SIMULIZI RIWAYA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2022
- 417
- 1,285
- Thread starter
- #61
THE MODERN WAR
(Vita ya kisasa)
Sehemu ya...............39
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA...
Kwa kuwa nguo alizokuwa amevaa Osward zilikuwa ni sawa kabisa na nguo alizovaa Inspekta Aron kuanzia juu mpaka chini walinzi waliamini moja kwa moja kuwa huyo ndio yule yule mtu waliyekuwa wakimuandama tangu awali mtu aliyempiga risasi ya kifua Waziri wa afya Dokta Gondwe, hakuna aliyejua mabadilishano yaliyotokea ndani ya sekunde chache kabla ya wao kufika.
Je nini kitafuata?
SASA ENDELEA...
"Wanataka kuniuzia kesi" Aliwaza Inspekta Aron ni kama aliweza kuelewa kwa haraka ni nini kinaendelea hadi dakika hiyo. Kitendo cha akina Osward kumtupa maeneo yale kisha kuondoka na kumuacha tayari kilimfanya aielewe mbinu hiyo hasa baada ya kuwaona wale walinzi wanakuja nyuma yake kwa kasi sana.
"Kwani Osward kafanya tukio gani? hapana siwezi kukubali" aliwaza Aron huku akisimama haraka.
"Usijaribu tena kuendelea kukimbia tutakumwaga ubongo wako, simama na ujisalimishe mwenyewe" alisema mlinzi mmoja ambaye yeye alikuwa na mbio kuwazidi wenzake tayari alikuwa amefika jirani kabisa na alipokuwa Inspekta Aron.
"Hapana siwezi kuwa na mwisho wa kizembe namna hii, haiwezekani kabisa" Aron aliwaza na hapo akaanza kukimbia kwa kasi lakini kabla hajapiga hatua hata tano mara alihisi kitu cha moto kimezama kwenye paja lake la kushoto ikifuatiwa na maumivu makali.
Inspekta Aron hakuweza tena kuunyanyua mguu wake alishika sehemu ile yenye maumivu kwa mkono wake wa kulia, alipoutazama mkono wake ulikuwa umelowa damu. Naam Inspekta Aron alikuwa amepigwa risasi.
Kufumba na kufumbua polisi wengine wa mtaa pamoja na trafiki wa barabarani wakatokea mbele yake wakija kwa kasi huku siraha zao zikiwa mbele.
"Nimekwishaa..." Alijisemea Inspekta Aron huku akilegea mwili na akili.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Dakika tano tu mara baada ya Dokta Gondwe kupigwa risasi gari la wagonjwa liliwasili kwa kasi eneo hilo, upesi wahuduma wa afya walifika na kuanza kutoa huduma ya kwanza kabla ya kumuingiza kwenye gari. Kwanza walijaribu kuzuia damu nyingi iliyokuwa ikimtoka Dokta Gondwe na baadae kujaribu kuunganisha mfumo wake wa upumuaji na mtungi wa gesi waliokuja nao.
Wakati jitihada hizi zikiendelea Najma alikuwa pembeni akilia kwa uchungu huku akiwa ameshikiliwa na baadhi ya watu wakijaribu kumzuia ili awaache madaktari wafanye kazi yao. Hofu ilikuwa ni kubwa si kwa Najma tu bali kwa kila mtu aliyekuwepo eneo hilo kila mtu aliyekuwa akishuhudia au kuliona na kulisikia tukio hili kupitia vyombo vya habari.
Baada ya kupambana sana kuyaokoa maisha ya mtu mkubwa serikalini Dokta Isaack Gondwe hatimaye jitihada zao zilionekana kugonga mwamba kwani risasi ilikuwa imepenya sehemu mbaya mno haikuwa rahisi hata kidogo Dokta Gondwe kusalimika.
Naam, Waziri wa afya Mheshimiwa dokta Gondwe aliaga Dunia pale pale kabla hata jahaingizwa kwenye gari kupelekwa hospitali.
Wataalamu wa afya waliokuwa wamemzunguuka Dokta Gondwe wakipambania maisha yake walianza kutoka mmoja baada ya mwingine na kurudi kwenye gari, sura zao zilitoa tafsiri harisi ya kile kilichokuwa kikiendelea. Hakukuwa hata na sababu ya kuuliza kwani walio salia waliufunika mwili wa Dokta Gondwe na shuka la kijani kuanzia juu mpaka chini na kisha kuubeba kwenye machela hii ilionyesha wazi kuwa tayari Roho ya Waziri wa afya imekwisha kuacha mwili.
