba yako alikuwa ni mwanaharakati wa kupigania haki na usalama wa Taifa na watu wake, bahati nzuri wewe pia alikulea katika misingi ya kuhakikisha utaendeleza harakati zake hata bila yeye kuwepo ndio maana uko hapa. Tunayo mambo mengi sana ya kufanya kwa ajili ya kupigania nchi yetu lakini la kwanza na la muhimu ambalo ndilo tunapambana nalo kwa wakati huu ni kuhusu virusi vya V-COBOS, najua hili neno sio geni kwako, acha nikuelekeze kiundani jinsi hali ilivyo."

Hapo Rais Dkt Alfredo Zumo alianza kueleza kiundani kabisa kuanzia siku vimelea vya V-COBOS vilivyoingia nchini kwa siri, baadae baba yake Aron akakataa kuwa mshirika wa watu hao kutoka Mexico wenye lengo la kusambaza ugonjwa wa ajabu utakao enea Dunia kote ukianzia hapa nchini. Alimweleza pia namna baba yake alivyopambana na kuiiba chupa ya kijivu ambayo inakinga na tiba dhidi ya vimelea hao hatari na baadae umauti ukamfika huku kaka yake Tino akihusika moja kwa moja na kifo chake. Rais akaeleaza jinsi mama yake Aron yaani Sultana alivyoachiwa jukumu la kuendeleza harakati za marehemu mume wake akiwa karibu na Jasusi Shadow, jinsi alivyolazimika kujifanya mgonjwa na kulazwa hospitali kwa zaidi ya miezi sita ili tu Tino asiweze kumdhuru kwani anajua mama yake Sultana ndiye mtu pekee anayefahamu ilipo chupa ya kijivu yenye dawa na kinga ya virusi vya V-COBOS lakini baadae inakuja kujulikana kuwa kumbe hata Sultana naye alikuwa na nia ovu kama wengine ya kuvitaka vimelea vya V-COBOS kwa tamaa zake mwenyewe kinyume kabisa na matakwa ya marehemu mumewe.
Yalikuwa ni maelezo yaliyomshtua sana Aron, sio kumshtua tu hata kumuumiza pia, kumbe kwa kipindi chote familia yake ilikuwa kwenye VITA KALI bila yeye kujua. Taarifa za kaka yake Tino kuhusika na kifo cha baba yake zilimuumiza zaidi Jambo lingine kubwa ni kuhusu kuumwa kwa mama yake kumbe kipindi chote wanahangaika pale hospitali ya Mountenia mama alikuwa anaigiza tu wala haumwi.

"Pole Aron najua ni taarifa ngumu sana kuzipokea lakini ili twende pamoja ni lazima uujue huu ukweli ambao ni mchungu kwako, natoka nitarudi tena baadae" Alisema Rais huku akiinuka akavaa koti lake na kuweka tai vizuri kisha akatoka, mlangoni alikutana na Sandra.
"Mwenzako yuko wapi?" Aliuliza Rais, akimaanisha Jasusi Shadow.
"Ametoka kwenda kuonana na Sultana" alijibu Sandra
"Sawa mwambie anipe taarifa akirudi kutoka huko, kuwa karibu na Aron bado atakuwa na maswali mengi ya kuuliza mweleze kila kitu kuhusu sisi"
"Sawa Mheshimiwa"
"Okay baadae"
[emoji294][emoji294][emoji294]

Ndani ya hospitali ya Mountenia tayari kupitia njia zilezile za panya Shadow alikuwa ameshaingia na kama kawaida akawa anaelekea chumba cha Sultana. Alifika akafungua mlango na kuingia ndani huku akiwa makini kuhakikisha hakuna anayemuona.
Ulikuwa umepita muda tangu alipokutana na Sultana kwa mara ya mwisho wakakubaliana kuwa anakwenda maabara kuu ya taifa kuiba ile chupa ya kijani yenye vimelea lakini wala Shadow hakwenda alikuwa bize kupambana kumuokoa Inspekta Aron. Lakini hadi anaingia mle ndani tayari alikuwa ameshapanga nini cha kwenda kumueleza Sultana.