"Baaabaaaaaaaa!!" Najma alipiga kelele huku safari hii akiwazidi nguvu watu waliokuwa wamemshika, akakimbia na kwenda kusimama mbele ya wataalamu wa afya walioubeba mwili wa baba yake. Najma alianza kuutikisa mwili wa baba yake huku akilia kwa uchungu, baadhi wa watu walifika na kushika tena kwa mara nyingine huku wakijaribu kumtuliza binti huyo ambaye alimpenda mno baba yake.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati sekeseke hilo likiendelea mheshimiwa Profesa Cosmas Kulolwa Rais mstaafu alikuwa bado yuko juu kabisa ghorofani katika nyumba yake ya kifahari. Alikuwa akifuatilia kwa kila hatua juu ya mambo yaliyokuwa yakiendelea wakati huo. Kila kitu kilikuwa kinaenda kama alivyopanga, yote yaliyokuwa yakiendelea wakati huo ilikuwa ni ndani ya mpango madhubuti wa mzee huyu Profesa Cosmas Kulolwa. Tayari alishapata taarifa ya kifo cha rafiki yake kipenzi Dokta Gondwe, sasa alikuwa akisubiri taarifa mbili muhimu wakati huu. Ya kwanza ilikuwa ni kukamatwa kwa Inspekta Aron akiwa kama mtuhumiwa namba moja wa kesi ya mauaji ya Dokta Gondwe na taarifa ya mwisho ilikuwa ni hukumu ya kijana wake Osward mahakamani muda mfupi ujao.
Wakati akiwaza hayo mara simu yake iliingia ujumbe wa maandishi katika mtandao wa WhatsApp ujumbe uliombatana na picha. Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Profesa Fernando wa mexico mkurugenzi mtendaji wa maabara ya ZMLST. Picha iliwaonyesha wazungu wawili ambao sura zao hazikuwa ngeni kwake lakini nyuma yao wakiwa wamesindikizwa na watu weusi watatu waliojazia misuli huku wakiwa na vipara vilivyong'aa sana kichwani. Profesa Kulolwa aliitazama ile picha kisha akasoma ujumbe uliopo chini.
,,,,,,,,,,as we talked before, we have already started an official trip to your country to come and find our gray bottle and then spread the COBOS virus, you have definitely done your job,,,,,,,,,,,
(kama tulivyoongea kabla, tayari tumeanza safari rasmi kuja nchini kwako kwa ajili ya kuja kutafuta chupa yetu ya kijivu na kisha kusambaza ugonjwa wa virusi vya COBOS bila shaka umeshafanya kazi yako)
Baada ya kuusoma ujumbe huu Profesa Cosmas Kulolwa alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu.
"Kumekucha" Alisema Profesa Kulolwa.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili ile gari aina ya Noah ilizidi kuchanja buga kwa kasi huku binti mrembo Asia akiwa ndio dereva, wakati huo Osward alikuwa bize kubadilisha nguo zake akavaa nguo za magereza zile alizotoroka nazo usiku wa jana kisha akamalizia na koti kubwa jeusi kwa juu.
Dakika chache baadae gari ilifika na kuingia hadi ndani kabisa ya lile jengo chakavu walilokuwepo mwanzo.
Asia aliingiza gari ndani na kufungua breki kali, bila kupoteza muda mlango wa gari ukafunguliwa Osward na wale malaika weusi wakashuka kwa haraka.
"Sasa warembo mimi narudi gerezani kisha nitapelekwa mahakamani alafu baada ya hapo nitarudi uraiani tutakuwa pamoja sawa" alisema Osward huku akisogea kwenye moja kati ya pikipiki nne zilizokuwa zimeegeshwa katika mstari mmoja ndani ya jengo hilo.
"Sawa kila la kheri Osward sisi tunarudi eneo la tukio kuangalia kinachoendelea kama ilivyopangwa, jukumu letu la mwisho ni kuhakikisha unashinda kesi bila pingamizi lolote" alijibu Elina huku yeye na wenzake wakivua zile baibui sasa wakabaki na nguo nyingine walizovaa ndani. Vipensi vya jeans vilivyoacha mapaja yao nje, kitopu na kijikoti cha mikono mifupi kwa juu. Waliongeza kwa kuvaa miwani ya jua na mwisho kabisa walichukua siraha kama visu na bastola wakazichomeka kwenye mifuko ya ndani ya koti. Wakati huo Osward alishawasha pikipiki na kuondoka kwa kasi sana.
Baada ya kukamilisha kila kitu Erica Elina na Asia kila mmoja akiwa na pikipiki yake walitoka kwa mwendo wa taratibu nje kabisa ya jengo hilo baada ya kufika umbali wa mita kadhaa wakasimama.
Erica alivua miwani yake na kuwatazama wenzake, wote wakaonyesha ishara kuwa afanye alichokusudiia kufanya. Haraka Erica alitoa rimoti fulani ndogo kwenye mfuko wa pensi yake akabinya kitufe chenye rangi nyekundu hapo mlipuko mkubwa ukatokea kwenye kile jengo walilokuwepo. Kila kitu kikasambaratika na kuteketea kwa moto ikiwa ni pamoja na lile gari Noah nyeusi vyote vilikuwa vikiungua kwa moto wakati huo Erica Elina na Asia wakawa wanaondoka eneo hilo kwa mwendo wa taratibu sana kila mmoja akiwa na pikipiki yake.
ITAENDELEA....
Simulizi ni shillingi 1,000/= lipia kwa mpesa namba 0756862047 jina saul au Airtel money namba 0788967317 jina saul kisha njoo WhatsApp inbox namba hizo hizo