Baada ya kuingia Jajusi Shadow alipata mshtuko kiasi mara baada ya kugundua kuwa kitandani palikuwa patupu hapakuwa mtu. Aliangaza macho huku na hule lakini hakumuona bosi wake Sultana. Haikuwa kawaida kabisa Sultana kutoka bila kumuaga Shadow alihisi lazima kuna kitu hakipo sawa.
"Amekwenda wapi? Mbona sio kawaida? Au tayari wale wamexico wameanza kazi yao? Mbona mapema sana..." Shadow alikuwa akijiuliza mwenyewe bila kuwa na majibu sahihi, wakati akiwa kwenye hali hiyo mara ghafula alihisi kuna kitu cha baridi kimemgusa shingoni.

"Tulia hivyo hivyo, ukijaribu kujitikisa hata kidogo nakumwaga ubongo" Ilisikia sauti laini ya kike kutokea nyuma yake.
Shadow alitulia kama alivyoelekezwa huku akili yake ikifanya kazi upesi kujaribu kuangalia ni jinsi gani anaweza kujiokoa kwenye balaa lililoko mbele yake.

"Weka mikono yako kichwani alafu piga magoti chini" Ile sauti ya kike ilitoa amri
Jasusi Shadow alitulia kwa muda kisha akafanya kama alivyo amrishwa. Baada ya hapo aliwaona watu watatu kila mmoja akiwa na bunduki mkononi huku sura zao zikiwa zimefunikwa na vinyago vyenye muundo wa kichwa cha simba wakipita na kusimama mbele yake.

Je, nini kitafuata?
Ni akina nani hawa?
Sultana yuko wapi?
Vipi kuhusu Aron, Najma, Osward na Annah

ITAENDELEA...
 
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya............54
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Jasusi Shadow alitulia kwa muda kisha akafanya kama alivyo amrishwa. Baada ya hapo aliwaona watu watatu kila mmoja akiwa na bunduki mkononi huku sura zao zikiwa zimefunikwa na vinyago vyenye muundo wa kichwa cha simba wakipita na kusimama mbele yake.


SONGA NAYO....
Jasusi Shadow aliwakagua mmoja baada ya mwingine akagundua kuwa wote watatu walikuwa ni wanawake. Hakujua ni nini kimetokea hasa kwenye chumba cha bosi wake Madam Sultana. Akiwa katika hali ya kufikiri mara akasikia vishindo vya watu zaidi ya wawili wakiingia kutokea nyuma yake, walitembea taratibu na kusimama mbele yake.
Jasusi Shadow alipowatazama moyo wake ulipiga Paaa!! Kutokana na mshituko mkubwa alioupata, alikuwa ni Jesca yule mke wa Tino akiwa na Madam Sultana pamoja na Daktari wa hospitali hiyo ambaye ndio mtu pekee hospitalini hapo anayeijua siri ya Sultana.
"Unashangaa nini hukutegemea kutuona? Unafikiri ungeendelea kutuchezea akili mpaka lini Shadow?" Aliongea Madam Sultana huku akiwa anamtazama Jasusi Shadow kwa macho makali.
"Nini shida bosi?" Aliuliza Jasusi Shadow akitaka kujua ni nini hasa kilichomfanya Sultana amuweke chini ya ulinzi, alihisi mambo tayari yameharibika akataka kujihakikishia.
"Shadow najua umekuwa mwaminifu kwetu tangu enzi za marehemu mume wangu ila tangu ujue mipango yangu ni wazi umeanza kwenda kinyume na mimi, unanisaliti" Alieleza Sultana.
"Kivipi bosi mbona sielewi?"
"Ahh! Usijifanye hujui kitu najua unanielewa vizuri, tulikubaliana na marehemu kuwa utakuwa bega kwa bega na mimi ukinilinda nyakati zote haijarishi nini kitatokea sasa mbona unakwenda kinyume? Unaweza kuniambia kuanzia tulipoachana hapa kwa mara ya mwisho ulikuwa wapi?"

"Bosi ulitakiwa kuniuliza kwanza na sio kuni...."
Alisema Jasusi Shadow lakini kabla hajamalizia kuongea Sultana alichomoa bastola iliyokuwa ndani ya baibui lake akaikoki na kufyatua risasi ambayo ilipiga sakafuni katikati ya miguu ya Jajusi Shadow.

"Unafikiri natania Shadow, now tell me everything...!! ni nani unaeshirikiana naye na mnapanga kufanya nini usiponiambia ukweli nakuhakikishia leo ndio utakuwa mwisho wako" Sultana aliongea kwa kumaanisha huku akisogea karibu kabisa na alipo Shadow.
Ni kweli Sultana alikuwa amedhamiria kufanya kile anachokisema tayari alishagundua kuwa kijana wake wa muda mrefu Shadow alikuwa anamzunguuka kwa namna moja au nyingine.

"Haukwenda kule tulikopanga, haujaenda kuleta chupa ya kijani tuliyokubaliana, hiyo ndio sababu haukutaka nikupe watu wa kukusaidia kumbe unamambo yako ya siri unayafanya, haya unaweza kuniambia ulikuwa wapi? na nani? mnafanya nini?"
Aliuliza Sultana.
Wakati wote huo Jajusi Shadow alikuwa kimya huku akiwaza nini afanye. Alishaona kabisa tayari mambo yameharibika Sultana kamshitukia.
Uwezo wa kupambana na kutoka kwenye balaa hilo alikuwa nao, kwa namna Sultana alivyomsogelea angeweza kumvaa na kumteka kisha kutoka akiwa salama lakini aliwaza kama atakuwa mbali na Sultana basi ni ngumu kujua ilipo chupa ya kijivu yenye kinga na tiba dhidi ya vimelea vya V-COBOS, hakuna mtu mwingine anayefahamu chupa hiyo ilipo zaidi ya Sultana mwenyewe.

"Huna cha kujibu au unafikiri unàweza kutoka hapa ukiwa salama Shadow ukweli nakuua leo" aliongea Madam Sultana kisha akatoa ishara fulani wale wanawake waliweka bunduki zao sawa na kuzielekeza alipo Jajusi Shadow, Jesca na Sultana nao walimnyoshea bastola zao zilizofungwa kifaa maalumu kinachozuia mlio wa risasi kusikika 'silencer'

"Haya Jajusi endelea kuwaza namna ya kutoroka mimi sina muda wa kupoteza nahesabu mpaka kumi kama hujaongea ukweli basi nakuondoa duniani, Kumi...tisa....nane....saba.....sita....tano...nne...tatu....mbi...."

"Nitaongea! nitaongea! nitaongea ukweli bosi Sultana.." Jajusi Shadow alidakia kabla Sultana hajamaliza hesabu yake na kufyatua risasi.

"Ongea nakusikiliza.."
"Ukweli sikwenda kuvamia maabara Madam" Alisema Shadow huku akiwaza namna gani ataweza kujiokoa mwenyewe
"Najua.. eleza mtu unaeshirikiana naye kunizunguuka na usijaribu kudanganya nitakuua"
"Hakuna ninayeshirikiana naye madam ila wakati najiandaa kwenda maabara kuu ya serikali nilitekwa na watu nisio wafahamu sijui waliwezaje kunipata, baadae nikagundua ni wale wazungu kutoka Mexico namaanisha wale wamiliki halali wa virusi vya V-COBOS. Sultana hawa watu tayari wapo hapa nchini na tayari wameshachukua vimelea kutoka maabara kuu ya serikali na sasa wanaitafuta ile chupa ya kijivu niliwasikia wakiongea kuwa tayari wameshajua ilipo na jioni ya leo wataenda kuichukua" Shadow alidanganya.
Sultana alitulia kwa muda akijaribu kutafakari maelezo hayo ambayo kwa kiasi yalimuingia. Habari za wamexico kuwepo nchini ndio zilizomchanganya zaidi, kusikia virusi vimetolewa maabara na sasa wanavyo wao ilikuwa ni habari mbaya mno kwa Sultana. Ndoto aliyoihangaikia kwa muda mrefu sasa ilikuwa mbioni kuzimwa kama mshumaa uliopulizwa na upepo.

"Wewe uliwezaje kutoka?" Aliuliza Sultana huku safari hii sauti yake ikiwa ndogo
"Niliwatoroka"Alijibu Shadow. Kukawa na ukimya tena, mwisho Sultana akaongea.

"Jesca andaa kikosi kazi muondoke kuifuata chupa yangu ya kijivu" Alisema Sultana lakini kauli hii ilimshtua sana Jesca
"Madam tutawezaje kwenda bila wewe, kumbuka chupa ilikabiziwa kwa chifu wa kabila hawawezi kuitoa bila wewe kuwepo"
"Tumieni nguvu ikibidi hata kuua"
"Sultana lile kabila sio rahisi kupambana nalo mbona uki..."
"Jescaaaaa! Umeanza lini kunipa ushauri, fanya kama nilivyosema nendeni mkailete chupa hapa mimi nina kazi ya kufanya au hujasikia kama wazungu wamechukua vimelea vyao, unafikiri kama wote tukienda huko hivi vimelea tutavipataje, kumbuka tunahama kutoka plan A kuja plan B"Sultana alifoka, kisha akageuka na kumuangalia Shadow.

"Na wewe nikigundua kuwa unatudanganya nitakuua kifo kibaya sana. Haya mhamisheni hapa mpelekeni kwenye ngome hakikisheni mnamlinda na msisahau kwamba huyu ni mtu hatari sana kosa moja linaweza kuwaghalimu. Siwezi kumwamini kwa sasa mpaka mambo yatakapokaa sawa"

Baada ya Sultana kusema hivyo, Daktari wake aliingiza mikono kwenye mifuko ya koti lake akatoa kichupa kidogo na bomba la sindano akavuta ile dawa kisha akasogea karibu na Jajusi Shadow.

Wakati huo wote Shadow alikuwa ametulia kimya kabisa tayari uongo wake ulikuwa umefanya kazi kwa asilimia kadhaa alipata akachokitafuta. Tayari alishajua mazingira ambayo chupa ya kijivu inaweza kuwepo japo hakujua ni wapi. Maneno aliyoyazingatia katikati majadiliano ya Sultana na Jesca ni haya...

,,,,Chupa ilikabidhiwa kwa chifu wa kabila,,,,,,
,,,Lile kabila sio rahisi kupambana nalo,,,,,,

Haya ndio maelezo muhimu shadow aliyoyapata, angalau alikuwa na kwa kuanzia. Wakati daktari akiwa amefika karibu yake Shadow alitazama saa ya ukutani akaona ilikuwa ni saa nane na nusu mchana kisha akaminya kitufe furani kilichokuwa kwenye saa yake ya mkononi. Shadow alijua nini anafanya.

Yule daktari alifika na bila kusita iliinua mkono wake kwa nguvu kisha akaizamisha ile sindano kwenye shingo ya Shadow na kusukuma ile dawa. Hazikupita sekunde 30 Shadow alianguka chini na kupoteza fahamu.

"Mbebeni mpelekeni kwenye ngome, nasisitiza tena kuweni makini"
"Sawa bosi"
Walijibu wale wanawake walioshika bunduki.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati ule Jajusi Shadow amebonyeza kitufe cha saa yake ya mkononi upande wa pili saa aliyokuwa amevaa Sandra ilitoa mtikisiko na kisha kuanza kuwaka mwanga mwekundu. Akiwa nje ya ile nyumba msituni alikimbia hadi kwenye gari moja iliyokuwa imeegeshwa pembeni kidogo na nyumba akafika na kumuamsha mtu mmoja ambaye alikuwa amepumzika ndani ya gari hiyo.

"Fungo Fungo" Sandra aliita huku akigonga gonga kioo cha gari hiyo.
Fungo ni kijana mmoja mtaalamu wa kompyuta na mtandao ambaye ni kati ya wale watu watatu wanaofanya kazi chini ya Mheshimiwa Rais Dkt Alfredo Zumo kwa siri. Ndio huyu aliyeweza kuliendesha gari la Tino akiwa nje ya gari na mwisho akalitupa darajani ndani ya maji.

"Nini Sandra"
"Hivi hujaona saa yako"
"Kwani vipi?" Aliuliza Fungo huku akivaa miwani yake mikubwa na kuangalia saa yake ya mkononi. Kama ilivyokuwa kwa Sandra saa ya Fungo pia ilikuwa ikitoa mwanga mwekundu.

"Nini kinaendelea?"
"Ni Jajusi Shadow atakuwa kwenye matatizo"
"Jesus Christ..!!"
"Angalia haraka ni wapi alipo ngoja nimshtue Aron"
"Aron alitoka.." Alijibu Fungo huku akifungua kompyuta yake na kuanza kucharaza vidole vyake kwa kasi ya ajabu.
"Nini! Aron kaenda wapi?"
"Aliniaga kaenda kwenye kaburi la baba yake"
"Sasa kwa nini ulimruhusu?"
"Jesus Christ! Sandra unanichanganya hebu acha kwanza nimtrace Jajusi Shadow... Ningeanzaje kumkatalia asiende kwenye kaburi la baba yake na unajua kapewa historia nzito hayuko sawa. Usijali nilimpa mavazi mazuri hawezi kujulikana, ila kaondoka na pikipiki yako"
Alijibu Fungo huku akiendelea kucharaza kompyuta yake ndogo kwa kasi sana.

"Huyu hapa nimempata, yuko Hospitali ya Mountenia" Alisema Fungo
"Mh! Hospitali, yupo kwa Madam Sultana sasa kuna shida gani hadi aombe msaada au kashitukiwa"
"Jesus Christ! Mungu aepushie mbali"
"Washa gari twende pitia makaburini tumchukue Aron pia"
"Jesus Christ! Makaburini tena huoni kama tutachelewa"
"We twende bwana"
[emoji294][emoji294][emoji294]

Inspekta Aron alionekana maeneo ya makaburini mbele ya kaburi la baba yake marehemu jenerali Phillipo Kasebele. Alikuwa amevaa nguo nyeusi kofia na barakoa nyeusi pia, kofia yake aliishusha chini sana kiasi cha kufanya macho yake pekee ndio yawe wazi, haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kumtambua.
Mambo aliyokuwa ameelezwa na Mheshimiwa Rais yalikuwa ni mazito mno kwa Aron. Kilichomuumiza sana ni kuambiwa mtu aliyemuua baba yake ni kaka yake Tino tena mbaya zaidi kwa ajili ya tamaa ya kuvitaka vimelea vya V-COBOS ambavyo mpaka sasa wanagombania yeye na mama yake Sultana. Habari hizi hazikuwa njema hata kidogo kwa Inspekta Aron.
Alimaliza kuomboleza akageuka tayari kuondoka lakini uso kwa uso anakutana na mwanamke anayemfahamu akiwa amesamama nyuma yake. Alikuwa ni Najma. Inspekta Aron aliduwaa kwa muda

"Au naota" Aliwaza Aron

Je, nini kimetokea? Imekuwaje? Kwa nini Najma yuko hapa? Vipi kuhusu Sultana na Jesca?
Jasusi Shadow atakuwa salama?

ITAENDELEA....
 
Back
Top Bottom